Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,302
9,729
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda ametoa maagizo ya chama kwa waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Pangani Haraka sana.

Hii ni baada ya kukutana na kero nyingi sana katika halmashauri hiyo zilizotolewa na wananchi pamoja na Wafanyabiashara mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa huduma kwa halmashauri lakini hawalipwi pesa zao ,na wanapodai haki zao za kulipwa madai yao wamekuwa wakipewa majibu yasiyoridhisha huku mkurugenzi akijifanya Mungu mtu.

Mheshimiwa Makonda pia ametoa maagizo kwa Mh waziri kuhakikisha kuwa anaunda timu na kuipeleka Pangani kwenda kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali ambayo yamekuwa ni kero na kulalamikiwa na wananchi . Pia amezungumzia suala la kukwama kwa miradi ya serikali na masuala mengine mengi sana yanayochochea chuki ya wananchi kwa serikali yao.

Katika hatua nyingine Ametoa pia kauli nzito sana iliyotetemesha na kuibua shangwe kwa wananchi baada ya kuagiza wakurugenzi wote nchini kushugulikia kero za wananchi ,na kwamba mahali ambapo itaonekana mkurugenzi ameshindwa kutatua kero basi chama hakitasita kutoa maagizo kwa serikali ya kusimamishwa kazi kwa mhusika. Lakini pia amewaagiza wenyeviti wote wa CCM nchini wilaya na mikoa kutoa taarifa juu ya wakuu wa mikoa,wilaya ,wakurugenzi na watendaji wengine wa serikali wanaoshindwa kufanya kazi na kutimiza majukumu yao vizuri ili wachukuliwe hatua.

Ndugu zangu Watanzania kupitia jukwaa hili niliwatahadhalisha sana na kuwasihi sana viongozi wote wa serikali mikoani na wilayani kuwa waanze kufanya kazi na kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao.niliwaambia ya kuwa ziara za Mheshimiwa Makonda zitakuwa za moto sana tena sana na zitasomba wengi sana hasa wale wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea na kujifanya miungu watu hawatasalimika wala kuachwa salama katika ziara za Mheshimiwa Makonda. Kwa sababu kila mtu anafahamu ya kuwa Mheshimiwa Makonda hanaga huruma wala subira wala uvumilivu kwa wazembe kazini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Taarifa mpya ya hivi punde.

Ni kuwa Tayari muda huu mkurugenzi amesimamishwa kazi na waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kama alivyoelekezwa na kuagizwa na chama. Amesimamishwa ili kupisha uchunguzi.
View attachment 2878884
 
na hiyo?
IMG-20240121-WA0053.jpg
 
Makonda anampa amri Waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Chama ndicho kinampa maagizo waziri. Kumbuka na elewa ya kuwa CCM Ndio iliyounda serikali na siyo serikali iliyounda CCM. Ni CCM ndiyo itakayo kwenda kwa wananchi kuomba kura kwa hiyo ni lazima CCM iwakatae na kuwawajibisha kupitia serikali yake watendaji na viongozi wote wanaoonekana kuwa vikwazo katika kuwahudumia wananchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
 
Rubbish, Makonda amekuwa Waziri Mkuu? hizi nafasi yafaa ziwe zinatangazwa watu waombe, pia kama Wilaya kuna DC/DAS/DED inatakiwa wote waondoke wameshindwa kuleta maendeleo.
Huu Ujinga wa kua Kiongozi alafu unasubiri Kiongozi fulan ndo afanye maamuzi, ndo umekua kikwazo kikubwa sana hapa Nchini.


Tena sio tu Makonda.... Inamaana hiyo halmashauri Haina Mwenyekiti? Mkuu wa Wilaya ? Mkuu wa mkoa??.


Ujinga mtupu
 
Makonda anampa amri Waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki chama cha Mapinduzi kime laanika.
Wana wa Israel walipo acha kumtii Mussa na Harun, Mungu aliwa piga laana.
Kila mmoja aka anza kuongea lugha yake.
Fundi akiagiza mwiko ana oewa fito, akiagiza fiti ana pewa mchanga.
Maana walipoteana lugha.
Katibu mkuu ana ssma hiki, katibu mwenezi ana sema hiki.
Lugha gongana.
 
Back
Top Bottom