Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Samahani natoka kidogo kwenye mada kuu but along the line....

Kama kuna mtu alitazama Mahojiano kati ya Tido na Asha R Migiro TBC1 ijumaa saa tatu usiku. Walisema it was the live program.....! Was it so?

Kama ukifutilia vizuri na kwa makini...some of the discussion zilishatoka kabla kama sehemu ya maandalizi ya matangazo kwa ajili ..ya Kipindi hicho....If I am right....kwa nini....Walituambia...ni live brodcasting..? wakati kulikuwa na some portion..very clear..tulikuwa tumezisikia kabla...Why all that?

Tulitakiwa kupiga simu...kuongeana na Asha if we wanted....but hawakutoa namba...etc ..Kama ingekuwa live ..hahisi wangetoa namba pale pale kwenye screeen yao...why?

Bwana mmojatu alipiga simu....kutoka tarime...kitukama hicho ...ni kweli ilikuwa live? ....Why?

My concern is tulidanganywa ..? And why?

Kama siko sahihi..Basi Nielimishwe what realy took place...!
 
hakuna kitu cha hatari kwenye jamii wakati vyombo vya habari vinakuwa vimefungamana na watawala. Ni rahisi sana kumanipulate the masses.
 
Mkamap, naona na wewe umeamua kuingia kwenye kundi la wakandiaji wa JF lakini haushi kushinda hapa. Na nilikuambia tangu mwanzo kabisa kama JF ni ya Mbowe au Chadema na haiko huru hivyo na unailinganisha na magazeti ya propaganda kwanini wewe usiwe ni mmoja wa wanufaika wa huyo Mbowe ila kinyume tu? Kama siyo, kwanini uko hapa usiende au kuanzisha jukwaa huru ambalo utatuhakikishia halina maslahi na Mbowe?


Nyie hamuheshimu UHURU wa mawazo ya Mtu ,mtu akitofautiana nanyi mnamwita ni fisadi na ametumwa na RA ,Nyie mkihusishwa na kitu kiduchu mwaja juu. Mimi siumii kuhusishwa na RA kwa sababu najua si kweli lakini anayeumia ukweli unakua umemgusa.

Siende kwenye mtandao HURU mpaka huu mtandao usio HURU utakapokamilika na kua HURU .Mfano Siwezi kwenda kuwapa matajiri utajiri ila nitakwenda kuwapa masikini utajiri Ama siwezi kuenda uingereza kufundisha namna ya demokrasia na uhuru pia haki za mwanadamu Ila nitaenda TZ kufanya hivyo,Na ndio maana YESU alisema hakuja kwa wema bali wenye dhambi.
Mwanakijiji MIMI ndio maana nipo hapa ktk chombo kisicho huru.
 
Nakubaliana na MkamaP, mnampa sifa za bure RA, yaani kila kitu RA. Hata fisadi ana haki yake hapa duniani. Tumshambulie RA kwenye scandals ambazo anahusika kama EPA lakini kweli hata mauaji ya Wangwe tunamwingiza RA?

Ndio maana wengine hatusomi magazeti ya wanasiasa. Sioni tofauti kati ya RAI na Tanzania Daima inavyokuja kuandika mambo ya siasa. Yote ni magazeti ya propaganda. Sorry kwa mnaosoma, ila mimi sisomi mambo ya siasa kwenye hayo magazeti.

Ile statement ya Mnyika kwa mkuu wa polisi ilikuwa ndio mwanzo wa kuingiza siasa kwenye kifo cha Wangwe. Wengine pia walivyoona, wakaingia kwa styles zao. Haikuwa muhimu kwa wakati ule ilipotolewa.

Ifike mahali tukubaliane uchunguzi huru umefanyika na matokeo yake wote tunatakiwa kuyaheshimu. Kama mtu ana ushahidi tofauti basi aulete au aupeleke kwa waandishi wa habari na polisi, vinginevyo tunajaza bytes bure kwenye JF.
 
Mimi naamini kifo cha WANGWE ni cha ajali lakini tatizo huyu fisadi RA anataka kutake advantage ionekane kuwa CHADEMA wamehusika ndio maana anahonga media ili ionekane hivyo

Mkamap wewe unaishushia hadhi JF nafikiri Kiranja na MKJJ wamekujibu
 
Mkamap ,kuna mambo unapaswa kuyaelewa kwanza hapa, ni kuwa kilichomsukuma Rostam kukutana na wahariri wa magazeti na kuandika habari za kupikwa kilikuwa kitu gani?

Kwa nini alifikia hatua ile?alikuwa anataka kuficha kitu gani?

Ajali ilipotokea alikuwa Nje ya Nchi ila akarudi usiku uleule tena kwa kutafuta ndege kwa nguvu kubwa sana hapo alipokuwa , nini kilimsukuma kufanya vile?

Ukiweza kupata majibu unaweza ukaelewa kinachoongelewa hapa .


Hata Mbowe naye alikua NJE.Ni nini kilimfanya Mbowe ahairishe mikutano yake Afrika kusini??
 
Kabla Amina Chifupa hajafariki hapa JF kuna watu walishatabiri na ikatokea kweli, the matter of fact hata kifo cha Balali, kilishatabiriwa mapema hapa, halafu ninaomba nikuhakikishie kuwa nimewahi kuongea sana watoto wa Mwaikambo, Kolimba, na Kombe, niliyoyapata ni Kolimba peke yake ndiye aliyefariki kifo cha Mungu, kwa ugonjwa aliokuwa nao, kwa sababu kila siku ya Mungu, alikuwa akifuatana na mtoto wake aliyekuwa akimshikia dawa zake maalum za moyo, alipoitwa kwenye kikao maalum cha CC, mtoto wake hakuruhusiwa kuingia, akaamua kwenda kupumzika hotelini ndilo hasa kosa lilopelekea baba yake kufa, kwa sababu alipoanza kuumwa, wakanza kumtafuta huyu kijana, by the time wamekuja kugundua kuwa yupo hotel, it was too late, na besides kaka yake Kolimba alihusishwa kwa 100% na uchunguzi wa mwili wa ndugu yake na kuridhika na kila step kuwa hakukuwa na faulo, Lakini sio vifo vya hao wengine wawili ninam-challenge kiongozi yoyote wa taifa bongo anayeamini kuwa hawakuuliwa kwa makusudi, tuzichambue facts chini,

[/B]

Mkuu FMES,

Nimecheka kweli kweli hiyo ya Kolimba. Naamini hapa tuna madaktari, si ajabu na wao wanacheka kama mimi. Sikujua siku hizi kuna dawa ya ugonjwa wa moyo inafanya kazi kama dawa ya kisukari kwi kwi kwi!!!!!

Huu mjadala mimi nimejitoa kuchangia, ila hii ya mbeba dawa pembeni imenichekesha mno, sikuweza kujizuia tena.
 
Nyie hamuheshimu UHURU wa mawazo ya Mtu ,mtu akitofautiana nanyi mnamwita ni fisadi na ametumwa na RA ,Nyie mkihusishwa na kitu kiduchu mwaja juu. Mimi siumii kuhusishwa na RA kwa sababu na si sahihi lakini anayeumia ukweli unakua umemgusa.

Siende kwenye mtandao HURU mpaka huu mtandao usio UHURU utakapokamilika na kua HURU .Mfano Siwezi kwenda kuwapa matajiri utajiri ila nitakwenda kuwapa masikini utajiri Ama siwezi kuenda uingereza kufundisha namna ya demokrasia na uhuru pia haki za mwanadamu Ila nitaenda TZ kufanya hivyo,Na ndio maana YESU alisema hakuja kwa wema bali wenye dhambi.
Mwanakijiji MIMI ndio maana nipo hapa ktk chombo kisicho huru.

Siyo suala la Uhuru wa mawazo; unapotoa madai yako ambayo hayana uthibitisho ndio unaleta uhuru kwenye chombo kisicho huru? Hivi wewe umefurahi na kukubali jinsi magazeti yalivyoandika kuhusu Mbowe na JF ikiweka rekodi straight basi inamtetea Mbowe na hivyo basi ni mali yake au ana maslahi?

Hivi kweli unataka kudai JF haiko huru? Unataka kusema Mtanzania, Majira, na wenzao ni vyombo huru kuliko JF? Maana ukiniuliza mimi kama wewe ni mpigania uhuru kweli ungeenda mahali ambapo hakuna uhuru. Ila kama una maana JF haiko huru na majira na ndugu zangu ndiyo vyombo huru basi nimekuelewa. Endeleza mapambano.
 
kitu kingine nilicho notice kwenye hilo gari ni kwamba upande mmoja umebondeka sana, kuliko upande mwingine, iwapo gari lilipinduka mara tano, ni upi uwezekano wa upande mmoja kubonyea mno, na mwingine ubonyee kidogo?
 
Hata Mbowe naye alikua NJE.Ni nini kilimfanya Mbowe ahairishe mikutano yake Afrika kusini??

Mkamap, hizi ndio statements zinazokufanya credibility yako hapa JF ishuke.

Halafu unapenda mno kutoa sweeping statements zenye uswahiliuswahili mwingi ndani, km, JF ni ya Mbowe, Chadema wanahusika, etc. Simple and careless statements kama hizi tumezizoea kutoka kwa akina Kada, Nungwi na hivi karibuni Mgagaiko, ambao hawa tumeshawajua na tunawaelewa.

Sasa mtu kama wewe unapojiingiza pia kutoa statements simple and loose kama hizi lazima watu waje juu kwa sababu sio tu kwamba zinashusha hadhi yako lakini pia zinatishia credibility ya JF!

Watu wakikushupalia hapa usipate shida; ni kwamba wanakuchukulia kwa umakini mkubwa na wanatishwa na kasi ya kuporomoka kwa umakini wako!
 
Huo mkono wa RA utafika kote lakini JF hawezi

...never say never!, ...it is 'Cancerous'! ...unapokuja kutahayari ishaenea kote 'mwilini'. BTW, uliona kikatuni cha masudi Kipanya majuzi?
 
Siyo suala la Uhuru wa mawazo; unapotoa madai yako ambayo hayana uthibitisho ndio unaleta uhuru kwenye chombo kisicho huru? Hivi wewe umefurahi na kukubali jinsi magazeti yalivyoandika kuhusu Mbowe na JF ikiweka rekodi straight basi inamtetea Mbowe na hivyo basi ni mali yake au ana maslahi?

Hivi kweli unataka kudai JF haiko huru? Unataka kusema Mtanzania, Majira, na wenzao ni vyombo huru kuliko JF? Maana ukiniuliza mimi kama wewe ni mpigania uhuru kweli ungeenda mahali ambapo hakuna uhuru. Ila kama una maana JF haiko huru na majira na ndugu zangu ndiyo vyombo huru basi nimekuelewa. Endeleza mapambano.


Hata madai ya kuhusishwa RA ktk Habari hizo ama kuhusishwa RA kuwa ni mwajiri wangu nayo hayana uthibitisho na mnayaacha yapite free.

Lakini mimi nikikuhusisha wewe na Mbowe waja juu.Hapo ndipo unaona hakuna UHURU humu ndani.Na lazima kuhakikisha kila taasisi ya MTZ inakua huru,Hiyo ni moja ya wajibu wangu.

Ama UHURU uliomo humu mtu yeyote akipinga maada zenu lazima awe wa RA na anayehusishwa na MBOWE basi uhuru unakua umeingiliwa??
 
Nimekupata mkuu, mimi sio dakitari wala sina idea kabisa kuhusu haya magonjwa, lakini ninajua for fact kuwa yuela kijana alikwua akifuatana na baba yake akiwa akiwa na hizo dawa, inaweza kwua zilikuwa dawa za something else, lakini viongozi wengi walithibitisha kuwa sio mara moja wala mbili Kolimba aliwahi kuzidiwa wakiwa kwenye shughuli zao siasa, na huyu kijana akatoa hizo dawa, kama zilikuwa za moyo au kisukari siwezi ku-argue maana sijui lolote lakini ndivyo kijana alivyonithibitishia,

Na niaamini zaidi kwa sababu, aliyekuwa katibu wa Kolimba akiwa msaidizi wa Sokoine, aliwahi kuhamishiwa ofisi moja na ndugu yangu mmoja, naye nikaamuuliza vipi Kolimba na hii ishu, akanihakikishia kuwa ni kweli mara kwa mara alipokuwa akimfanyia kazi alikuwa na hayo matatizo na huyu mtoto wake alikuwa mara nyingi ndiye anakuja na hizo dawa,

Kama ni za moyo au za kisukari sina uhakika, na wala siwezi ku-argue on that, kwa kweli Tanzania tumeona mengi sana mkuu ndio maana imani na serikali inatoweka, kwa mfano kuna wakati Kawawa alikuwa na hawara mmoja kwenye ofisi moja ya shirika la umma mjini, yaani Bima, siku moja watu wa uwt walimfuata yule kijana na kumtisha sana kuwa aaache, yeye akaleta ubishi kama wetu wa hapa sometimes, hivi mkuu unajua kuwa siku moja walimchukua yule kijana wa kichagga na kumpeleka kizuizini for the next three years, siku moja wakamuachia tu bila sababu, kijana alihama kabisa mijini Dar na kurudi kwao mpaka leo, sasa mambo kama haya ukiyasema utaonekana kuwa unachochea uongo, lakini ni fact na watu waliona kwa macho yao, na kijana yupo pia!

Kwa hiyo mkuu JF ni kuchambua ukweli na kuacha uongo, serikali ndiyo imetufikisha hapa tulipo na besides, ni demokrasia makini anyways kuuliza ukweli wa kila neno la serikali. Unajua mkuu toka nianze kuongea na viongozi wa serikali kuhusu hii JF, sijawahi kumsikia hata mmoja wapo akisema kuwa hap[a pana habari za uongo, ila ninwasikia wakiuliza hizi habari huwa tunazipata wapi maana zingine ni nzito mno?




Ahsante Mkuu!
 
Ile statement ya Mnyika kwa mkuu wa polisi ilikuwa ndio mwanzo wa kuingiza siasa kwenye kifo cha Wangwe. Wengine pia walivyoona, wakaingia kwa styles zao. Haikuwa muhimu kwa wakati ule ilipotolewa.
Huyu Mnyika huwa anaandka statement zake akiwa bar nini?......kila kitu siasa inaingia hata kwenye masuala ya kitaalamu....
 
Mkuu FMES,

Nimecheka kweli kweli hiyo ya Kolimba. Naamini hapa tuna madaktari, si ajabu na wao wanacheka kama mimi. Sikujua siku hizi kuna dawa ya ugonjwa wa moyo inafanya kazi kama dawa ya kisukari kwi kwi kwi!!!!!

Huu mjadala mimi nimejitoa kuchangia, ila hii ya mbeba dawa pembeni imenichekesha mno, sikuweza kujizuia tena.

Mtanzania,

Yani huku sina mbavu hata kidogo na hiyo narration yake. Kolimba alijua dawa zake za kufa na kupona kashika mtoto halafu akakubali mtoto asiruhusiwe kuingia nae ndani.....mtoto akaenda hotelini na kifurushi cha dawa baba akafa....ha ha hahahahah....can't beat that one....

You know what, kama nia yake ni kutu entertain basi kiwanda chake cha dataz kina put out a good product, kisifungwe. Ni kwamba wengine tulikuwa hatujapata user manual ya product zake. Kumbe dataz zake sio za ku-inform. We're on the same page now.
 
Nasikitika kuona kwa miaka yooote bado watanzania hawajatambua kuwa CCM ni mafia na mabingwa wa propaganda (siasa za uongo)....

Ntumaini waliosoma habari za hazeti la HOJA waligundua hilo
 
Mkamap, hizi ndio statements zinazokufanya credibility yako hapa JF ishuke.

Halafu unapenda mno kutoa sweeping statements zenye uswahiliuswahili mwingi ndani, km, JF ni ya Mbowe, Chadema wanahusika, etc. Simple and careless statements kama hizi tumezizoea kutoka kwa akina Kada, Nungwi na hivi karibuni Mgagaiko, ambao hawa tumeshawajua na tunawaelewa.

Sasa mtu kama wewe unapojiingiza pia kutoa statements simple and loose kama hizi lazima watu waje juu kwa sababu sio tu kwamba zinashusha hadhi yako lakini pia zinatishia credibility ya JF!

Watu wakikushupalia hapa usipate shida; ni kwamba wanakuchukulia kwa umakini mkubwa na wanatishwa na kasi ya kuporomoka kwa umakini wako!

Ni SWEEPING statements lakini zina ujumbe mkuu bila hekima ni ngumu kuuona na zinamaana gani.

Ngoja nitafasiri hizo statement maana zitachanganya wengi.

Mbowe alirudi kutoka safari yake ni kutokana na moyo wa binadamu na mtu anayemfahamu kwa karibu na wamefanya kazi pamoja ,Vivyo hivyo RA naye alirudi ktk Msiba wa rafiki yake na mtu anayemfahamu na wamefanya kazi kwa pamoja Bungeni ni watu wanaofahamiana kwa karibu .

Huyo mwenye sweeping statements na zisizo na mantiki ni yule anayeona kurudi kwa RA yakwamba alipopata habari RIP kafariki hapo hapo RA wazo likaingia kama computer vile na kutafuta ndege ya fasta ili aje na a plan na kuitekeleza mipango ndani ya masaa kadhaa.

Sweeping statements ndizo yawezekana zikawa hazionekani na zikaonekana statement zenye mantiki kua ni sweeping.

Sishangai sana maana ni tabia yetu wengi mtu anayesema nipeni URAIS nitawajengea mabomba ya maziwa na barabara angani kuonekana mkweli .Na yule anayesema nipeni URAIS tutafanya kazi kwa nguvu na tutaongeza masa ya kufanya kazi ili tujiimalishe anaonekana mwongo na mzushi.
 
1.
na hata JF Very Senior members ambao mara nyingi kutokana na utashi na ushawishi mkubwa credibility ya 'source of info' na posting 'zao/zetu/zenu' zinaaminiwa na wengi.

2.
2. Originally Posted by Kuhani

Mtaje!

Si "unakoma nyani giladi," na umeshataja wengi wakubwa. Mtaje!
Waziri aliyekwambia ametoka kudanganya Bunge nani ? Usipotaja ni udaku!


3.
3. Mtanzania,

Yani huku sina mbavu hata kidogo na hiyo narration yake. Kolimba alijua dawa zake za kufa na kupona kashika mtoto halafu akakubali mtoto asiruhusiwe kuingia nae ndani.....mtoto akaenda hotelini na kifurushi cha dawa baba akafa....ha ha hahahahah....can't beat that one.... You know what, kama nia yake ni kutu entertain basi kiwanda chake cha dataz kina put out a good product, kisifungwe. Ni kwamba wengine tulikuwa hatujapata user manual ya product zake. Kumbe dataz zake sio za ku-inform. We're on the same page now.

Mkuu heshima yako, nilijua kuwa nimekukamata pabaya na ujanja wako wako mwingi, sasa hizi ndio akili zako nyingi ambazo sasa karibu watu wote hapa wameanza kuzielewa ukishikwa pabaya basi ni unageuka kinyonga unabadili rangi na kuwa nyoka, najua ulifikiri utaweza kui-control hii forum na hiyo janja yako lakini unajua kuwa kwangu umekwama!

Kwa taarifa yako tu ni kwamba viongozi wa CCM kwa niaba ya CCM waliiomba radhi rasmi familia ya Kolimba kwa kitendo cha kumkatalia mtoto wake asiingie kwenye kile kikao, na hata kum-offer ndugu yake kugombea ubunge wa ndugu yake,
Naona unateseka sana na dataz zangu, maana unajaribu sana kui-control hii forum, kwa kutuchezea vichwa watu hapa lakini ni mimi peke yangu ndiye ninakukwamisha, na ninakuhakikishia kuwa as long as nipo hapa, utabadilika na ukinyonga wako mapaka uwe kufutu, lakini nipo nyuma yako bro, mpaka kieleweke!
 
kitu kingine nilicho notice kwenye hilo gari ni kwamba upande mmoja umebondeka sana, kuliko upande mwingine, iwapo gari lilipinduka mara tano, ni upi uwezekano wa upande mmoja kubonyea mno, na mwingine ubonyee kidogo?

...Lakini amini nakwaambia kuwa ingawa facts zinaonesha hivyo lakini bado kuna mijitu itaendelea kutuhadaisha kuwa gari ilipinduka-pinduka...
Hata mie nilijiuliza iweje gari iliyobiringita mara kadhaa isibonyee roof yote sana sana one side imebonyea as if iliangukiwa na kitu kizito???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom