Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Unaporipoti tukio unaliripoti kutoka na mtitiriko ulivyokuwa.ikiwa sikukuu ya uhuru kama kuna magazeti yameandika kitatofautiana kichwa cha habari tu lakini habari itakuwa kama ilivyokuwa.
ukiripoti mpira kama goli alifunga DROGBA kila gazeti litaandika kuwa ni DROGBA.
Huwezi kuumuliza mwanakjj kwani sio EXPERT wa Journalism, wala huwezi kuyakosoa magazeti ambayo yameajiri watalaam wa fani hiyo ya habari.

Hivi wewe unafikiri tulioko hapa ni mbumbumbu eeh, mimi ni ni EXPERT, na ndio maana nimeliangalia tukio zima na kuamua kulifuatilia, kwenye hili huwezi kumtetea kwani amechemsha Rostam Azizi.
 
His legacy will always live, na kuanzia hapo ndo mtajua effect ya kifo chake itaibua wangapi kama yeye na zaidi ya yeye.
 
vyombo vya habari tanzanai vinatia aibu! maana havina hata mtu wa kupitia habari basi wakaona makosa??!!
 
Mengi yatasemwa lakini kifo cha WANGWE kuna utata mkubwa,jamaa alikuwa na influence kubwa sana kwa wananchi sijui kama kuna mbunge anayependwa kwa kuwatetea wananchi kama yeye wengine wote MAFISADI nafikiri hata CCM wameona jinsi wananchi walivyokuwa wanampenda mbunge wao
Historia yake kweli inaonyesha jamaa alikuwa MWANAMAPINDUZI kwani jamaa aliwahi kufungwa jela akatoka na akaendelea na mapambano hadi kupata nafasi ya kuwakilisha wananchi wake ,alikuwa kama MANDELA
Pamoja na kuwa wabunge wanakopeshwa MASHANGINGI lakini jamaa alikuwa na COROLA
Jamani naomba tumzike ndugu yetu apumzike kwani ninavyojua nchi zetu za kiafrika hakuna haki
......EE MUNGU MPUMZISHE KWA AMANI CHACHA WANGWE..........
.....................AMEN..................
 
Last edited:
Jukwaa la wahariri limeshap taarifa za kuwepo kwa coocked stories from tarime, litakutana kesho kujadili
 
I am so stressed i dont know what to do, i cant stand this jamani, it hurts so bad, until when lakini? ah, am out of here.
 
vyombo vya habari tanzanai vinatia aibu! maana havina hata mtu wa kupitia habari basi wakaona makosa??!!

walikuwa wanakimbilia kutenda dhambi (ya uongo) na MUNGU amewaumbua.
Itabidi editors wa haya magazeti watajwe hapa ili waanze kuaibika. Aibu kubwa sana wameipata.

Walitaka kuleta vita na vurugu Tarime na matokeo yake MUNGU amewaumbua hadi wanashindwa kumtaja mwanasiasa ambaye amekuwa kwenye siasa za Tanzania kuanzia wakati wa Mwinyi -Mbatia.
 
Kiranja naona nikushukuru kwa post kabisaaaaa

RA tunamtaka peupe. Leteni habari yake hapa tumshughulikie.
Iweje ndani ya nchi yetu tunakuwa treated kama vijinzi tu??

Nitamtaka Mtikila atoe tamko la kuwashughulikia Magabachori sasa hivi.

This is our country Let no one trouble us here.

Mkuu,huu uwezo wa kuamrisha watu unautoa wapi?
 
Invisible, Kiranja:

Kwa maelezo yenu ni wazi kwamba akina Rostam na mafisadi wenzake katika CCM wameamua kuutumia msiba huu na ugomvi uliokuwepo kati ya marehemu na viongozi wenzake kama njia ya kutokea. Hata hivyo mbinu hii mimi hainishangazi kwani inatarajiwa katika uongozi ambao hawana cha kujivunia na wamepoteza sifa za kutawala isipokuwa watumie ghiliba, ujanjaujanja, umafia na mapepo.

Kinanishangaza na kunisikitisha ni hawa watanzania wenzetu wanaofanya kazi ya uandishi wa habari katika haya magazeti yaliyoandika hizi habari; iweje hawa wenzetu wakubali kuuza utu na uhuru wao na kukubalika kutumika kiasi hiki? Kwa nini waandishi wa habari watanzania wamekubali kuwekwa kwenye mfuko wa mtu mmoja anayeitwa Rostam kwa visenti? Kwa nini wameamua kujidhalilisha namna hii?

Ni hawahawa waandishi waliowalisha watanzania sumu pale walipomvalisha JK ngozi ya malaika kiasi kwamba watanzania kwa mamilioni wakapagawishwa, wakiwemo viongozi wetu wa dini hadi wakaenda mbali na kusema JK ni chaguo la Mungu. Leo hii JK mambo yamemshinda, sio kwa kupenda bali kwa kuwa hakuwa na bado hana sifa alizopewa, wamebaki kukodoa macho, na visenti walivyopewa walishakula na wala havikuwasaidia kupeleka watoto wao shule. Lakini bado hawakujifunza na wanaendelea kuwalisha watanzania sumu ya habari kwa ajira ya visumuni.

Mimi nasema katika kazi kubwa tuliyo nayo huko mbele ni kuwatoa kwenye umateka hawa wenzetu wanaofanya kazi ya uandishi wa habari. Ni kazi ngumu lakini lazima tuifanye.
 
huwezi kukosea hadi jina la Mbatia.

Eti na hili linahitaji taaluma ya uandishi wa habari.

Nguvu iliyokuwa hapa jana inaonyesha kabisa kuwa FISADI aliyekuwa anaimbisha watu alikuwa siyo wa kawaida.

Nafikiri mafisadi wote walikuwa wameongeza nguvu zao.

Lakini wajue watanzania wameisha toka usingizini kidogo, wakigundua wanachukua hatua haraka sana kama lile jambo la kupeleka msaada kanisani.

Hili suala baada ya wiki litakuwa wazi na watu wataumbuka na magezeti husika yataumbuka tu, na pia kama TBC1 wanatumiwa mwisho wa siku watakuja kujuta tu. Nimeamini mafisadi wana nguvu za kutisha.
 
mbowe_phixr.jpg

Hapa ndio walikuwa wanafika msibani ambako vurugu ilitokea au ndio walikuwa njiani? hadi Mbowe akakimbizwa wakati alipofika tu?
 
It is absolutely unfair to group all people of Mara by using the ideas of one person, that is totally unfair Mr.Majita.Nevertheless I failed to get your logical by asking gibberish questions to Mr.magabhe, anyway this is Africa, and I’m not worrying because the people of your breed are so many in Tanzania and they always try to impel good Tanzanians from the topics on discussions. What I could wish to see, is become one on the issues which makes many people to be in dilemma, by entertaining these behaviours don’t expect to end evils in Tanzania.
 
mbowe_phixr.jpg

Hapa ndio walikuwa wanafika msibani ambako vurugu ilitokea au ndio walikuwa njiani? hadi Mbowe akakimbizwa wakati alipofika tu?

Mzee Mwanakijiji,

Kuna watu walijenga dhana kuwa watu wa Tarime ni wanyama na wakilishwa sumu kidogo tu na TV ya serikali na magazeti basi watakimbia kama mbwa wa mwitu na kushambulia makabila, koo, na wengine ambao wametofautiana nao kiitikadi.

Walitaka kuchonganisha wachaga na wakurya, wanyabasi na watimbaru na zaidi sana kuchonganisha wanatarime kwa misingi ya itikadi za vyama. Walipata aibu ya mwaka pale walipoona hakuna fujo wala vita inayotokea Tarime (nadhani TBC wameumia sana maana walikuwa wamejiandaa kureport mapigano na fujo za Tarime). Wakaamua sasa kuandika habari za uongo na sasa wanaumbuka kwa kuchapisha habari ambayo inaonekana hata haikufanyiwa uhariri.

Habari katika magazeti yote haya inafanana hadi nukta? wanakosea jina la Mbatia na hakuna editor hata mmoja aliyeona hili? Only in Tanzania.
 
DADA YANGU Sakina ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri najua kuwa wewe sio FISADI na unapinga UFISADI, sasa kama ni kweli kuwa kesho mtakutana lazima mseme ukweli na kuwaomba radhi watanzania , la sivyo MAFISADI wakiwazidi nguvu na kukuzidi wewe tafadhali jiuzulu uenyekiti kwa masilahi ya taaluma ya habari na hakika hutakufa njaa kwa kuwa sio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri.

Kama hutachukua hatua dhabiti hakika hili litakuwa ni jambo la hatari na hata historia yako ambayo tayari umeiweka inaweza kufuatwa na jinamizi hili .

Andika historia kwenye hili na hapo utaweza kuiokoa taaluma ya uandishi wa habari.
 
mbowe_phixr.jpg

Hapa ndio walikuwa wanafika msibani ambako vurugu ilitokea au ndio walikuwa njiani? hadi Mbowe akakimbizwa wakati alipofika tu?

hapo itakuwa baada ya kwenda mbio .......huoni walivyokuwa wanavuja jasho na damu kwa mbali!
 
This is discussion is not healthy at all. What I suggest let us go back and start looking at EPA an putting some more and more pressures on RICHMUND
 
I am so stressed i dont know what to do, i cant stand this jamani, it hurts so bad, until when lakini? ah, am out of here.

Don't give up! One day, one day yes, we will raise up. Be courageous, be strong, be smart, stay safe and alive. One day, yes one special day.
 
Invisible, Kiranja:

Kwa maelezo yenu ni wazi kwamba akina Rostam na mafisadi wenzake katika CCM wameamua kuutumia msiba huu na ugomvi uliokuwepo kati ya marehemu na viongozi wenzake kama njia ya kutokea. Hata hivyo mbinu hii mimi hainishangazi kwani inatarajiwa katika uongozi ambao hawana cha kujivunia na wamepoteza sifa za kutawala isipokuwa watumie ghiliba, ujanjaujanja, umafia na mapepo.

Kinanishangaza na kunisikitisha ni hawa watanzania wenzetu wanaofanya kazi ya uandishi wa habari katika haya magazeti yaliyoandika hizi habari; iweje hawa wenzetu wakubali kuuza utu na uhuru wao na kukubalika kutumika kiasi hiki? Kwa nini waandishi wa habari watanzania wamekubali kuwekwa kwenye mfuko wa mtu mmoja anayeitwa Rostam kwa visenti? Kwa nini wameamua kujidhalilisha namna hii?

Ni hawahawa waandishi waliowalisha watanzania sumu pale walipomvalisha JK ngozi ya malaika kiasi kwamba watanzania kwa mamilioni wakapagawishwa, wakiwemo viongozi wetu wa dini hadi wakaenda mbali na kusema JK ni chaguo la Mungu. Leo hii JK mambo yamemshinda, sio kwa kupenda bali kwa kuwa hakuwa na bado hana sifa alizopewa, wamebaki kukodoa macho, na visenti walivyopewa walishakula na wala havikuwasaidia kupeleka watoto wao shule. Lakini bado hawakujifunza na wanaendelea kuwalisha watanzania sumu ya habari kwa ajira ya visumuni.

Mimi nasema katika kazi kubwa tuliyo nayo huko mbele ni kuwatoa kwenye umateka hawa wenzetu wanaofanya kazi ya uandishi wa habari. Ni kazi ngumu lakini lazima tuifanye.

Isije kuwa ndiyo maana aliamua kuwatetea waandishi uchwara na kusema wasiitwe kanjanja kisa kwa sasababu anataka kuandikwa vizuri. Nonesense and pathetic suggestions!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom