Jana Nimepanda Daladala la London nikapitishwa Kituo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,856
JANA NIMEPANDA DALADALA LA LONDON NIKAPITISHWA KITUO.

Anaandika, Robert Heriel
kijana Chakaramu.

Yagayagayagayaga!
Wazimu ukanipanda, ukanisonda nikahisi kukonda, niilikuwa zangu nimesimama stend ya Daladala huko katikati ya jiji nikiwa nimechoka, Kwa kweli shughuli za jiji hili zilinichosha, mwili wangu ulikuwa umepoa ungedhani mgonjwa wa presha ya kushuka, mapigo ya Moyo yalikuwa chini mno, ngozi yangu ilikuwa ya Moto sio Kwa sababu ya joto la mwili bali kuunguzwa na Jua Kali la jiji.

Taikon nikatulia zangu nikisubiri Daladala nirudi zangu nyumbani baada ya siku nzima kuhangaika huko mjini kutafuta riziki ya Mbwa iliyopo miguuni mwake. Lakini siku ya leo haikuwa nzuri kwangu, sikupata kibarua hivyo nilikuwa narudi nikiwa na masikitiko makubwa huku nikiwaza kesho itakuwaje kwani sikuwa hata na nauli ya kuja mjini.

Ningali nimekaa kusubiri Daladala nilichoshwa na dhihaka ya Magari ya kifahari yaliyokuwa yanapita, niliona jinsi yalivyokuwa yananikebehi Kwa miondoko Yao ya madaha, Kama hiyo haitoshi kelele za honi za daladala na pikipiki nilihisi walikuwa wakinipigia Mimi. Hivyo kila nilipozisikia imagine nilikuwa naruka vuupu! Kwa kushtuka nikidhani nipo barabarani, kumbe hata! Yaani maisha haya acheni tuu. Watu wachache waliokuwa pale walikuwa wakinishangaa vile nilivyokuwa naruka Kwa kushtuka.
Pengine walihisi nina Busha, wengine walihisi huenda nimechanganyikiwa, basi kila mtu na mawazo yake kichwani, Mimi hayakunihusu.

Kituo kile cha Daladala kiliangaliana na jengo moja kubwa la Ghorofa Kama kumi hivi lenye Vioo. Punde si punde wala sio kunde za mama mkude ule wazimu niliousema ulionipanda ndio huu sasa nauelezea, ukanishika.
Macho yangu yalishuhudia Mwanamke mzuri sijapata kufikiri achilia mbali kuona hata kwenye filamu, hata kwenye katuni za masudi, hata kwenye Riwaya sijawahi kusoma mwanamke mzuri kama Yule niliyemuona, huenda ni Wale wanawake WA peponi waliozungumziwa na Manabii. Doooh! Taikon matatani.

Yule mwanamke akiwa upande wa barabara akitaka kuvuka, watu wote eneo lile tukaacha kila tulichokuwa tunakifanya, macho yetu yote yalikuwa yanamtazama Mrembo Yule,
Alikuwa mwanamke mwenye Sura nzuri Sana yenye utukufu Kama mwezi sijapata kufikiri, nywele zake alikuwa kazifunga Kwa nyuma zikiwa zinaning'inia kama kishada, sitaki Mimi Kueleza habari za maziwa yake jamani, nahisi machozi ya furaha yananitoka, yalikuwa maziwa makubwa kiasi yaliyosimama Dede ambayo mbele yake zilikuwepo chuchu zikiwa zimechoma kile kiblauzi alichokuwa kakivaa. Sitaki Mimi kukumbuka, kila nikikumbuka nahisi napaa naenda paradiso kutokana na uzuri wa Yule Dada.
Buriani Taikon, mwendo nimeumaliza,
Tutaonana peponi, uhondo sitobakiza,

Kile kiblauzi cha Rangi ya karoti chenye Kola nyeusi alikuwa amekichomekea kwenye Sketi nyeusi maridadi iliyomkaa vyema, iliyokuwa ikihangaika kuyatuliza mapaja yake manene kiasi laini yaliyokuwa yanatikisika wakati akiwa anavuka barabara, nilitamani ningekuwa nyuma yake nishuhudie kile kilichokuwa kinatokea huko nyuma yake, nilikuwa na uhakika kuwa alikuwa amejaza furushi la viazi vya gairo kutokana na kiuno chake kuwa chembamba kisichokusa na uwiano mzuri na nyonga zake.

Hamadi! Alikuwa amevuka na kufika pale kituoni, Kwa aibu akachukua simu na kuanza kubonyabonya akiwa ametugeuzia mgongo na kutuacha watu wote pale tukiwa tumeshika kalamu zetu ku-calculate eneo lililotiwa kivuli.
Sina hakika kama kila mmoja wetu pale kituoni alikuwa anakumbuka kanuni za kutafuta mzingo wa maumbo Kama Yale.
Hapo nikarudisha akili zangu nyuma huko miaka kumi na kitu nikiwa nasoma kijinini kwetu MAKANYA,
Ilikuwa ni "Pai D H square" "Noo! Hapana, ilikuwa ni Two Pai R" "mmmh" "Okay nimekumbuka, ni Pai D H underoots". Nilikuwa kwenye mahesabu makali ya kutafuta eneo la lilifungwa upande mmoja lenye kivuli.
Hata hivyo nilikuwa nashindwa kutoa Hesabu zangu Fresh Kwa Sababu Yule mrembo alikuwa akijitingisha mara hivi mara hivi, mara vile mara vile hali iliyokuwa inapelekea Matako yake kutingishika na kunisababishia nibadili Fomula za Nusu kipenyo times diameter.

Sikukumbuka njaa iliishia wapi, sikukumbuka habari za kukosa vibarua, mrembo Yule asiye na mfano alikuwa amefyonza hayo yote akabaki yeye Kama yeye, punde si punde Kwa sekunde mawazo yangu yalikatika baada ya kuona Coaster ya Staffs ikisimama pembeni ya Yule Dada, kisha Yule akawa anapiga hatua zake kuufuata mlango wa Ile coaster uliokuwa unafunguka, Kwa upesi nikaamka kumfuata Yule mrembo akiwa tayari kaweka mguu mmoja kwenye mlango wa Coaster.
Nilipofika, nami nikataka kuingia, watu wakawa wananishangaa lakini hilo sikulijali Sana.
Nikasema nipo na huyu dada, Yule mrembo akageuka akiwa ananishangaa lakini kama vile Zali la mentali akakubali huku akinitathmini.

Tukazama ndani kwenye Daladala la London. Safari ikaanza hata hivyo sikujua Daladala Ile ilikuwa inaelekea wapi, sikujali kwani mule ndani kulikuwa na warembo wa maana sijapata kuona, kuna wakati nilifikiri nimepanda Dadadala la Allien. Pisikali za kwenda, wazuri wazuri tena.

Dadadala la London sio lelemama,
Kiyoyozi chapuliza bila kuumiza,
Chabembeleza bila kubeza,
Muziki wake wachombeza, utamu koleza,
Daladala la walamba asali, lambalamba ulimi usiutoe mdomoni ati hiyo ndio kanuni.

Bahati ilioje kukaa Siti moja na Mdada mrembo Kama Yule. Hakuonyesha Kama anajua lugha za binadamu Kwa jinsi alivyokuwa mzuri. Hata hivyo nilijipa moyo kuwa atakuwa anaelewa baadhi ya misamiati ya lugha yetu.

Nikamgusa akanitazama Kwa mshangao Kwa kikike huku macho yake yakinisemesha Hellow! What's up Boy?"
Nikawa naongea Kwa ishara ya lugha za Alama nikimuambia " Namshukuru Kwa ukarimu wake" akawa anashangaa kana kwamba anastaajabu kuwa iweje Mimi niwe Bubu wakati nilimsemesha pale mlangoni.
Akaniambia, " kwani wewe ni Bubu? Mbona uliongea wakati unaingia"
Nilihisi usingizi unanipitia, alikuwa na sauti nzuri Kama Kinubi.
" Kwa uzuri wako Dadaangu Sikujua kama unajua lugha za binadamu, kumbe hata Kiswahili unajua baadhi ya maneno mpaka kutunga sentence"
Dada akacheeeka mpaka nikabaini jino lake la mwisho lilikuwa na dosari ya kuoza. Doooh!
Hata hivyo cheko lake lilikuwa kama pambo kwenye Sura yake uzuri wake uliongezeka maradufu na kuuzidishia moyo wangu mahangaiko.

Tayari tulikuwa tumefika Mwenge Mataa tukitokea Mjini. Tulikuwa tunapiga tukiwa tumezoenaa kiasi. Hata hivyo nilimdanganya nakaa Bunju baada ya yeye kuniambia anaishi Mbezi Beach.

Hatimaye Daladala likasimama, aliyekuwa anatakiwa kushuka ni Mrembo Careen, nikaona nishuke naye.
Daladala lilipoondoka akawa ananishangaa mbona nimeshuka, nikamjibu nimemfuata yeye.
Akabaki ananiangalia huku watu wa eneo lile wakitushangaa pia.

Nikamuomba namba za simu, Hakuwa na hiyana, ni Kama alishaona macho yangu deep down inside yanaongea Jambo nyeti la kikulungwa.
Akachukuliwa na Bodaboda na kuniacha pale Tangibovu nikipiga Hesabu za Kurudi nyumbani Tandale Kwa Mtogole, mfukoni kucheki nauli sina, kile kimia tano changu sijui kiliangukia kwenye Daladala la London.
Duuuh! Njaa iliyokuwa imenyamazishwa Kwa utukufu wa Yule mrembo ikazuka, michosho ikaamka, mfukoni sina hata Mia, sasa hapa ni kutembea mpaka Tandale na bahati mbaya njia hiyo haikuwa na shortcut.
Hata hivyo sikujilaumu Kupanda Daladala la London.
Kwa sababu Yule mrembo sio tuu kwamba alinifurahisha machoni Bali pia aliiponya Nafsi yangu.

Nilifika tandale saa kumi na mbili jioni. Baada ya kutembea Kwa masaa mawili.
Mtoto Careen tumepanga kuonana leo Jioni pale Mlimani City.

Kwa wale mliomaeneo ya Mlimani City jioni mida ya saa 12 hivi mje hapa Mlimani city, nitakuwa na Careen, na Careen amesema atakuja na wenzake wa Daladala la London.
Wengi wao wapo single,

Taikon ninafanya maandalizi unaweza kudhani naenda kukutana na Malkia, hata hivyo Kwa uzuri wake ni zaidi ya malkia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kijana upo mukulu kulu mpepesa macho haiba ya dunia,mpelupelu kama shingo ya kongoni,mwana kindakindaki Toto la kiafrika hongera sana kwa simulizi bashasha yenye wingi wa tashtiti na nomino,
Shukurani,Taikoni.
Tutiriri kiswahili hudhulungi,chenye haiba ya kipekee,tuwaoneshe usanifu wetu kwa lugha yetu ndiyo ni yetu..
 
Kijana upo mukulu kulu mpepesa macho haiba ya dunia,mpelupelu kama shingo ya kongoni,mwana kindakindaki Toto la kiafrika hongera sana kwa simulizi bashasha yenye wingi wa tashtiti na nomino,
Shukurani,Taikoni.
Tutiriri kiswahili hudhulungi,chenye haiba ya kipekee,tuwaoneshe usanifu wetu kwa lugha yetu ndiyo ni yetu..

Hapa umeniweza Mkuu.
🔥🔥🔥🔥
 
Kwa wale mliomaeneo ya Mlimani City jioni mida ya saa 12 hivi mje hapa Mlimani city, nitakuwa na Careen, na Careen amesema atakuja na wenzake wa Daladala la London.
Wengi wao wapo single
Anakuja na nani?!!! Usije tu kuaga unaenda uani halafu ukapotea kusikojulikana!
 
Back
Top Bottom