Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Baada ya kuripotiwa Shule ya Msingi ya Mlembea inayomilikiwa na Serikali katika Tarafa ya Mashati, Halmashauri ya Rombo Mkoani Kilimanjaro kuandikisha Wanafunzi watatu pekee kwa ajili ya Mwaka wa Masomo 2024, uffanuzi umetolewa.
Awali imeelezwa kuwa baadhi ya sababu za na uhaba wa Wanafunzi ni imani za kishirikina na Vijana wengi kudaiwa kujiingiza kwenye ulevi na kushindwa kuendeleza familia na wengine kukimbilia Mjini kutafuta maisha, zaidi soma hapa - Kilimanjaro: Shule ya Msingi ya Serikali yaandikisha Wanafunzi watatu (3) kuanza Darasa la Kwanza
MAJIBU YA SERIKALI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo, Godwin Chacha ameelezea kinachoendelea kwa kusema:
Ni kweli Wanafunzi waliokuwa wameandikishwa ni Watatu na wameongezeka kufikia nane lakini matarajio ya Shule ni kuwa wanaweza kuongezeka lakini hawatazidi kumi na moja (11).
Sababu zipo kadhaa, baadhi ni Wazazi wengi kuwapeleka Watoto wao kwenye Shule za binafsi, pia maeneo ya mipakani kuna Wazazi wanapeleka Watoto wao kwenda kusoma Kenya.
Kwa kuwa tuna ujirani mwema kuna magari yanayokuja kubeba Wanafunzi wanaenda huko kusoma kisha jioni wanawarudisha.
Sababu nyingine ni kuwa ‘population’ sio kubwa sana hapa na Watu wengi wamesambaa na wanasambaa hivyo kusababisha baadhi kuwahamisha Watoto wao pia.
Kingine ni kuwa Kilimanjaro watu wamesoma sana na hivyo suala la kuzaa Watoto wengi sio jambo linalopendelewa sana kama ilivyo maeneo mengine, watu wengi wana Watoto chini ya watatu au wawili.
Hivyo, niweke wazi kuwa hakuna imani za kishirikina kama baadhi wanavyodai (kwamba siku za nyuma Wanafunzi walikuwa wakianguka wenyewe shuleni hapo), ni haki ya mzazi kuamua mtoto wake akasome anapotaka.
Hali hiyo ya uchache wa Wanafunzi hauwezi kuathiri Wanafunzi au Walimu, wakiwa wachache wanaweza kupewa elimu bora zaidi kuliko wale ambao wangekuwa wengi kwenye darasa moja, japo hatusemi kuwa tunafurahia kuwa na idadi ndogo ya Wanafunzi.
Tunakaribisha wadau ikiwemo mbalimbali ikiwemo Wanahabari waje waone mazingira na inawezekana ikachangia kuongeza uwekezaji pia.