Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mimi siku hizi mbona siipati kabisa KLH News? Kulikoni....nimepewa indefinite ban nini? I miss podomatic...ile ilikuwa haina mizengwe....
 
MP Wangwe`s burial put on hold

2008-08-01 10:49:29
By Bigambo Jeje, PST, Tarime


Arrangements for the burial of Tarime legislator Chacha Zakayo Wangwe (52) were shelved yesterday following demands by members of his family for a police report with full details on the cause of his death.

Family spokesman Prof. Samwel Wangwe, who is also the late MP’s elder brother, revealed that clan members had met a few hours before the scheduled burial time and decided that a family doctor should examine the body to certify the cause of the death.

The decision followed suspicions that the opposition Chadema MP sustained bullet wounds and had not actually died in a car accident as officially reported.

``As clan members, we have unanimously resolved to put his burial on hold until our family doctor arrives from Dar es Salaam and conducts a thorough examination of the body and issues an official report on his death,`` said Prof. Wangwe.

The professor explained that a second medical examination by a medical expert in whom family members had full confidence was of fundamental importance ``because the family has no faith in the first medical report that suggests that he died in a road accident``.

The family members also called on the police to ``interrogate very closely`` Deus Mallya, the person said to have been with the legislator at the time of the said accident.


Habari hizi zatatanisha hasa maelezo ya huyo Mallya kwamba kabla ya ajali kutokea alikuwa akisinzia na aliambiwa na marehemu akae kiti cha nyuma ili ajipumzishe.
Sasa kama gurudumu la gari lilipasuka basi Mallya lazima alisikia mlipuko. Kama kuna risasi ilipigwa garini lazima Mallya alisikia mlipuko wa bastola au bunduki.
Mallya lazima aeleze kinaganaga kwamba gari hiyo ilikuwa na abiria wangapi yeye tu au kulikuwa na mtu au watu wengine na ni kina nani?

Gari kama limechunguzwa kutaoenekana masalio ya risasi kama bastola ilitumika. lLakini kwa upande mwengine tujiulize kama marehemu alikuwa anayo bastola ameivaa kwapani. Kama hivyo basi huweza ilifyatuka wakati wa ajali.
LAKINI TUKUBALIANE KWAMBA KILA KITU,KILA KIUMBE AMBACHO KIMEUMBWA NA MUNGU KITAKUFA.
WAKATI MWINGINE HATUWEZI KUELEZA KIFO KIMEYOLEAJE.

KILICHOBAKIA NI KUMUOBEA MAREHEMU AWEKWE MAHALI PEMA.
 
Hold on a minute... huyu kijana alihusika na ajali nyingine nairobi (sources zinasema hivyo) ambapo gari ilichakaa nyang'anyang'a hadi kulazimu kukatwa ili kumtoa; hata hivyo alitoka mzima kama alivyotoka kwenye hii nyingine. Just that you should know.
 
Hold on a minute... huyu kijana alihusika na ajali nyingine nairobi (sources zinasema hivyo) ambapo gari ilichakaa nyang'anyang'a hadi kulazimu kukatwa ili kumtoa; hata hivyo alitoka mzima kama alivyotoka kwenye hii nyingine. Just that you should know.

Basi mwenzetu huyu ana upendeleo maalumu kutoka kwa "Bwana"!
 
Hivi Hizi Romours Kuwa Marehe Chacha Wangwe Amekuwa Murdered Zinatoka Wapi Na What Is The Reason Behind People To Speculate Like That, Sielewi Kwa Nini Watu Wanashindwa Kuamini Kuwa Ajili Huwa Zinatokea Na Baadhi Ya Watu Wanapona Na Wengine Kupoteza Maisha!

Siku Hizi Kumekua Na Hulka Mtu Yoyote Maarufu Akifariki Kunakuwa Na Rumours Nyingi Juu Ya Kifo Chake, Jamaa Ya Watanzania Imeanza Kujengwa Na Hofu Na Kutoaminiana, Kitu Ambacho Kinaweza Kuleta Maafa Makubwa Sana.

Tafadhali Wana Forum Wenzangu Naomba Ufafanuzi Wa Kina Kwa Wale Wote Wanao Speculate Kuwa The Guy Was Assassinated Or Something?

Let Us Be Realist!

Watu huwa wanauawa kimitindo, EXECUTIVE, na ku speculate sio vibaya.

The thing is, nadharia zilizoletwa so far - TLP na NCCR wameua ili wapate kiti, au CCM wameua ili kuwagombanisha CHADEMA, n.k - zote ni, well, ngoja nisema tu nyepesi nyepesi, japo kuna namna sahihi zaidi ya kuzi describe kwa jinsi ambayo inaweza kuwakatisha watu tamaa wakaacha kujaribu kuleta nadharia nyingine na shinikizo kwa officials, halafu tukazika marehemu kumbe ana risasi kichwani.
 
Basi mwenzetu huyu ana upendeleo maalumu kutoka kwa "Bwana"!

Acha hizo usimuingize kabisa Mungu kwenye uuwaji na ujangili na unyama huu!

Si mapenzi ya Mungu Wangwe AFE..Unless PROVEN OTHERWISE.

Na wewe Mkumbo kama ni chadema ni heri uache propaganda sasa hivi...Sitokubali hadi Munieleze ni kivipi wakibosho ni wasaliti kwasababu ya Sina na Deus Mallya...Na pia unieleze usafi huo unaouzungumzia wa chadema tukianzia na EPA.

HUYU DOGO SI ALIKUWA ANA PRINT MAMBO YA BOTH ccm na chadema KAMA ALIVYOKUWA WANGWE AKIDEAL NA ISSUES?

MKUMBO TUNAOMBA UREKEBISHE KAULI ZAKO NA UTOWE MCHANGO AMBAO HAUTAJAZA THREAD HAPA...SEMENI KAMA UHUSIANO WENU UKO VIPI NA HUYO GAIDI DEUS...TENA INAWEZEKANA UMESHAWAHI KUKUTANA NAYE...TAFADHALI USISEME DEUS NI ANA UPENDELEO KUTOKA KWA BWANA....SEMA ANA UPENDELEO KUTOKA ccm na chadema.
TUNATAKA MGOMBEA HURU!
 
Hold on a minute... huyu kijana alihusika na ajali nyingine nairobi (sources zinasema hivyo) ambapo gari ilichakaa nyang'anyang'a hadi kulazimu kukatwa ili kumtoa; hata hivyo alitoka mzima kama alivyotoka kwenye hii nyingine. Just that you should know.

Atakuwa Ninja!!!!!!
 
watu Huwa Wanauawa Kimitindo, Executive, Na Ku Speculate Sio Vibaya.

The Thing Is, Nadharia Zilizoletwa So Far - Tlp Na Nccr Wameua Ili Wapate Kiti, Au Ccm Wameua Ili Kuwagombanisha Chadema, N.k - Zote Ni, Well, Ngoja Nisema Tu Nyepesi Nyepesi, Japo Kuna Namna Sahihi Zaidi Ya Kuzi Describe Kwa Jinsi Ambayo Inaweza Kuwakatisha Watu Tamaa Wakaacha Kujaribu Kuleta Nadharia Nyingine Na Shinikizo Kwa Officials, Halafu Tukazika Marehemu Kumbe Ana Risasi Kichwani.

Nadharia Ni Epa Na Wewe Usianze Ubishi Wako Wa Nature Usiolenga Point.
Nadharia Hapa Ni Epa...mrema Hana Kashfa Ya Epa Msilete Umamluki Wenu Hapa...mrema Yuko Kwenye Listi Ya Wazalendo Na Ni Yeye Peke Yake Wa Kusafisha Nchi..wengine Kanyaboya Kwa Sana Tu.
 
Hatimaye Chacha Wangwe azikwa kwao Tarime
Frederick Katulanda, Tarime


Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe ambaye kifo chake kimezua utatanishi, hatimaye amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwao Kimakorere baada ya familia kuridhika na uchunguzi uliofanyika na daktari wao.


Wangwe alizikwa jana majira ya saa 12:00 jioni huku kukiwa na hali tata, wakati baadhi ya ndugu wakigoma na wengine kukubali.


Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa nchini ambao pia walikuwapo katika uchunguzi uliofanyika kabla.


Akizungumza kabla ya mazishi kwa niaba ya familia muda mfupi baada ya kutoka ndani ya chumba cha uchunguzi, Prof Samwel Wangwe alisema jana kuwa uchunguzi walioutaka familia umekamilika na kwamba sasa wameridhika kuwa mbunge huyo alikufa kwa ajali na si vinginevyo.


Prof Wangwe alisema kutokana na kuridhika na uchunguzi huo, sasa wameamua kufanya mazishi ya marehemu huyo nyumbani kwake na kusema kuwa taarifa kamili itatolewa na daktari baada ya kukamilika na kukabidhiwa jeshi la polisi.


"Baada ya uzushi mwingi tuliamua kama familia kufanya uchunguzi ambao umefanyika leo. Ingawa taarifa kamili itaandikwa na daktari sisi tunasema tumeridhika kuwa marehemu alikufa kwa ajali na sasa tunakwenda kuzika," alieleza.


Uchunguzi huo ambao ulifanywa katika hospitali ya Wilaya ya Tarime kuanzia saa 5: 27 hadi 9:40, ulimuhusisha daktari wa serikali Charles Shija kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, maofisa wa Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Mbunge Zitto Kabwe kwa niaba ya Chadema na daktari wa familia ambaye mpaka sasa familia imesema haitamtangaza.


Hata hivyo Zitto alichelewa kufika hospitali na kukuta uchunguzi umeanza lakini baadaye aliruhusiwa kuingia baada ya kuruhusiwa na maofisa wa Jeshi la Polisi.


Majira ya saa 9: 42 Zito alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya chumba hicho na kuzungumza na waandishi wa habari kuwa kwa niaba ya chama chake kwamba ameridhika na uchunguzi huo.


"Mimi kwa niaba ya chama changu ambacho nilikuwa nawakilisha, nimeridhika na uchunguzi huo" alisema Zitto.


Awali Samson Chacha toka Tarime aliripoti kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani walijikusanya katika hospitali hiyo wakisubiria taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu Wangwe.


Waliokuwapo ni Augustino Mrema wa TLP, Joseph Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, ambao walisema hawawezi kuondoka kabla ya mazishi ya mpiganaji mwenzao huyo.


Profesa Lipumba aliwaomba wananchi na wafiwa kuwa na msikamamo wasiyumbishwe na baadhi ya wanasiasa wanaotaka kusambaratisha vyama vya upinzani kupitia kifo cha shujaa huyo kwani ukweli utabainika tu.

Haya ma- Spin Doctor tuleteeni spinning nyingine ...
 
Haya ma- Spin Doctor tuleteeni spinning nyingine ...

Masatu, ni kitu kimoja kukubali matokeo ya uchunguzi wa mwili, na kingine kabisa kuchunguza chanzo cha ajali. kwa sababu haikuonekana risasi basi kifo cha Wangwe ni cha kawaida na ajali yake ni ya kawaida? Walichochunguza kwenye mweli ni ajali na wakaweza kuielezea kuwa ni ya kawaida; au walikuwa wanachunguza nini?

Kwa sababu ninaamini aliyeleta hoja ya "risasi" kuwa kapigwa risasi amefanikiwa kuyumbusha mjadala kwa sababu kama walijua hakuna risasi, basi watu wataamini kuwa hakuuawa kwa risasi; je waliangalia sumu? je waliangalia ajali yenyewe ilivyotokea? Je kutokukuta risasi ina maana hakuuawa?

No sir, walichojaribu ni kuspin mjadala tu, lakini kesho tunawarudishia wao squarely.
 
Masatu, kwanini unafikiri kwa sababu haikuonekana risasi basi kifo cha Wangwe ni cha kawaida na ajali yake ni ya kawaida? Walichochunguza kwenye mweli ni ajali na wakaweza kuielezea kuwa ni ya kawaida; au walikuwa wanachunguza nini?

Kwa sababu ninaamini aliyeleta hoja ya "risasi" kuwa kapigwa risasi amefanikiwa kuyumbusha mjadala kwa sababu kama walijua hakuna risasi, basi watu wataamini kuwa hakuuawa kwa risasi; je waliangalia sumu? je waliangalia ajali yenyewe ilivyotokea? Je kutokukuta risasi ina maana hakuuawa?

No sir, walichojaribu ni kuspin mjadala tu, lakini kesho tunawarudishia wao squarely.

Mkuu rekebisha kauli yake hakuna mahala nimesema nafikiri kwa kuwa hawakuona risasi then hajauawa.

Nimeweka bandiko hapo juu linalo wakariri msemaji wa familia Prof Wangwe na mwakilishi wa Chadema Mh Zitto wakisema kutokana na uchunguzi "wanaridhika" kuwa amekufa kwa ajali ya kawaida na si vinginevyo!
 
Masatu, kwanini unafikiri kwa sababu haikuonekana risasi basi kifo cha Wangwe ni cha kawaida na ajali yake ni ya kawaida? Walichochunguza kwenye mweli ni ajali na wakaweza kuielezea kuwa ni ya kawaida; au walikuwa wanachunguza nini?

Kwa sababu ninaamini aliyeleta hoja ya "risasi" kuwa kapigwa risasi amefanikiwa kuyumbusha mjadala kwa sababu kama walijua hakuna risasi, basi watu wataamini kuwa hakuuawa kwa risasi; je waliangalia sumu? je waliangalia ajali yenyewe ilivyotokea? Je kutokukuta risasi ina maana hakuuawa?

No sir, walichojaribu ni kuspin mjadala tu, lakini kesho tunawarudishia wao squarely.

MKJJ...Watu wengine kukaa pembeni kwa tuhuma za ukabila pia kulipelekea kina mgagagigikoko wakitumia nafasi hiyo kupenyeza chuki!
Na mimi nimeshasema watanzania SINA HAMU NA WABONGO KABISA!
Na kwa kweli kwa style hii UKOMBOZI NI NDOTO...NO WONDER WATU WANARUDI ccm NA UFISADI UNAPAMBA MOTO...Kina Mwinyi na Mkapa walisema nikachukia na kuwaona hawana UBINADAMU..Lakini kwa kusema ukweli sisi NI WANAFIKI KAMA MAFISI!
Yani ukiwa mpambanaji unafanywa uonekane MVUTA BANGI MPENDA VURUGU KAMA ILIVYOFANYIKA KWA MAREHEMU...Kumbe UKIWA HAI UNADHARAULIKA HADI UFE!

Ndio maana ninasema chadema wasithubutu kusema huyu jamaa ni mpiganaji na wakati alikuwa akipigana nao pia!

ccm nao hawawezi kufanya hivyo...Mtu mwenye legacy ya kupambana na ccm na mamluki wa upinzani ni MREMA PEKE YAKE!

Huyo kwasasa ndiyo APEWE ULINZI!

Halafu hata ukifa hakuna mabadiliko unakuwa umekufa KIBUDU!

HUU NI UPUUZI!

TOKA KINA LOWASSA WAPOKELEWE NA KINA CHENGE NILIGUNDUWA KUWA SI KWELI TAZANIA NI MOJA TENA!

Na sasa kuna wahuni na MAFIA ambao wametayarishwa na MAFISADI kujidai wao ni wakurya wenye kudai haki ya Wangwe kuuwawa na wachagga...Kwanza kama ingekuwa ni haki watu hao wangekamatwa mara moja!

Na ccm wamekuwa wakitawala kimafia kwa kupenyeza mapandikizi yao UPINZANI NA KUUWA DEMOKRASIA

NB:Kama marehemu alipigwa risasi...Basi amepigwa risasi na wataalam..Na wa kulaumiwa ingekuwa serikali iliyotowa kauli ya kwanza...Kwani kama risasi ilimpata mwilini...Kabla ya ku conclude any possibilities za risasi...Wao hufanya vipimo vya GUN POWDER..ILI KUONA KAMA KULIKUWA NA BULLET...Kwenye nguo ya marehemu...Kwenye mwili wake nk.
Gari lingefanyiwa uchunguzi...Kwani kama awali ilionekana ni planting.
Lakini kama FAMILIA WAMEKUBALI KWA PAMOJA BILA KUDAI ALIUWAWA NA WACHAGGA...Basi hatuwezi kuingilia mambo ya familia na huo utakuwa UNAFIKI...Hivyo kwasasa baada ya kauli hizo za serikali na chadema...Naonelea nisubiri kuangalia kama UKABILA UTAENDELEA KUPEWA NAFASI KWA KUWATUMIA MAFISADI AMBAO SASA WANAONGOZA NCHI.
 
Nimechelewa sana kwenye kikao hiki; inawezekana nimeshakosa mengi.

(a) Unajua ni hiyo hiyo familia ya merehemu ndiyo walioanzisha huu wasiwasi kuwa mwili wa marehemu ulipigwa risasi mbili shingoni zikitokea mdomoni na tumboni. Kama sasa wameridhika kuwa hakuna risasi kabisa, basi na mimi moyo wangu umetulia sasa kwa vile nilikuwa nimeshapandwa na hasira sana niliposikia taarifa hiyo ya risasi. Kwa sasa turudi tulikoanzia kuwa ile ilikuwa ni ajali kama zilivyo nyingine, tuendelee kuiombea roho ya marehemu ipumzike kwa amani huko peponi.

(b) Kinachobaki ni kuchunguza mazingira ya ajali kama ilivyo kawaida ya ajali nyinginbe zote. Kwa wanaofahamu, je muhtasari huu hapa chini ndiyo timeline sahihi kuhusu muda wa mwisho wa uhai wa marehemu? Kama ni sahihi, basi mwanaye Zakaria pamoja na rafikiye Mallya wanajua mengi kuhusiana na mazingira ya ajali hiyo; wakihojiwa sawasawa wanaweza kutoa habari nyingi zitakazosaidia katika kuelewa chanzo cha ajali ile.

Hapa tunawaletea dondoo chache za siku ya kifo chake ambayo ni Jumatatu, Julai 28, 2008, ambacho kimsingi kimeacha maswali mengi kuliko majibu.
Saa 12 asubuhi
Anaamka na kutaka kwenda kuoga lakini anashindwa, hivyo inawalazimu watoto wake kumpelekea maji bafuni. Hii ni kutokana na hali yake kutokuwa nzuri kwa muda wa siku tatu.
Saa 2:10
Wangwe anaingia katika Jengo la Bunge na kumuuliza Naibu Spika, Anna Makinda kama atapata nafasi ya kuwasilisha hoja yake binafsi. Makinda anamuomba amsubiri Spika wa Bunge, Samuel Sitta kwani yeye ndiye anayeweza kumpa muda wa kuwasilisha.
Saa 8 mchana
Anarudi katika makazi yake Dodoma na kumwambia mtoto wake Zakaria Chacha (18) kwamba ameshindwa kuwasilisha hoja yake binafsi, hivyo ameamua kusitisha ili aweze kuendelea na shughuli nyingine.

Mwanaye anampa maji anakunywa lakini hayamezi, ikabidi achukue vidonge na kumnywesha, alimeza kisha akala matunda na kuamua kwenda kulala huku akitaka aamshwe majira ya jioni.

Saa 11 jioni
Anaamshwa na kuiambia familia yake anakwenda Dar es Salaam kwenye mazishi ya Bhoke Munanka.
Saa 12 jioni
Anaanza safari ya kwenda Dar es Salaam akifuatana na rafiki yake Deus Mallya, lakini wakati yuko safarini maofisa wa Bunge wanahaha kumsaka katika eneo lote la Bunge ili aje awasilishe hoja yake binafsi lakini jitihada za kumpata zinashindikana.

Saa 12.10 jioni
Anaipigia simu familia yake na kuwaambia analazimika kurejea Dodoma kwani walipofika eneo la Ihumwa gari yao ilipata matatizo hivyo inabidi arudi mjini ili kulipeleka gereji liweze kutengenezwa.

Saa 12.30 jioni
Baada ya gari lao kutengemaa anapitia nyumbani kwake ili kuchukua chaja ya simu aliyokuwa ameisahau, huku gari likiwa linaendeshwa na rafiki yake.
Saa 1 usiku
Safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza, huku akipanga kulala Morogoro mjini kwani alihofu wataingia usiku sana ili kesho yake alfajiri waanze tena safari ya kuelekea jijini humo.

Saa 2.55 usiku
Chacha Wangwe anafariki baada ya gari linalodaiwa alikuwa akiliendesha kupinduka zaidi ya mara tano ikiwa ni baada ya kuserereka umbali wa mita 50 kutoka barabarani.
 
Mkuu rekebisha kauli yake hakuna mahala nimesema nafikiri kwa kuwa hawakuona risasi then hajauawa.

Nimeweka bandiko hapo juu linalo wakariri msemaji wa familia Prof Wangwe na mwakilishi wa Chadema Mh Zitto wakisema kutokana na uchunguzi "wanaridhika" kuwa amekufa kwa ajali ya kawaida na si vinginevyo!

nimekupata vizuri, kwa hiyo kitakachosemwa chochote baada ya kauli hizo ni spin. Got you.
 
Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa hakuna risasi (uchunguzi wa Dodoma); Ndipo baadaye rumors za risasi zilipoanzishwa na kutiliwa mkazo na kutumia watu kadhaa kudai mwili ufanyiwe uchunguzi mwingine na serikali kuridhia pasipo shaka wakijua hakuna cha risasi. Uchunguzi wa pili ulipoonesha kuwa hakukuwa na dalili ya risasi kutumika basi umewafanya watu waamini kuwa mchezo mchafu haukuchezwa.

Waliobadili hoja toka kwenye ajali kwenda kwenye risasi kwa kweli wamefanikiwa kubadili mjadala. Waliofanikiwa kubadili hoja toka kwa Malya kwenda kwa Mbowe nao walifanikiwa sana; na kwa sababu hiyo, tukubali tu kama tulivyokubali vifo vingine huko nyuma, na kama tutakavyokubali vifo vingine huko mbele.

Ni vizuri kuanzia sasa kuja na sera inayokataza uchunguzi wa vifo vyenye utata. Tukubali yaishe.
 
Kichuguu...Watu wangeacha madharau na kuweka maanani mchango wa wengine..Basi mambo yasingekuwa hivyo....Kwasababu toka mwanzo niliwaambia wale waliokuwa wakileta UKABILA...Nilwaambia kuwa ni MUHIMU HICHO ALICHOKUWA AKIWAKILISHA KAMA HOA BINAFSI KITUPIWE MACHO!
Nilimwomba MKJJ lakini na yeye hana...Ni majukumu yetu kujuwa hayo.
Halafu kama Deus alikuwa kwenye nyumba ya marehemu wakati wote huo..Basi alishamwekea sumu na kama angekufa kwa sumu basi ingeonekana ni ccm..Wakampa kijana jina la kichagga haraka haraka wakaenda kumpandikiza kwenye mauwaji hayo na kujifanya ni mtoto mwema na dereva...Tena hata urafiki gaidi hilo likajenga na watoto wa marehemu!
Kweli sijui!
Haya....TAIFA LIRUDI PAMOJA TULIPONYE...HAKUNA NJIA...LA SIVYO KUTATOKEA MAPIGANO NA HATUTAKI.
Spika na yeye aliagwa na anajuwa hoja yake ndio maana alilia sana...Tatizo ni kama akiombwa kopi ya hoja hiyo...Hawawezi kuitowa na hata familia haiwezi kuitowa na hiyo kwa mara nyingine...RIP RASTA WANGWE!
 
Daktari wa familia alisema ni risasi ndugu awatangazia kuwa kuna alama za risasi wataita daktari maalum anaehusika kutoka kenya,daktari kutoka Kenya akataliwa ,Wandugu hawataki kumtaja daktari wa familia ,Zitto atangaza ni ajali , Na wandugu wautanganzia umma kama ni ajali ya kawaida.
Je daktari wa familia anaweza kutoa upinzani ,na kama yamekwisha ,sawa kwani wengi wetu si watu tuliokuwepo au tulioona tuukubali ukweli kuwa Marehemu amekufa kwa ajali ,ila tukumbuke jambo moja kwa sisi tuliokuwepo hai kuwa ukweli siku zote utakuja juu tu ,na uongozi huu tuliokuwa nao sio utakaokuwepo kesho kwa maana hiyo ,siku ukweli ukichomoza na watakaokuwa hai wakaulizwa basi sheria zitafuata mkondo wake kwa kila aliehusika kwa mauaji haya na yaliopita,kama tunavyoona walioshiriki viota vya Hitler wanapandishwa kizimbani ,wauaji wa Bosnia wanapandishwa kizimbani na mauaji yanayotokea tanzania kama yatakuwa na ukweli utakaokuja juu basi ,naamini wahusika watatiwa mikononi leo wana nguvu na jeuri lakini kuna siku nao watakuwa pembeni na wenye nguvu kuwa wengine.Hilo waliweke akilini ,hakuna lisilo kuwa na mwisho.
 
Ni vizuri kuanzia sasa kuja na sera inayokataza uchunguzi wa vifo vyenye utata. Tukubali yaishe.

Square that with this:

Kama kuna wakati ambapo uchunguzi huru kweli unahitajika ni kwenye hiki kifo cha Mhe. Wangwe. Hakuna kitu kitakachosemwa na serikali au taasisi ambacho watu watakikumbatia na kukubali na bila ya shaka vitakavyosemwa na familia au jamaa zake na Chadema nacho kitakuwa na utata. Nimeandika kwa urefu "utata" huo kwenye gazeti la kesho, na kwa makini sijahusisha suala la risasi hata kidogo kwa sababu siamini kuwa ilikuwa ni risasi. Walipogeuza kuwa ni suala la risasi wamebadilisha mjadala kabisa kwa sababu kwa makosa watu wanaweza kuhitimisha kuwa "no bullet, no assassination" kitu ambacho kinaweza kuwa kosa kubwa sana.

Suala la madai ya kifo cha risasi ni kupoteza lengo sana; Tangu juzi nimeitisha kuwa kuna haja ya Kikosi cha Scotland Yard kuitwa kufanya uchunguzi huru kwani uchunguzi wa serikali si huru na ule wa familia si huru kwani vyote viwili vimeangalia mwili kitu ambacho kinafanywa katika ajali nyingi.

Suala zima ni mazingira ya safari na ajali yenyewe kwani kufanya kitu kibaya kwa mtu siyo lazima utumie risasi.

Kuhusisha kifo hiki na CCM au Chadema ni kosa kubwa na kwa yeyote anayesoma maandishi yangu sijaelekeza tuhuma kwa Chama chochote kile au mtu isipokuwa kuonesha utata uliopo na ya kuwa ufunguo wa utata huo Malya na ushahidi uliopo.

Naamini kama wabunge wa CCM na wa Upinzani na viongozi wao wakiungana kuitisha NSY waje kufanya uchunguzi kama walivyoitwa kwenye kifo cha Ouko, Bhutto, au hivi karibuni huko Antigua naamini ndio njia pekee ya kuonesha ukweli na kuondoa utata.

Yule ambaye hatotaka NSY kuja na kupewa ushirikiano wote mara moja; huyu ndiye nitamshuku. Sasa nani atakuwa wa kwanza kuitisha kwa NSY na hana kitu cha kuficha na yuko tayari NSY kufanya uchunguzi wote na yeye kutoa ushirikiano wote?

Miye nasema tuitishe NSY kama hakuna cha kufichwa na ni kweli na tukubaliane lolote watakalosema lifunge mjadala au lianze criminal procedure. Vinginevyo tukubali tu yaishe, tusubiri mwingine aondoke kwa ajali ya baiskeli.
 
Kuhani.. jaribu kunielewa ninachosema, ama sivyo nitakuwa na kazi kweli ya kufafanua kila kitu. Kuna wakati natumia irony, sarcasm, etc. Itabidi unisome vizuri au itabidi niwe nafafanua kila kauli ili kuianisha iko kundi gani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom