Mr Lukwaro
JF-Expert Member
- Jun 3, 2023
- 357
- 621
π° π¨π©πππ πππ¨π§
ποΈ πππ’π¦π§π 31, 2023
FAHAMU KUHUSIANA NA TEUZI YA NAIBU WAZIRI MKUU KIKATIBA IMEKAAJE?
Reuben Paul Mboje, Mwanasheria-UVCCM KIUT
Tarehe 30/08/2023 watu wanashangazwa kuona barua kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi inayohusu uteuzi na kuhamishwa kwa mawaziri katika nafasi walizokuwa kwenda nafasi zingine tofauti.
Lakini ngoja tujikite kwenye hii nafasi ya NAIBU WAZIRI MKUU
ambayo watu wameshangaa kuona au kusikia NAIBU WAZIRI MKUU jambo ambalo wengi hawakulifahamu limekaaje kikatiba kwa maana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 haijataja cheo hicho.
Sasa, kama ulikuwa hujui na unataka kujua pitia kurasa hii. Kwa mujibu wa Ibara ya 36(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 hii inasema kwamba Rais ana mamlaka ya kuanzisha ofisi yoyote iliyopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa maana hiyo, ofisi ya Naibu Waziri Mkuu imeanzishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa sababu ana mamlaka hayo kikatiba.
Hivyo alivyoanzisha tu ofisi hiyo hawezi akaiacha ikiwa wazi bila mtendaji wa ofisi hiyo, ndipo ikabidi afanye uteuzi wa NAIBU WAZIRI MKUU ambaye ni MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO.
Maana mwenye nyumba amejenga nyumba safi na anahitaji iendelee kulindwa anahitaji nyumba yake ipate mkazi au mpangishwaji.
Ambapo uteuzi alioufanya ametumia mamlaka aliyonayo kikatiba kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 36(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayo inasema, kwa tafsiri isiyo rasmi, kwamba, Rais atakuwa na mamlaka ya kuteua watu/mtu kushika nafasi za uongozi zinazohusiana na utungaji wa sera katika idara na taasisi za serikali, na kiongozi mkuu ambaye atahusika katika usimamiaji wa utekelezaji wa majukumu katika idara hizo, na idara hizo zitajazwa na kufanyiwa kazi na wateule wa Rais.
Hivyo uteuzi huu uliofanywa na Mhe. Rais wa NAIBU WAZIRI MKUU umefanywa kikatiba na kwa kujali maslahi mapana juu ya utendaji kazi wa shughuli za serikali kwa wananchi wake.
Rais Samia alimteua aliyekuwa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu, nafasi ya Uongozi ambayo mara ya mwisho ilitumikiwa mwaka 1994 na Hayati Augustino Mrema
Pia, Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye amewahi kuwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alihudumu katika nafasi hiyo mwaka 1986 hadi 1989 chini ya Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi.
Aidha, Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi tunaendelea kumpongeza mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya teuzi katika nafasi zote kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za serikali zinafanyika kwa ufasaha na kuwajali wananchi wanyonge mpaka waliopo sehemu zisizofikika.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Makala hii imeandaliwa na REUBEN PAUL MBOJE
Mwanasheria-UVCCM
KIUT.
31/08/2023
#AlipoMamaVijanaTupo
#SisiNaMamaMleziWaWana
#CCMImaraSerikaliImara
#KulindaNaKujengaUjamaa
#KaziIendelee