Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 532
- 1,089
Mkuu tindo tatizo lako dogo tu. Ilikuwa mara ya kwanza kulima ulipaswa uanze kidogo ili ujifunze kwa gharama kidogo. Biashara yoyote unapoianza mara ya kkwanza mieleka ni kawaida, kama unapojifunza kuendesha baiskeli.
Mtu asitarajie anapoanza jambo kwa mara ya kwanza apige bingo haiko hivyo. Pia ukae ukijua kuwa kunapokuwa na mafuriko ya zao sokoni wanunuzi wote na si madalali peke yao hunyanyasa sana wakulima. Hali hiyo ipo katika kilimo cha nyanya pia.
Mkoa wa Morogoro ukilima nyanya za kiangazi mwezi wa nane hadi wa kumi na moja huwa kuna mafuriko ya nyanya. anaevuna miezi hiyo na kkama ni mara yake ya kwanza ataapa kwamba nyanya si biashara. Kuna msemo huku NYANYA NINYANYUE NYANYA NINYANYASE. Soko zuri la vitunguu ni mwwezi March hadi June. Ukiweza kuwa na kitunguu majira hayo huna maumivu. wateja wanakutafuta na unaweza kuuza kwa utaratibu unaotaka wewe. wakati huo wewe mwenye mali ndio mjanja. suala la madalali linakuwa halina umuhimu na wala si lazima upeleke sokoni na hata ukipeleka sokoni mzigo wako utagombaniwa.
Tumia utaallam uweze kuhifadhi kitunguu uweze kulifikia soko la Mwezi March, au lima vitunguu uvune February au uvune kuanzia mwezi May hadi July. Ukilima kitunguu cha msimu ambacho kila mtu analima maumivu yake ndiyo hayo.
Kwenye suala la soko kunapokuwa na mafuriko hakuna serikali itakayokusaidia hapo utakuwa umeumia tu. wewe mkulima ndiyo unatakiwa uchemshe bongo kuona utalifikia vipi soko la mwezi March hadi July. Hii miezi hakuna dalali atakae kunyanyasa. Na pia sio lazima upeleke mzigo sokoni kunawanunuzi wazuri tu hufuata mazao mashambani. watu wengi wanafanikiwa sana kwa kuuzia mashambani. kama huna uzoefu afadhari ukauzia shamba ukapata bei utakayoridhika nayo kuliko kwenda mjini ukakutana na madalali wajanja ukarudi kijijini na story tu huna pesa mfukoni.
Kwa hiyo Mkuu kila biashara inachangamoto zake. Tumia muda mwingi kujifunza kwa wazoefu badala ya kulalamika hivyo. Ulikosea kuanza kwa kulima pakubwa ukapata hasara ukarudia makosa yaleyale kwa kulima pakubwa zaidi huku hujarekebisha kilichokutia hasara ulipo anza. Ushauri wangu msimu wa kwanza jifunze mbinu za kilimo cha vitunguu uzijue changamoto zake.
Msimu unaofuata boresha uzalishaji kwa kutatua changamoto, pata ushauri kwa wazoefu. Panua eneo kadri unavyopata uzoefu. Hata kama unauwezo mkubwakifedha usianze kuwekeza eneo kubwa kama huna uzoefu. Usivutiwe na takwimu tamu unazosikia nyingi hufikiwa na wazoefu na nyingi ni exagerated.
Ukizalisha eneo dogo inakupa picha halisi itakayokufanya uamue iwapo kilimo hicho kinalipa au la. Na hapo ndiyo utaamua kupanua eneo la shamba kwa kutokana na picha halisi uliyoiona na changamoto zake.