Aisee kitunguu kinalipa kama utaweza kusimamia mwenyewe kwa ukaribu ila ukiwatumia vijana wa mtaani watakukondesha kwa mawazo.
Mimi nimejaribu maeneo ya Mtandika japo wameniliza ila nimeshajua jinsi ya kutoka kwani ujinga ni wakati wa kwenda tu.
 
Gharama nilizoingia wakati nalima

ActivityElaborationsCalculationsAcre 1Acre 2Acre 3
Kukodi 250000*1250000500000750000
Kutifua 100000*1100000200000300000
Arrow 70000*170000140000210000
Kutengeneza majaruba 600*10060000120000180000
Kupanda 500*10050000100000150000
Mbolea 70000*2140000280000420000
Mbegu 30000*7210000420000630000
DawaMajani (Megasate)20000*360000120000180000
Wadudu (Profecron)20000*360000120000180000
Kumwagilia 200000*1200000400000600000
Palizi (Kupiga Godi) 700*10070000140000210000
Palizi ya Pili 700*10070000140000210000
Mlinzi 700000*1700000700000700000
Kung'olea 600*10060000120000180000
Kukata Majani 700*10070000140000210000
My travel costs 100000*5500000500000500000
Emergency 500000700000900000
Total 317000048400006510000

Mkuu Bavaria, naomba umalizie pia hapo... kwa kila Ekari moja unaweza kupata kilo Ngapi kwa makadirio? Na mapato pia kwa bei ya soko ikoje? Pia hizi details ni maeneo gani?

Shukrani mkuu kwa details nzuri.
 
Gunia 70-100 kutegemea na ulivyolima.
 
Kwa ekari moja ya kitunguu

Haipungui Milioni 2.5

kUNA GHARAMA NYINGI SANA

KUNA gharama za shamba kukodi, (Kuandaa)= tsh 250,000, vibarua-300,000, Mbolea za kupandia na kukuzia (Mfano yara Miller Winner, yara Nitrabo)=200,000 dawa za wadudu (Selecron, Dudu all)=40,000, Dawa za kuua majani (HII NI DAWA MAALUMU YA KUUA MAGUGU KATIKA VITUNGUU TU-INAITWA OXYFEN AU SUFEN)=35000, Vibarua wa kupandikiza na kutengeneza matuta au Majaruba, kumbuka kitunguu kinachukua wiki 6 hadi 8 katika kitaluuu, Gharama za maji kwa siku 120, si chini ya tsh 900,000 (Gharama kubwa ipo katika mafuta), Gharama ya mbegu kama unaanza usinunue hybrid za juu labda kama Neptune F1, Au Jambar F1, ANZA TU NA OPV kama Red Cleore, kwa ekari moja utahitaji si chini ya Kilo 4 ambazo ni kama 350,000tsh . Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold au, Ebony (Mancozeb na Metalaxin) tsh 25,000, Booster Copper Mix (tsh 15,000), Bado gharama ya nauli, Gharama ya Magunia, na Vibarua wa kuvuna, na kupakia, Bado gharama za kusafirisha.. KWA HIYO KAMA UNA CHINI YA 2.5 MILIONI HUTAFANIKIWA KWA KWELI

MAVUNO KITUNGUU
UKILIMA KITAALAMU SI CHINI YA GUNIA 70 HADI 120/EKA, KUTEGEMEA NA AINA (Mbegu kama Neptune F1, Red Cleore, Jambar F1, au Red Rinoy F1) Zinakupa HAYO MAVUNO
 
Niulize hapahapa tu mkuu, hakuna maneno.

Kwanza, linitaka kujua hizo data ulizotoa hapo ni kwa maeneo gani. Mfano gharama ya kukodi shamba hope inaweza kuvary kutokana eneo na eneo... mimi nataka kufanya Kilosa.

Pili, gharama ya unwagiliaji hiyo inahusisha pump za kusukuma maji au aina gani ya umwagiliaji inatumika?

Tatu, ulisema Akari 1 inatoa gunia 70 - 100. Je, gunia moja linakuwa na Kg ngapi? Au mauzo yanafanyika kwa Gunia? If yes bei zikoje za shamba aitha kwa Kg au gunia?
 
Okay hizo ni gharama ambazo nilikutana nazo mimi binafsi nililima ruaha mbuyuni. Nimeweka hapo ili upate overview ya gharama zote, ndio zinaweza kubadilika kutoka eneo moja kwenda jingine.

Pia umwagiliaji ilikuwa wa pump ila wewe ukipata eneo ambalo lipo karibu na maji ni sawa tu kupunguza gharama. Yani sio lazima gharama zako ziwe sawa na hizo, zinaweza kuzidi au kupungua.

Gunia haliuzwi kwa KG, wanauza as gunia, na bei pia inategemea na msimu na mavuno kwa kipindi hiko.

Kuna wakati gunia linaweza kufika hadi 40,000 au 120,000 kutegemea na muda uliovuna.

Sijui nimekujibu kama unavyotaka?
 
Yeah nimekuelewa vzr kabisa na umejibu vyema. May be nijui upi msimu mzuri wa kulima ili kuweza kuvuna katika kipindi ambacho bei inakuwa iko juu??!
 
Yeah nimekuelewa vzr kabisa na umejibu vyema. May be nijui upi msimu mzuri wa kulima ili kuweza kuvuna katika kipindi ambacho bei inakuwa iko juu??!

Misimu inatofautiana kutokana na maeneo.

Mfano kwa Ruaha msimu unaanza March hadi july. Sasa wewe anza kulima kuanzia september hadi february japo ni risky.
 
Habari zenu wana "U"?
Naomba mwenye uzoefu wa kilimo cha vitunguu maeneo ya iringa. Mimi nasoma tumaini iringa 2nd year, nataka nitumie boom lang kwa ujasiliamali coz Maisha sahv ni very tight.

Sasa, nataka nijue wapi shamba linapatikana maeneo gani na gharama kwa hekalu moja kwanza.

Mwaweza nisaidia pia na masomo yake.
 
I mean kwa hekali moja na masoko yake pia .
 
Any place kwenye maji mengi Tanzania hii unaweza kulima vitunguu. Hata ukichimba kisima waeza kuanza kilimo cha vitunguu mkuu. Iringa kuna mashamba mengi yenye rutuba, Ruvu chini, Hata mikoani anywhere as long as una ardhi vitunguu yake maji tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom