SoC02 Kipi kipewe kipaumbele kati ya Elimu-Taaluma na Elimu- Ufundi hapa Tanzania?

Stories of Change - 2022 Competition

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,857
UTANGULIZI

Elimu ni njia utumiwayo na jamii kusambaza maarifa, ujuzi, mitazamo na maendeleo. Elimu hutolewa kwa njia kuu mbili, elimu rasmi ( itolewayo shuleni kwa miongozo maalumu) na Elimu isiyokuwa rasmi ( hutolewa nje ya darasa ( pasipo kufuata miongozo maalumu)

Hapa Tanzania, elimu ilianza zamani hata kabla ya Uhuru na baadae tulipopata Uhuru, serikali ikaweka miongozo yake ya namna gani elimu yetu nchini itolewe. Elimu yetu nchini ina historia ndefu lakini kwasasa naweza kuelezea mfumo uliopo nchini.
Mfumo uliopo kwasasa ni

2+7+4+2+3...
Huu ni mfumo wa elimu nchini Tanzania ukiwa na maana ya kwamba
2- mtoto anaweza kusoma madarasa ya elimu ya awali kwa miaka miwili kabla hajajiunga na Elimu ya Imsingi. Kwa mjibu wa mtaala wa elimu ya awali uliopo sasa, elimu ya awali inaanza na watoto wenye umri Kati ya miaka 4-5

7= Huu ni mfumo wa elimu ya msingi nchini unaolenga mtoto kuanza darasa la kwanza akiwa na miaka sita na atasoma kwa miaka saba kabla ya kujiunga na Elimu ya sekondari. Katika mfumo wa elimu ya msingi, mtoto hupimwa kwa awamu mbili kabla ya kuhama darasa, hupimwa akiwa darasa la nne na akiwa darasa la saba.

4= Huu ni mfumo wa elimu ya sekondari-ngazi ya chini.
Mwanafunzi husoma kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Elimu ya sekondari-ngazi ya juu.
Katika ngazi hii, mwanafunzi hupimwa kwa awamu mbili pia. Akiwa kidato Cha pili (form two ) na akiwa kidato Cha nne ( form four ).
2= Elimu ya sekondari-ngazi ya juu, hii ni ngazi ya sekondari ambayo wanafunzi husoma kwa miaka miwili ( form 5 and form 6 kabla ya kujiunga na Elimu ya juu ( vyuo vikuu)


MIKONDO YA ELIMU

Hapa nchini Tanzania, tunayo mikondo miwili ya elimu, ambayo ni:-
1. Elimu-Taaluma
2. Elimu- Ufundi

1. Elimu- Taaluma ni mfumo wa elimu unaokusudia kumwandaa mwanafunzi katika utaalamu ( professionals). Mkondo huu wa Taaluma ndiyo unaojulikana waziwazi na wanafunzi wengi kwamba, amalizapo masomo yake, atapata kazi Kama kuwa
  • Daktari
  • Rubani
  • Mwalimu
  • Nesi
  • Mfamasia
  • Mhasibu
  • Mwanasheria
  • Mkandarasi nk.

2. Elimu- Ufundi, huu ni mfumo wa elimu usiofuata mfumo wa elimu-Taaluma.
Mfumo huu hauna vigezo vingi vya namna ya kujiunga kwasababu, mwanafunzi yeyote anaweza kujifunza kulingana na level anayoiweza. Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kupata mafunzo ya Ufundi uashi hata Kama hana elimu ya ngazi yoyote mkondo wa TAALUMA. Lakini pia mwanafunzi anaweza kujiunga na Elimu Ufundi baada ya kupata ngazi moja au mbili ya elimu mkondo wa TAALUMA. Hivyo, elimu mkondo wa Ufundi hautegemei Sana ulazima wa elimu mkondo wa taaluma hata Kama ni muhimu.


UPI NI MKONDO MZURI WA WANAFUNZI KUFUATA?

Mikondo yote ya elimu tajwa hapo juu inakusudia Kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ajira kwa Vijana na kuleta maendeleo katika nchi.

Pamoja na ufanano wa malengo ya mikondo ya elimu, Kuna haja ya mikondo hii ya elimu kupitiwa upya na kuona namna nyingine ya kuboresha ili kufikia malengo tarajiwa. Wanafunzi wakijua umuhimu wa kila mkondo na changamoto zake, wataamua mkondo upi ni mzuri zaidi katika kutimiza ndoto zao za maisha.


MKONDO MZURI WA ELIMU

Mikondo yote tajwa hapo juu ni mizuri na yote inategemeana. Pamoja na kutegemeana, upo mkondo ambao unaonekana kuwa ni afadhali kuliko mwingine. Wewe binafsi Kama msomaji, utakubaliana nami ni mkondo upi una uafadhali katika kujifunza kwa mwanafunzi.

Binafsi naamini mkondo wa Ufundi ndiyo mkondo mzuri zaidi kuliko mkondo wa TAALUMA kwasababu zifuatazo:-

1. Mkondo wa Ufundi huibua karama za mwanafunzi zilizojificha wakati mkondo wa TAALUMA huficha karama za mwanafunzi. Hii ni uhakika kwasababu, wapo watu mpaka sasa wanaishi professional ambazo hazikuwa ni karama zao lakini kwasababu ya kujikuta wamefuata mkondo wa TAALUMA, wamejikuta wao ni waalimu, wahasibu, Rubani, madaktari, wanasheria nk. Hawa utawajua tu kutokana na ufanisi wa kazi zao.

2. Mkondo wa elimu-ufundi hauna kufelisha sana wakati mkondo wa elimu-taaluma unaferisha sana .Hii nikwasababu, takwimu zinaonyesha, wanafunzi wengi walisomea Ufundi hufaulu zaidi katika UPIMAJI WA MITIHANI YAO kuliko Upimaji wa mitihani katika ngazi ya elimu mkondo wa TAALUMA.
3. Muda wa ujifunzaji wa elimu mkondo wa Ufundi ni mfupi kuliko mkondo wa elimu taaluma.
4. Wahitimu wengi kutoka mkondo wa elimu- Ufundi wanaajirika kuliko wahitimu wa mkondo wa elimu taaluma.


CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI ELIMU MKONDO WA UFUNDI:

Pamoja nakuonekana elimu- mkondo wa Ufundi kuwa ni mzuri Sana, lakini umekuwa na changamoto nyingi zaidi Kama ifuatavyo:-

1. Serikali imeshindwa kuhamasisha zaidi wanachi wake kuhusu elimu mkondo wa Ufundi. Hii imepelekea jamii kujua Kuna mkondo mmoja tu wa elimu, na kila mzazi amekuwa akiweka malengo ya mtoto kwa kuegemea elimu mkondo wa TAALUMA.

2. Wizara ya elimu imekosa mfumo mzuri wa kupeleka wanafunzi katika elimu mkondo wa Ufundi nakupelekea wahitimu wengi kusalia mtaani wasielewe nini Cha kufanya. Hapa serikali lazima iandae mazingira mazuri ya vyuo vinavyotoa elimu mkondo wa Ufundi wa namna ya kupata wanafunzi wengi zaidi. Mfano, kuanzia darasa la saba asiwepo mwanafunzi anayefeli mtihani, badala yake mwanafunzi apewe machaguo ya either aende MKONDO WA ELIMU-TAALUMA au ELIMU MKONDO WA UFUNDI

Hapa zitawekwa grades kuwabaini watakaoenda mkondo moja wapo wa elimu. Kwa mfano, wale wote watakaopata wastani kuanzia B kushuka chini, waende mkondo wa elimu Ufundi. Tukifanya hivyo, mkondo wa elimu Ufundi utapata wanafunzi wengi kuliko taaluma na Taaluma itapata watu wachache wabobezi katika masomo yao kuliko kwenda na wengi wasiojiweza na siyo karama zao.


HITIMISHO

Kutokana na mrundikano wa wahitimu wengi Elimu mkondo wa TAALUMA, serikali ione haja ya kugeukia elimu mkondo wa Ufundi. Serikali iweke nguvu nyingi katika mkondo huu kuliko ilivyo sasa. Elimu bila Ada ihamishiwe mkondo wa Ufundi.

Serikali kupitia media mbalimbali ihamasishe vijana wengi kupenda kusomea elimu mkondo wa Ufundi kwani ndiko Kuna uhakika wa ajira za moja kwa moja baada ya kuhitimu.

Zifuatazo ni fani/ courses zinazotolea mkondo wa elimu Ufundi.
  • uashi
  • umeme
  • udarizi
  • ususi
  • upishi
  • makenika
  • seremala
  • uchomeleaji
  • udreva
  • Ufundi wa vifaa vya elekroniki
  • Ukarabati
  • computer
Nk.

Katika kufanikisha hili, uandaliwe mtaala mzuri utakaowaongoza vyema wanafunzi watakao chagua elimu mkondo wa Ufundi, pia wasibanwe kujiendeleza kuendelea na Elimu ya juu hata kupata UZAMIVU/ DOCTORATE kupitia mkondo huohuo wa elimu Ufundi. Kila mtu atakuwa na furaha na Elimu aliyoichagua na hatutakuwa na vijana wa mtaani kwasababu watoto wote watakuwa masomoni.

Mwisho kabisa, nichukue fursa hii kuwashukuru wote mliotumia muda wenu kujisomea makala hii. Usiache kushare kwenye magroup mbalimbali ya WhatsApp na Facebook ili mawazo haya yawafikie viongozi wetu wapate kuyafanyia kazi.

Usisahau kunipigia kura yako Kama umependezwa na wazo langu. Nawatakia kilakheri katika shughuri zenu
🙏🙏🙏🙏🙏🙏✍️✍️✍️
 
Tafadhari wadau wa elimu changieni maoni yenu ni muhimu Sana haswa sasa ambapo serikali inajaribu kutafuta suhuru la tatizo la ajira nchini
 
Back
Top Bottom