Sisi wa mikoani mtu akitoka dsm utasikia kiswahili chake sasa...!
Umenchekesha Sana...
Kweli huwa ni shida sana, huwa tunawambia wamekula nazi.
Ahahahah mbavu zanguu...wanaongea kama wazaramo
Jamani kwa nini kila mtu akikanyaga tu lango la kuingilia mlimani city anaanza kuongea kingereza? Utasikia cha kuungaunga mara IS na WAS kibao. Kwani mkiongea Kiswahili chenu mtakuwaje? Acheni uzuzu ubitozi na usister duu!
Mbona huwa naenda pale mara nyingi tu na huwa siongei Kiingereza?
sehemu za heshma twatumia lugha ya heshma.jamani kwa nini kila mtu akikanyaga tu lango la kuingilia mlimani city anaanza kuongea kingereza? Utasikia cha kuungaunga mara is na was kibao. Kwani mkiongea kiswahili chenu mtakuwaje? Acheni uzuzu ubitozi na usister duu!
Kwani wakiamua kuongea Kiingereza wao wanakupunguzia nini wewe?
mkuu Kiranga, tatizo wanakosea sana hiyo lugha. Mfano last week nilikuwa nimepumzika namsubiri mwanangu achorwe usoni
kwenye bench wamekaa mabinti wawili, mmoja anasema "am listening to Diamond musics, they are delicious"
mkuu Kiranga, tatizo wanakosea sana hiyo lugha. Mfano last week nilikuwa nimepumzika namsubiri mwanangu achorwe usoni
kwenye bench wamekaa mabinti wawili, mmoja anasema "am listening to Diamond musics, they are delicious"
​Ina maana kama kienglish hakipandi sidhani hata bidhaa za huko utaziweza kaka..LOLKama englishi ndio lugha ya taifa la mlimani city...inabidi wakina sie tuishie nje na tuagizie wakalimani wakatununulie bidhaa huko ndani....
​Ina maana kama kienglish hakipandi sidhani hata bidhaa za huko utaziweza kaka..LOL
Wapii kaka, hao waongeaji english wanaosemwa hapo wala sio wanunuzi ni watembezi tu..Hata sisi wa kisambaa hapo mwake tu .Kwa wakina sisi tuliozoea kizaramo hapo hapatufai...unaweza ukaanguka kwa presha kwa mshangao...utakapoambiwa sambusa elfu tano..wakati hiyo ni bajeti yako ya siku mbili....
Wapii kaka, hao waongeaji english wanaosemwa hapo wala sio wanunuzi ni watembezi tu..Hata sisi wa kisambaa hapo mwake tu .
Wabongo bwana 😂😂😂
Mtu unamsemesha kiswahili anakuchanganyia lugha, ukiongea kingereza anaanza kuchanganya R na L humo humo kingerezani, past tense zinakuwa future na future zinakuwa present, present tense zinakuwa mixed grill😂😂😂
Imesimama kama Islamic State!
Hahaaa kiongozi, kuna sarcasm hapo.
Ila kuna watu waonavyo hivyo, kwamba Kiingereza ni ishara au alama ya ustaarabu.
Hujawahi kukutana na Wabongo ambao hawajawahi hata kuishi Uingereza au popote pale nje ya Tanzania lakini wanajifanya kama hawakijui Kiswahili?
Kuna mtu anayejifunza lugha ya kigeni bila kukosea?
Wasipojifunza mnawasema kwamba wabongo kiingereza kituo cha polisi, wakijifunza mnawasema wanakosea.
Mimi mtu anayejifunza lugha ya kigeni nategemea akosee, si lugha yake ati.
Hao ni wa kupongezwa kwa kujitahidi kujifunza lugha ya kigeni bila aibu, si wa kubezwa.
Sasa wewe unayejua na kukerwa na makosa hayo uliwaelekeza?