Kijana amwagiwa Tindikali Igunga

Kijana amwagiwa Tindikali Igunga

haaaaa wamemtia huyu kijana kilema cha maisha
3.jpg
 
[h=2]Mwanachama CCM amwagiwa tindikali[/h]

Na Sharon Sauwa

11th September 2011

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

acidIgunga.jpg

Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha baada ya kumwagiwa tindikali.

Mchuano wa vyama vya siasa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani Tabora, umeingia doa baada ya kijana mmoja mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha (24), kuunguzwa usoni kwa kemikali aina ya tindikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Jeshi la Polisi, Isaya Mungulu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akielezea alisema tukio hilo limetokea saa 5:00 usiku Barabara ya Singida ambapo alipigwa na watu zaidi ya watano kabla ya kumwagiwa tindikali.
Alisema mara baada ya polisi kupata taarifa hiyo, walianza kufuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa. Kuhusu tukio hilo kuhusishwa na mambo ya kisiasa, Mungulu alisema bado haijajulikana kama ni la kisiasa ama la.
Alisema bado wanaendelea na upelelezi zaidi, ili kubaini chanzo chake.
Hata hivyo, Mungulu hakumtaja mtuhumiwa huyo kwa kile alichoeleza uchunguzi unaendelea.
Kijana wa Green Guard, aliyemuokoa majeruhi huyo, Farahani Farahani, alidai kuwa alikutana na majeruhi huyo karibu na shule inayojulikana kama Jitegemee na kwamba wakati anarudi alikutana na wanaume wawili na majeruhi huyo akiwa katikati.

"Nikasema kwamba Katibu alinipigia simu kuwa kuna kijana anatafutwa ametekwa na watu wa Chadema , nikasema ngoja nirudi kama kutekwa na mimi nitekwe kwa sababu tayari nilishapata taarifa kuwa kuna kijana anatafutwa basi nageuza wale vijana wakanisimamisha samahani bwana huyu kijana hebu mpeleke kituo cha polisi," alidai.
Alidai alipomchukua na kumfikisha katika ofisi za wilaya za CCM hatimaye polisi wakamchukua kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga. Akizungumzia tukio hilo juzi usiku, Katibu wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Mwigulu Nchemba, alisema Chadema wameainisha katika mpango wao kuwa watatumia nguvu kushinikiza kupata ushindi katika uchaguzi wa jimbo la Igunga.
"Ukizingatia kuwa ndio tu wametoka kuzindua inaelekea haya ndiyo maelezo yao ili kuweza kuwatishia wananchi sasa hiki si kitendo cha uungwana niseme waliofanya hiki kitendo na wote waliowatuma wote ni wanyama kabisa na niseme hata shetani sidhani kwamba anaweza akafanya kitendo hiki,"alisema.
Naye Mganga wa zamu, Godfrey Cyril, alisema majeruhi huyo anasadikiwa kujeruhiwa kwa kuunguzwa kwa kemikali aina ya tindikali.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Joseph Kisara, alisema majeruhi huyo alihamishiwa jana mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. Aliondoka na ndege jana saa 7:00 kwenda katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga (Chadema), Waitara Mwikabe, amesema hawajui lolote kuhusiana na tukio hilo. Alisema hakuna mwanachama wa Chadema ambaye anaweza kufanya tukio kama hilo.
"Siku zote hiyo ni biashara ya CCM, wanafanya matukio ili kutengeneza propaganda, "alisema na kuongeza kuwa wanachama wote wa chama hicho wanafanya kazi walizopangiwa.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Jamani hii ni mbaya sana sana. Jiulize ikikutokea wewe?? au ndugu yako? Chama gani kinakuwa na ufidhuli na unyama wa jinsi hii? Nimewachukia sana sana
 
Mmmm! je waliomwaga tindikali walivalia gwanda la cdm? Kumbuka kuna vyama 8 vinagombea Igunga pia kuna wagombea binafsi---------!
 
jana kuliripotiwa katika vyombo vya habari na hata huku jf kuwa chaema wamemwagia kijana wa ccm titindikali hapa igunga,leo katika hali ya kuhuzunisha kijana mwengine tena wa kike amepigwa na mawe baada ya kumkataa mmoja wa vijana wa chadema katika kijiji cha itumba,tarafa ya igunga wilayani hapa,

kwa maelezo ya binti huyu maria solomon,jana alifuatwa na afisa huyu akaombwa penzi,akakubali lakini baada ya jamaa ruzuku yake kuwa ndogo binti akaamua kuchomoa,lakini akawa tayari kishalamba soda mbili aina ya fanta ya kada wa cdm,mshakaji akalalishwa mlango wazi na binti astokee,sasa leo katika pitapita si kamuona?? mawe yakaanza!
 
Usifikiri kwa uwezo wa chupi wa kuhifadhi nyeti,fikiri kwa uwezo zaidi ya hapo.
 
Kumbe wachaga nao ni wanachama wa CCM? Tangu lini? nakumbuka Nape Nauye aliwahi kusema kuwa CDM ni chama cha Wachaga,iweje leo Tesha amwagiwe Tindikali na Wanachadema?.Democrasia ina garama.
 
nasikitika sana watu wanaoleta siasa wakati jamaa kaumia sana,wakat anamwagiwa mm nilikuwepo kwenye gar tukimsubiria abandike zeni tusogee mbele mara wakatokea watu wakisema pipozzz ngoja tukuonyeshe nguvu ya umma wakamwagia tukafikir ni maj mara jamaa analia sana na kumchek mtu kaungua uso na kupofoka macho,nasema wakiletwa mbele yangu wale vjana waliokuwa wakisema pipoz nawakumbuka mpaka sasa.najiuliza ccm na cdm nani anatindikali nyingi? mnatupeleka wap?haya

kama hakuna uthibisho kuwa waliomwaga tindikali ni vijana wa Cdm, kwa kuwakamata hao vijana na kuthibitisha kuwa wametumwa na cdm basi habari hii ilipaswa iwekwe vizuri.
 
Mbinu za namna hii tulishazzoea ktk muda kama huu wa uchaguz. Mnataka kusafsha matapsh yenu kwa nguo walzovaa wengne. Kkubwa n kwamba kama wewe ndo ultapka labda ukanawe kwa maj saf na sabun, la cvyo tutakugundua2.
Mbinu chaf kama hz zlshatumika na Adolf Hitler alpotaka kuwa kiongoz ujeruman. Polen na mbinu zenu dhaif.
 
kama ni kweli tunampa pole kijana, siungi mkono vurugu, pia siamini uwekaji mabango ya matangazo ni chanzo cha vurugu za hivyo, nikimkumbuka H. Kolimba machozi yanitoka. yaweza kuwa ni mchezo mchafu wa ccm kuomba huruma ya wanaigunga.

Below average thinking. Aliyemwagiwa tindikali wala hata siyo mgombea na pengine hana udugu na mgombea wa CCM. Sasa watu watato sympathy votes kwenda CCM kwa namna gani? Hili tukio ni la kinyama na kwa vyovyote vile ushahidi wa kimazingira unaonyesha hii ni kazi ya CDM. Nina hakika angefanyiwa mfuasi wa CDM basi kinara wa vurugu Lema sasa angekuwa anongoza genge la wahuni wenzie kufanya vurugu na maandamano. Hivi ni lazima mtu ushinde ubunge baada ya kutekteza maisha ya mwenzio? Hili ni tukio moja tu la uchaguzi na litapita lakini maisha ya mtu yaliyoharibiwa yatamgharimu maisha. Halafu bila hata kumuogopa Mungu mtu unaanza kupepesa lugha ya kudai ushahidi. Shameless ******!
 
Mmmm! je waliomwaga tindikali walivalia gwanda la cdm? Kumbuka kuna vyama 8 vinagombea Igunga pia kuna wagombea binafsi---------!

Angefanyiwa mfuasi wa CDM bado ungekuwa na fikra hizo hizo kwamba vyama viko zaidi ya 8?
 
Mwanachama CCM amwagiwa tindikali

Kijana wa Green Guard, aliyemuokoa majeruhi huyo, Farahani Farahani, alidai kuwa alikutana na majeruhi huyo karibu na shule inayojulikana kama Jitegemee na kwamba wakati anarudi alikutana na wanaume wawili na majeruhi huyo akiwa katikati.

"Nikasema kwamba Katibu alinipigia simu kuwa kuna kijana anatafutwa ametekwa na watu wa Chadema , nikasema ngoja nirudi kama kutekwa na mimi nitekwe kwa sababu tayari nilishapata taarifa kuwa kuna kijana anatafutwa basi nageuza wale vijana wakanisimamisha samahani bwana huyu kijana hebu mpeleke kituo cha polisi," alidai.
Alidai alipomchukua na kumfikisha katika ofisi za wilaya za CCM hatimaye polisi wakamchukua kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Yaani kwa maelezo haya tu yanaonyesha huu ni unyama wa ccm. Ndugu zangu mnaojiita ccm kuweni makini wanambinu chafu sana.
 
Hivi huwa "unajisikiaje" unapotoa habari za uongo namna hii?Ebu jaribu kuzirejea akili zako then soma ulicho post!
 
jana kuliripotiwa katika vyombo vya habari na hata huku jf kuwa chaema wamemwagia kijana wa ccm titindikali hapa igunga,leo katika hali ya kuhuzunisha kijana mwengine tena wa kike amepigwa na mawe baada ya kumkataa mmoja wa vijana wa chadema katika kijiji cha itumba,tarafa ya igunga wilayani hapa,

kwa maelezo ya binti huyu maria solomon,jana alifuatwa na afisa huyu akaombwa penzi,akakubali lakini baada ya jamaa ruzuku yake kuwa ndogo binti akaamua kuchomoa,lakini akawa tayari kishalamba soda mbili aina ya fanta ya kada wa cdm,mshakaji akalalishwa mlango wazi na binti astokee,sasa leo katika pitapita si kamuona?? mawe yakaanza!

Mimi mgeni katika hili jamvi lakini nimegundua walio wengi humu wanaakili za kutosha kwaujumla ni Magreat thinker, kuwaletea habari hii sijua kama watakuelewa! kama huna cha kupost kaa kimya kama mimi.
 
Chadema hawana sera..hata kutongoza hawajui! Ndio maana waishia kuoa wake za watu na wanawake walioachika!
Pia wengi asilimia kubwa wako 30+ lakin bado hawajaoa
 
habari ni habari hata kama hukubaliani nayo.....! NGUMI MKONONI KWA YEYOTE ANAYEKATAA, LAZIMA MJUE ASILI YA CHAMA CHETU NI WAPI ARAAA
 
Chadema hawana sera..hata kutongoza hawajui! Ndio maana waishia kuoa wake za watu na wanawake walioachika!
Pia wengi asilimia kubwa wako 30+ lakin bado hawajaoa
SUGU.......mke wa JAFFARAI
ZITTO....mke na marehemu wa marehemu MPAKANJIA
SLAA....mke wa mfanyakazi wa bandari
-------......mke wa DJ maarufu.
na kadhalika na kadhalika
 
Back
Top Bottom