Paul Makonda asimikwa kuwa Chifu Nsumbantale, yaani Msaidizi wa Chifu Mkuu Hangaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa machifu mkoa wa Shinyanga Kidola njange amesema ya kuwa umoja wa machifu na watemi mkoa wa Shinyanga kwa pamoja na umoja wao wamekubaliana kumsimika katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda kuwa Chifu Nsumbantale,yenye maana ya Msaidizi wa Chifu mkuu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa. Ambapo sasa baada ya usimikwaji huo atakuwa msaidizi wake katika masuala ya siasa.

Ambapo katika usimikwaji huo Mheshimiwa Makonda amevishwa shuka jeusi lenye maana au lenye kuashiria wingu zito la mvua ambalo ni neema kwa watu ,kwa kuwa linashusha mvua ambapo mvua siku zote ni baraka na neema,kwa kuwa ni katika mvua tupatapo mazao ya aina mbalimbali ikiwepo ya chakula na biashara.

Mheshimiwa Makonda alivishwa pia shuka jekundu lenye maana au kuashiria utayari wa kulinda chama na serikali ya chama cha Mapinduzi.

Lakini pia Mheshimiwa Makonda alikabidhiwa mkuki wenye maana ya kumkumbusha juu ya ulinzi wa chama na serikali ya chama cha Mapinduzi

Pia alivalishwa mkufu wenye kuashiria kuwa watu wa Shinyanga wapo pamoja naye wakati wote na yeye ndiye anayetegemewa sana.

Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Paul Makonda ukienda kule Shinyanga anatambulika na kufahamika kama Chifu Nsumbantale yaani msaidizi wa chifu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa.

Bila shaka hii yote ni kutokana na kuguswa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda nakuona namna anavyofanya kazi kubwa ya kumsemea Rais Samia na mwenyekiti wa CCM Taifa kila anakopita na kukanyaga lazima alitajwa jina la Rais Samia kwa heshima kubwa sana na kueleza mambo makubwa aliyoyafanya katika kila sehemu.

Kwa hakika Paul Makonda siyo mtu wa kawaida ndugu zangu. Ni mtu mwenye ushawishi na nguvu kubwa sana isiyopimika . Angalieni anakopita huko namna wananchi wanavyofurika na kumiminika kama mafuriko ya maji.anavuta maelfu ya watu kama sumaku ikutanapo na chuma. Kwa hakika Rais Samia alicheza karata ya karne kwa kumleta Paul Makonda wakati huu.angalia namna anavyompigania na kumsemea kwa nguvu zote kwote apitapo huko mikoani.

Mungu aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kupambana kuhakikisha kuwa anawafikia wananchi wengi sana na kuwasikiliza kero zao ili kuziwasilisha kwa viongozi wa serikali kwa utatuzi zaidi.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
phd washazibaka wamekimbilia kwenye uchifu sasa.bado kusimikwa uganga na uwanajeshi
Fanya kazi na chapa kazi kwa bidii uguse maisha ya watu na kuleta matumaini, tabasamu na furaha kwa wengi uone kama jamii haita kuunga mkono na kukupatia heshima kama apewayo Mheshimiwa Makonda kila apitako.
 
Raha ya hawa wasimika machifu wa mchongo, kesho Katibu mkuu wa CCM akifika hilo eneo na yeye atasimikwa kuwa Chifu nsumbantale pia. Au hata Mnyika akifika hapo na yeye atasimikwa kuwa Chifu nsumbantale.

Ni kama vile taifa la watu waliochanganyikiwa.
Mwambie basi Mnyika naye aende huko akasimikwe.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa machifu mkoa wa Shinyanga Kidola njange amesema ya kuwa umoja wa machifu na watemi mkoa wa Shinyanga kwa pamoja na umoja wao wamekubaliana kumsimika katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa

0742-676627.
 

Attachments

  • 5613740-24d2613f26c985434fdda7e186b6728f.mp4
    10.2 MB
Makonda atabaki kuwa kiongozi pekee nchini aliyepigwa marufuku kukanyaga ndani ya ardhi ya nchi nyingine kwa kosa la kukatisha uhai wa wananchi wake,kwa hiyo makonda atabaki kuwa ni muuaji until his innocence proved.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom