Kilimanjaro: Shule ya Msingi ya Serikali yaandikisha Wanafunzi watatu (3) kuanza Darasa la Kwanza

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Mlembea, ni moja ya Shule ya Serikali iliyopo Wilaya ya Rombo katika Tarafa ya Mashati Mkoani Kilimanjaro ambapo kwa Mwaka huu wa 2024 imeandikisha Wanafunzi watatu tu (3) kuingia darasa la kwanza kitu ambacho sio kawaida.

Shule hiyo ya Msingi Mlembea jumla ya idadi ya wanafunzi katika shule nzima Kuanzia chekechea hadi darasa La saba inakadirwa kuwa na wanafunzi tisini (90) tu.

Sababu kuu mbili za shule hiyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kuliko shule nyingine inatajwa kuwa ni mambo ya kishirikina yaliyotokea miaka ya nyuma ambapo wanafunzi walikuwa wanadondoka wawapo shuleni hivyo kufanya wazazi kuhamisha watoto wao na kuwaandikisha katika shule nyingine. Ndani ya Tarafa hiyo.

Sababu ya pili inatajwa na baadhi ya wadau ni masuala ya uzazi. Idadi ya Vijana wamekimbilia Mijini na idadi ya vijana waalibaki kuingia kwenye ulevi na hivyo kushindwa kujenga familia.

Sema Uchagani wamebaki wazee kiukweli. Nilienda kuhesabiwa, niliona wazee wengi sana, kila unapopita/enda wazee tu vijana wachache sana.

Ni kweli vijana wengi Uchagani wanakimbilia Mijini. Kwaiyo hata uzazi pia lazima uwe kidogo.
 
Sema Uchaga wamebaki wazee kiukweli..,nilienda kuhesabiwa, niliona wazee wengi sana, kila unapopita/enda wazee tu vijana wachache sana.

Ni kweli vijana wengi Uchagani wanakimbilia Mijini!
Kwaiyo hata uzazi pia lazima uwe kidogo.
... ardhi ya kule imebaki kwa ajili ya kwenda kuzika tu na kugeuza.
 
Nakumbuka miaka ya 93 kuna shule moja ya msingi darasa la saba walikuwa 27 tu!wavulana 11 na wasichana 16
 
Mlembea, ni moja ya Shule ya Serikali iliyopo Wilaya ya Rombo katika Tarafa ya Mashati Mkoani Kilimanjaro ambapo kwa Mwaka huu wa 2024 imeandikisha Wanafunzi watatu tu (3) kuingia darasa la kwanza kitu ambacho sio kawaida.

Shule hiyo ya Msingi Mlembea jumla ya idadi ya wanafunzi katika shule nzima Kuanzia chekechea hadi darasa La saba inakadirwa kuwa na wanafunzi tisini (90) tu.

Sababu kuu mbili za shule hiyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kuliko shule nyingine inatajwa kuwa ni mambo ya kishirikina yaliyotokea miaka ya nyuma ambapo wanafunzi walikuwa wanadondoka wawapo shuleni hivyo kufanya wazazi kuhamisha watoto wao na kuwaandikisha katika shule nyingine. Ndani ya Tarafa hiyo.

Sababu ya pili inatajwa na baadhi ya wadau ni masuala ya uzazi. Idadi ya Vijana wamekimbilia Mijini na idadi ya vijana waalibaki kuingia kwenye ulevi na hivyo kushindwa kujenga familia.
double kick ni noma!!!
 
Nasikia wachagga tangu wakiwa wadogo hawapendi ishi ama fanya biashara mahali penye mambo ya kishirikina sanaaa
 
Back
Top Bottom