Kijana mzalendo amvaa Paul Makonda ahoji ukimya wake mkataba wa bandari

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
604
1,410
UCHAMBUZI WA KIJANA MZALENDO NKINDIKWA DAVIDKUHUSU TATHMINI YA ZIARA YA KATIBU WA ITIKADI NAUENEZI WA CCM TAIFA, NDG. PAUL CHRISTIANMAKONDA ALIYOIFANYA KATIKA MIKOA YA KANDA YAZIWA MWEZI NOVEMBA 2023.

1. UTANGULIZI

Ndugu waandishi wa habari leo jumatatu tarehe 20/11/2023 nimewaitaili kuzungumza nanyi kuhusu tathmini ya ziara ya Katibu wa Itikadi naUenezi wa CCM, Ndugu Paul Makonda aliyoifanya katika mikoa yaKanda ya Ziwa mwezi huu wa 11 mwaka 2023.

Ni dhahiri kuwa uteuzi wake ulifurahisha watu wengi nikiwemo mimiMwenyewe Kijana Mzalendo Nkindikwa David kutokana na ukwelikuwa Makonda ni miongoni mwa viongozi jasiri, mwenye uthubutu,mkweli na asiyeogopa kusimamia kile anachokiamini. Tunakumbukaalipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye utawala waawamu ya tano chini ya Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuliambapo utendaji wake ulikuwa wa kusisimua sana na kugusa makundiya watu masikini, wasio jiweza na wasio na sauti kwenye umma. Mfano,kutetea machinga, bodaboda, mama lishe, wajane na yatima, watuwaliodhulumiwa Ardhi zao, kuleta meli ya matibabu bure kwa wananchiwa Dar es Salaam.

Pia alithubutu kutaja hadharani majina ya watu wanaojihusisha nabiashara haramu za Madawa ya Kulevya na wakaanza kuripoti Kituokikuu cha Polisi Central kwa uchunguzi zaidi, alienda mbali zaidi nakutaja mtandao mzima wa wauzaji wa madawa ya kulevya ukiwahusishabaadhi ya watu mashuhuri kwenye jamii wakiwemo wafanyabiashara naViongozi wakubwa wa kisiasa, wasanii nk. Jambo ambalo Viongozi wengi wanaliogopa kushughulika nalo kwa kuhofia maisha yao nawengine kuligeuza suala hilo kitega uchumi.

2. HOJA ZINAZOGUSA HISIA ZA WATANZANIAKUTOSIKIKA KWENYE ZIARA YAKE

Baada ya uteuzi wa Paulo Makonda nilitegemea atashughulika nakuyasemea matatizo makubwa yanayowakabili wananchi kwa sasaambapo sehemu kubwa ya Viongozi wanapofika kwenye ziara zao mikoani wanatumia muda mwingi kumsifia Rais, Viongozi wa Chama na Serikali wanamsifia rais, wabunge wanamsifia rais huku matatatizo makubwa ya wananchi yakikosa nafasi ya kujadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi.

Chakushangaza Ndugu Paul Makonda ametumbukia kwenyemkumbo huo huo wa kuacha matatizo makubwa yanayowasibuwananchi na kukimbilia vitu vidogo vidogo vya mwananchi amenyimwachumvi jirani yake.Yapo mambo mengi makubwa kuhusu ugumu wa maisha na Usimamiziwa fedha na mali za umma ambapo watanzania wengi tuliyatarajiaataueleza umma ukweli na namna mambo hayo yanavyoshughulikiwa ndani ya Chama cha Mapinduzi na ndani ya Serikali kwa ujumla wake.

(i) Mkataba wa Bandari

Hili suala la mkataba wa bandari limepigiwa kelele na wananchi na watalaamu mbalimbali wa Sheria, Viongozi wakubwa wa Serikali wastaafu, Viongozi wa Dini, Wanaharakati mbalimbali wa kutetearasilimali za taifa wakipinga vipengele vya Mkataba wa IGA uliowezesha kusainiwa Mikataba ya utekelezaji wa Uendeshaji wa Bandari ya Dar es Saalaam.

Kuhusu Mkataba wa Bandari tunasikia tu mara tunaambiwa ni mkatabawa miaka 30, mara tunaenda kugawana mapato asilimia 60 kwa asilimia340 anapewa DP World lakini hatuambiwi huyu mwekezaji DP World anawekeza shilingi ngapi na anawekeza kwenye nini hadi apewe hiyohaki ya kuchukua asilimia 40 ya mapato yetu. Mkataba umeshasainiwana Bahati nzuri siku Mikataba hii inasainiwa ndiyo siku hiyo ameteuliwa Makonda kuwa Mwenezi maana yake analifahamu vizuri suala hili nini kinamchomfanya Makonda apatwe na kigugumizi cha kueleza ukweli wa jambo hili.

Lakini tumeshuhudia jambo kubwa kama hili tutosikika katika ziara yaMakonda mikoa ya Kanda ya Ziwa huku watanzania wote wakilia kuwabandari zao zimeuzwa kwa Mwarabu. Lakini nimkumbushe Makonda kuwa wakati Mheshimiwa Magufuli anatoa hotuba za kukataa Mikatabaya kitapeli kama hii ya bandari alikuwepo pale Ikulu ya Magogoni mwaka 2019 akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na alipiga makofi kuunga mkono msimamo huo wa Mh Magufuli. Nini kilimchofanya Makonda kushikwa na kigugumizi kuzungumzia suala hili kubwa?

(ii) Ufisadi ripoti ya CAG

Nimesoma na kupitia ripoti ya CAG, nimesikiliza taarifa za Kamati zaKudumu za Bunge za PAC na LAAC na michango ya wabunge kwakweli nikiri kuwa baadhi ya wabunge walijitahidi kuzungumza kwa sauti kubwa wakimaanisha kuwa wameumizwa na ufisadi mkubwa katikaripoti ya CAG na wengine walienda mbali zaidi na kupendekeza Barazala mawaziri livunje (Mheshimiwa Philipo Mulugo Mbunge wa Songwe-CCM), wengine wakisema mafisadi wanyongwe na wakaanza kukusanya sahihi za wabunge hadi kufikia 200 wanaounga mkono kutungwa sheria ya kunyongwa mafisadi (Mheshimiwa NikodemusMaganga Mbunge wa Mbogwe na Mheshimiwa Mwita WaitaraMbunge wa Tarime Vijijini wote CCM) , lakini wengine waliwataja kwa majina baadhi ya mawaziri, wakuu wa mashirika ya umma waliohusika na wizi na ufisadi wa fedha za umma wakamatwe na4washitakiwe kwa makosa ya uhujumu uchumi(Mheshimiwa Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa-CCM).

Wengine wakionyesha kuwa katikataarifa ya CAG kuna upigaji wa zaidi ya Trilioni 30 ambapo pia Dk.Mwigulu Nchemba, Profesa Makame Mbarawa, Januari Makamba, Masanja Kungu Kadogosa, Emmanuel Tutuba, Maharage Chandewalitajwa kuhusika na ufisadi wa kutisha.Nilitegemea Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndugu Paulo Makonda,angekemea rushwa na ufisadi unaondelea nchini na angeeleza hatuazilizochukuliwa dhidi ya mafisadi hao kwani ninavyofahamu mimitangu ripoti ya CAG itolewe Machi 2023 hakuna hatua yoyoteiliyochukuliwa na Chama wala Serikali.

Pamoja na agizo Chama cha Mapinduzi kupitia kikao chake cha Kamati Kuu cha Aprili 2023 kiliagiza watuhumiwa wote wa ufisadi waliotajwa na CAG wachukuliwe hatua lakini hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa pamoja na kwamba baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi huo ni Wajumbe wa HalmashauriKuu ya CCM Taifa (Wa-NEC).Cha kushangaza jambo kubwa kama hili ambapo fedha nyingi za watanzania masikini zimeliwa na wahusika wapo bado kwenye ofisi zaSerikali, huku watanzania wakitaabika wengine wakikosa hata hela za matitabu na wengine kukosa hela za kukomboa maiti za ndugu zao mahospitalini, nini kilichomfanya Mwenezi Makonda aliyejipambanua kwamba yeye ni kiboko cha mafisadi kutolizungumzia suala hili katika ziara yake yote ya Kanda ya Ziwa.

(iii) Kukatika kwa umeme

Tumeshuhudia migao ya umeme isiyoisha baada tu ya Mheshimiwa John Magufuli kufariki dunia na alipotumbuliwa nafasi ya Waziri wa Nishati Mheshimiwa Medardi Matogolo Kalemani mwishoni mwa mwaka 2021 hadi leo mwaka 2023 watanzania wanalia makali ya mgao wa umeme uliosababisha kuharibu kabisa uchumi wa wananchi hasa wale wa chini wanaoishi kwa kutegemea umeme mfano wauza barafu,wauza juice, watu wa saluni za kike na za kiume, stationary,wachomeleaji, wafyatuaji matofali, wauza samaki na wauza nyama nk. Kuadimika na kupanda kwa bei za bidhaa za chakula na vifaa vya ujenzi kutokana na viwanda kushindwa kuzalisha, viwanda kufungwa na ajira kupotea, kupoteza maisha mahospitalini na kwa ujumla shughuli zauzalishaji mali kusimama na kupoteza wawekezaji nchini.

Malalamiko haya ya mgao wa umeme ni ya muda mrefu na hatawabunge wetu wamekuwa wakiyasema ndani ya Bunge kwamba mgaohuu wa umeme ni wa kutengeneza, lakini hata Mzee wetu Mstaafu Spika Mheshimiwa Job Ndugai hapa majuzi tu amenukuliwa na vyombo vyahabari akiilalamikia TANESCO kwamba inarudisha nyuma maendeleoya wananchi. Sasa ukiona hadi wazee kama Ndugai ambao walikuwawameamua kunyaza wanajitokeza hadharani kupaza sauti kulalamikia uhuni huu ujue hali ni mbaya kiasi gani.

Lakini pia tumemsikia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dotto Mashaka Biteko akieleza kuwa asilimia 65 ya umeme unaotumikanchini unatokana na gesi kutoka Mtwara lakini alipofika kwenye visimavya gesi alikuta kuna mashine imeharibika miaka miwili bilakutengenezwa.

Pia bomba limeharibika bila matengenezo na bila sababuza msingi. Je kama hizi sio hujuma kwa taifa ni nini? wanayoyafanya haya wapo nawako kazini badala ya kuwa jela kwa makosa ya uhujumu uchumiLakini hatujasahau kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Januari Makamba alisema Bungeni Februari 2023 kuwa tatizo la kukatika umeme halitakwisha hadi ipatikane shilingi Trilioni 1. Kwa ajili ya mradi wake wa gridi imara. Pamoja na wananchi kulalamika kwa muda mrefu juu ya mgao waumeme lakini hakuna majibu yoyote yanayotolewa na serikali kuhusutatizo hili. Tulitegemea Msemaji wa Chama Ndugu Makonda angetoakauli thabiti juu ya uhuni huu wanaofanyiwa watanzania.

(iv) Uhaba na Kupanda kwa bei ya mafuta

Tumeshuhudia mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti wananchi wakipanga foleni ndefu kwenye vituo vya mafuta kutokana na uhaba wa mafuta nakupanda kwa gharama ya mafuta ambapo tumewasikia wabunge kadhaa wakilalamika kuchezewa kwa tenda ya mafuta akiwemo Mheshimiwa Hamisi Tabasamu, Mbunge wa Sengerema ambapo kwa bahati mbayaSpika wa Bunge alimzuia asizungumzie suala hilo kwa madai kwambani jambo zito ambapo madhara yake ndio tunayaona leo. Mafuta yamepanda mara dufu kutoka shilingi 2,400 kwa lita hadi kufikia 3,500ya sasa, Nauli zimepanda na kusababisha wananchi kushindwa kumudugharama za maisha.

Jambo kama hili, Mheshimiwa Mwenezi Makonda alipofika Sengerema alipaswa ampe nafasi Mheshimiwa Tabasamu aeleze kinagaubaga nini kilichojificha katika suala zima la kupanda kwa bei za mafuta ili mwenezi aweze kupiga simu kwa Spika wa Bunge kumhoji kwanini alimzuia Mbunge huyo asieleze ukweli wa jambo hili, na angewezakutoa Maelekezo mafuta yashuke bei ili kuwapunguzia mzigo mkubwa wananchi.

(v) Manyanyaso dhidi ya wafugaji

Tumeshuhudia Malalamiko ya wafugaji kuporwa mifugo yao nakuachwa masikini kabisa, mifugo inakamatwa na kuuzwa kiholela tenakwa bei ya kutupwa ya wastani wa shilingi 100,000 kwa ng’ombe beiambayo ni ndogo kuliko hata bei ya mbuzi au kondoo, hata wananchiwalioshinda kesi mahakamani mifugo yao haijarejeshwa na serikali mpaka leo. Familia nyingi zimefilisiwa na kuachwa na ufukara wakutupwa, mifugo mingi inakufa kwa kukosa malisho, maji, dawa nachanjo ikiwa imeshikiliwa kwenye hifadhi. Lakini mbaya zaidioperesheni hizi kwa sehemu kubwa zinaenda kinyume cha sheria na nikwa maslahi binafsi.

Ipo mifano ya hivi karibuni ya Oktoba naNovemba mwaka 2023 ambapo unyanyasaji wa wafugaji na mifugo yaokatika wilaya za Ngorongoro, Bunda na Meatu na maeneo mbalimbalinchini. Licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa agizo Bungeni lakupiga marufuku ukamataji holela wa mifugo na utozwaji wa fainikinyume cha sheria.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa alitoa tamko Bungeni kupigamarufuku ukamataji holela wa mifugo na utozwaji wa faini kinyume chasheria agizo ambalo watumishi wa TAWA, TFS, TANAPA na NCAA waliyadharau na kukaidi agizo lake na kuendelea na operesheni hizo haliiliyopelekea wabunge kulalamika Bungeni na mheshimiwa Spika akatoamwongozo kwa kukiri kuwa maagizo ya Waziri mkuu yalipuuzwa nawasaidizi wake na kupelekea operesheni za dhuluma na kinyume chasheria kuendelea. Hata baada ya mwongozo huo wa Mheshimiwa Spika operesheni hizo zinaendelea hadi sasa huku wananchi wakiendeleakuumizwa na kufilisika.

Kwa muktadha huu, ni dhahiri kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa amekosa sifa za kushika wadhifa huo na kamaameshindwa kujiengua yeye Mwenyewe basi ninawaomba waheshimiwawabunge wamuondoe kwa mujibu wa Katiba kwa kuwa ameshindwakumudu majukumu ya Uwaziri Mkuu.

Upande wa Ndugu Makonda, Katika matukio haya wananchi wa Kandaya Ziwa ndiyo waathirika wakubwa wa matukio haya lakini Katibu wetuwa siasa na uenezi, Paulo Makonda alitumia muda mwingi kuzungumziamatatizo madogo madogo ya mtu mmoja mmoja badala ya kushughulikana matatizo makubwa yanayoihusu jamii nzima. Tulitegemea angetoa8tamko la Chama dhidi ya dhuluma wanazofanyiwa wafugaji na Serikaliya CCM.

(vi) Kuhujumiwa kwa zao la Pamba

Zao la Pamba ndio dhahabu nyeupe kwa wananchi wa mikoa ya Kandaya Ziwa lakini cha kushangaza baada ya Magufuli kuingia kaburini zaola pamba limeanguka bei kutoka wastani wa shilingi 2,200 kwa kilo hadikufikia wastani wa shilingi 1,000 kwa kilo, hii inapelekea kuwa nawasiwasi mkubwa zao hili linahujumiwa kwa makusudi na baadhi yaviongozi ambao ni wanunuzi wa zao la pamba, kwa mfano mzee wanguGachuma ambaye ni Mjumbe wa NEC, Mnunuzi mkubwa wa Pamba nandiye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba unaweza ukaona mkulimaatatetewa na nani. Haya ndio maswala mheshimiwa Makonda alitakiwakuyasemea na kuweka msimamo thabiti wa kuwabana wotewanaowahujumu Wakulima masikini.

Lakini Makonda ameshindwaje kuzungumia hujuma wanayofanyiwaWakulima ya kuuziwa dawa za kuua wadudu bandia ambazo ukipulizakwenye pamba badala ya wadudu kufa ndio wananepa na kuendeleakushambulia pamba na kusababisha mavuno kidogo na mkulima kupatahasara kubwa.Haya tulitegemea yakemewe na kupigwa marufuku na kiongozi huyu waChama.

(vii) Uvuvi haramu

Tunafahamu kuwa Kanda ya Ziwa imezungukwa na Ziwa Victoria namoja ya shughuli kubwa ya uchumi wa kanda ya ziwa ni mazao ya uvuviambayo ni samaki sangara, sato, kamongo, dagaa, mabondo nk ambaposhughuli za uvuvi zilikuwa zinaajiri watu takribani milioni 6. Lakinibaada tu ya Mheshimiwa Magufuli kufariki, shughuli za uvuvi zikaanza9kudorora kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu na Matumizi yazana haramu hali iliyosababisha samaki kuadimika na kuvurugamnyonyoro mzima wa uchumi utokanao na mambo ya uvuvi, mfanomdogo umetolewa hivi majuzi Bungeni na Mbunge wa Musoma Mjini, Mheshimiwa Mathayo Manyinyi ambapo alisema viwanda takribanivitano vimekufa kutokana na kukosa malighafi ya samaki.

Kundi dogo la wahalifu (Wavuvi haramu) limeachwa limalize samaki wote baharinina katika maziwa yetu kinyume cha sheria ya uvuvi na sheria za ulinziwa rasilimali. Suala hili nilitegemea mwenezi Makonda alizungumziekwa upana na kutoa Maelekezo mahususi kwani shughuli za uvuvi nishughuli zinazotegemewa Kiuchumi na chakula na watu wengi hukuajira zikipotea.

(viii) Watu kufukuzwa kwenye maeneo yao ya asili Mbaralina Ngorongoro na Mwanduhubanhu Uvinza Kigoma

Suala la wananchi kufukuzwa kwenye maeneo yao limeota mizizi natumeshuhudia wananchi wa Mbarali, Ngorongoro, MwanduhubanhuUvinza Kigoma, Kaliua Tabora na maeneo mengine wakifukuzwakwenye maeneo yao kama vile sio raia halali wa nchi hii wakatitunakumbuka, kuna kamati ya mawaziri 8 iliundwa na MheshimiwaMagufuli na ilizunguka nchi nzima na kuja na mapendekezo ya vijiji 920 vilivyokuwa kwenye maeneo ya hifadhi zilizopoteza sifa wananchi wakewaendelee kuishi na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi, miakamiwili baadaye wananchi wale wanaanza kuondolewa.

Mbaya zaidi mfano suala la mbarali tulimsikia Makamu Mwenyekiti waCCM, Mzee wetu Mheshimiwa Kinana alipofika kwenye kampenimbarali aliwaambia wananchi kuwa hawataondolewa na Tayari Mheshimiwa Rais ameruhusu waendelee na shughuli zao, lakini baadaya uchaguzi kupita Tayari waanza kufukuzwa hadi tumeona Mbunge wa Mbarali Mheshimiwa Bahati Ndingo ikamlazimu kumuandikia barua10mheshimiwa Rais kuomba kuonana naye ili kuzungumzia hatma yawananchi wa Mbarali, lakini tumeona Mbunge wa Ngorongoro, Mheshimiwa Ole Shangai akikamatwa na kufikishwa polisi kwenyeharakati za kuwatetea wananchi wa ngorongoro bila msaada wowotekutoka ngazi yoyote serikalini wala chama. Nilitegemea maonevu haya Makonda alipaswa atoe neno na kutoamaagizo ili wananchi hawa waishi kwa amani kwenye nchi yao pendwaya Tanzania.

(ix) Kusuasua kukamilika kwa miradi mkubwa ya kimkakati

Tumeona namna miradi mikubwa ya kimkakati ya SGR ikishindwakukamilika na ni kama vile miradi hii imesimama hakunakinachoendelea, mfano kipande cha Dar es Salaam-Morogoro ambacholeo ni miaka karibia 6 mradi uko asilimia 98 haujakamilika nahaujulikani utakamilika lini. Kipande cha Morogoro- Makutupora nachoujenzi unasuasua uko 95 miaka 6 sasa haijulikani utaisha lini, kipandecha Makutupora- Tabora uko asilimia 12 na kipande cha Tabora-Isakakiko asilimia 5 na Tabora-Kigoma asilimia 0.3 takribani miaka 3 sasatangu Mikataba hiyo isainiwe na haijulikani utaisha lini na kipande chaMwanza-Isaka ujenzi uko asilimia 41 takribani miaka 4 sasa nahaijulikani mradi huu utaisha lini.Kusuasua miradi ya kimkakati kama vile SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, miradi ya umeme vijijini kutazuia ulaji wa baadhi ya watu wanaonufaika na kuchelewa kwa miradi hii huku taifa lilipata hasara kubwa. Nini kimemfanya Makonda ashindwe kuhoji sababu za kusuasua kwa miradi hiyo mikubwa ya kimkakati?

3. HITIMISHO

Pamoja na kazi nzuri aliyoifanya Makonda ya kusikiliza kero zawananchi mmoja mmoja na kujaribu kutafuta ufumbuzi, kitendo chayeye kunyamazia matatizo makubwa ya kitaifa kama ugumu wa maishana kupanda kwa bei za bidhaa, ubadhirifu wa fedha za umma kwamujibu wa ripoti ya CAG, wananchi kuporwa Ardhi na mifugo yao naSerikali, Mikataba Mibovu kama mkataba wa bandari, kusuasua miradiya kimkakati, tatizo la umeme, uhaba na kupanda kwa bei ya mafuta,ukosefu wa dola, utoaji duni wa huduma za afya nk kinamuondolea uhalali wa kuwa kiongozi makini na kwamba hana nia njema kama alivyojinasibu baada ya kuteuliwa.

Ndugu Paul Christian Makonda usipoyafanya kwa vitendo maapizo yako, machozi na maneno uliyoyatoa kwenye kaburi la Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli na maapizo uliyoapizwa na wazee wakimila wa Kanda ya Ziwa ya kutaka ukasimamie haki, kukomesha dhuluma kwa watu masikini, yatageuka kuwa laana kwako na anguko lako kubwa la kisiasa.

Mungu ibariki Tanzania,Asanteni sana kwa kunisikilizaNi Mimi Kijana Mzalendo, Nkindikwa David Levi
0685 446 343

View: https://www.youtube.com/live/RxCxNc1IL_E?si=x594vbtroW2U7NM4
 
Attachments

  • MAKONDA MZALENDO(1) (1).pdf
    505 KB · Views: 4
Sioni makonda wa kukujibu zaidi ya Dp world kushusha mawinchi yao ya kubebea vitu vizito hayo ndio majibu ya chama na serikali!
 
Sijasoma mpaka mwisho ila nimemuelewa. Labda kwa kumsaidia huyo bwana ajaribu kupitia clips zote za Makonda, je kuna mahali popote ilipotolewa nafasi ya kuuliza maswali kuna raia yeyote aliyeuliza suala la bandari?
Kama hakuna maana watu wengi wa chini wanayotaka kusikia ni yale yaliyowasilishwa na Makonda.

Sisi tuendelee tu na bandari.
 
Wewe ni kijana zaidi ya Paul Makonda mbona unaonekana umemzidi umri?

Jibu ni kwamba hayo uliyoyaanisha hakutumwa na Chama chake kuyasemea.

Labada kama unataka Chama chake iyachukue kisha wampe mwenezi majibu akayaseme kwenye umma vinginevyo hutamsikia akiyataja. Mjumbe hauwawi
 
SHOOOO YA MTANZANIA HII
 
Attachments

  • Capture.JPG
    Capture.JPG
    41 KB · Views: 3
Makonda hajawahi kuwa serious zaidi ya kujikomba kupitia projects zisizoisha
 
Back
Top Bottom