Kilimo cha Canola (Rapeseed) kinaweza kutupunguzia uhaba wa mafuta ya kula

Inabidi kujifunza kutoka Kenya make wanao lima ni wachache sana au labda ni kwa sababu mazingira ya kulima ni ya miinuko ambako Kenya nimachache sana,
 
Ushauri limeni alizeti na michikichi kwa ajili ya mafuta.
Rapeseed linatakiwa lilimwe sehemu za baridi,pia kilimo chake ni cha mzunguko, mwaka huu ukilima canola mwakani unatakiwa ulime maharage/mahindi, kwahiyo kama unalima kibiashara kila mwaka utakuwa unatafuta shamba jipya.
Ingawa linatoa mafuta mengi kuliko alizeti kwenye eka moja.
 
Nimejaribu kufuatilia sijaona wala kusikia wapi Canola inalimwa hapa Tanzania.

Lakini nadhani upatilanaji mbegu siyo tatizo sana, nimeelekeza wadau wangu wanisakie huko Kenya. Ila najua kupitia Jamiiforums pia tunaweza kufanikiwa kuipata maana hapa tupo wadau wengi.
Tuwasiliane tuongee na Watu wa Sua- wao wana ujuzi wa kutuambia wapi Tanzania inastawi na ulimaji wake na isitoshe Morogoro kuna maeneo mengi yapo yanapatikana kwa kilimo karibu PM tuyajenge
 
Maeneo ya Miinuko hasa maeneo wanako lima Ngano, Haihitaji SUA, mfano Arusha sio yote, Kilimanjaro sio yote, Manyara, Mbeya, Iringa, Njombe, wanaweza lima, Morogoro wapi unazungumzia? Msiforce mambo
 
Unaposema sio maeneo yote- ulifanya Utafiti wa Kisayansi au Viroba ndo vinakupelekesha??Acha ujuwaji No research no right to speak! Unaposema Haihitaji SUA unamaanisha nini?? Unajuwa Sheria ya Mimea?? Unajua kuwa ni kosa kuingiza Mbegu bila kushirikisha Wizara ya Kilimo?? Unajua kwa Mfano Mbegu ya Miwa ya Kutengenezea Sukari ili Ipate kibali cha kulimwa hapa Nchini toka uombe na kuleta Sample yake inachukuwa miaka 10!Serikali ya Tanzania Kukupa Kibali chake- kitu kama ujui usikurupuke na kupayuka
 
Mie natumia mafuta ya canola miaka mingi sasa, yanatoka America.

Kama tutaanza mchakato hapa Kwetu itakua habari njema mbona
 
Unaposema sio maeneo yote- ulifanya Utafiti wa Kisayansi au Viroba ndo vinakupelekesha??Acha ujuwaji No research no right to speak! Unaposema Haihitaji SUA unamaanisha nini?? Unajuwa Sheria ya Mimea?? Unajua kuwa ni kosa kuingiza Mbegu bila kushirikisha Wizara ya Kilimo?? Unajua kwa Mfano Mbegu ya Miwa ya Kutengenezea Sukari ili Ipate kibali cha kulimwa hapa Nchini toka uombe na kuleta Sample yake inachukuwa miaka 10!Serikali ya Tanzania Kukupa Kibali chake- kitu kama ujui usikurupuke na kupayuka
So unaweza kulima mfano Kahawa Singida? Wabongo tunajifanyaga wabishi wakati information ziko wazi, sio kila kitu SUA infirmation ziko wazi, Kenya unajua wanako lima ni maeneo gani? Au wao no wajinga ndo hawajui? Wacha ujuaji wa kenge
 
Tupe research uliyofanya kuthibitisha haya unayosema.

#MaendeleoHayanaChama
hio iko wazi kuna Machapisho ya kutosha, kuhusu hili zao, sio zao geni, Basi kalime kule Bagamoyo then utarajie kuvuna make tumejawa ujuaji mbuzi sana
 
Unaposema sio maeneo yote- ulifanya Utafiti wa Kisayansi au Viroba ndo vinakupelekesha??Acha ujuwaji No research no right to speak! Unaposema Haihitaji SUA unamaanisha nini?? Unajuwa Sheria ya Mimea?? Unajua kuwa ni kosa kuingiza Mbegu bila kushirikisha Wizara ya Kilimo?? Unajua kwa Mfano Mbegu ya Miwa ya Kutengenezea Sukari ili Ipate kibali cha kulimwa hapa Nchini toka uombe na kuleta Sample yake inachukuwa miaka 10!Serikali ya Tanzania Kukupa Kibali chake- kitu kama ujui usikurupuke na kupayuka
We mjinga kweli, watu wanalima mbona Kula Arusha? Au Arusha ni nchi inayo jitegemea? Kuna vitu vingi vinalimwa ambavyo ni vigeni sana nenda kwenye Mashamba ya Wazungu uone watu wanalima mazao ya ajabu sana ambayo hujawahi yaona kokote kule.
 
Canola inalimwa maeneo yenye ubaridi hasa miinuko, sehemu wanako zalisha Kahawa au Ngano basi Canola inafanya vyema huko, Pia sio zao rahisi lina kazi sana inahitaji jitihada sio ya kulima kwa simu kama mahindi, Pia uoteshaji wake haupishan sana na wa ngano make lazima kufanya kitu kinaitwa harrowing.Na kama ni shamba kubwa basi inabidi kutumia planter kama ya kupandia ngano kwenye kuotesha make huwezi otesha kama unavyo otesha mahindi, sana ni kama tunavyo otesha ulezi.
 
Unaposema sio maeneo yote- ulifanya Utafiti wa Kisayansi au Viroba ndo vinakupelekesha??Acha ujuwaji No research no right to speak! Unaposema Haihitaji SUA unamaanisha nini?? Unajuwa Sheria ya Mimea?? Unajua kuwa ni kosa kuingiza Mbegu bila kushirikisha Wizara ya Kilimo?? Unajua kwa Mfano Mbegu ya Miwa ya Kutengenezea Sukari ili Ipate kibali cha kulimwa hapa Nchini toka uombe na kuleta Sample yake inachukuwa miaka 10!Serikali ya Tanzania Kukupa Kibali chake- kitu kama ujui usikurupuke na kupayuka
Hao SUA wako wana impact gani katika nchi hii? au unazungumiza ule Ujirani mwema wa kuwasaidia vijiji vinavyo wazunguka?
 
SUA wana impact kubwa sana,mabwana shamba wengi Tanzania ni wa SUA,madaktari wanaotibu mifugo yetu Ni wa SUA,walimu wanaofundisha mabwana shamba na wafugaji kwenye vyuo vya kati ni kutoka SUA.
Watafiti wengi wa kilimo na mifugo. Wamesoma SUA.
Kama unabisha nenda kwenye kituo chochote cha utafiti cha kilimo TARI uulize waliposomea TARI wanafanya kazi nzuri sana pia nenda kituo chochote cha utafiti wa mifugo TALIRI uulize waliposomea nao wanafanya kazi nzuri sana.

TARI wamefanya utafiti wa mbegu mbalimbali zikiwemo za korosho,michikichi,alizeti,mpunga nk.

TALIRI wamefanya tafiti mbalimbali za mifugo ikiwemo ng'ombe,mbuzi nk.

Tusidharau vyuo vyetu.
 
Back
Top Bottom