Kipondo havi kwa shemeji....

Kipondo havi kwa shemeji....

kaka umeongea kwa hasira ila umeongea point kabisa.
KIPIPI soma hapo.

Husninyo nimesoma na nimeelewa! In what way unaeza sema kwamba huyu kaka alienda kuingilia ugomvi wa dada na shemejie? Logic ya hiyo post nimeipata but I strongly disagree unless kama wangeanza kugombana mtu na mkewe then kaka mtu akaingilia na kuanza kumbonda shemejie! Haya ugomvi ungeamuliwaje?
 
Dah! waswas wang huyo dadako kamfia huyo bondia, uwe makini aweza rudi wakakufunga bana sababu ndo shahidi wa pekee hapo km mkienda mahhakamani. mimi sijafurahishwa naye natoa sh kwenye maamuzi yako, punguza hasira jela haitokuwa mbali nawe.
mimi napinga sana kumtembelea dada angu kwake, kwani kuna mitihan mingi ukikutana na wahuni kama huyo shemejio unless uwe mvumilivu sana. ukimmiss dada ako mwambie kwako bana, mambo ya kuwa akifukuzwa mnatoka wote siyawezi au km ivyo mnatukanwa ukoo mzima na shukuru umemuwahi yeye, mtakuja pigwa wote na dada yako.
picha ninayoipata ni km vile ni mvuta bangi fulani so usisahau anaweza amua lipiza akirudi, km anathubutu mfuata mke wake na kuwakoromea.
 
Maoni yangu naona nyinyi ndio mliomuendekeza,mpaka kufikia hapo.Mtu ampige dada yenu mpaka amvunje mkono mara mbili,akumwagie chai, ampige dada mbele yako kwa kumkanyaga kwenye mkono wenye POP,aseme atawaoa ukoo mzima,amesha ua na bado uwekewe kikao kwa action uliyochukua,Sio bure ipo sbabu,huenda anawasaidia kifedha hivyo mnamuogopa au familia yenu hamna upendo na umoja,kwa ujumla iko sababu ya ukweli nyuma ya pazia sio bure.
 
safi sana mkuu, ulifanya vyema hasa, ila mimi nailaumu familia yako hasa wale ambao wanaona kitendo ulichokifanya ni sawa na kuingilia ndoa ya dadako, walipaswa wakusapoti ili kumkomesha huyo shemeji yako na vitendo vyake vya kipuuzi, hiyo ni kesi ndogo sana if the matter goes to worse na kesi ikafikishwa mahakamani niPM nitakuunganisha na wanasheria.
 
You have done the right thing.... especially kwasababu jamaa alikukosea heshima wewe in person.... ingekua wrong endapo jamaa angekuonyesha heshima na wewe ukaamua kuwa mtemi

I am sure he wont do it to any relative wenu from now on....

Uppuzi una mipaka ila yeye alishindwa kujua mipaka yake

next time akileta piga zaidi
 
kwani huyo dada yenu mnashindwa kumteka usiku,mkamfunga kitambaa machoni mkaenda kumbwaga mahali asipopajua akae hadi akili timamu irudi? mleteni kwangu niwafichie,ebooo!
aisee,nakubaliana na mtm,mwanaume kudharauliwa na mwanaume mwenzio haifai! na usiache kwenda kumsalimia tena dadako na akileta dharau vunja kiuno ili dadako aweze kuamua kuondoka! dada yenu anahitaji proffessional help aisee.
 
aiseeeeeeeeeeeeee

bange kweli mwanaharamu, kuku wako mwenyewe ya nini umnyatie??
 
afu wewe!!!! bahati yako leo nimefunga sunnah!
sasa kama mtu anapigwa kila siku na hashauriki? aisee,nnavyompenda mdogo wangu ule upendo wa ashadii,kama niisingemteka yeye ningemteka huyo kenge na angeipata khabari yake! afu na mtoa mada nae, talaka haidaiwi chumbani! huyo bidada si aondoke talaka itamfuata huko aliko? mi nakasirika kweli mwanamke kushindwa kujitambua!

aiseeeeeeeeeeeeee
bange kweli mwanaharamu, kuku wako mwenyewe ya nini umnyatie??
 
Hongera sana kaka yaani ulichokifanya umesaidia kupunguza waume wakorofi. Nina uhakika akitoka hapo ameshika adabu! Lakini pia uwe makini maana kama alishaua mtu anaweza akawa ni mtu wa kisasi!
 
Kwanza wewe ni mwanaume wa maukweli kabisa maana kuna mijitu haina ubinadamu wanatesa dada zetu wakijua wakishaoa wanaona kama wametoa mahari za ngamia kuanza kuwafanya punch bag huku wanawake wakivumilia eti ndiyo ndoa za ki africa mimi kwetu tuna hazina ya wadada wa kutosha na nilipoona mmoja anapigwa sikuvumilia zaidi ya kumwambia arudi home na yule ambaye alinisikiliza nilimfundisha karate kidogo ya kukabiliana na mumewe sasa akileta mdomo anashikishwa adabu na amenyooka ndoa yake imetulia sasa wanakula maisha bila matatizo ya vibondo.

Back to Topic: Ni hivi hakuna kuomba msamaha wala nini waonyeshe kuwa haujutii ulichokifanya na hata hapo akiendelea kuleta nidhamu zake za ki masaburi utampatia kichapo cha ziada na hakikisha dada yako hatoki hapo home mpaka akubali kwa maandishi kuwa hata mgusa hata siku moja na siku akifanya hivyo ndiyo mwisho wa hiyo ndoa na utamchukua dada yako utamsaidia kimaisha na asije kutia mguu hapo utakapompangishia nyumba.

NB: Na nyie wadada muwe mnaangalia mahali pa kuolewa na siyo mnaolewa milango ya nane mtakuja kuolewa na hata mashetani.
 
Husninyo nimesoma na nimeelewa! In what way unaeza sema kwamba huyu kaka alienda kuingilia ugomvi wa dada na shemejie? Logic ya hiyo post nimeipata but I strongly disagree unless kama wangeanza kugombana mtu na mkewe then kaka mtu akaingilia na kuanza kumbonda shemejie! Haya ugomvi ungeamuliwaje?
ishu ni kwamba uwepo wake pale umesababisha kwa kiasi kikubwa hayo yote yatokee. Kwanini huyu kaka asingetulia kwake? Dada mtu ameshajichagulia hayo maisha ya u-tyson. Jamaa anaona amemdhibiti shemeji lakini hiyo haitorejesha amani katika ndoa hata kidogo. Kifupi jamaa, shemeji na dada wote wana makosa. Sioni haja ya kumpongeza jamaa alichokifanya otherwise aje mwanasheria aniambie kisheria sister wako akidundwa kumvunja mguu na mkono shemeji inaruhusiwa.
Ngoja nitafute na watu wa imani waniambie.
 
ubaya haulipwi kwa ubaya sangara. Kwani hakukuwa na namna nyingine ya kumaliza tatizo?
Hivi kwa mfano huyu mama angechezea kichapo hadi mauti yakamkuta ungesemaje? Sometimes we have to cross lines leo umevunjwa mkono wa kulia kesho wa kushoto, keshokutwa kiuno siku inayofuata mauti halafu tunasema kuna njia nyingine za kumaliza tatizo kama watu wameishakaa vikao na kumuongelea mtu halafu habadiliki matokeo ni yale yale what do you expect Husninyo
 
Kwanza wewe ni mwanaume wa maukweli kabisa maana kuna mijitu haina ubinadamu wanatesa dada zetu wakijua wakishaoa wanaona kama wametoa mahari za ngamia kuanza kuwafanya punch bag huku wanawake wakivumilia eti ndiyo ndoa za ki africa mimi kwetu tuna hazina ya wadada wa kutosha na nilipoona mmoja anapigwa sikuvumilia zaidi ya kumwambia arudi home na yule ambaye alinisikiliza nilimfundisha karate kidogo ya kukabiliana na mumewe sasa akileta mdomo anashikishwa adabu na amenyooka ndoa yake imetulia sasa wanakula maisha bila matatizo ya vibondo.

Back to Topic: Ni hivi hakuna kuomba msamaha wala nini waonyeshe kuwa haujutii ulichokifanya na hata hapo akiendelea kuleta nidhamu zake za ki masaburi utampatia kichapo cha ziada na hakikisha dada yako hatoki hapo home mpaka akubali kwa maandishi kuwa hata mgusa hata siku moja na siku akifanya hivyo ndiyo mwisho wa hiyo ndoa na utamchukua dada yako utamsaidia kimaisha na asije kutia mguu hapo utakapompangishia nyumba.

NB: Na nyie wadada muwe mnaangalia mahali pa kuolewa na siyo mnaolewa milango ya nane mtakuja kuolewa na hata mashetani.

nimependa maamuzi uliyochukua baada ya kuona dada zako wanateswa. Sijaona sehemu uliyosema umemtwanga mangumi au kumvunja kiuno shemeji yako.
 
ishu ni kwamba uwepo wake pale umesababisha kwa kiasi kikubwa hayo yote yatokee. Kwanini huyu kaka asingetulia kwake? Dada mtu ameshajichagulia hayo maisha ya u-tyson. Jamaa anaona amemdhibiti shemeji lakini hiyo haitorejesha amani katika ndoa hata kidogo. Kifupi jamaa, shemeji na dada wote wana makosa. Sioni haja ya kumpongeza jamaa alichokifanya otherwise aje mwanasheria aniambie kisheria sister wako akidundwa kumvunja mguu na mkono shemeji inaruhusiwa.
Ngoja nitafute na watu wa imani waniambie.
Hapa nakataa kwani mimi dada yangu akiolewa siruhusiwi kwenda kumtembelea? Hata kama nimekuja kukutembelea kwako kisiwe chanzo cha kunijazia matusi hey i want allow that, wakati huyu dada anapigwa na mumewe nani amesababisha kwa kiasi kikubwa hayo yatokee?? Mimi naamini kwenye imani lakini mambo mengine tusisubiri hadi watu mauti yawafike ndio tuanze kuchukua hatua zingine ni bora kuchukua pre-cautions mapema kabisa, halafu wewe Husinyo inaonekana unapenda sana kuchezea kipondo ngoja nirudi home utanitambua lazima niondoke na mguu wako mmoja lol!!
 
Hivi kwa mfano huyu mama angechezea kichapo hadi mauti yakamkuta ungesemaje? Sometimes we have to cross lines leo umevunjwa mkono wa kulia kesho wa kushoto, keshokutwa kiuno siku inayofuata mauti halafu tunasema kuna njia nyingine za kumaliza tatizo kama watu wameishakaa vikao na kumuongelea mtu halafu habadiliki matokeo ni yale yale what do you expect Husninyo

finest hadi navunjwa viungo vyote hivyo nimetulia tu hapo hapo? Hiyo interval ya siku moja moja ya kuvunjwa viungo ningekuwa nishasepa kabla hajafika kwenye mkono wa pili.
 
Hapa nakataa kwani mimi dada yangu akiolewa siruhusiwi kwenda kumtembelea? Hata kama nimekuja kukutembelea kwako kisiwe chanzo cha kunijazia matusi hey i want allow that, wakati huyu dada anapigwa na mumewe nani amesababisha kwa kiasi kikubwa hayo yatokee?? Mimi naamini kwenye imani lakini mambo mengine tusisubiri hadi watu mauti yawafike ndio tuanze kuchukua hatua zingine ni bora kuchukua pre-cautions mapema kabisa, halafu wewe Husinyo inaonekana unapenda sana kuchezea kipondo ngoja nirudi home utanitambua lazima niondoke na mguu wako mmoja lol!!
kama ni kuchukua hatua huyu jamaa kashachelewa maana sist wake alishakula vichapo vya kutosha(alichokifanya ni kupunguza hasira na si kutatua tatizo). Hebu msome derimto hapo chini.
 
Inasikitisha sana kuona haya mambo yanaendelea kwenye jamii yetu katika karne ya 21! The weak get abused sana katika society, na ndio sababu ya sheria. Ivi talaka ni mpaka mkubaliane? Sidhani! Hata akigoma, mwambie dada yako aondoke tu. Kwani kuna shida gani? Ulichofanya chaweza kuwa ni sahihi, lakini ki-sheria ni assault. Lakini pia unaweza kumwambia dada yako na wewe mfungue kesi ya assault pia. Ngoma droo.
 
nimependa maamuzi uliyochukua baada ya kuona dada zako wanateswa. Sijaona sehemu uliyosema umemtwanga mangumi au kumvunja kiuno shemeji yako.

Kwanza nilikuwa mdogo wakati naona dada yangu mkubwa amezabwa vibao mbele yangu wakati hakuwa na kosa la maana niliona hiyo dharau kubwa sana ukizingatia nilikuwa nawafahamu dada zangu fika na tabia zao na ndiyo maana sikupenda hicho kitokee kwa wadogo zangu na yule niliyemfundisha wa kwanza akanielewa haraka ndoa yake ya kwanza ilivunjika baada ya kupata mwanaume kimeo alimbonda vizuri sana na mwanaume ikabidi achape lapa sasa ameolewa na Muingereza mwenye asali ya Iran anayeheshimu na kujua nini maana ya mwanamke
na pia nchi wanayoishi hakuna tena mambo ya ngumi za kishamba kama hapa kwetu eti unampiga mwanamke ili ajue wewe ni mwanaume atakuheshimu UPUMBAVU MTUPU.
 
safi kabisa, uje uchukue juice yako...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom