Ukienda ugenini usiende mikono mitupu!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
UKIENDA UGENINI USIENDE MIKONO MITUPU!

Anaandika, Robert Heriel

Kama mtu unayejielewa, heshima sio kitu cha bure ingawaje huwezi inunua. Moja ya malezi bora ambayo kijana wa kike au Wakiume unapaswa kuwa nayo ni pamoja na mafunzo kuhusu kwenda na kuishi ugenini. Ukienda ugenini usiende Mikono mitupu.

Ni vizuri kubeba chochote kitu kinachoendana na uwezo wako na ambacho kitawarahisishia wenyeji wako pindi utakapokuwa katika nyumba Yao. Unaweza ukabeba vizawadi kama chakula, nguo, viatu, pamoja na zawadi zingine. Kama utakuwa mvivu kama Mimi basi beba Pesa ambazo zitarahisisha ugeni wako Kwa wenyeji wako.

Haijalishi unaenda Kwa Nani. Haijalishi mnauhusiano gani, iwe ni Kaka, Dada, shemeji, Mama, Baba au Ndugu au rafiki, ni lazima ubebe zawadi. Kama unaakili timamu.

Tena Kwa Mwanaume ndio kabisa! Zawadi ni Jambo la lazima. Epuka kuwa mzigo Kwa MTU. Fanya kadiri uwezavyo usiwe mzigo Kwa mtu.

Ukizaa Watoto na ukawa na familia, ukataka Watoto wakasalimie ndugu zako(Baba zao, Mama zao au wajomba au mashangazi, au Bibi na Babu) usiwapeleke Watoto wako mikono mitupu Huko waendako.
Wape chochote waende nacho, wape salami za zawadi, lakini pia wape chakula kitakachowatosha kuwasaidia wenyeji wao kuwahifadhi Watoto wako muda watakaokuzaa Huko. Huo ndio undugu.

Ukishafikisha umri wa miaka 20+ na unaishi ugenini(iwe Kwa Kakaako, dadaako, Shemeji yako, mjomba au Baba au rafiki) epuka kuwa mzigo/tegemezi. Kamwe usijipe sababu ya kuwa mzigo Kwa MTU mwingine. Sijui Maisha ni magumu, sijui hakuna kazi, hizo ni sababu zinazotolewa na watu wavivu na wazembe. Fanya kazi hapo nyumbani kwake, safisha nyumba, panda Bustani ya Maua na mbogamboga, jiweke Busy muda wote.

Yakobo alipomkimbia Esau nduguye, akaenda Kwa Labani mjombaake(Dadaake mamaye) kule hakwenda kuwa mzigo licha ya kuwa alikimbia matatizo. Lakini alikuwa akichunga Mifugo ya mjomba wake, Labani.
Nabii Musa alipokimbia Mkono wa Farao Baada ya kumuua Mmisri, akakimbilia Midiani, huko akapata bahati ya kukutana na Yethro(ambaye baadaye alikuja kuwa Mkwewe) Musa hakuwa mzigo Kwa Baba mkwe wake. Alichunga Mifugo ya Mkwe wake, hapohapo akapewa na MKE aitwaye Sipora.

Undugu sio kigezo cha kuwa mzigo Kwa MTU. Matatizo(yasiwe ya afya) sio sababu ya kuwa mzigo Kwa MTU. Kuwa mzigo Kwa mtu ni tatizo kubwa kuliko matatizo yote Duniani, hivyo ndivyo mitazamo ya Watu Werevu ilivyo.

Mikono mitupu ndicho nikisemacho, huna cha kutoa(ku-offer), wewe ulishwe, upewe malazi kama mtoto Mdogo. ATI kisa Fulani ni ndugu au rafiki yako, come on! Huo sio uungwana. Hiyo ni Dhambi, na kujidharau kisha kutafuta Kwa nguvu kudharauliwa.

Hata Mungu(wakwenye Biblia) amesema hapokei MTU mikono mitupu, amesema; usije kwangu mikono mitupu. Hata ukienda Kwa miungu ya kijadi(waganga na waganguzi wa kienyeji) kamwe hautopokelewa mikono mitupu.
Ni aibu kwenda Kwa Watu mikono mitupu. Ni aibu kuishi Kwa mtu bila mchango wowote, kumuelemea MTU.

Vijana na mabinti, hukupewa Akili na Nguvu ili umtegemee mtu mwingine. Hakikisha mchango wako chanya unaonekana. Hiyo ndio maana ya kuishi. Usiwe kama mfu anayetembea.

Niliwahi waambia Wanawake, na wenye Akili walinisikia, yakuwa; kamwe usikubali kuwa mzigo Kwa Mumeo. Wewe ni MKE, hadhi ya MKE ni kuwa msaidizi Kwa Mumewe na sio kuwa tegemezi/mzigo. Yaani uhudumiwe kila kitu. Niliyasema hayo na ninayarudia mara Kwa mara kuyasisitiza Kwa sababu najua impacts zake.
Mwanamke mchapakazi, asiye mzigo huzaa Watoto wachapakazi wasiomizigo. Lakini Mwanamke mlemavu(asiyefanyakazi) na mzigo huzaa Watoto mizigo na waliolemaa.
Mama ndiye anayefundisha Watoto heshima na adabu, uchapakazi na tabia zingine.

Attitude ya kutokuwa mzigo Kwa mtu chimbuko lake ni Kwa wazazi. Ni lazima ujitegemee. No excuse katika kujitegemea. Na kama haujitegemei kulingana na Hali Fulani ngumu basi kamwe usiwe mzigo Kwa MTU mwingine.

Taikon nimemaliza, mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
UKIENDA UGENINI USIENDE MIKONO MITUPU!

Anaandika, Robert Heriel

Kama mtu unayejielewa, heshima sio kitu cha bure ingawaje huwezi inunua. Moja ya malezi bora ambayo kijana wa kike au Wakiume unapaswa kuwa nayo ni pamoja na mafunzo kuhusu kwenda na kuishi ugenini. Ukienda ugenini usiende Mikono mitupu.

Kwa sasa Dar es salaam
Pointfull mkuu, lakini wazazi ndio chanzo cha watoto wetu kua wavivu na wazembe utakuta mzazi anafanya kazi anarudi ucku mtoto anarudi shule anafanya kazi zake analala mtoto huyu hata kushika jembe atakua hajui kutokana na uangalizi mbovu was wazazi
 
Pointfull mkuu, lakini wazazi ndio chanzo cha watoto wetu kua wavivu na wazembe utakuta mzazi anafanya kazi anarudi ucku mtoto anarudi shule anafanya kazi zake analala mtoto huyu hata kushika jembe atakua hajui kutokana na uangalizi mbovu was wazazi

Ni Kweli, baadhi ya Wazazi hawatimizi wajibu wao, hasa kina Mama. Jukumu kubwa la Mama ni kuzaa na kuhakikisha mtoto anakuwa katika malezi Bora, ikitokea changamoto ya malezi anaiwasilisha MWA Mzee ili mtoto apewe Dawa ya ugonjwa WA kitabia. Lakini hayo Kwa baadhi ya Wazazi hawayafanyi.
Hawajali na bila Shaka hawawapendi Watoto wao
 
Ni Kweli, baadhi ya Wazazi hawatimizi wajibu wao, hasa kina Mama. Jukumu kubwa la Mama ni kuzaa na kuhakikisha mtoto anakuwa katika malezi Bora, ikitokea changamoto ya malezi anaiwasilisha MWA Mzee ili mtoto apewe Dawa ya ugonjwa WA kitabia. Lakini hayo Kwa baadhi ya Wazazi hawayafanyi.
Hawajali na bila Shaka hawawapendi Watoto wao
Wanashindwa kutofautisha malezi bora na kudekeza mtoto, wanawadekeza watoto AF wanasema no malezi bora
 
UKIENDA UGENINI USIENDE MIKONO MITUPU!

Anaandika, Robert Heriel


Kwa sasa Dar es salaam
Uko sahihi100asilimia,kuna watu hawayajui haya!Hilo nilijifunza toka kwa bibi yangu,na sasa Nina miaka53kwa Sasa kazi ya kuajiriwa ilikoma!Nimekuwa gumzo kwa ndugu na jamaa kwamba nilikuwa NOMA!kwa zawadi
 
UKIENDA UGENINI USIENDE MIKONO MITUPU!

Anaandika, Robert Heriel

Kama mtu unayejielewa, heshima sio kitu cha bure ingawaje huwezi inunua. Moja ya malezi bora ambayo kijana wa kike au

WEWE NI MJINGA TU NA ULIYEJIFUNGIA FIKRA ZAKO KWA KUKULIA KIJIJINI NA HUO UALIMU WAKO.

UNAJIKUTA UNA UTASHI WA KUCHAMBUA MAMBO NA HICHO CHETI CHAKO CHA UALIMU

NAKUSHAURI ANDAA MAANDALIO YAKO YA KISWAHILI NA FASIHI NA UACHE KU”GENERALIZE” VITU.

HUKO KWENU MUWE MNABEBA KUKU NA MAHINDI MKITEMBELEANA
 
Je Kama huna hizo zawadi inakuaje au tuendelee kukaa huku Bukoba tulime mpunga?

Inatengeneza mentality mbovu kuzoesha watu kila ukienda una kitu mkononi matokeo yake ni kuwa badala ya kufurahia ugeni watu wanafurahia na kuwa na hamu kitu gani utawapelekea
 
Mtu anakuja kwako bila aibu anasema maharage huwa Hali Tena kanyooka kwenye kochi lako!Wakati wanao unawaambia hapa ni kukaa tuu!Noma hiyo

😂😂😂
Kama anacheti cha Daktari asikilizwe. Lakini kama Hana ni mapenzi yake basi hanabudi kujinunulia mboga. Ratiba ya familia itafuatwa kama ilivyo
 
Back
Top Bottom