Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda: Mitaala ya mipya ya Elimu imeanza Shule ya Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Snapinsta.app_430218013_18342532396103230_2987892124817677517_n_1080.jpg

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
Snapinsta.app_429827565_18342532480103230_1411779955375004373_n_1080.jpg

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya Elimu ya awali msingi sekondari na Ualimu.

Prof. Mkenda amewaeleza Wahariri wao kuwa serikali imeanza kutekeleza Sera na Mitaala hiyo kwa baadhi ya ngazi za elimu huku akisisitiza kuwa utekelezaji huo unafanywa kidogo kidogo ili kuhakikisha unakuwa na mafanikio.

Aidha, ameongeza kuwa ifikapo Mwaka 2027 watakaokuwa darasa la sita na wale wa darasa la saba watamaliza elimu ya msingi kwa wakati mmoja na kufanya makundi mawili kuingia elimu ya sekondari kwa wakati mmoja na hapo ndipo itakapoanza elimu msingi kuwa ya miaka kumi.
Snapinsta.app_429792660_18342532363103230_8935939118028970573_n_1080.jpg




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda anazungumza na Wanahabari kuhusu Sera na Mitaala ya elimu Nchini, leo Machi 7, 2024 kwenye Ukumbi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Jijini Dar es Salaam.

Snapinsta.app_430252888_18342530479103230_2008157696056269910_n_1080.jpg

Prof Carolyne Nombo

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Carolyne Nombo amesema serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu hasa katika Ujenzi wa miundombinu na kutoa mafunzo Kwa Walimu kazini.

Amesema hayo Machi 7, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo ameongeza kuwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mbali ya uwekezaji huo imefanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kuja na Toleo la 2023

"Ndani ya miaka miwili tuliweza kufanya majadiliano na jamii ya Kitanzania kuweza kupata maoni na mahitaji ya Watanzania namna gani wanataka elimu yao iwe" amesema Nombo.

Kiongozi huyo amesema pamoja na kwamba zimetumia mbinu mbalimbali za kuelimisha umma wa Watanzania lakini bado wizara iliona umuhimu kukutana na kujadiliana na wahariri ili wapate uelewa wa mabadiliko yaliyofanyika ili waweze saidia katika kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
 
Tatizo kwenye elimu yetu kila mtu ni msemaji na mpangaji.Ukienda kwenye halmashauri nadhani utakuta Kila mmoja anafata taratibu zake kama vile ni nchi tofauti.Mimi nadhani hizi sera serikali ikataze watu wengine kuongea mambo yao hususan katika ngazi za chini.Kwani utakuta mfano DEO wa Kaliuwa anataratibu zake na wa Kibondo ana ya kwake kitu ambacho sicho.
 
Yataongewa mengi sna ila yote hayo yanahitaji budget kubwa na sio maneno yanayopinduliwa Kila Leo kwenye makaratasi
 
Sera mpya ni maslahi Bora na mazuri kwa walimu bila hivyo ni mark time tuu.

Mabadiliko ya Elimu yawe ni mabadiliko ya maslahi ya walimu bila hivyo HAKUNA KITU.
 
propesa porojo porojo na maneno mengi hajawahi kuwa na kitu cha maana huyu chawa wa kichagga kimsingi hamna msomi hapo, nimekaa paleee mje mniue.
 
propesa porojo porojo na maneno mengi hajawahi kuwa na kitu cha maana huyu chawa wa kichagga kimsingi hamna msomi hapo, nimekaa paleee mje mniue.
Sa kulikuwa na haja gani hadi kutaja kabila la mtu kwenye jambo alilofanya au Lina uhusiano gani na utendaji kazi wake na kabila.
 
Tatizo kwenye elimu yetu kila mtu ni msemaji na mpangaji.Ukienda kwenye halmashauri nadhani utakuta Kila mmoja anafata taratibu zake kama vile ni nchi tofauti.Mimi nadhani hizi sera serikali ikataze watu wengine kuongea mambo yao hususan katika ngazi za chini.Kwani utakuta mfano DEO wa Kaliuwa anataratibu zake na wa Kibondo ana ya kwake kitu ambacho sicho.
Siku hizi wanasema silaba iishe mwezi wa nne
 
Yataongewa mengi sna ila yote hayo yanahitaji budget kubwa na sio maneno yanayopinduliwa Kila Leo kwenye makaratasi
Hii nchi ngumu sana,yy profesa alifanya mtihani wa kuingia kwenye ajira,
Hili ndo tatizo kuku kuvikwa kilemba,yaani mtihani ndo umeonekana punguza watu kwenye ajira 🤔
Profesa hana jipya,ukiona product hainunuliwi basi punguza uzalishaji wa hiyo product
 
Sijajuwa tuna bolesha elim au tanazidi kuibomoa manayake ata awa wanao ishia darasa la 7 awajui kusoma awa wanao ishia la 6 itakuwaje
 
Hiyo 2027 hao watoto watakaorundikana sekondari watafundishwa na nani ajira amuajiri tuna wazoom tu
Wanaleta siasa kila mara,eti wamejikita kuelimisha walimu walioko kazin,kuajiri wanaajiri mara chachechache,wanaleta siasa ili waendelee kula pesa za mafunzo.Watoe ajira za walimu tupate ahueni ya maisha.We are tired.
 
Imagine mwalimu anayeajiri amefaulu mitihani za necta kadhaa nacte na TCU ambazo ni vyombo vya serikali akakabidhiwa vyeti Kama qualified teacher akakaa mtaani akijihangaisha kutafuta ugali wake wa kila cku huku akickilizia ajira za ualimu mpka 5-10 year then waziri anakuja anasema utafanya mtihani ili uajiriwe na akifeli that means vile vyeti alivohangaikia miaka yote zinakuwa useless duh nchi hii ngumu Sana
 
Mwaka jana mlisema watoto walio kuwa darasa la tatu mwaka jana ndio watasoma hadi darasa la sita mwisho. Leo tena naona taarifa mnasema kwamba waliopo darasa la tatu mwaka huu ndio watasoma hadi darasa la sita. .

Vipi mbona mnatuchanganya? Hebu toeni taarifa inayo eleweka
 
aisee hii nchi wanacho kiaangariza ni kuona namna gani secta ya elimu wafanya kazi wake hawafaidi tena keki ya taifa. sasa lengo la kumpa mtihani mwajiriwa ili aingie kwenye mfumo wa ajira ni nini haswa. kama lengo ni kupata wafanyakazi wenye ufanisi wa hali ya juu mbna tayari tunao. tuseme tu ukweli bira kuficha ficha. huyo profesa yeye alipo ingia kwenye mfumo wa ajira alipewa mtihani ?. kwanin tunaumizana wenyewe watanzania. kila kuitwapo leo ufauru unaongezeka kwa vijana wetu sio standard 4 sio standard 7 sio kidato cha 2 wala cha 4 mpaka form 6 levels zote hizi ufauru unapanda kila mwaka pasina kuwapa mitihani wafanyakazi. na maeneo yanayo ongoza kwa kuferisha ni maeneo ya vijijini to ambao mazingira sio rafiki sana kwa wanafunzi kusoma, ndio maana inatia ugumu katika ufundishajii na kujisomea kwa wanafunzi. sasa ni jukumu la chama cha waalimu kusimama na kuona namna gani wanaweza kupinga fikra mbovu za huyoo profesa. basi kama ni hivyo TCU waanze kutoa mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa vyuo kama ilivyo kwa levels nyingine. ma sio kumpa mamlaka mkufunzi wa chuo kwenye swala la mitihani ya mwanafunzi.
 
Back
Top Bottom