Kijiji chote kimesombwa na Mafuriko, Kanisa limebaki

KISS 100

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
525
1,098
GAg8JSEWcAA3YSX.jpeg

"Kwenye madhara haya tumepata majeruhi pia wapatao 116, wanaume ni 56 na wanawake ni 60, ndugu Watanzania haya maafa ni makubwa sana, pia tumepata uharibifu mkubwa wa nyumba za kuishi, mashamba na mitambo mbalimbali ya magari, nimepata bahati ya kwenda Gendabi nyuma ya milima, kile kijiji nyumba zimeachwa upande wa kulia na kushoto eneo la katikati nyumba zote zimeondoka limebaki kanisa tu, hali sio nzuri,"

Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

===

Salamu,

Huko Hanan'g kijiji cha Ngendabi nyumba zote zimesombwa na maji ila kanisa limesimama vilevile.
Je hii ni sababu ya matereal za ujenzi au Koroho zaidi?
 
Hapo nadhani ubora wa ujenzi na mazingira. Tukitaka kujenga nadharia ya kiroho inabidi tuweze kutofautisha kwanza kati ya Kanisa na jengo la kanisa. Kanisa ni muumini/waumini, na jengo la kanisa ni mahali popote pale palipojengwa na muumini/waumini wanapoweza kukutana. Hata bar unaweza kuikodisha na kuitumia kwa shughuli za kuabudu.

Simple waumini huabudu katika majengo mbalimbali pakiwemo kumbi za starehe na burudani, shuleni, vyuoni, hospitalini, sokoni, Bar, hosteli, ofisi, na majengo kadhaa ya umma na binafsi.
 
Uko sahihi kwa uelewa wako mdogo
 
Salamu.Huko Hanan'g kijiji cha Ngendabi nyumba zote zimesombwa na maji ila kanisa limesimama vilevile.
Je hii ni sababu ya matereal za ujenzi au Koroho zaidi?
Nimesikia mahali Wazee wa Hanang wanadai Hilo janga limeletwa na hasira za mizimu kwa watu kutotambika eneo lile. Kwa muktadha wa habari hii Bila shaka ndio maana kanisa limeshindikana.
 
Uko sahihi kwa uelewa wako mdogo
Hapa kijijini nilipo, mwaka jana kuna upepo mkali ulipita usiku mmoja, ukang'oa paa la jengo la Kanisa tu, nyumba zingine zote mapaa yalibakia salama. (Miezi michache kabla ya hilo tukio, mhandisi mmoja wa hilo dhehebu alipita na kuona uduni wa namna hilo paa lilivyojengwa na kutoa angalizo kuwa, upepo mkali wowote unaweza kuling'oa hilo paa kirahisi, hivyo warekebishe mapema).

Sasa embu tuambie kiroho imekaaje?
 
Back
Top Bottom