Wakuu Palantir na Kudo
Alishawahi kusema Nikita Krushchev "What the Scientists have in the briefcase is terrifying"
Hili swala hebu tuliangalie katika mapana yake kabisa kama watu wasio na utaalamu wowote kuhusu Sayansi ya Mambo ya chembechembe za Uhai (Genetics) lakini kama watu wenye uwezo mzuri wa kuuliza maswali, kuchambua na kuelewa. Natumai wengi wetu tupo kwenye hili kundi la watu wa pili. Hivyo tuulize, tuchambue na mwishowe tujaribu kuelewa kila hoja inayoletwa hapa kwenye mjadala huu kwasababu wote hapa tunachangia kutokana na kile ambacho tumeamini kwa utashi, kusikia na kusoma: Hakuna aliyefanikiwa kushuhudia ukweli wowote kuhusu hili kwasababu kama kweli ipo basi hii ni FORBIDDEN SCIENCE ambayo ni hatari kwa ustawi wa binadamu. (Speaking on philosophical point of view)
Tafiti na majaribio yote ya Kisayansi huwa yanakuwa na taratibu zake (Research Ethics) ambazo zinatakiwa kufuatwa na kila mwanasayansi wa dunia hii bila kupindishwa. Sheria za kimataifa pamoja (Customary International Law), Sheria za mataifa (Municipal Laws) na Sheria za dini (Religious Laws) mbalimbali zinakataza kabisa majaribio na tafiti ambazo hazitumiki kwa manufaa ya afya ya binadamu.(Unethical Human Experimentation is strictly prohibited)
Haya yote tumeyaleta baada ya kuona kilichotokea kabla na baada ya 1945 (Vita vya pili vya dunia). Ujerumani wakati wa Hitler kulikuwa na Aribert Heim A.K.A Dr Death na mwenzake Joseph Mengele ambao katika kutaka kuwa mbele kwenye kila wakati wa vita waliwachukua binadamu na kuanza kuwafanyia tafiti. Mengele alikuwa anawanyia Wayahudi upasuaji bila ganzi ili kupima mwanadamu anaweza akaka muda gani bila miguu au mikono. Heim alikuwa anawapandikizia virusi na bakteria mbalimbali ili kuweza kufanya majaribio ya silaha.
Najua tunaweza kusema Human Cloning hailingani kabisa na majaribio ya moja kwa moja ya binadamu kwasababu tunachokifanyia majaribio hapa ni Seli tu. Hata hivyo tunaweza kusema kwamba watu hawalazimishwi (Voluntary), lakini binafsi mimi nitauliza lengo la kutengeneza mtu mwingine anayefanana na mimi ni nini ??? Mkuu Da'Vinci kasema lengo la haya majaribio ni kudhoofisha binadamu. Hivyo mimi nachelea kusema kwamba hii ni Advanced Version of Biological Warfare ambayo ni hatari kuliko SARS, MK-ULTRA na SMALL POX. Huenda tukasema hii sayansi iruhusiwe lakini isitumike vibaya kama ilivyo kwenye teknolojia ya Nyuklia: Ntajibu sawa lakini kuna haja ya kutengeneza mwanadamu mwingine ambaye anafanana na Palantir au Malcom ?? (Hapa haitojalisha kama hii teknolojia ipo au haipo)
Hebu tuangalie katika mapana zaidi ya upande wa Sheria:
Je, kama kweli wakafanikiwa au wameshafanikiwa kutengeneza nakala za watu kama Kanye West.
What will be the Legal Status of a clone ???
- Will he be recognized as a Human Being or A property ???
- Will he be called Kanye West or Given a Specimen Number ???
- What of Human Rights and Freedoms, Will he be inherently entitled to their protection? (eg Freedom of Movement)
Such questions are very pressing to me, ndiyo maana hata kama wamefanikiwa hawawezi kutuonyesha kwasababu:
Mosi, hizi tafiti ni kinyume kabisa na Sheria (Unethical Research)
Ukisoma Tamko la Helsinki (The Declaration of Helsinki of 1964) lilitolewa na World Medical Asssociation, Kanuni za Mahakama ya Nuremberg (Nuremberg Codes 1940's) na Sheria za kimataifa (Customary Law) zimekataza kabisa aina hizi za majaribio. Kama wamekataza unategemea Wamarekani, Warusi, Wachina, Waingereza, Waisraeli na mataifa mengine yenye teknolojia kubwa yatasema kweli ??? Nani anataka kuleta rundo la maneno kutoka kwa washika dini wa Vatican na Uarabuni ??? JIBU HAPA NI HAKUNA ANAYETAKA.
Pili, teknolojia hii kama ipo kweli hivi tumefikilia swala zima la madhara yake katika mbio za utengenezaji silaha (Arms Race) ??? Maan kama hii teknolojia imefanikiwa au itafanikiwa na Wamarekani, unategema Uchina na Urusi hawatataka kuwa nayo ili kuweka mzani wa nguvu (Balance of Power) sawa na Marekani ??? tuliona haya kwenye Nyuklia. Walianza Wanazi, Wamarekani nao wakaunga (The Manhattan Project), Wakaja Wasovieti mwaka 1949, Wachina na mwishowe hadi Africa kwetu silaha hizi zikafika. Sasa hebu fikiria mnaingia kwenye mashindano ya kutengeneza watu ambao ni silaha za vita (Just think about it. Somebody is solely produced to kill and wage war). Kitu kama hiki kitaifikisha wapi dunia yetu ??? Au Taifa gani linaweza kukubali kuweka kitu kama hichi wazi ???
Tatu, hii teknolojia inavunja kabisa kanuni za Uhuru wa kifikra. Freedom of Conscious kama ifahamuvyo ina sura nyingi sana sana. Hata mtoto wako uliyemzaa na kumbeba tumboni kwa miezi tisa kuna muda huwezi kumpangia Imani au Matakwa. Lakini tunaambiwa teknolojia hii inachukua kila kitu kutoka kwa Palantir na kuzalisha Palantir wa pili. Sasa je, hivi hatuoni kwamba kama tunatengeneza binadamu mwingine mpya lakini anakuwa na fikra kama za Palantir, hapa si tunauwa tunavunja Uhuru wa mawazo wa mtu ??? Ndiyo maana nikauliza swali hapo juu: Je, huyu CLONE au REPLICA atakuwa ni Binadamu au Mali. Kama tutamuita ni binadamu basi haturuhusiwi kumpangia chochote kile lakini kama atakuwa ni mali inayouzwa (Silaha) kama silaha nyingine basi tunaweza kumfanya chochote tutakacho. Lakini bado tunarudi palepale ni Taifa gani au Serikali gani ya dunia hii inaweza kukubali kuulizwa haya maswali ??
NB: Ikumbukwe mwaka 1967 baada ya CIA kuabishwa bungeni kwa kufanya majaribio ya binadamu kwenye Project MK-ULTRA basi nchi nzima na dunia nzima walipiga makelele hadi ule mradi ukafungwa. Sasa kama wameanza tokea miaka ya 1960's hadi leo 2018 jiulize wametumia pesa nyingi kiasi gani. Jiulize kama wakisema na watu waandame unadhani hawatalazimika kufunga hiyo miradi kweli ???
Hapa nimeongea katika mtizamo wa kinadharia tu,
Lakini ukweli mchungu ni kwamba wanasayansi wa dunia hii wana vitu vya ajabu ambavyo hatujawahi kuvifikiri.
Makufuru yote haya wanayoyafikiri ni kutokana na Roho Mbaya, Chuki, Ulafi, Uvivu wa kitaalamu na Ubaguzi. Ukijuliza hadi leo kwamba Teknolojia ya Nyuklia tangu kugunduliwa imeleta faida au hasara utapa jawabu dogo tu: Faida chache kwa baadhi ya watu (Selective Profit) lakini Hasara Kubwa sana kwa dunia nzima (Non-Selective loss because we all fear nuclear war). Hivyo hata kwenye cloning nadhani kama watafanikiwa au wameshafanikiwa itakuwa hivyo hivyo tu, kuna mataifa watakuwa wanatumia hiyo teknolojia huku wakikataza wengine wasiwe nayo, hata kama itatumika kwa manufaa ya kiafya huku wakileta kisingizio kwamba Inaweza ikatumiwa vibaya au kutua kwenye mikono ya magaidi,
Nawasilisha....
Malcom Young, Jr.
CC: zitto junior , chige , mitale na midimu , TUJITEGEMEE , Red Giant ,Consigliere , major mwendwa , Graph Theory , SirChief , Prof Naombeni msaada wa kimawazo katika hili.
Mkuu,Malcom Lumumba Amani iwe nawe ndugu. siku nyingi sijakusikia but I hope everything is well with you sir. Kwa mtazamo wangu teknolojia ya HUMAN CLONING ni mojawapo ya undisired technology in 21 century, ingawa kuna mixed reaction kuhusu human cloning. Baadhi ya nchi zimekataza human cloning huku nyingine zikiruhusu na nyingine zikibaki kuwa silent. Takribani nchi zaidi ya 25 zimezuia cloning ya binadamu ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza,, Canada, Ufaransa na Ujerumani. Dunia inalichukulia suala la human cloning kama ni tafiti hatarishi na mbaya zaidi katika maendeleo ya Binadamu. Ingawa kuna nchi kama Korea ya kusini, china etc wao wanaruhusu. Kwa mfano, nchi kama;-
INDIA: India haina sheria Mahususi kuzuia tafiti or human cloning yenyewe. hata hivyo Baraza la Utafiti wa Matibabu (ICMR) na Idara ya Bioteknolojia (DBT) ilikataza cloning ya uzazi wa kibinadamu kama kwa "Mwongozo wa Taifa wa Utafiti wa Cell Cell" 2017, iliyoandaliwa na NAC-SCRT. India inaruhusu cloning ya wanyama, na inatilia mkazo utafiti katika eneo hilo.
UNITED STATES: Kwa mujibu wa muswada wa Marekani, HR 3498, tarehe 11 Septemba 2015, cloning ya binadamu imepigwa marufuku nchini Marekani lakini utafiti hauzuiliwi kufanyika ikiwa ni pamoja na utafiti katika matumizi ya uhamisho wa nyuklia au mbinu nyingine za cloning ili kuzalisha molekuli, DNA, seli zisizo za binadamu majani, tishu, viungo, mimea, au wanyama wengine zaidi ya wanadamu.
UNITED KINGDOM: Kwa mujibu wa sheria ya Human Fertilisation and Embryology Act 2008, uingereza inakataza human cloning.
UNITED NATIONS: The United Nations General Assembly approved (Mar 2005) ilipiga marufuko utafiti, ubashiri na hatua zozote za uzalishaji/urutubishaji wa binadamu yaani human cloning.
Hivyo basi nikijaribu kujibu hypothesis hapo juu kama zilivyouliza kuwa:-
(a) Will he be recognized as a Human Being or A property ???
(b) Will he be called Kanye West or Given a Specimen Number ???
(c) What of Human Rights and Freedoms, Will he be inherently entitled to their protection? (eg Freedom of Movement)
Nikianzia na swali la kwanza, he/she will be a human being. though depend how and from which angle your definition is based. I mean spritial or scientific perspectives. kwa mfano katika kilatini (Latin Humanus) inamtambulisha binadamu kama mnyama (as an animal and/or monster as distinct from the ancient). Hivyo basi Kwa mtazamo wangu, binadamu or Homo Sapiens anaweza kuwa kiumbe chochote kilicho na tabia zilizotofanana na zetu sisi tunaojiita binadamu ( based on scientific facts and analysis). kwa upande mwingine human being can be property and this goes back to slavery era. However, in contemporaly world There are no longer any legal grounds for men being the property of other men. There are, however, unexpected consequences of modern inheritance laws in many Western countries, where biological offspring have the right to a stipulated, usually lion, part of their parents's wealth—whether the parents so wish or not (in the same vein parents inherit their children. (b) Will he be called Kanye West or Given a Specimen Number ???
(c) What of Human Rights and Freedoms, Will he be inherently entitled to their protection? (eg Freedom of Movement)
Kwa mtazamo wa leo na kwa mjibu wa sheria mbalimbali za nchi na za kimataifa , binadamu hawezi kuwa bidhaa/property ingawa kwa namna moja ama nyingine binadamu aliwahi kuwa property na ameendelea kuwa property (Modern slavery). pitia case ya Somerset v Stewart (1772) kuna mengi ya kujifunza huko.
(b) whether Will he be called Kanye West or Given a Specimen Number? I think the answer is yes. kwa mtazamo wangu jina is not a big deal. we even name our pets after human names...
(c) Human right is universal rights ingawa haiko absolute kwani kuna nchi kadha kwao human right ni terminology ngumu kwao. It sounds like a priviledge. kuhusu legal protection iko subject to discussion. nafikiri tatizo ni kuwa hatujapata jawabu la human cloning...A real human from test tubes. nafikiri, sheria zinaweza kubadilika just to accomodate new experience.