Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kitila,

Mimi ni kama namfahamu MkamaP, sio CCM kabisa ila baadhi ya mambo na matusi yanayoandikwa na vijana wa CHADEMA hapa yanawafanya watu wengine wachukue upande wa pili ili kuleta balance.
Japo wengi wao si ajabu hata si wanachama wa CHADEMA, lakini comments zao zinaweza kuwakosesha CHADEMA wanachama na viongozi wa baadaye.

Hivi mkuu kuna mtu aliyesema kwamba 'two wrongs can make one right?.Je,unaunga mkono yeye kufanya uovu kwa sababu kafanyiwa? Uneweza tu kutoa ushauri uliotoa mwishoni bila kuitetea hiyo point ya kuleta balancing
 
kama magazeti yote yanategemea mwandishi mmoja, basi whats the point ya kuwa na vyombo vya habari tofauti?
 
Jambo kubwa na ambalo ningetaka wenzangu humu mulijadili kwa kina na kuangalia kinachoendelea ni kuwa ukisoma magazeti yote ya leo isipokuwa Tanzania daima na Mwananchi ambayo yaliripoti taarifa hiyo utaona ya kuwa mwandishi wa habari hiyo alikuwa ni mtu mmoja.

Ukianza kusoma Nipashe,majira,mtanzania,kulikoni,uhuru na habari leo utaona hiki ninachosema ,kwani kuna paragrafu tatu zinafanana kila sentensi na ni zile zinazohusiana na Mbowe jinsi alivyowasili Kemakorere.

Nimefanya uchunguzi wangu tangu asubuhi leo na nimeweza kujua kuwa habari hiyo ilitumwa na Mwandishi mmoja ambaye naomba kumtaja baadae huyu mwandishi ni mwandishi wa IPP Media,na yuko based Mkoa wa Mara.

Nowashuri muweze kusoma hicho ninachosema kwenye magazeti niliyotaja ,na kisha mtaweza kuupata ukweli wenyewe jinsi ulivyo, haiwezekani waandishi tofauti wakaandika kitu kile kile kwa maneno yaleyale na paragrafu zilezile,na kila penye koma,nukta na hata mkato pakawa ni pale pale.

Nimegundua kuwa Rostam Aziz jana amekutana na wahariri na wale ambao hawakwenda aliwapigia simu kuanzia saa tisa na dakika 26 jioni na kuanza kufanya kazi yake,na ilipofikia jioni akakutana na wahariri wa habari na kuwapa bahasha maalum kwa ajili ya kuitumia story hiyo, na kuwaahidi kuwapatia donge nono na hizi nina uhakika nazo nasubiri muda wa kuziweka hadharani .

Tatu, waandishi ambao majina yao yametumika kwenye magazeti niliyotaja hawapo na kwa vile vyombo vilivyoandika majina ni majina ya kutungwa kwani waliokuwepo huko leo wamekaa na kutoa msimamo kuwa ni kwanini habari zao hazikutumika kama walivyotuma .

Prof. Wangwe anategemewa kutoa tamko jioni hii kuhusiana na habari zilizoandikwa kuhusiana na Mbowe kutimuliwa kwa mapanga,marungu n.k. ila alikuwa anashauriwa na watu watatu waliokuwa naye kuwa asifanye hivyo ila yeye anaonekana kuwa na msimamo wa kutaka kusema kilichojiri na kutoa tamko rasmi la familia .

Naenda tena kupata habari nyingine za kina kwani imebidi nikaweka watu maalum huko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa napata habari za kweli na kuna siku nitajitambulisha rasmi kuwa mimi ni nani ,na haya maandishi yangu yataendelea kuwa ni ukweli, nakumbuka jana niliandika na kuna mtu aliniuliza humu kama ninayoandika kuhusiana na magazeti yataripoti nini kama ni ukweli nami nilimjibu kuwa ni ukweli..Ndugu,Mtanzania unakumbuka ni wewe uliniuliza jana majira ya mchana saa za huku ila ilikuwa majira ya jioni huko nyumbani kama sio usiku.

Habari za ndani kabisa zinasema kuwa maamuzi ya familia yanaelekea kwenye kuzika mwili ili yaishe. Keba na Samuel (Prof) Wangwe wanajulikana Tarime kwa kutopenda maneno mengi na mwelekeo hapa ni kuwaambia wana Tarime kuwa yamekwisha na watu wazike, walie, waomboleze, na kisha kuendelea na kazi zao za maendeleo.

Katika hili, inaonekana chochote kile kitakachoonekana kwenda kinyume na yale yanayotakiwa kufanyika kitakumbana na vikwazo na usumbufu mwingi huku pia watu wa Tarime tukiwekwa hostage na kuamshwa emotions zetu kiaina kwa propaganda bab kubwa inayoendeshwa na TBC1 na magazeti yote ya Rostam Azizi na wapambe wake.

Katika hili, ukweli utajulikana mioyoni mwetu no matter what they do. Sisi sio wajinga na watu wa Tarime sio wanyama kama wengine wanavyotuonyesha hapa. Thanks GOD hakuna ugomvi au mapigano yaliyotokea kama wengine wenye nia mbaya na Tarime walivyotaka. MUNGU ashukuriwe kwa kuwalinda na kuwatunza watu wote wa Tarime.

Chacha Wangwe, umepigania mengi sana kwa maisha ya wana Tarime. Kwa miaka zaidi ya 15 umekuwa mstari wa mbele kutusaidia watu wa Tarime kwa kila kitu - kuanzia sheria batili za ulinzi wa sungusungu hadi kwenye sheria onevu za watoza kodi wa halmashauri ya Tarime. Umekuwa mstari wa mbele kwa sana kuwaunganisha wamiliki wadogowadogo wa machimbo ya madini kupambana na makampuni makubwa ya kifisadi ambayo sasa yatafurahia kuondoka kwako.

Chacha umekuwa mstari wa mbele kujaribu kusuluhisha migogoro ya ardhi Tarime hata pale ambapo serikali ilionekana kupuuzia. Nakumbuka nilipokuwa shule ya upili ulianzisha kampeni ya kuondoa adhabu zisizo na maana kwa watoto wa shule, kampeni ambayo ilikuchukua karibu miaka kumi kufanikiwa. Chacha Wangwe - rastafarian, nakumbuka ulinifundisha maneno halisi ya nyimbo za Bob Marley na Dube na kuniambia tafsiri yake nikiwa kinda tu.

Chacha Wangwe, watu wa Tarime tutakukumbuka milele kwa yote mema uliyofanya na tutasahau milele zile tofauti za kawaida za kibinadamu ambazo zimeweza kuwa zimetokea.

MUNGU wa mbinguni ailinde familia yako na ndugu zako. Kuna watakaodhani kuwa wameshinda kwa yaliyotokea lakini MUNGU wa mbinguni ataleta Chacha mwingine kutoka kwa jamii ya wakurya wa Tarime ambaye atafanya yote yale uliyotaka yafanyike na kuendeleza mazuri zaidi. Kuna wanaodhani kuwa huu msiba wako ndio utamaliza upinzani Tanzania. Hata kama Chadema na NCCR - vyama ambavyo ulivihamasisha sana Tarime vitakufa, bado ari na nia ya kuwa na serikali bora Tarime na Tanzania itaendelea kuwa mioyoni mwa wana Tarime forever and ever.

Kwaheri Wangwe, kwa heri rasta man, kwa heri mpambanaji, kwa heri murra, kwa .....inhi inhi inhi hiiiiiiiiiiiiiiiii inhi .... uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ENOKWE ikuhituke naghukuha ahasi ha kumunya hano YESO aricha.

Amen
 
Huyu anayejifanya kuwa alikuwepo, asome jinsi ambavyo hadi koma kwenye habari hiyo zimewekwa sehemu moja na nukta sehemu moja .
 
Jambo kubwa na ambalo ningetaka wenzangu humu mulijadili kwa kina na kuangalia kinachoendelea ni kuwa ukisoma magazeti yote ya leo isipokuwa Tanzania daima na Mwananchi ambayo yaliripoti taarifa hiyo utaona ya kuwa mwandishi wa habari hiyo alikuwa ni mtu mmoja.

Ukianza kusoma Nipashe,majira,mtanzania,kulikoni,uhuru na habari leo utaona hiki ninachosema ,kwani kuna paragrafu tatu zinafanana kila sentensi na ni zile zinazohusiana na Mbowe jinsi alivyowasili Kemakorere.

Nimefanya uchunguzi wangu tangu asubuhi leo na nimeweza kujua kuwa habari hiyo ilitumwa na Mwandishi mmoja ambaye naomba kumtaja baadae huyu mwandishi ni mwandishi wa IPP Media,na yuko based Mkoa wa Mara.

Nowashuri muweze kusoma hicho ninachosema kwenye magazeti niliyotaja ,na kisha mtaweza kuupata ukweli wenyewe jinsi ulivyo, haiwezekani waandishi tofauti wakaandika kitu kile kile kwa maneno yaleyale na paragrafu zilezile,na kila penye koma,nukta na hata mkato pakawa ni pale pale.

Nimegundua kuwa Rostam Aziz jana amekutana na wahariri na wale ambao hawakwenda aliwapigia simu kuanzia saa tisa na dakika 26 jioni na kuanza kufanya kazi yake,na ilipofikia jioni akakutana na wahariri wa habari na kuwapa bahasha maalum kwa ajili ya kuitumia story hiyo, na kuwaahidi kuwapatia donge nono na hizi nina uhakika nazo nasubiri muda wa kuziweka hadharani .

Tatu, waandishi ambao majina yao yametumika kwenye magazeti niliyotaja hawapo na kwa vile vyombo vilivyoandika majina ni majina ya kutungwa kwani waliokuwepo huko leo wamekaa na kutoa msimamo kuwa ni kwanini habari zao hazikutumika kama walivyotuma .

Prof. Wangwe anategemewa kutoa tamko jioni hii kuhusiana na habari zilizoandikwa kuhusiana na Mbowe kutimuliwa kwa mapanga,marungu n.k. ila alikuwa anashauriwa na watu watatu waliokuwa naye kuwa asifanye hivyo ila yeye anaonekana kuwa na msimamo wa kutaka kusema kilichojiri na kutoa tamko rasmi la familia .

Naenda tena kupata habari nyingine za kina kwani imebidi nikaweka watu maalum huko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa napata habari za kweli na kuna siku nitajitambulisha rasmi kuwa mimi ni nani ,na haya maandishi yangu yataendelea kuwa ni ukweli, nakumbuka jana niliandika na kuna mtu aliniuliza humu kama ninayoandika kuhusiana na magazeti yataripoti nini kama ni ukweli nami nilimjibu kuwa ni ukweli..Ndugu,Mtanzania unakumbuka ni wewe uliniuliza jana majira ya mchana saa za huku ila ilikuwa majira ya jioni huko nyumbani kama sio usiku.
My man, kumbe na wewe ulizipata za RA kufanya hii kitu? Leo napewa taarifa na jamaa yangu akidai mwandishi wa habari kwa magazeti yote leo ni mmoja ila kwa majina ya kutungwa, nafika hapa nakuta umeweka ujumbe huu pia. Hii inadhihirisha ukweli wa jambo hili. Why this lakini? Hizi siasa za kuchafuliana majina zinatokana na nini? Kwanini msiba huu utumiwe kuchafuana kwa namna hii kwa njia ya vyombo vya habari?

Inasikitisha sana kwani ulichosema ni kweli habari hizi zimefanana SANA na nadhani hawakujua kuwa si wote waliolala.

Kudos mate!
 
Kuna habari kwamba Wangwe anazikwa jioni hii kijijini kwake na hii ni baada ya Postmortem iliyochukua saa 4, katika hospitali ya wilaya ya Tarime. Habari zaidi baadaye.
 
Kwamba wewe unataka kuwaambia watu kuwa Mbowe hakuwa kwenye wakati mgumu, na wala hakuondolewa pale akisindikizwa na askali. Mimi nilikuwepo jana na hivi niko Mwanza yaliyoandikwa ni kweli ndivyo ilivyo kuwa na kama hamuamini muone kama siku ya mazishi Mbowe atakuwepo. Halafu kuhusu habari kufanana hiyo siyo ajabu inategemeana na chanzo cha habari

PIA UNAWEZA UkAWA MUONGO! Maanake sasa hivi karibia kila mtu AnajidAi yuko msibAni.Kama wewe ni mkweli basi natanguliza apology.
 
My man, kumbe na wewe ulizipata za RA kufanya hii kitu? Leo napewa taarifa na jamaa yangu akidai mwandishi wa habari kwa magazeti yote leo ni mmoja ila kwa majina ya kutungwa, nafika hapa nakuta umeweka ujumbe huu pia. Hii inadhihirisha ukweli wa jambo hili. Why this lakini? Hizi siasa za kuchafuliana majina zinatokana na nini? Kwanini msiba huu utumiwe kuchafuana kwa namna hii kwa njia ya vyombo vya habari?

Inasikitisha sana kwani ulichosema ni kweli habari hizi zimefanana SANA na nadhani hawakujua kuwa si wote waliolala.

Kudos mate!

This justifies my speculations that kama ni CHADEMA wangekuwa wameua CCM ingefanya juu chini kuhakikisha wauaji wanadakwa ila nilisema either the govt or a very powerfully political figure is behind these!RA is too much!Am vexed beyond words.
 
Kwamba wewe unataka kuwaambia watu kuwa Mbowe hakuwa kwenye wakati mgumu, na wala hakuondolewa pale akisindikizwa na askali. Mimi nilikuwepo jana na hivi niko Mwanza yaliyoandikwa ni kweli ndivyo ilivyo kuwa na kama hamuamini muone kama siku ya mazishi Mbowe atakuwepo. Halafu kuhusu habari kufanana hiyo siyo ajabu inategemeana na chanzo cha habari

Hata kama chanzo ni kimoja, kama waandishi ni tofauti kufanana kwa habari mstari kwa mstari, inaonyesha kati yao, kuna ambaye hajafanya kazi yake bali amenakili ya mwingine. Huo ni wizi na kosa kisheria. kwani kazi za waandishi ziko protected na copyright laws kama nyingine nyingi.

Kama sio ajabu kwako basi tuna tatizo kubwa zaidi kw upande wako
 
Mwanakijiji elewa jambo moja Chadema walikuwa wakitaka ruzuku za Wangwe kupitia jimbo la Tarime, kwa vile priority ya Chadema ni RUZUKU NA UKABILA wasingeweza kumnyanganya uanachama,angekuwa si mwanachama wa Chadema nao makao makuu wangepata Ruzuku, kwa hiyo kilichokuwa kinambakiza Wangwe chadema ni lile kundi la Tarime linalizalisha Ruzuku Makao makuu.

Wangwe alibaki kuwa Mwanachama kwa ajili ya ruzuku si vinginevyo.

SASa kama unajua hivyo,mbona kuna mahali uliandika kuwa CHADEMA wamehusika na kifo cha Wangwe? Ina maana kama suala lilikua ni ruzuku,je CHADEMA sasa hivi wahazihjitaji ruzuku? Acha hizo wewe!

Hilo suala la ukabila ndilo linakuweka wewe hapa,maanake kila saaa uko hapa kueneza chuki za kikabila.Nenda ukaishi kwa wakisii huko Kenya kwenye ukabila na si kuleta huu upuuzi hapa katika nchi yetu tuipendayo TANZANIA
 
Ben karibu katika mtandao.
Nafikiri hilo ni kubwa zaidi kwako. kukaribishwa na kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Nikuhakikishie kuwa ndani ya huu mtandao kuna watu ambao kamwe hawatajinyima uhuru wa kufikiri, kusikiliza na kusema hadharani.
Nikuhakikishie mpendwa kuwa hoja zako kadhaa hapa jukwaani zinatoa taarifa kuwa ama hutaki kufikiri au hutaki watu wafikiri.

Sasa kwa wale wanaofikiri huwa wanaunganisha habari kwa ajili ya kuchambua na kufikia ukweli uliofichika.

Kuhusu CHADEMA: mimi sifikiri kuwa CHADEMA inahitaji wanachama wanaowafuata kimkumbo. Nitakiheshimu chama kama kinawapa fursa watu wake kuchunguza mambo, kujadili mambo na kuyasema hadharani. Unaposema kuwa matusi na madongo kutoka kwa wanachama wa CHADEMA hapa mtandaoni vimewafanya baadhi kujiengua na kuside na CCM. Hii ninakupinga sana na ninakuomba usilete jukwaani propagana za kishamba namna hiyo tena.

Sasa tunahitaji vichwa vitumike hadi tupate uhakika kuwa nini kilimuua Chacha. Tunahitaji kutumia vichwa ili wale ambao tayari wameaminishwa vinginevyo wajue ukweli halisi.

Ben tafadhali tutendee haki, kabla hatujakulist upande ulio kinyume nasi.
 
Hebu tuangalie mlingano huo wa habari:

Baadhi ya viongozi hao wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Salehe Ramadhan Feruzi, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Bw. Makongoro Nyerere, Mjumbe wa NEC, Christopher Gachuma, walilazimika kutimuka mbio baada ya tangazo la kuahirisha mazishi, kufuatia vijana kuanza kurusha mawe hovyo hali iliyoleta mtafaruku mkubwa. - Nipashe

Na katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, jana alinusurika kuuawa kwa mapanga baada ya kuwasili katika kijiji cha Kemakorere kuhudhuria mazishi ya marehemu Wangwe.

Hali hiyo ilianza kujitokeza saa 8:00 mchana baada ya Bw. Mbowe kuwasili kijijini hapo akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustine Mrema (TLP), Bw. Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Bw. Bob Makani kiongozi mstaafu wa CHADEMA. - Nipashe

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amenusurika kauawa kwa mapanga na mishale, baada ya kuwasili katika kijiji cha Kemakorere, kuhudhuria maziko ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe.
Sakata hilo lilianza kujitokeza jana saa nane mchana baada ya Bw. Mbowe kuwasili kijijini hapo akifuatana na viongozi wengine wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustino Mrema (TLP), Bw. Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Bw. Bob Makani Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA. - Majira

“Viongozi mashuhuri kwa nini hufa kwa ajali na BP?”, “Tungelikagua mwili tungeridhika”, “Wangwe umekufa kweli kwa ajali au kwa risasi au kwa ushirikina?” Baadaye wengine walitoa mapanga na mikuki, hali iliyowalazimu polisi kumchukua Mbowe na kumwingiza ndani ya nyumba ambako walikuwa wamekaa wabunge wengine 20.

Kuona hivyo vijana wengine walianza kurusha mawe kuwaelekezea viongozi hao. Viongozi hao kuona hivyo walitimua mbio wakihofia maisha yao. Baadhi ya viongozi waliotimua mbio pamoja na Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Salehe Ramadhan Feruzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, Zitto Kabwe ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mwenyekiti wa CCM Mkoani Mara, Makongoro Nyerere na Mjumbe wa NEC wa CCM wa mkoa wa Mara, Christopher Gachuma. - Habari Leo

My Take:
Kuna mtu alikuwa anaimbishwa kama kasuku!
 
Huyu anayejifanya kuwa alikuwepo, asome jinsi ambavyo hadi koma kwenye habari hiyo zimewekwa sehemu moja na nukta sehemu moja .

Asante sana Kiranja,

Watu wenye kuelewa mambo tunaona yote wanayofanya na tunawashangaa tu. Inaonekana kuna watu bado wanajiona kuwa na nguvu sana na wanatuamulia cha kufanya na kututisha kuwa tukikurupuka tu watatuondoa kama nzi na kisha kueneza habari za uongo kuwa tulileta kinyesi kwenye chakula chao.

Inaumiza sana, hata kama wakituua bado kila mwaka watakuwa wanazaliwa machacha na mamwita mengine na yataendelea kupeleka vinyesi kwenye vyakula vyao.
 
utasema mwongo kwa sababu sina std mbili.Kwa vile nasema CHADEMA ichunguzwe ndio waja juu sishangai hili ni tatizo la wana CHADEMA wengi.

Naheshimu Michango yako mingi lakini kwa hili lazima tutatofautiana tu maana na wewe yawezekana una nafasi ama unaiwania CHADEMA na hili ndilo TATIZO la sisi wtz.

Mfano ccm likitokea jambo hua wanaitana kuwekana sawa waje na msimamo wanaoujua wao mara nyingi ni wa kishetani na si kumtetea mwananchi ila wanalazimika kufanya hivyo kwa vile wanaabudu matumbo yao.

Ndivyo hivyo CHADEMA hakuna tofauti yaleyale wakishutumiwa nao wanawekana sawa ili iweje?

kama mtu uko msafi mtu kakutuhumu kua wewe ni mvuta bangi kwanza wewe ndio inabidi uwe wa kwanza kufanya iniatives za uchunguzi kitalaam ili umuumbue yule jamaa. Sasa tunaposema uchunguzi huru uchukuliwe na uanzie CHADEMA kama uko safi unaogopa nini?? mi nadhani ndio mda wakuchukua ujiko yani usafi wako machoni kwa watu.

Mtu ukiona anapinga kufanyiwa uchunguzi huru jua kuna jambo.Mtu akikutuhumu kwako ndani kuna gongo na wachunguzi huru wakaja kukagua ndani mwako kama kuna pombe ya gongo na kama wewe ni msafi na gongo hiyo haimo ndani utachekelea na kuwakaribisha kwa furaha.

Ok hizo halimashauri kuna nyingine kama sikosei ni ya ZITO ,nyingine sijui

Acha kubahatisha wewe.Kazi kudandia fani za watu tu
 
Katika hili, inaonekana chochote kile kitakachoonekana kwenda kinyume na yale yanayotakiwa kufanyika kitakumbana na vikwazo na usumbufu mwingi huku pia watu wa Tarime tukiwekwa hostage na kuamshwa emotions zetu kiaina kwa propaganda bab kubwa inayoendeshwa na TBC1 na magazeti yote ya Rostam Azizi na wapambe wake.

Amen

Mimi natamani sana kuona tatizo la TBC1... kwa sababu hawa mabwana kila kitu wanachosema wanaonyesha... I need to learn it.
 
Mwanakijiji angalia kile kipengele kinachosema baada ya kuona hayo,maafisa usalama.........ndio utaona hadi koma zipo sehemu moja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom