Kiingereza cha Mlimani City

Kiingereza cha Mlimani City

Kuna mtu anayejifunza lugha ya kigeni bila kukosea?

Wasipojifunza mnawasema kwamba wabongo kiingereza kituo cha polisi, wakijifunza mnawasema wanakosea.

Mimi mtu anayejifunza lugha ya kigeni nategemea akosee, si lugha yake ati.

Hao ni wa kupongezwa kwa kujitahidi kujifunza lugha ya kigeni bila aibu, si wa kubezwa.

Sasa wewe unayejua na kukerwa na makosa hayo uliwaelekeza?

Kiranga mkuu, vibinti na samsung s4 selfie hadi wanakwambia uwapishe! Leo uje uwakosoe? Nishazeeka miye siwezi aibishwa mbele za watu
 
Last edited by a moderator:
Inategemea umeenda muda gani. Mbona wengi wanaoendaga "Mlimani city" ni watoto.
 
Jamani kwa nini kila mtu akikanyaga tu lango la kuingilia mlimani city anaanza kuongea kingereza? Utasikia cha kuungaunga mara IS na WAS kibao. Kwani mkiongea Kiswahili chenu mtakuwaje? Acheni uzuzu ubitozi na usister duu!

....mbona mimi nikiwa na mwana huwa nakifurumusha cha poti....
 
kingereza cha kuunga unga cha mademu wa mlimani city:kwa sauti ya kidem "i asked my bae to kunipitia hapa mlimani city and he was like what!!!?.....,so i had to kumsubiri pale marry brown,i waited for like an hour.....so nikamcall nijue what's wrong,he was like ooh samahani dear i'm stuck at mwenge,ooh sijui road traffic...

kwa wale wenzangu na mimi,ukishasikia demu anaongea hivyo mlimani city,lazima utoke nduki tuu.:eyebrows:
Ah keimamae, ukute mtoto kashuka kwenye bodaboda.....
 
Sisi wengine huwa tunapita hapo kupigwa kiyoyozi kabla ya kuendelea na safari ya kurejea makwetu...
Mwenzio nilikuwa napenda kuingia benk hasa NMB Nakaa kwenye kiti kama mteja anayesubiri huduma huku lengo likiwa ni kiyoyozi,siku moja wakavamia wazee wa njaa kali... usifanye mchezo maana jinsi nilivyowekewa mtutu kichwani ingefika dk tano tu kojo lingenitoka, toka siku hiyo sina hamu na viyoyozi vya maeneo kama hayo.
 
hahahahahahahahaha utumwa wa lugha halafu katika nchi yako
.......hatari sana.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom