Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Viongozi hao pia walithibitisha habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuwa vurugu zilizotokea siku ya yalipoahirishwa maziko ya Wangwe zilisababisha baadhi ya viongozi kuamriwa na Polisi kuondoka eneo hilo. “Hali ilikuwa mbaya sisi wenyewe tuliingizwa kwenye chumba cha maiti kuhemea humo tukakaa dakika 10 na akina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) ndipo tukaondoka katika eneo hilo,” alisema Mrema.

Naye Mbatia alikiri kuwa vijana walikuwa wamebeba silaha za jadi na kama isingekuwa busara ya Polisi na ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, kulikuwa na uwezekano wa kutokea vurugu. Alisema viongozi wengi wakiwamo wabunge na mawaziri waliruka uzio kutokana na hali kuwa tete kwenye msiba na hiyo inatokana na utata wa kifo cha Wangwe.

Alisema hata fulana zilizoandaliwa kwa heshima ya marehemu zilichomwa moto pamoja na bendera za baadhi ya vyama vya siasa. Hata hivyo hakutaja vyama ambavyo bendera zake zilichomwa moto. Juzi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alikanusha habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuhusiana na vurugu hizo. Alizielezea habari hizo kuwa zilikuwa za uzushi zenye lengo la kukiua chama cha Chadema.


Habari yote hii hapa;

ikumbukwe kwamba wanazi wa chama fulani walisema hakupakuwa na tatizo lolote.

Oh, please! And you believe all those craps!!
 
Kwamba ni Jasusi ama la hilo sidhani kama linaweza kutushughulisha sana kwa sasa. Na kama ni kweli inaweza andikwa ya kwamba "Mission Accomplished"... Sasa Task kubwa zaidi inayofuata kama kweli yeye ni Jasusi hao Viongozi watatu walioyaongea haya watuambie kitu kimoja, Handler(s) wake ni kina nani.!
 
hivi mtu akisema "nilipokuwa mjini, mvua ilinyesha" ina maana mvua imemnyeshea? Wale wanaotoka maeneo ya Mbulu watatambua kwamba ukiitisha watu wa Mbulu kuwatangazia mpango wa maendeleo ya ujensi wa shule karibu wanaume wote watakuja na fimbo zao ndefu tu. Mgeni kama ukisema "walikuwa na fimbo nyingi" utakuwa sahihi.

Nina uhakika kulikuwa na watu wengi waliokuwa na kamera kule, basi tuonesheni angalau picha ya moja ya mtu aliyebeba panga.

Huu ni mfano wa picha ambayo inaweza kuletwa toka Tarime. Hii ilipigwa Kenya baada ya vurugu za uchaguzi. HIvyo wale waandishi waliokuwa kule Tarime walete picha ambayo inaonesha Mbowe angalau anafukuzwa na mapanga na mikuki hadi kwenye gari; hiyo itathibitisha maneno yao na mjadala utafungwa. Mwenye picha aiweke hapa JF anakomwa nyani giledi! NI picha tu ndiyo itakata ngebe za Chadema.

r214082_828024.jpg

Mimi nilikuwepo naomba kuambatanisha baadhi ya picha, katika picha hizi zote fimbo moja ya kwanza ni ile ya Nimrodi mkoni ndiyo ambayo nimeona katika picha zangu. Nitaendelea kuweka nyingine zaidi kadri mambo yatakavyoendelea.
lakini nasisitiza picha za mapanga na marungu sina na wala sikuziona. wenye nazo wanisaidie hapa.
 

Attachments

  • P1010245.JPG
    P1010245.JPG
    253 KB · Views: 130
  • P1010252.JPG
    P1010252.JPG
    533.5 KB · Views: 99
  • P1010262.JPG
    P1010262.JPG
    359.4 KB · Views: 98
  • P1010261.JPG
    P1010261.JPG
    292.2 KB · Views: 94
Mimi nilikuwepo naomba kuambatanisha baadhi ya picha, katika picha hizi zote fimbo moja ya kwanza ni ile ya Nimrodi mkoni ndiyo ambayo nimeona katika picha zangu. Nitaendelea kuweka nyingine zaidi kadri mambo yatakavyoendelea.
lakini nasisitiza picha za mapanga na marungu sina na wala sikuziona. wenye nazo wanisaidie hapa.

Thanks mkuu kwa kutuwekea pics!! Huyu ndugu Ryatonga naye sasa ame-data. Mimi naona kama Lipumba/Mremba and that other guy wanajichana/kandamiza mamisosi huku wakionyesha nyuso za furaha. Sioni anayewatishia kuwachinja.
 
Mkuu PM,

Unaonekana kuwa na agenda ndugu yangu, mbona na wewe una habari nyingi sana ambazo zimekaa ki-Rostam Rostam, kulikoni mkuu?

Halafu siku zote maelezo yako yanakuwa very vague, kwa mfano unasema Mallya alienda huko Libya na watu wenye vyeo flani katika jamii yetu, lakini husemi Mallya alifuatana nao kwa msingi gani? Meaning akiwa na cheo gani au wadhifa gani?

Naomba unisaidie hilo swali Mallya, alifutana na hao viongozi Libya akiwa kama nani katika hili taifa, maana vyeo vya wengine uliowataja kuwa walienda naye Libya vinafahamika?
 
Wenyeviti wa NCCR-MAGEUZI(James Mbatia), TLP (Augustine Mrema) na CUF (Ibrahim Lipumba) wameueleza umma wa watanzania kuwa wanao ushahidi kuwa rafiki wa karibu wa marehemu Chacha Wangwe na ambaye alikuwa na marehemu wakati wa ajali Deus Mallya ni jasusi na mtu hatari.

Jana profesa Lipumba alithibitisha kuwa wanaoushahidi kuwa Mallya alipitia mafunzi ya miaka 6 ya ugaidi huko Libya na kwamba anamiliki vitambulisho tofauti zaidi ya kimoja vikiwa vimeandikwa kiarabu.

Wakuu hao wa vyama vya upinzani wameahidi kuliwasilisha suala hilo kwa IGP lishughulikiwe.

Hizi habari zinazidi kuchanganya na kuibua maswali mengi kuhusu kifo cha Wangwe na mazingira ya kifo chenyewe.
1. Kweli Mallya ni jasusi?
2. Uhusiano wake na Wangwe una muda gani?
3. Kama ni jasusi,je alikuwa upande wa nani na ni nani alimtuma?
4. Tuziamini tuhuma za Upinzani?
5. Hivi ni nani aliyeondoka na laptop ya marehemu na ilikuwa na nyaraka gani?

Naamini kuna mambo mengi chini y busati na yasipoibuliwa kuna kila dalili kuwa mambo ni mabaya ndani ya nchi.

Hebu tujadili wana JF
 
You know, kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba: kwa wakurya (esp. in rural areas) kutembea na silaha za jadi kama rugu, panga, sime, bakora ni kitu cha kawaida kabisa. Ni kitu cha kawaida kwasababu ya nature ya maisha yao (ufugaji/uwindaji/ukulima) inayo demand wao kutembea na silaha hizo za jadi at any time. Kama ilivyo kwa wazaramo kushindia vijiweni na vikombe vya kahawa na kashata (most of the time), wakurya nao kutembea na paga/sime/rugu/bakora muda wote (walioko vijijini hususani) is a part of who they are. So, hata kama hayo mapanga yalikuwepo msibani (na hukuna aliyeripotiwa kujeruhiwa), then sioni point ya kulishikia bango suala hili. Besides, Wangwe alikuwa anapendwa sana! So you can see kwanini damu za watu/wakurya zilikuwa zina boil-up siku ya mazishi.

Bongo Tz
Watu hawataki kusoma na kuelewa taratibu, tamaduni na wasifu wa kabila la aina fulani! Sitoshangaa watu wa aina hii,,, kukurupuka ni aina fulani ya tamaduni vilevile. Je, ingekuwa ni umasaini ingekuwaje. Wamasai kama walivyo Wakurya wanaasili ya kubeba silaha tena tunaweza kuziita za kivita! Rungu, Sime, mkuki, fimbo na siyo moja hata mbili,,,,, hata wakiwa wanaenda kwenye sherehe! Hatuoni ajabu kwa hawa wenzetu kubeba mapanga na silaha nyingine za kijadi! Ni tamaduni zao,, tuwaache kama walivyo.
Suala la Mbowe kwenda au kutokwenda ni la kiitifaki tu. Pia kama ambavyo wenzetu wana hasira naye (Mbowe) sioni ajabu hata hao Jamaa zetu Wakurya kwa nini wasiew na hasira, ukizingatia pia kuwa hata wao wanaweza wakalichukulia hili kisiasa zaidi kuliko kimaisha ya kawaida.
Hii yote ilikuwa mipango ya Mungu tu na siyo mkono wa mtu.
 
kwa sasa turudi kwenye UFIDASI kama kawaida,tujue hatma ya Tanzania na UFISADI
 
Insurgent,

Nakubaliana na theory yako. Naamini Mallya alikuwa anaendesha gari na Wangwe alikuwa kiti cha nyuma na most likely hakufunga mkanda. Atakuwa alichoka na kuamua kujipumzisha.
Kuumia alikoumia ni dalili ya mtu ambaye hakufunga mkanda. Ukifunga mkanda ni ngumu sana kupasuka kichwa labda ugonge mwamba au mti.

Duniani kote, wanaosababisha ajali husingizia waliokufa. Siamini kwamba kulikuwa na mtu wa tatu.

Kwa hiyo ushahidi wa mzee aliyemfungua mkanda Marehemu umeshaamua kuutupilia mbali?
 
Tunaomba mods afunge topic hii sasa turudi kuwakong'oli mafisadi.Tayari mpiginaji wetu anapumnzika kwenye nyumba ya milele.
 
Nimemshangaa Zito Kabwe na nimewashangaa sana baadhi ya wachangiaji kutaka kupotosha ukweli juu ya vurugu na vyote vilivyotokea kwenye mazishi ya marehemu Chacha Wangwe.
 
Mkuu PM,



Halafu siku zote maelezo yako yanakuwa very vague, kwa mfano unasema Mallya alienda huko Libya na watu wenye vyeo flani katika jamii yetu, lakini husemi Mallya alifuatana nao kwa msingi gani? Meaning akiwa na cheo gani au wadhifa gani?

Naomba unisaidie hilo swali Mallya, alifutana na hao viongozi Libya akiwa kama nani katika hili taifa, maana vyeo vya wengine uliowataja kuwa walienda naye Libya vinafahamika?

Support mkuu,

Huyo kijana huko Libya katika msafara huo alikuwa na jukumu gani?
Atoe maelezo yaliyojitosheleza!
 
I cant believe Prof Lipumba could sink that low!. This is what politics can do to a Man...................
 
Support mkuu,

Huyo kijana huko Libya katika msafara huo alikuwa na jukumu gani?
Atoe maelezo yaliyojitosheleza!

Tupo ukurasa mmoja wakuu,
Hapa tunaambiwa alienda na Muft na wabunge wa CCM kama nani? je ana uhusiano gani na CCM? je uhusiano wake na the late Wangwe aliyekuwa wa CHADEMA ''as his best friend'' ni wa muda gani? what about the dots with CCM???

tick tack!!!
 
hivi mtu akisema "nilipokuwa mjini, mvua ilinyesha" ina maana mvua imemnyeshea? Wale wanaotoka maeneo ya Mbulu watatambua kwamba ukiitisha watu wa Mbulu kuwatangazia mpango wa maendeleo ya ujensi wa shule karibu wanaume wote watakuja na fimbo zao ndefu tu. Mgeni kama ukisema "walikuwa na fimbo nyingi" utakuwa sahihi.

Nina uhakika kulikuwa na watu wengi waliokuwa na kamera kule, basi tuonesheni angalau picha ya moja ya mtu aliyebeba panga.

Huu ni mfano wa picha ambayo inaweza kuletwa toka Tarime. Hii ilipigwa Kenya baada ya vurugu za uchaguzi. HIvyo wale waandishi waliokuwa kule Tarime walete picha ambayo inaonesha Mbowe angalau anafukuzwa na mapanga na mikuki hadi kwenye gari; hiyo itathibitisha maneno yao na mjadala utafungwa. Mwenye picha aiweke hapa JF anakomwa nyani giledi! NI picha tu ndiyo itakata ngebe za Chadema.

r214082_828024.jpg

mzee mwanakijiji haya mambo ya kuteteatetea yatakuvunjia heshma yako ya miaka mingi..naona si lazima kuzungumza kwa kila topic inayoletwa humu ..sometimes unaweza kusoma na kuacha kuandika kwa kuipuuzia na itaishia yenyewe kwa kuendelea kubishabisha na kupinga unaifanya issue hii izidi kuwa kubwa na kuipatia hoja hii umaarufu ambao unajaribu kuuzima ila nasikitika kuwa unaongeza discussion tu.
ubarikiwe.
 
Alafu humu ndani watu wanasema jamaa hana sifa ya kuwa jasusi na paspoti yake inaonyesha alienda Libya siku 4 tu... mi napenda kujua kwanza uwezekano kwa yeye kuwa na paspoti zaidi ya moja, maana ninavyofahamu usalama wa taifa kokote duniani wapo wa aina tofauti. Wapo wale wanaotumia majina yao na huwa wanakuwa tu na vyeo mbalimbali kuwawezesha kusafiri. Alafu wapo wale ambao ni faceless na nameless na wanabadili majina, muonekano wao n.k. Hao ni maoperatives. Sasa Mallya anaweza kuwa operative. Hao wanaojifanya wanamjua Mallya watoe hapa CV yake, ni mchagga kweli? Alizaliwa wapi? Alisoma wapi? Ana qualification gani mpaka alisafiri na mufti na wabunge? Wengine tunajua usalama wa taifa wa kwetu wanajifanya wanamichezo, PR afisa msaidizi, n.k. alomuradi wajichanganye katika msafara. Mi sijawa-convinced that this guy is clean.
 
Mongoiwe asante kwa picha!

Sasa mjadala huu ujadiliwe kwa picha na wala si kwa kusikia! Na hao (CHADEMA/ CCM na TBC/ Wahariri) na wao waonyeshe picha za huko Tarime ili tuweze kuhoji?

Tukae tukijua hakuna kipimo sahihi (SI Unit) cha vurugu! Maana tukisema tumsikilize Zitto/ Mrema/ Lipumba/ Machibya kila mmoja ana kipimo chake cha kusema hii ni vurugu au la.

Kwenye picha za Mongoiwe haswa ile ya mwisho hali inaonekana ilikuwa si shwari (lakini si vurugu)!

Mwenye picha na aweke, na tuendee kujadili picha na wala si kauri za watu! Mpaka sasa panga sijaona, nimeona rungu moja kwenye picha ya mwisho!
 
Tusim under rate Deus Malya maana hatujajua kwa kina sura yake ya pili hasa katika hizi ajali za Nairobi na Dodoma.Majajusi hawajitangazi kazi zao hufanyika sirini( secret society).

Hapo Tanzania Visiwani(Pemba) alitokea kijana mdogo kama Deus aitwaye Ahmed Khalfan Ghailan na akafanikisha kulipua ubalozi wa Marekani Tanzania na hata alipokuja kukamatwa kule Pakistan haikuwa rahisi maana polisi tena wa nchi kama Pakstani walipambana naye kwa masaa 14 ndipo akasalimu amri.

Ukiwauliza wazazi wa ghailan wanakwambia kijana alikuwa mwema na msikiti kwa sana na alikuwa mtulivu.

Huyu Deus achunguzwe kwa kina ni mtu wa aina gani?
 
Hivi akina mbatia na lipumba wana inteligence agency iliytowawezesha kujua habari hizi zote za mallya?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom