Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Katika Tanzania nimejifunza kitu kimoja nacho ni matapeli/mafisadi ni wa kuogopa sana. Migogoro ilipo anza Chadema wengi wetu waligawanyika sana. Na baadhi ya watu tuliowaamini sana hata hapa JF walikuwa hawaoni tena mbali. Wakati nipo JKT waliniambia kwamba wakati unasonga mbele ni vizuri kujua adui wako vizuri na anatumia mbinu gani.

Watanzania wanapigana hawajui maadui wanatumia mbinu gani. Na hilo tutaedelea kulalamika milele. Kuna watu ambao leo wanapigana lakini adui akitokea nyuma yao wanaweza kuweka maswali kwamba huyo si adui bali ni mwenzao tu. Kwa haya Jmushi anayesema hana haja tena na bongo na mimi namsapoti kwa kusema tumepoteza nchi, anayekubalina na mimi akubali asiyekubali na aendelee kuamini.

Tumeanzia ujambazi, tukaenda UFISADI tumekuja na watu wa madini na hawa wote ni watu ambao wana pesa. Haijalishi wewe uko wapi hawa watu wanaweza hata kubadili aliye rafiki yako leo akawa adui yako kesho(kuwa makini na hili). Ni kuomba tu maana mimi kuna hata baadhi ya watu hapa hapa JF sihamini kama mawazo waliyokuwa wakitoa kama kweli ni mawazo huru.

Bado wengine wakati mwingine huwa tunasoma mawazo ya watu lakini kupoteza watu huwa pia tunaona. Atakayetaka kuona spin angalia mawazo yaliyotolewa hata na watu tunaowajua sana. Huwezi kuwa unapigana na adui na wakati huo huo hauwezi kujua adui atatokea wapi au atatumia mbinu gani.

Ukisikiliza vizuri taarifa ya habari ya TBC1 ya jana huna haja ya kujua walikuwa wanasema nini na huna haja ya kujua walitumiwa katika hii issue.

Suala linakuja huyo aliye weza kuandaa waandishi mpaka wakafika TARIME, TBC1, JF(maamuruki) nk alitoka wapi na hiyo kazi ilifanyika lini? Je alijua Kuna mtu atakufa?

Nafikiri ukisikiliza taarifa/magazeti mbali mbali nategemea watu wafungue kesi nyingi maana ushahidi upo kuwa hizo information hakuna mtu ambaye ni mataaluma anaweza kuzitoa. Anyway hiyo inaweza kufanyika tu tanzania mabayo inaelekea kupoteza mwelekeo.

Mwisho Tanzania yetu ya amani na utulivu itatoweka kama hatutaweza kusimama na sheria zetu na kuwa na viongozi wanaoweza kusimamia sheria kikamilifu.

Mkuu maneno yako yana thamani kuliko almasi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mumeanza mengine mapya... hakuna lolote... kama mlivyopigia makelele risasi na CCM na CHADEMA ndivyo na hili lingine litakuwa hivyo hivyo...

By the way waanzilishi wa hizi hoja ni waandishi ambao through hizo hoja wanapata articles... na through articles wanapata pesa.... na through pesa ndio wanaishi.

Tuendelee kuchangia ili waandishi wapate nyama nyama za kujazia kwenye article zao...

Kuna watu wengi sana wanataka waTanzania wawe wana uwezo wa kuthubutu kuua lakini mpaka leo pamoja na majaribio mengi kupitia marehemu hawa Mh. Amina Chifupa, Mama. Mbatia..., Dr. Ballali

Hakuna ushahidi hata mmoja ambao umeonyesha dhahiri mpaka leo kwamba kwenye listi zote za marehemu waliodhaniwa wameuwawa hakuna hata mmoja aliyedhihirika hivyo.

Tunakubaliana kwamba huo umemafia uko kwenye nchi munazoishi lakini sisi bado... to that extent.
 
Kasheshe... nani ambaye kifo chake kilichunguzwa independently na kushindwa kuoneshwa? Pick any?
 
Ninawasiwasi kuhusu yafuatayo:
1. Uchunguzi waliofanya mara ya pili ni kiini macho?
1. Je Deus Francis Mallya ni jina lake kweli ama ametumia jina bandia?
2. Hiyo kesi aliofunguliwa Mallya ni kiini macho cha kutusahaulisha tulio na machungu kuhusu Mhe. Wangwe?
3. Je! Mallya anauhusiano gani nafamilia ya marehemu?
4. Yule mtu wa tatu ni nani na kwanini alitoweka inawezekana walikuwa pamoja na kina Mallya katika safari?
5. Kama Mallya alitumwa kufanya kazi alioifanya alitumwa na kina nani?
6. Hiyo pistol aliokutwa nayo je anaimiliki kihalali pamoja na umri wake 27yrs?
7. Kazi ya Mallya na Makazi yake hasa ni wapi na alikwenda Dodoma kufanya nini?
8. Shughuli anazozifanya Mallya zinamruhusu kumiliki silaha?
9. Familia ya Mallya iko wapi na imeshajitokeza hadharani kumtetea?
 
Bado tuko ndani ya Wingu zito ambalo hajajua mwisho wake nini kitatokea
 
Kuchomolewa kwa Simcard si tatizo kubwa
Record zote za simu nani kampigia nani, saa gapi, wameongea muda gani, na huyo nanii alimpigia nani baada ya kupokea simu toka kwa Malya hizo zote zipo katika mitambo ya simu ya mashirika husika.
Mtu asijifanye kujaribu kuzifuta taarifa hizo.
On demand zinapatikana tu.

Technology haina usiri hata kidogo.
Hilo gari la Marehemu Wangwe likikaguliwa na Magwiji wa Scotland Yard kuna mengi yatasikika.
Tunaweza pata picha nzima ya kilichotokea isipokuwa kumrudisha Marehemu Wangwe katika uhai wake tu.

Polisi wanaweza kuishurutisha kampuni ya simu, ikibidi kwa mamlaka ya mahakama (subpoena) itoe rekodi za simu za mteja fulani ili kuendesha uchunguzi.

My concern is, if the players are big enough, the right person's palm at the telephone company can be oiled, the records deleted in time and by the time a slopoke police comes to ask nothing controversial will be found.
 
Familia ya Mallya haijajitokeza ama kumtetea wala kumkana ,na ijulikane kuwa miongoni mwa wanafamilia kuna kigogo ambaye alikuwa na bado ni naibu waziri sasa, alianzia mambo ya nje na sasa yupo viwanda biashara na masoko, huyu ni Mheshimiwa Cyril Chami.

Kuna wezwkana kabisa kuwa familia inataka kukaa mbali ,na hapo lazima ijulikane ni kwa nini familia inakaa mbali ama wameambiwa mambo yatakwisha wasijali ama wametishwa na kuogofya.
 
Mimi mwenzenu huwa ni mwaathirika wa taratibu na ushahidi. Madamu imetoka taarifa rasmi ya kitaalamu kutoka kwa mamlaka husika ikionyesha kuwa ilkuwa ni ajali, nashindwa tena kuendelea na hizi hisia zingine. Naona mambo mengine yote ikiwemo hilo la marehemu kuwasilisha hoja kuhusu Barick kuwa ni bad coincidence tu. Na nafikiri ni kwa mara ya kwanza katika utata wa vifo hivi angalau tumeweza kupata taarifa rasmi ya uchunguzi. Anyway, watu wanaweza kuendelea ku-speculate as usual hadi itakapotokea issue ingine nzito ya kututoa kwenye mada hii.

Mjadala huu unatoa fundisho tena kwa vyombo vyetu vya mamlaka kuwa wananchi hawaviamini tena, kiasi kwamba wanaamini hisia zao zaidi kuliko matokeo ya uchunguzi wa kitaalamu. Wajirekebishe, waanze kufanya kazi zao kwa mujibu wa utaalamu na maadili ya kazi zao badala ya kufuata matakwa na maagizo ya wanasiasa, vinginevyo watafik mahala watadharaulika kabisa.

Kasheshe: sio vizuri kufikiri kwamba wanaoendelea kuhoji mazingira ya kifo hiki wanafanya hivyo kwa maslahi ya kupata article za magazeti ili wapate pesa. Hisia za namna hii ni hatari na zinakatisha tamaa wenzetu wanaojtahidi kutafuta ukweli wa jambo hili na mengine. Tunatofautiana na ndio raha ya kuwa binadamu inayotutofautisha na wanyama wengine katika Mammalian Class; kama wewe hutaki kuendelea na mjadala huu, waachie wengine.
 
Mkuu wangu Kasheshe,

Heshima mbele bro, kuna siku ninakumbuka nilikuwa bunegni wakati bado likwa Dar, nikaona waziri wa fedha akipigana na maswali ya wabunge mpaka anataka kulia machozi kuwa anayosema kwenye bajeti yake ni sawa kabisa ila wabunge wako wrong,

Alipomaliza tu, behind the scene nikamuuliza duh! ile leo ilikuwa kazi waziri kubwa sana maana nimekuona ukisimama kidete mkuu? Akanijibu, kijana kwani unafiriki ni kweli yale niliyokuwa ninasema? Yatakuwaje kweli wakati hotuba yenyewe ni ile ile ya mwaka juzi ila zimebadilishwa namba tu!

Nafikiri wewe ni mtu mzima hapa unanielewa ninachosema, wanaposimama mbele ya umma na kusema hakukuwa na dosari yoyote, huku behind the scene wakisema maneno tofauti ina maana kuna something hapa, mimi ni mmoja wa wasioamini maneno ya authority on this na silipwi na mtu yoyote kufikiri hivyo kama ambavyo ninaamini na wewe hulipwi na mtu yoyote kufikiri kuwa authority inasema ukweli,

Kama ninakuelewa kinachokuchanganya ni kutoelewa haki ya uhuru wa mawazo katika demokrasia, kwamba inakubali wananchi kutofautinaa na authorities kwa hoja na bila ugomvi, na ndicho hasa sisi tusiokubali tunachokataa hapa, tunakataa hadithi kwamba Mallya alitoka kwenye ile gari la ajali akiwa mzima bila hata tone la damu au kuchubuka! Ni haki yetu kisheria kuamini hivi kama ilivyo yako.

Ahsante Mkuu!
 
Kingine ni kuwa Mallya alikuwa na funguo za gari mkononi alizichukua wakati gani?kama ni baada ya ajali je?inawezekana kuwa eneo la funguo halikuumia?ziliwezaje kutoka?je?alichukua funguo kabla ya ajali?na kama ni kabla maana yake ni kuwa gari haikupata ajali kwani ilikuwa imesimama?

Angalieni tena picha za ajali, juzi na jana walifanikiwa kuhamisha mjadala badala watu kuangalia chanzo cha ajali tulijikita kuangalia kama ni risasi ama sio risasi na hapo tukapotea njia moja kwa moja.

Huu mjadala wa risasi ulitokea wapi? ni kwanini ulisemwa hivyo?aliyeanzisha mjadala wa risasi ni nani?
Naambiwa kuwa aliyeanzisha mjadala huo sasa kaanzisha mwingine kuwa kuna rushwa ilitolewa jana kwa familia na daktari ili wakubaliane na uchunguizi ,sasa hapa lazima sisi kama tunatafuta ukweli tuende hatua moja mbele na kuwa mbele yao na kuwa independent ili kuweza kuangalia chanzo cha ajali .
 
Ni kuwa TBC jana walishindwa hata kutoa taarifa za kule Msibani Tarimew baada ya wao kuamua kuondokA JANA sasa sijui kilichowaondoa kule kilikuwa ni kitu gani na ni kwanin i waliudanganya umma kuwa jana wangemsikia Prof.Wangwe ,badala yake walishindwa kabisa.

TBC kuna kitu kilitokea tangia juzi na ni lazima tukitafute mpaka kijulikane kuwa ni kitu gani.

Wao TBC lazima waseme nyaraka za kesi pamoja na press statement waeitoa wapi ?ama wao ndio walikuwa wanamwandalia hiyo press statement na ni kwa masilahi ya nani?
 
Serikali yetu imejifikishaje hapa pa kutokuaminiwa karibu katika kila jambo? Itarudishaje IMANI kwa Wananchi wake? Hatima ya hali kama hii ni nini huko tuendako? Binafsi namshukuru Muumba wetu haya mambo yamemalizika hivyo yalivyomalizika.
 
Ni kuwa TBC jana walishindwa hata kutoa taarifa za kule Msibani Tarimew baada ya wao kuamua kuondokA JANA sasa sijui kilichowaondoa kule kilikuwa ni kitu gani na ni kwanin i waliudanganya umma kuwa jana wangemsikia Prof.Wangwe ,badala yake walishindwa kabisa.

TBC kuna kitu kilitokea tangia juzi na ni lazima tukitafute mpaka kijulikane kuwa ni kitu gani.

Wao TBC lazima waseme nyaraka za kesi pamoja na press statement waeitoa wapi ?ama wao ndio walikuwa wanamwandalia hiyo press statement na ni kwa masilahi ya nani?

Kweli hawa TBC wana lao jambo labda tusubiri baada ya mwezi mmoja Tido atatoa press release kama ile kushindwa kutoa hotuba ya Dr Slaa

hata suala la waandishi wa habari kupresent matukio naona kuna jambo check hii taarifa ya Ippmedia leo wameficha majina ya waandishi
Maziko ya Wangwe: Vigogo watimka, mmoja adakwa

2008-08-01 18:11:54
Na Waandishi Wetu, Tarime na Jijini

Baada ya ndugu na jamaa wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Marehemu Chacha Wangwe kugomea mazishi hapo jana, vigogo karibu wote waliokuwa wamefurika kijijini Kemakorere kwa ajili ya msiba huo wamelazimika kutimkia mjini Musoma.
 
Serikali yetu imejifikishaje hapa pa kutokuaminiwa karibu katika kila jambo? Itarudishaje IMANI kwa Wananchi wake? Hatima ya hali kama hii ni nini huko tuendako? Binafsi namshukuru Muumba wetu haya mambo yamemalizika hivyo yalivyomalizika.

Hili ndio swali muhimu sana. Ni kwamba hawaaminiki kwa kila jambo kwa sababu wametanguliza maslahi ya kisiasa kwa chama chao kwa kila jambo. Kila jambo wanataka kulitumia kwa manufaa ya kisiasa.
 
Naendelea kulifuatilia hili kwa ukaribu mkubwa sana kwani linaweza kutoa ushahidi fulani na watu wakatakiwa kuisaida polisi na haswa Rostam Azizi kwanini alijihusisha kiasi hicho?

Magazeti ya leo wameshindwa kusema kuwa juzi Mbowe alikoswakoswa na mapanga na mishale kama walivyosema jana .

Waandishi walioandika habari jana ni hawa;

1.Nipashe-Bigambo Jeje-PST.

2.Majira-George John -Tarime na Reuben Kagaruki DAR.

3.Habari Leo -Makubo Haruni

4.Uhuru -Mwandishi wetu

5.Mtanzania-George Mwita.


Waandishi walioandika leo ni hawa;

1.Nipashe-Mary Edward PST.

2.Habari Leo-Halima Mlacha.

3.Majira -George John

4.Mtanzania-Christopher Gamaina

5.Uhuru-Mwandishi wetu.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa je?waandishi hawa walipelekwa jana huko Tarime?
Majina yaliyoripoti juzi inamaana hawaaminiki tena ama wamefukuzwa kazi?
Habari za leo kila gazeti limekuwa na maandishi yake na hakuna kufanana kama jana japo wameripoti tukio hilohilo .
Kikao cha jukwaa la wahariri kinaendelea sasa ,ntawapa yatakayojiri huko punde.
 
Mimi mwenzenu huwa ni mwaathirika wa taratibu na ushahidi. Madamu imetoka taarifa rasmi ya kitaalamu kutoka kwa mamlaka husika ikionyesha kuwa ilkuwa ni ajali, nashindwa tena kuendelea na hizi hisia zingine. Naona mambo mengine yote ikiwemo hilo la marehemu kuwasilisha hoja kuhusu Barick kuwa ni bad coincidence tu. Na nafikiri ni kwa mara ya kwanza katika utata wa vifo hivi angalau tumeweza kupata taarifa rasmi ya uchunguzi. Anyway, watu wanaweza kuendelea ku-speculate as usual hadi itakapotokea issue ingine nzito ya kututoa kwenye mada hii.

Mjadala huu unatoa fundisho tena kwa vyombo vyetu vya mamlaka kuwa wananchi hawaviamini tena, kiasi kwamba wanaamini hisia zao zaidi kuliko matokeo ya uchunguzi wa kitaalamu. Wajirekebishe, waanze kufanya kazi zao kwa mujibu wa utaalamu na maadili ya kazi zao badala ya kufuata matakwa na maagizo ya wanasiasa, vinginevyo watafik mahala watadharaulika kabisa.

Kasheshe: sio vizuri kufikiri kwamba wanaoendelea kuhoji mazingira ya kifo hiki wanafanya hivyo kwa maslahi ya kupata article za magazeti ili wapate pesa. Hisia za namna hii ni hatari na zinakatisha tamaa wenzetu wanaojtahidi kutafuta ukweli wa jambo hili na mengine. Tunatofautiana na ndio raha ya kuwa binadamu inayotutofautisha na wanyama wengine katika Mammalian Class; kama wewe hutaki kuendelea na mjadala huu, waachie wengine.

Kitila,

Huo ndio ukweli wenyewe, hii case ukiiangalia toka mwanzo ilikuwa inaonyesha ni ajali lakini bahati mbaya TZ kila jambo lazima tutafute mchawi.

Tatizo ni lile lile la kutokufuata sheria. Ukiona mbunge anaendeshwa na dereva asiye na leseni, je kuna madereva wengine wangapi wa namna hiyo ambao wako mitaani?

Karibu kila ajali tunayosoma hapa kwasehemu kubwa ni matokeo ya madereva wabaya. Pia sisi wenyewe kupenda kuwahi nako ni tatizo, utakuta kigogo anamwambia dereva mbona speed ndogo?

Ifike mahali tuache kulaumiana na labda turudi kujadiliana juu ya kwanini hizi ajali zinatokea na tufanye nini ili kuzipunguza. Wangwe sio wa mwisho, kuna wengine tutaondoka pia kwa hizo ajali kama hatufanyi juhudi kujifunza juu ya hili tatizo sugu.

Pole sana tena kwa familia namarafiki wa Chacha Wangwe.
 
UCHUNGUZI WATHIBITISHA

Wangwe: Siyo risasi

*Uchunguzi wathibitisha jeraha lake ni la ajali
*Waonyesha alipasuka fuvu, ubongo ulimwagika
*Profesa Wangwe asikitishwa na habari za uzushi
*Akana Mbowe kuokolewa, kunusurika mapanga

*Zitto Kabwe aziita taarifa hizo kuwa za kizushi


Na Joseph Senga, Tarime


HATIMAYE mazishi ya Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (Chadema) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari, Jumatatu wiki hii, yamefanyika jana baada ya matokeo ya uchunguzi uliofanyika kutangazwa.
Mazishi hayo ambayo awali yalikuwa yafanyike juzi, yalikwama baada ya wanafamilia kutaka ufanyike uchunguzi mwingine huru kutokana na kuwapo kwa utata katika mazingira yaliyosababisha kifo cha mbunge huyo.
Uamuzi huo wa wanafamilia kutaka kufanyika kwa uchunguzi huo, ulikwenda sambamba na kuibuka kwa hali ya wasiwasi na kutishia kuibuka kwa vurugu katika Kijiji cha Kemakerere.
Akitangaza matokeo ya uchunguzi huo jana, mbele ya wananchi waliofurika, Profesa Samuel Wangwe ambaye ni kaka wa marehemu, alisema uchunguzi huo ulifanywa na daktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye hata hivyo hakutajwa kwa sababu za kiusalama.
Profesa Wangwe alisema uchunguzi huo uliofanyika kwa zaidi ya saa mbili, ulibainisha kuwa, ajali ilisababisha mdogo wake apasuke fuvu la kichwa kutokana na kujigonga kwa juu na kisha ubongo ukamwagika sambamba na taya kuvunjika.
Uchunguzi huo ulioanza jana asubuhi majira ya saa 5:15, ulifanyika chini ya uwakilishi wa wanafamilia watatu, Jeshi la Polisi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyekiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Profesa Wangwe aliwaeleza wananchi waliokuwa wakimsikiliza kwamba, yeye na wanafamilia wenzake walikuwa wamekubaliana na kuridhishwa na taarifa hiyo ya uchunguzi, na hivyo kukubali kumzika ndugu yao.
Mbali ya hilo, alisema daktari alikuwa akitarajia kuiwasilisha taarifa kamili ya maandishi ya uchunguzi alioufanya akiambatanisha na picha zilizopigwa.
Baada ya taarifa hiyo ya uchunguzi iliyotolewa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime ulikofanyika, safari ya kwenda Kemokerere kwa ajili ya mazishi ilianza.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa Tarime waliitaka familia hiyo kuahirisha mazishi hadi leo, ili kuwapa fursa watu wengine ambao walikuwa wameshaondoka kuhudhuria, ombi ambalo hata hivyo halikukubaliwa na wanafamilia.
Mwili wa marehemu ulipofika nyumbani kwake, shughuli za mazishi zilianza kwa salamu za rambirambi kutolewa kwanza na umoja wa vyama vya upinzani vinavyoshirikiana na Chadema; NCCR Mageuzi, TLP na CUF.
Akizungumza kwa niaba ya vyama hivyo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema aliwataka wananchi wa Tarime kushikamana na kuendeleza mema yote aliyoyatenda marehemu Wangwe wakati wa uhai wake.
Mbali ya kutoa ubani wa shilingi 300,000 Mrema aliwataka kuanza kuangalia wanachama kutoka katika kambi hiyo ya upinzani ili kumtafuta mtu atakayerithi mikoba ya ubunge ya Wangwe.
Wengine waliotoa salamu za rambirambi ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Luteni Kanali mstaafu, Issa Machibya aliyetoa ubani wa shilingi 100,000 na kilo 50 za mchele kusaidia shughuli za msiba.
Ibada ya mazishi ya Wangwe iliendeshwa kwa mahubiri ya Kikristo na Nancy Msafiri na ikahudhuriwa na wananchi wa Tarime, viongozi wa kisiasa, ndugu, jamaa, marafiki, watoto na wake watatu wa marehemu waliojulikana kwa majina ya Gati, Dotto na Mariam.
Jeneza la marehemu Wangwe lilianza kuteremshwa kaburini saa 11:50 jioni.
Awali, muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchunguzi jana, Profesa Wangwe alizungumza na wanahabari na akaeleza kusikitishwa kwa familia yao na taarifa za uzushi zilizoripotiwa katika vyombo kadhaa vya habari juzi na jana, kuhusu hali ya usalama wakati wa msiba huo.
Profesa Wangwe alisema yeye na wanafamilia wenzake, walikuwa wamesikitishwa na taarifa zilizokuwa zikidai kwamba, kulikuwa na kikundi cha watu wenye mapanga waliokuwa wakimuwinda Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbali ya hilo, Profesa Wangwe alieleza kushangazwa kwake na taarifa alizozielezea kuwa zisizo sahihi, zilizokuwa zikidai kuwa Mbowe alilazimika kuondolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa polisi ili kumnusuru na mapanga hayo.
‘‘Hakuna mapanga yaliyokuwa pale, wala hakukuwa na vurugu za kutumia silaha na wala Mwenyekiti wa Chadema Mbowe (Freeman) hakuondolewa chini ya ulinzi wa polisi,” alisema Wangwe huku akiyataja baadhi ya magazeti (si Tanzania Daima) ambayo yaliandika taarifa hizo.
Akifafanua, Profesa Wangwe alisema, Mbowe aliondolewa uwanjani hapo juzi akiwa na viongozi wengine wa juu wa kiserikali na kisiasa kutokana na ushauri uliotolewa na Mkuu wa Mkoa baada ya mabishano kuhusu uhalali wa kumzika marehemu ulipoibuka.
Hata hivyo, taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata baadaye juzi jioni na jana kutoka Musoma na Tarime zinaonyesha kwamba, kulikuwa na kikundi maalum kilichokuwa kimeandaliwa kwa malengo ya kisiasa na watu wasiojulikana, kwa lengo la kumdhuru Mbowe.
Wakati Mbowe akiwasili katika Kijiji cha Kemakorere hiyo juzi, hali ilikuwa ni tofauti kwani alilakiwa na vijana wa Chadema ambao walimuongoza hadi katika jukwaa kuu.
Katika hali ambayo si rahisi kuielezea, pamoja na Mbowe kuwasili na kuondoka uwanjani hapo salama, tena pasipo kusindikizwa na polisi, vyombo kadhaa vya habari vilianza kuripoti kuhusu kunusurika kwake kwa mapanga hata kufikia hatua ya kuokolewa na polisi.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Zitto alizielezea taarifa hizo za mwenyekiti wake kunusurika kuwa ni za uzushi uliokuwa umeandaliwa kwa malengo ya kisiasa na kwa nia ambayo haikuwa nzuri.
‘‘Huku hakukuwa na kinachoitwa vurugu, wala hakukuwa na hali ya hatari dhidi ya mwenyekiti. Kuna propaganda kali inasambazwa kuwa mwenyekiti kaokolewa na polisi. Hizi ni taarifa za uongo,” alisema Zitto alipoulizwa kuhusu nini kilikuwa kimetokea.
Akizungumza na Tanzania Daima kutoka Musoma jana, Mbowe pasipo kutaka kuingia kwa undani, alieleza kusikitishwa na taarifa hizo na akasema baada ya kufanya mashauriano na washauri wake na viongozi wengine wa chama hicho, alikuwa ameamua kurejea Dar es Salaam.
 
wahaini!wahaini hawa, rostam azizi na pesa zake za wizi, ameamua kuliweka taifa rehani, wanatarime wenye maduka mjini moshi walikuwa na wasiwasi mkubwa! na wachagaa huko tarime hivyoo hivyoo. interahamwe rostam azizi na vibaraka wake wafikikishwe mbele ya mkono mkubwa wa sheria kwa uhaini dhidi ya taifa letru la tanzania. uhaini si kwa ajili ya kumpindua rais hata kwa kuchocea maasi

Ee taifa langu la Tanzania,
tazama nimekupenda mno ,
tena dhidi ya wanafiki wako,
tena dhidi ya wazandiki,
tena dhidi ya mapandikizi
tena dhidi ya mafariasao

amka ee taifa langu
amka sasa usilalae tena,
adui zako wako mlangoni
nao si wengine,
ni wale mafarisao waandikao
kwa kalamu zao baada ya rupia
ni wale msadukayo,
ni wale wanaokula vya yatima
AMKA EE TAIFA LANGU
 
CONSPIRACY THEORIES,i fear for this country,at every turn,we come with these theories,most of them unfounded,this monster which has taken hold of our medulla's is throwing this once proud nation deeper down the abyss.the damage of most of these unfounded allegations divides us further.HITTING the keyboard immediatly,before proper gathering facts only to be proved otherwise,to any patriot is worse then any FISADI,for the damage cannot be reversed.its time we sit down,take stock of our actions,FOR ABUSING THE FREEDOM OF SPEECH GRANTED TO US IS THE WORST SIN OF ALL
 
Hivi mlitegemea huyu daktari kutoka Kenya aje na kusema ameiona risasi ndani ya mwili wa marehemu? Yaani hao waliofanya uchunguzi wa mwanzo waikute hiyo risasi halafu waiache huko. Je, waliposema kuna majeraha au alama ambako inawezekana amepigwa risasi walijuaje? Je wao ni wataalamu wa kuweza kufahamu mahali ambako risasi imepita? Je huyu daktari kutoka Kenya ana uzoefu wa kuchunguza majeraha ya mtu aliyepigwa na bunduki? Au aliyelishwa sumu? Je alitumia vigezo gani kusema hayo majeraha ni ya ajali, au ana uzoefu wa kutambua majeraha ya ajali?

Familia ya Wangwe nahisi walionywa kwamba kukitokea machafuko watu wengi kufa zaidi itakuwa ni wao waliosababisha hilo. Hapa kuna magarasha tu yanachezwa, ni pale tu Watanzania watakapoamua kuwavalia njuga mafisadi na kuwaua bila huruma kama wezi wa kuku ndio tutaona mabadiliko ya kweli. Haiwezekani kila kukicha kunakuwa na mabomu kila kona. Mafisadi wameshikwa pabaya na hivi wanahaha kwani walipoamua kuishika CCM walifikiri wako salama lakini hivi sasa walalahoi wameamka. Nchi yetu inauzwa mithili ya watemi waliokuwa wanauza watumwa na viongozi wa serikali ya CCM wamekuwa mstari wa mbele kujikomba kwa m****** wao wa kizungu.


BTW hivi Tanzania tuna kitengo cha forensic experts au ndio ubabaishaji tu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom