Mwita25
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 3,831
- 1,173

Mkuu unatakiwa kuwa makini sana katika kuleta mada. Unapoanza kutoa shutuma kwa CDM inaonesha kuwa busara imekuwa pembeni. Hebu jiulize maswali yafuatayo

Je mtu akikwambia kuwa uliwaona waliomwagia kuwa ni CDM utamjibu ndiyo?,

Kama uliwaona unathibitisha vipi kuwa ni CDM?(i.e Umewakuta na kadi za CDM mifukoni?)

Je mtu mwingine akisema kuwa Kijana huyu alikuwa wa CDM anabandua matangazo ya CCM na vijana wa CCM wakamteka na kumwagia tindikali usoni na kumwambia aseme ni CDM ili apatiwe matibabu nje ya nchi na CCM vinginevyo watamwacha apofuke utakataa?

Kama hukuwepo, ni kigezo gani kimekufanya uwashambulie CDM kiasi hicho?

Je Mtu akisema kuwa kundi la CCM limemtoa kafara huyu kijana kwa kumwagia tindikali ili wahusishe tukio na CDM ili polisi wapate sababu za kuwakandamiza wafuasi wa CDM wasifanye siasa na hata kuwakamata wasipige kura tutakuwa tumekosea?

Katika post yako maneno pekee niliyaona yanabusara ni RED BOLDED kuwa kitendo hiki si kizuri hasa ukizingatia kuwa anapiganiwa mtu mmoja tu akasinzie bungeni na kupata posho. Je macho ya huyu kijana yanaweza kurudishwa?. Tuache ushabiki wa siasa, huwezi kuja na post biased kama hii halafu unusurike. Inaonesha wazi kuwa something is wrong. Hata maswa CCM walikimbilia conclusion kuwa Shibuda kaua na mkamuweka ndani bila sababu. Katika uchaguzi huu kila mtu anakuwa responsible kama yeye. Endapo tutasikia kauli ya viongozi wa CDM kuwataka vijana wanaowaunga mkono kuwamwagia tindikali wasiowaunga mkono hapo tutasema kuwa CDM inachochea fujo kama chama. Huu ni uzandiki mkubwa sana kuhusisha wahuni wachache na chama kinaochoonekana ni tishio. Sababu kama hizi ndizo zinatufanye sisi wengine tusio na chama kuzidi kuichukia CCM na kuomba siku moja chama chochote mbadala kishike nchi

Sheria za JF hazikatazi