Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Naona mkuu unazungumza utani katika swala ambalo lingehatarisha maisha ya watanzania, hasa TARIME. Hapa hakuna swala la kuvutiangozi kwake au la.JE WATU WA TARIME WANASEMAJE UTUELEZE? KAMA USIPOWEZA UNAWEZAJE KUPATA TAARIFA??

HIVI TAARIFA KUANDIKWA NA MTU MMOJA, WOTE WAKIFANYA MAKOSA SAWA, NUKTA,KOMA SAWA HAIKUINGII AKILINI? TENA VIKIWA NA WAMILIKI TOFAUTI WAKITUMIA MAJINA TOFAUTI.

MIMI SIDHANI KUWA KUNA SWALA LA MWAMBA NGOMA HUJIVUTIA KWAKE.

KITU GANI KITAKUFANYA UAMINI KUWA TANZANIA DAIMA WALIANDIKA HABARI YA KWELI? NA JE NI KITU GANI NA UNA UTHIBITISHO GANI KUELEZA KUWA UNA WASIWASI NA TANZANIA DAIMA-MKUU NASUBURI MAJIBU

''Suspicion is a mental picture seen through an imaginary keyhole"

Mkuu habari yako.
Kwanza kabisa japo utakua mdadisi habari nyingi ktk vyombo vingi kama ni msomaji wa magazeti mengi tofauti utakubaliana na mimi waandishi hawa ndio tabia yao ya KUDESA tangu siku nyingi.

mimi nimsomaji wa gazeti la nationmedia mzuri la kenya na kunawakati unakuta magazeti ya TZ yame copy na ku peste habari nzima kama ilivyo na kunakipindi hua wana copy BBC na kupest kama ilivyo. Ni tabia yao tena ya siku nyingi kama unauwezo fuatilia sehemu habari ambayo ilikua moto harafu yafuatilie magazeti hayo utakuta habari na maneno ni yaleyale.

Tatizo yawezekana vyombo vya habari huwa hawatumi wawakirishi wao na kutegemea kutoka kwa mwandishi mmoja ama wawili ama waandishi hawajiamini wamezoea KUDESA.

Kama hizi habari RA ndio kazipika basi RA kwa miono yenu ndio kamuua chacha na si kama wataalamu walivyosema.
Kama RA hakumuua chacha haiwezekani ndani ya masaa kadhaa awe ameandaa mkakati na kuutekeleza mara moja .

Siamini Tanzania daima habari yake kuhusu mbowe maana Mbowe ni la kwake .Na wewe nikuulize swali Je unaamini habari zinazoandikwa na kuhusus Rostam Azizi na magazeti yake? naomba jibu.
 
Ndio maana mimi habari zangu zote nasoma JF huku kuna habari za kweli
Ingawa kuna watu wa RA lakini habari tunazihariri baada ya majadaliano ya members lakini huko kwenye magazeti,TV,Radio waandishi wanakusanya habari zao then wanampelekea MHARIRI ambaye yeye anaamua niki kitoke .
Hakuna cha MAJIRA,NIPASHE,MTANZANIA,HABARI LEO,TANZANIA DAIMA,UHURU,MWANANCHI wote MAKANJANJA TU
 
JF mkono wa RA hauwezi kufika kwa sababu JF ni mkono wa Mbowe.

Kweli kumbe watu wa RA mko wengi but JF hatununuliki awe MBOWE,RA,EL
Nenda kamwambie aliyekutuma ataishia huko kwenye magazeti,redio na TV but JF mwambie asahau
 
Huko Dodoma naambiwa kuwa TBC wanaaibika sana kwani imebidi fundi mitambo wao aweke vifaa kwenye hema na studio imekuwa ni kwenye hema huko Bungeni kutokana na kuwa gari lao ama studio yao OB VAN haijawasili ikiwa inatokea Tarime ilikoenda kufuatilia na bila mafanikio ya kile ambacho walifikiri wataweza kukirusha kilikposhindikana sasa wameweka hema na vifaa vyao vipo hapo ndio studio.

Tido mhando angalia hao mtandao watakumaliza muda sio mrefu.

hapo ndipo kukosa ufanisi wa kazi! huku Tido akiwa amelewa mvinyo wa siasa!
 
Wamnabodi mtanisamehe nakurudisheni nyuma kidogo, siku ya jana Ijumaa nilikuwa nimeshikwa sana hivyo sikupata muda wa kuptia hapa..Naomba majibu ya mkato nisiwachukulie muda wenu maadam niweze kufuatilia hoja zinazofuata. Ama naomba nielekezwe mapi nitapata majibu niyasome kwa muda wangu.. Tafadhali wakuu naomba kuuliza;-
1. Je. kimetokea nini baada ya uchunguzi wa pili wa maiti maana nilipoacha juzi ni kwamba daktari kutoka Kenya alikataliwa, akapendekezwa Mtanzania..
2. Je, ni kitu gani kimemuua wangwe - cause of death.
Kama ni ajali ni sehemu gani ya mwili iliyosababisha kifo hicho..Nikiwa na maana kiungo gani hasa kilichokuwa chanzo cha kifo..
3. Gari lilifikaje huko maporini? maanake nimeona picha za gari lenyewe matairi yote yapo na moja tu la nyuma upande wa Abiria ndio limepungua upepo.. Ni kitu gani kilichosababisha gari lile kupinduka sijui mara ngapi!..

Na kama sio ajali ni kitu gani kilitokea? alipigwa risasi, alikabwa pumzi, sumu, madawa ya kulevya, Alipigwa rungu la kichwa, au kitu gani kulingana na upepelez kwa sababu kuuawa sio lazima iwe kwa risasi tu.
Daktari ni lazima aseme kitu kilichomuua hata kama ana majeraha mwili mzima kuna kitu kimoja dicho kimekuwa fatal kumwondoa.. ni kipi hicho?
 
kwa kuharibika huku kwa gari na muonekano huyo huyu deus kaponaje...???? mtu aliedangaya kuwa yeye ni invisible wa JF af kapona kwny ajali hiyo,,, nabaki na mshangao kiasi kikubwa
 
Kweli kumbe watu wa RA mko wengi but JF hatununuliki awe MBOWE,RA,EL
Nenda kamwambie aliyekutuma ataishia huko kwenye magazeti,redio na TV but JF mwambie asahau

Na watu wa Mbowe mpo wengi kweli tena kumbe kale ka Ruzuku kanakoishia makao makuu kanafanya kazi hii.

Mshaulini mfadhili wenu akipanue chama hadi vijijini na atapata majimbo mengi na Ruzuku itaongezeka na mtatuletea forums nyingine na malipo yenu yataongezeka.
Maana mkiwa na forums nyingi mtajigawa vizuri hamtarundikanana sehemu moja.
 
Mkama,
Naomba ujiheshimu, wewe unatoka musoma, tena naomba usitudharirishe hata kidogo watu wa mara, najua una hila ndani yako, kisha fikiri kabla ya kusema, na haya unayotulisha unataka tuyasadiki? sisi wakurya tunao upeo wa kuelewa na ndiyo maana siku zote sisi ni wana mageuzi

Naomba uchunge kauli yako, Umesikia?
 
Mkama,
Naomba ujiheshimu, wewe unatoka musoma, tena naomba usitudharirishe hata kidogo watu wa mara, najua una hila ndani yako, kisha fikiri kabla ya kusema, na haya unayotulisha unataka tuyasadiki? sisi wakurya tunao upeo wa kuelewa na ndiyo maana siku zote sisi ni wana mageuzi

Naomba uchunge kauli yako, Umesikia?

MWITA

MWANA WASU
Hila ipi hiyo? Ibainishe nitakubali majibu ama kuyapinga.
 
na hata JF Very Senior members ambao mara nyingi kutokana na utashi na ushawishi mkubwa credibility ya 'source of info' na posting 'zao/zetu/zenu' zinaaminiwa na wengi.

Mkuu Heshima yako, sina uhakika kama ninakuelewa vizuri lakini unaonekana kukimbia kivuli cha serikali yao, au chako mwenyewe either kwa sababu hujui historia au unajua ila umeamua kuikwepa, JF tuna sifa moja kubwa sana mbele ya jamii na hasa kwa viongozi karibu wote wa juu, nayo ni accuracy ya information zetu,

Ninajua kua wananchi wengi hapa hamlijui hili kwa sababu viongozi hao hawajaja hapa na kusema wazi, lakini kwa wale wachache ambao tuna access nao tunajua fika kuwa hata wao hapa ni mahali muhimu sana pa kupata habari zilizochambuliwa, ndio maana ukiona tunag'aka na habari fulani ujue kuna something tunajua, kwa mfano kwenye kifo cha Balali, viongozi wetu walikuwa wakisema kwa public kuwa amefariki katika hospitali ya Boston, ukweli ukawekwa hapa kuwa hakuwepo huko,

Sasa cha ajabu ni kwamba viongozi wale wale waliokuwa wanalihakikishia taifa kuwa amefariki, walikuwa wakitafuta watu hapa kuwathibitishia kama ni kweli, serikali yetu haikuwa inajua kuwa Balali alikua na permanent resident permit ya kuishi US, ukweli ni kwamba kuna kiongozi mmoja mkubwa sana kutoka Zanzibar, ambaye nilimfahamisha dakika ya mwisho anataka kuingia kwenye kikao cha NEC Butiama, ikabidi arekebishe hotuba yake na kunishukuru sana,

Kabla Amina Chifupa hajafariki hapa JF kuna watu walishatabiri na ikatokea kweli, the matter of fact hata kifo cha Balali, kilishatabiriwa mapema hapa, halafu ninaomba nikuhakikishie kuwa nimewahi kuongea sana watoto wa Mwaikambo, Kolimba, na Kombe, niliyoyapata ni Kolimba peke yake ndiye aliyefariki kifo cha Mungu, kwa ugonjwa aliokuwa nao, kwa sababu kila siku ya Mungu, alikuwa akifuatana na mtoto wake aliyekuwa akimshikia dawa zake maalum za moyo, alipoitwa kwenye kikao maalum cha CC, mtoto wake hakuruhusiwa kuingia, akaamua kwenda kupumzika hotelini ndilo hasa kosa lilopelekea baba yake kufa, kwa sababu alipoanza kuumwa, wakanza kumtafuta huyu kijana, by the time wamekuja kugundua kuwa yupo hotel, it was too late, na besides kaka yake Kolimba alihusishwa kwa 100% na uchunguzi wa mwili wa ndugu yake na kuridhika na kila step kuwa hakukuwa na faulo, Lakini sio vifo vya hao wengine wawili ninam-challenge kiongozi yoyote wa taifa bongo anayeamini kuwa hawakuuliwa kwa makusudi, tuzichambue facts chini,

Kama una tatizo na habari za uchochezi, basi wakaripie magazeti wanaolipwa na viongozi sometimes kuandika ukanjanja, halafu kwa nini usimlaumu Tido Mhando, kwa kuwadanganya wananchi na taifa letu kwa ujumla kuwa polls za BBC zinaonyesha kuwa Mtandao ndio wanaotakiwa kutawala, ni info kama zile ndio zinaweza kuleta maafa kwa taifa, looking at waht is going on now na uongozi wa Tanzania,

JF huwa tunachambua ishus kwa kutumia ushahidi mbali mbali ambao unakubalika kwa siasa za online, na siku zote huwa tuko wazi kujibu maswali yanayohusu hoja zetu hapa, huenda hufahamu kuwa kuna watu hapa ambao huwa wanaulizwa maswali mazito sana na serikali kulingana na ishus za hapa, tena kila siku ya Mungu, na serikali huwa inajibiwa na kuelewa, kwa hiyo mkuu mimi sipendi kuzunguka mbuyu, ni mmoja wa Senoir Expert hapa na JF na huwa niko mstari wa mbele sana kwenye kuchambua ishus na ku-speculate kwa kutumia ushahidi wa ground zero na wa online, na ninaomba nirudie kuwa mpaka nitakapopata majibu ya maswali mawili ndio nitaamini kuwa ile ilikwa ni ajali tu:-

1. Mallya alitokaje kwenye lile gari bila kuchubuka wala tone la damu.

2. Lile gari exactly lilipata ile ajali wapi? Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma na pale ajali ilipotokea ninapajua vizuri sana, hakuna mawe wala vyuma vya kuweza kuiumiza ile gari kiasi kile, na wala lile gari halikugonga jiwe wala vyuma vizito, sasa ni nini hasa kilichojiri na tena kulikoni mpaka gari kuwa noma kiasi kile?


So far nimewauliza karibu viongozi wengi wanaohusika na handling ya hii ajali hakuna mwenye jibu, kama unalo ninaliomba mkuu na nitaacha hapo hapo kuchangia tena hii ishu,

Otherwise A luta Continua!

Ahsante Mkuu.
 
MWITA

MWANA WASU
Hila ipi hiyo? Ibainishe nitakubali majibu ama kuyapinga.

Mkama najua una mapenzi na nchi yako, ila inakuweje kuwatetea hawa mafisadi? unataka mafisadi washinde ili watuaminishe kuwa kifo cha Wangwe kina mkono wa mtu?
 
Field Marshall Es,
1. Mallya alitokaje kwenye lile gari bila kuchubuka wala tone la damu.
Heee heee! mkuu nasikia acha tone la damu, nasikia hata nguo zake zilikuwa safiii matone ya hapa na pale, shati jeupeeeee!

Mkuu najua wewe una dataz naomba unieleze yaliyoajiri hadi sasa hivi..kusema kweli nipo kizani hasa baada ya kukaa nje jana nzima.
 
Je, kuna uwezekano CCM ilihusika katika hili ili kuisambaratisha zaidi CHADEMA? Pia badala ya habari za mafisadi na JK na serikali yake kutokuwa na uwezo wa kuiongoza nchi kutawala katika vyombo vyetu vya habari vikiwemo magazeti, TV na Redio, zitawale habari za 'kuuwawa" kwa Wangwe?
 

... kuna siku ninakumbuka nilikuwa bunegni wakati bado likwa Dar, nikaona waziri wa fedha akipigana na maswali ya wabunge mpaka anataka kulia machozi kuwa anayosema kwenye bajeti yake ni sawa kabisa ila wabunge wako wrong,

Alipomaliza tu, behind the scene nikamuuliza duh! ile leo ilikuwa kazi waziri kubwa sana maana nimekuona ukisimama kidete mkuu? Akanijibu, kijana kwani unafiriki ni kweli yale niliyokuwa ninasema? Yatakuwaje kweli wakati hotuba yenyewe ni ile ile ya mwaka juzi ila zimebadilishwa namba tu!

Mtaje!

Si "unakoma nyani giladi," na umeshataja wengi wakubwa. Mtaje!

Waziri aliyekwambia ametoka kudanganya Bunge nani ?

Usipotaja ni udaku!
 
Kuna siri kubwa zaidi hapa kwani ,kuna mazungumzo yalifanyika kati ya Marehemu Wangwe na viongozi wa ngazi za juu wa Chama na Serikali sasa ,tuendelee kufuatilia kwa kina , kuna taarifa pia kuwa Wangwe alikuwa anawarekodi kila alipokutana nao kwa faragha .

Sasa kama ni hivyo kuna tishio kubwa zaidi,ya jinsi tunavyoweza kufikiri, ila kwa kuwa haya maji wengiine tumeamua kuyavulia nguo basi hatuna budi kuyaoga nami nipo tayari kuyaoga.

Tuendelee kufuatilia ila kwa tahadhari kubwa.
 
Mkama najua una mapenzi na nchi yako, ila inakuweje kuwatetea hawa mafisadi? unataka mafisadi washinde ili watuaminishe kuwa kifo cha Wangwe kina mkono wa mtu?

Hapana mkuu
Ila kuna watu ndio wanataka kutuaminisha kua RIP CHACHA kauliwa na RA,kama unasoma katikati ya mistari.

Mwanzo wa post zangu kabisa nilisema mallya naye achunguzwe kama ajali majeruhi aliyoyapata ni ndani ama nje ya ajali la gari.

Na msisitizo nikaweka kama ajali imetokea nje ya gari basi lazima maeneo yote shukiwa yachunguzwe na pakuanzia ni CHADEMA.Sasa hapa watu wananishambulia nikuniita wa HILA kwa sababu tu nimesema CHADEMA nayo ichunguzwe.Wao walitegemea niseme maeneo ya kuchunguzwa ni RA,CCM na BARRICK ili wafurahie nyoyo zao.

Mimi nimekubaliana kabisa na UCHUNGUZI ya kwamba RIP kafa kwa ajali ya gari ila hao wanaohususha habari zilizotoka na RA ndio hao ambao hawakubali kua kafa kwa ajali badala yake wanatuambia RA kamuua CHACHA.Maana kwa akili nyepesi kabisa ajali imetokea RA yeye ni Genius kiasi gani? ndani ya masaa machache awe amepanga mipango na kuitekeleza.

Nikasema hizo habari zilizoandikwa ni kweli mtu mmoja kaandika lakini hiyo nitabia ya waandishi wetu na wasomi wetu kwa ku DESA.Kipi kipya ? hapo .

RA ni fisadi Lakini naamini hana Akili kiasi hicho na si kila kosa kwa vile yeye ni fisadi basi tumbebeshe mzigo.
MAFISADI SUGU ni watanzania weusi waliosomeshwa na serikali masikini ya TZ wao wamejificha wanatumia bomba la RA.Tukiwapata hao ufisadi utakoma mara moja RA nikama moshi tu ila moto wenyewe ni Watanzania weusi ,tikiwazima hawa ndio ufisadi utakoma.
 
Mkamap, naona na wewe umeamua kuingia kwenye kundi la wakandiaji wa JF lakini haushi kushinda hapa. Na nilikuambia tangu mwanzo kabisa kama JF ni ya Mbowe au Chadema na haiko huru hivyo na unailinganisha na magazeti ya propaganda kwanini wewe usiwe ni mmoja wa wanufaika wa huyo Mbowe ila kinyume tu? Kama siyo, kwanini uko hapa usiende au kuanzisha jukwaa huru ambalo utatuhakikishia halina maslahi na Mbowe?
 
Mkamap ,kuna mambo unapaswa kuyaelewa kwanza hapa, ni kuwa kilichomsukuma Rostam kukutana na wahariri wa magazeti na kuandika habari za kupikwa kilikuwa kitu gani?

Kwa nini alifikia hatua ile?alikuwa anataka kuficha kitu gani?

Ajali ilipotokea alikuwa Nje ya Nchi ila akarudi usiku uleule tena kwa kutafuta ndege kwa nguvu kubwa sana hapo alipokuwa , nini kilimsukuma kufanya vile?

Ukiweza kupata majibu unaweza ukaelewa kinachoongelewa hapa .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom