UCHUNGUZI WATHIBITISHA
Wangwe: Siyo risasi
*Uchunguzi wathibitisha jeraha lake ni la ajali
*Waonyesha alipasuka fuvu, ubongo ulimwagika
*Profesa Wangwe asikitishwa na habari za uzushi
*Akana Mbowe kuokolewa, kunusurika mapanga
*Zitto Kabwe aziita taarifa hizo kuwa za kizushi
Na Joseph Senga, Tarime
HATIMAYE mazishi ya Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (Chadema) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari, Jumatatu wiki hii, yamefanyika jana baada ya matokeo ya uchunguzi uliofanyika kutangazwa.
Mazishi hayo ambayo awali yalikuwa yafanyike juzi, yalikwama baada ya wanafamilia kutaka ufanyike uchunguzi mwingine huru kutokana na kuwapo kwa utata katika mazingira yaliyosababisha kifo cha mbunge huyo.
Uamuzi huo wa wanafamilia kutaka kufanyika kwa uchunguzi huo, ulikwenda sambamba na kuibuka kwa hali ya wasiwasi na kutishia kuibuka kwa vurugu katika Kijiji cha Kemakerere.
Akitangaza matokeo ya uchunguzi huo jana, mbele ya wananchi waliofurika, Profesa Samuel Wangwe ambaye ni kaka wa marehemu, alisema uchunguzi huo ulifanywa na daktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye hata hivyo hakutajwa kwa sababu za kiusalama.
Profesa Wangwe alisema uchunguzi huo uliofanyika kwa zaidi ya saa mbili, ulibainisha kuwa, ajali ilisababisha mdogo wake apasuke fuvu la kichwa kutokana na kujigonga kwa juu na kisha ubongo ukamwagika sambamba na taya kuvunjika.
Uchunguzi huo ulioanza jana asubuhi majira ya saa 5:15, ulifanyika chini ya uwakilishi wa wanafamilia watatu, Jeshi la Polisi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyekiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Profesa Wangwe aliwaeleza wananchi waliokuwa wakimsikiliza kwamba, yeye na wanafamilia wenzake walikuwa wamekubaliana na kuridhishwa na taarifa hiyo ya uchunguzi, na hivyo kukubali kumzika ndugu yao.
Mbali ya hilo, alisema daktari alikuwa akitarajia kuiwasilisha taarifa kamili ya maandishi ya uchunguzi alioufanya akiambatanisha na picha zilizopigwa.
Baada ya taarifa hiyo ya uchunguzi iliyotolewa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime ulikofanyika, safari ya kwenda Kemokerere kwa ajili ya mazishi ilianza.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa Tarime waliitaka familia hiyo kuahirisha mazishi hadi leo, ili kuwapa fursa watu wengine ambao walikuwa wameshaondoka kuhudhuria, ombi ambalo hata hivyo halikukubaliwa na wanafamilia.
Mwili wa marehemu ulipofika nyumbani kwake, shughuli za mazishi zilianza kwa salamu za rambirambi kutolewa kwanza na umoja wa vyama vya upinzani vinavyoshirikiana na Chadema; NCCR Mageuzi, TLP na CUF.
Akizungumza kwa niaba ya vyama hivyo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema aliwataka wananchi wa Tarime kushikamana na kuendeleza mema yote aliyoyatenda marehemu Wangwe wakati wa uhai wake.
Mbali ya kutoa ubani wa shilingi 300,000 Mrema aliwataka kuanza kuangalia wanachama kutoka katika kambi hiyo ya upinzani ili kumtafuta mtu atakayerithi mikoba ya ubunge ya Wangwe.
Wengine waliotoa salamu za rambirambi ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Luteni Kanali mstaafu, Issa Machibya aliyetoa ubani wa shilingi 100,000 na kilo 50 za mchele kusaidia shughuli za msiba.
Ibada ya mazishi ya Wangwe iliendeshwa kwa mahubiri ya Kikristo na Nancy Msafiri na ikahudhuriwa na wananchi wa Tarime, viongozi wa kisiasa, ndugu, jamaa, marafiki, watoto na wake watatu wa marehemu waliojulikana kwa majina ya Gati, Dotto na Mariam.
Jeneza la marehemu Wangwe lilianza kuteremshwa kaburini saa 11:50 jioni.
Awali, muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchunguzi jana, Profesa Wangwe alizungumza na wanahabari na akaeleza kusikitishwa kwa familia yao na taarifa za uzushi zilizoripotiwa katika vyombo kadhaa vya habari juzi na jana, kuhusu hali ya usalama wakati wa msiba huo.
Profesa Wangwe alisema yeye na wanafamilia wenzake, walikuwa wamesikitishwa na taarifa zilizokuwa zikidai kwamba, kulikuwa na kikundi cha watu wenye mapanga waliokuwa wakimuwinda Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbali ya hilo, Profesa Wangwe alieleza kushangazwa kwake na taarifa alizozielezea kuwa zisizo sahihi, zilizokuwa zikidai kuwa Mbowe alilazimika kuondolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa polisi ili kumnusuru na mapanga hayo.
'‘Hakuna mapanga yaliyokuwa pale, wala hakukuwa na vurugu za kutumia silaha na wala Mwenyekiti wa Chadema Mbowe (Freeman) hakuondolewa chini ya ulinzi wa polisi," alisema Wangwe huku akiyataja baadhi ya magazeti (si Tanzania Daima) ambayo yaliandika taarifa hizo.
Akifafanua, Profesa Wangwe alisema, Mbowe aliondolewa uwanjani hapo juzi akiwa na viongozi wengine wa juu wa kiserikali na kisiasa kutokana na ushauri uliotolewa na Mkuu wa Mkoa baada ya mabishano kuhusu uhalali wa kumzika marehemu ulipoibuka.
Hata hivyo, taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata baadaye juzi jioni na jana kutoka Musoma na Tarime zinaonyesha kwamba, kulikuwa na kikundi maalum kilichokuwa kimeandaliwa kwa malengo ya kisiasa na watu wasiojulikana, kwa lengo la kumdhuru Mbowe.
Wakati Mbowe akiwasili katika Kijiji cha Kemakorere hiyo juzi, hali ilikuwa ni tofauti kwani alilakiwa na vijana wa Chadema ambao walimuongoza hadi katika jukwaa kuu.
Katika hali ambayo si rahisi kuielezea, pamoja na Mbowe kuwasili na kuondoka uwanjani hapo salama, tena pasipo kusindikizwa na polisi, vyombo kadhaa vya habari vilianza kuripoti kuhusu kunusurika kwake kwa mapanga hata kufikia hatua ya kuokolewa na polisi.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Zitto alizielezea taarifa hizo za mwenyekiti wake kunusurika kuwa ni za uzushi uliokuwa umeandaliwa kwa malengo ya kisiasa na kwa nia ambayo haikuwa nzuri.
'‘Huku hakukuwa na kinachoitwa vurugu, wala hakukuwa na hali ya hatari dhidi ya mwenyekiti. Kuna propaganda kali inasambazwa kuwa mwenyekiti kaokolewa na polisi. Hizi ni taarifa za uongo," alisema Zitto alipoulizwa kuhusu nini kilikuwa kimetokea.
Akizungumza na Tanzania Daima kutoka Musoma jana, Mbowe pasipo kutaka kuingia kwa undani, alieleza kusikitishwa na taarifa hizo na akasema baada ya kufanya mashauriano na washauri wake na viongozi wengine wa chama hicho, alikuwa ameamua kurejea Dar es Salaam.
Freeman Mbowe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
Freeman Aikaeli Mbowe (born 14 September 1961) is a Tanzanian politician and chairman of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA – Party for Democracy and Development). Mbowe is a member of the Chaga ethnic group.
Mbowe CampaigningMbowe was elected to the National Assembly in 2000 representing Hai Constituency (Kilimanjaro Region). He won 64.5% of the vote, which was the highest percentage of votes won among constituencies with opposition MP's.
In preparation for the 2005 elections, Mbowe was nominated as CHADEMA's presidential candidate. Jumbe Rajab Jumbe, a Zanzibari was chosen as his vice-presidential candidate. The election was originally scheduled for 30 October 2005, but was postponed until 14 December due to the death of Jumbe.
Mbowe and Komu CampaigningMbowe criticized the lengthy postponement, saying a week's delay would have sufficed and that his party cannot afford to finance extra campaigning. Chadema eventually settled on Anna Komu to be the running mate.
He placed third out of ten candidates in the 14 December 2005 presidential election, winning 5.88% of the vote.
Mbowe is the owner of Club Bilicanas, one of the best nightclubs in Dar es Salaam. He is also the owner of Tanzania Daima, a national daily newspaper, as well as Protea Hotel Aishi Machame, a hotel in his native town of Machame, in Kilimanjaro region, Tanzania.
Mbowe is married to Lillian Mtei (daughter of Edwin Mtei, the first Governor of Bank of Tanzania). They were married on 17 August 1991. The two live happily with their children in Mikocheni A, a suburb of Dar es Salaam, Tanzania. Mbowe has three children: Dudley A. Mbowe (15), Nicole A. Mbowe (11) and Dennis E. Mbowe (8). All their children go the Dar es Salaam Independent School (D.I.S.), also in Mikocheni.