Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Hebu tuangalie mlingano huo wa habari:

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amenusurika kauawa kwa mapanga na mishale, baada ya kuwasili katika kijiji cha Kemakorere, kuhudhuria maziko ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe.
Sakata hilo lilianza kujitokeza jana saa nane mchana baada ya Bw. Mbowe kuwasili kijijini hapo akifuatana na viongozi wengine wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustino Mrema (TLP), Bw. Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Bw. Bob Makani Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA. - Majira

My Take:
Kuna mtu alikuwa anaimbishwa kama kasuku!

Yaani wapuuzi hata kubadilisha paragraph wanashindwa? Hata ku re-arrange order ya majina wanashindwa?

Yaani hata kama mnapeleka papers kwa mwalimu lazima awalime!

Hii ndiyo journalism yetu!
 
My man, kumbe na wewe ulizipata za RA kufanya hii kitu? Leo napewa taarifa na jamaa yangu akidai mwandishi wa habari kwa magazeti yote leo ni mmoja ila kwa majina ya kutungwa, nafika hapa nakuta umeweka ujumbe huu pia. Hii inadhihirisha ukweli wa jambo hili. Why this lakini? Hizi siasa za kuchafuliana majina zinatokana na nini? Kwanini msiba huu utumiwe kuchafuana kwa namna hii kwa njia ya vyombo vya habari?

Inasikitisha sana kwani ulichosema ni kweli habari hizi zimefanana SANA na nadhani hawakujua kuwa si wote waliolala.

Kudos mate!

Rest In Peace Chacha Wangwe.

Habari lazima zifanane sababu zinazungumzia tukio moja, lazima kuna maneno mengi ya kufanana.

kama magazeti yote yamesema habari inayofanana isipokuwa gazeti la MBOWE(Tanzania Daima) basi tufuate magazeti mengi kuliko kufuata gazeti la Mbowe ambalo haliwezi kutueleza jinsi MBOWE alivyokoswakoswa kuuawa.

CCM na Rostam hawawezi kumuua Wangwe wala kutumia nguvu za namna hiyo, chama kikuu cha upinzani ni CUF na ndio wamekuwa wakiisumbua CCM toka 1992 kama wana uwezo huo wangewaua watu wa CUFambao wameipaka matope serikali na CCM hadi umoja wa mataifa na nchi nyingi za ulaya,

Chadema hawana kubwa walilofanya kiasi cha Wangwe kupotezwa maisha yake na CCM.

baada ya kifo cha Wangwe watu wa chadema hasa Mwanakijiji wamekuwa wakitumia mitandao na kupeleka maoni kwenye magazeti kama Tanzania Daima la jumatano kuwa CCM wanahusika na hilo la Wangwe,kwanini ghafla wawe na mapenzi na Wangwe?

kuna sehemu Mwanakijiji ameandika kuwa simu ya WAngwe haikukutwa na number ya MBOWE,swali jepesi kwa wote inajulikana Wangwe alikuwa hasemi na Mbowe,sababu ipi itapelekea aisave kwenye simu yake namba ya hasimu wake?
lakini walipokufa kina Chifupa na mtoto wa Malecela wachawi walitafutwa ndani ya CCM, vipi kifo cha Wangwe mchawi atafutwe nje ya Chadema?
polisi wafuatilie ugomvi mkubwa kati ya Mbowe na kundi lake dhidi ya Wangwe wanaweza kupata ushahidi mzuri sana.
 
Ben karibu katika mtandao.
Nafikiri hilo ni kubwa zaidi kwako. kukaribishwa na kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Nikuhakikishie kuwa ndani ya huu mtandao kuna watu ambao kamwe hawatajinyima uhuru wa kufikiri, kusikiliza na kusema hadharani.
Nikuhakikishie mpendwa kuwa hoja zako kadhaa hapa jukwaani zinatoa taarifa kuwa ama hutaki kufikiri au hutaki watu wafikiri.

Sasa kwa wale wanaofikiri huwa wanaunganisha habari kwa ajili ya kuchambua na kufikia ukweli uliofichika.

Kuhusu CHADEMA: mimi sifikiri kuwa CHADEMA inahitaji wanachama wanaowafuata kimkumbo. Nitakiheshimu chama kama kinawapa fursa watu wake kuchunguza mambo, kujadili mambo na kuyasema hadharani. Unaposema kuwa matusi na madongo kutoka kwa wanachama wa CHADEMA hapa mtandaoni vimewafanya baadhi kujiengua na kuside na CCM. Hii ninakupinga sana na ninakuomba usilete jukwaani propagana za kishamba namna hiyo tena.

Sasa tunahitaji vichwa vitumike hadi tupate uhakika kuwa nini kilimuua Chacha. Tunahitaji kutumia vichwa ili wale ambao tayari wameaminishwa vinginevyo wajue ukweli halisi.

Ben tafadhali tutendee haki, kabla hatujakulist upande ulio kinyume nasi.

Kwanza kabisa nashukuru kunikaribisha mwenyeji ambae nilikuapo tena inawezekana kabla yako.

SASA NI WAPI NIMESEMA HAYO YOTE ULIYOANDIKA HAPO? Mimi nimefanya quotation na inaonekana kabisa.Sasa weweunanililia nini hapa? Si uwe unasoma kabla ya kuandika Na kama hujaelewa uliza.
 
Habari za ndani kabisa zinasema kuwa maamuzi ya familia yanaelekea kwenye kuzika mwili ili yaishe. Keba na Samuel (Prof) Wangwe wanajulikana Tarime kwa kutopenda maneno mengi na mwelekeo hapa ni kuwaambia wana Tarime kuwa yamekwisha na watu wazike, walie, waomboleze, na kisha kuendelea na kazi zao za maendeleo.

Katika hili, inaonekana chochote kile kitakachoonekana kwenda kinyume na yale yanayotakiwa kufanyika kitakumbana na vikwazo na usumbufu mwingi huku pia watu wa Tarime tukiwekwa hostage na kuamshwa emotions zetu kiaina kwa propaganda bab kubwa inayoendeshwa na TBC1 na magazeti yote ya Rostam Azizi na wapambe wake.

Katika hili, ukweli utajulikana mioyoni mwetu no matter what they do. Sisi sio wajinga na watu wa Tarime sio wanyama kama wengine wanavyotuonyesha hapa. Thanks GOD hakuna ugomvi au mapigano yaliyotokea kama wengine wenye nia mbaya na Tarime walivyotaka. MUNGU ashukuriwe kwa kuwalinda na kuwatunza watu wote wa Tarime.

Chacha Wangwe, umepigania mengi sana kwa maisha ya wana Tarime. Kwa miaka zaidi ya 15 umekuwa mstari wa mbele kutusaidia watu wa Tarime kwa kila kitu - kuanzia sheria batili za ulinzi wa sungusungu hadi kwenye sheria onevu za watoza kodi wa halmashauri ya Tarime. Umekuwa mstari wa mbele kwa sana kuwaunganisha wamiliki wadogowadogo wa machimbo ya madini kupambana na makampuni makubwa ya kifisadi ambayo sasa yatafurahia kuondoka kwako.

Chacha umekuwa mstari wa mbele kujaribu kusuluhisha migogoro ya ardhi Tarime hata pale ambapo serikali ilionekana kupuuzia. Nakumbuka nilipokuwa shule ya upili ulianzisha kampeni ya kuondoa adhabu zisizo na maana kwa watoto wa shule, kampeni ambayo ilikuchukua karibu miaka kumi kufanikiwa. Chacha Wangwe - rastafarian, nakumbuka ulinifundisha maneno halisi ya nyimbo za Bob Marley na Dube na kuniambia tafsiri yake nikiwa kinda tu.

Chacha Wangwe, watu wa Tarime tutakukumbuka milele kwa yote mema uliyofanya na tutasahau milele zile tofauti za kawaida za kibinadamu ambazo zimeweza kuwa zimetokea.

MUNGU wa mbinguni ailinde familia yako na ndugu zako. Kuna watakaodhani kuwa wameshinda kwa yaliyotokea lakini MUNGU wa mbinguni ataleta Chacha mwingine kutoka kwa jamii ya wakurya wa Tarime ambaye atafanya yote yale uliyotaka yafanyike na kuendeleza mazuri zaidi. Kuna wanaodhani kuwa huu msiba wako ndio utamaliza upinzani Tanzania. Hata kama Chadema na NCCR - vyama ambavyo ulivihamasisha sana Tarime vitakufa, bado ari na nia ya kuwa na serikali bora Tarime na Tanzania itaendelea kuwa mioyoni mwa wana Tarime forever and ever.

Kwaheri Wangwe, kwa heri rasta man, kwa heri mpambanaji, kwa heri murra, kwa .....inhi inhi inhi hiiiiiiiiiiiiiiiii inhi .... uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ENOKWE ikuhituke naghukuha ahasi ha kumunya hano YESO aricha.

Amen

Very emotional mura weito! Utaya Umunye Rasta
 
Kuna habari kwamba Wangwe anazikwa jioni hii kijijini kwake na hii ni baada ya Postmortem iliyochukua saa 4, katika hospitali ya wilaya ya Tarime. Habari zaidi baadaye.

Yanaelekea huku.

Walichotaka kitokee (mafisadi) wamekipata, Wangwe atazikwa na watu wa Tarime tutalia, tutaumia, na kisha tutaendelea na kazi zetu bila vurugu na vita wala chuki kwa mtu yeyote isipokuwa mafisadi. Hatutachukia kabila au itikadi au koo yoyote bali tutachukia ufisadi.

Wametuonyesha namna wasivyotupenda. wametumia TV ya serikali kutaka fujo na machafuko vitokee Tarime. Wametumia polisi na magazeti kutaka kuvuruga amani Tanzania. Watafaidika na nini Tarime kukitokea vita?

Wangwe amekwenda na wao wanatoa onyo kuwa hawataki kutusikia tukidai au kusema chochote kinachotuhusu. Wanataka tukae kimya kama wagonjwa wasio na tumaini lolote. Wanataka tuwaogope na hata tusijaribu hata kidogo kuibadili na kuiendeleza Tanzania.

Tutamzika Wangwe kama ndilo wanalotaka, lakini je watanyamazisha kila mtu, na kama wakitunyamazisha sisi, je watanyamazisha watoto wetu, wajukuu na vitukuu vyetu?
 
Kuna habari kwamba Wangwe anazikwa jioni hii kijijini kwake na hii ni baada ya Postmortem iliyochukua saa 4, katika hospitali ya wilaya ya Tarime. Habari zaidi baadaye.

Sometimes najikuta nacheka mwenyewe.... hivi hawa serikali wana lugha gani iliyo tamu kiasi cha kuwalainisha watu wenye machungu nayo?/ Nakumbuka kesi ya Marehemu Dito... wahanga wa kijana Ndonde sijui Mbonde mwanzo walikuwa wakali kisha wakaafiki kuwa ilikuwa bahati mbaya-- ile kesi ilikuwa imeshakwisha ilibaki geresha tu. sasa hapa najiuliza nini matokeo ya postmortum? au ndo yale yale ya lugha ya kutongozea wanayoitumia hawa wakulu? au ni vitisho ??
 
Kiranja naona nikushukuru kwa post kabisaaaaa

Naomba invisible utupe kinachoendelea katika mazishi hayo huko Kemakorere tafadhali.

Hakikisheni kuwa kila mwenye habari anazimwaga hapa. hakuna mtu wa kuogopwa nchini Tanzania. Kama ni kuonewa, kunyanyaswa na kudhalilishwa tumefanyiwa vya kutosha. RA tunamtaka peupe. Leteni habari yake hapa tumshughulikie.
Iweje ndani ya nchi yetu tunakuwa treated kama vijinzi tu??

Nitamtaka Mtikila atoe tamko la kuwashughulikia Magabachori sasa hivi.

This is our country Let no one trouble us here.
 
Niliandika haya maneno mapema zaidi ya masaa tisa yaliyopita sasa yanaelekea kutimia,yapo post 1037.

Nina taarifa kuwa liwalo na liwe leo watazika mwili na ndugu wa marehemu wataachwa kwenye mataa ,kwani tayari agizo limeshatolewa kuwa ni lazima wazike.
 
naENDELEA NA NITAENDELEA KUSEMA MPAKA THREAD HII IFUNGWE..................... HII NI CONSPIRANCY NA SERIKARI YA CCM INAHUSIKA KWA ASILIMIA 110 %%......NIA NI KUUSAMBARATISHA KABISA UPINZANI.UFISADI UENDELEE KAMA KAWAIDA...........NDUGU WANANCHI TUSIKUBALI HILA HII..............NARUDIA TENA POLE SANA NDUGU NA JAMAA WA CHACHA WANGWE KWA NDUGU YAO KUA VICTIM WA HII SECRET PLAN..... INAUMA SANA
 
siku tutakayo tamani tufe ni pale mbunge mpya wa tarime atakapokuja kumuuliza PM bungeni, mh. kwanini chacha alikufa? na majabu yatakapokuwa, ilibidi afe hili kulinusuru taifa.

Biko (Steve) was arrested by police in 1977 and died in detention, naked and manacled, from extensive brain damage, six days later. His death caused international protest and a UN arms ambargo. An inquest in the late 1980s found no one responsible for his death, BUT in 1997 former five policemen adamitted being involved.

Kifo cha MH. Wangwe kinaweza kuanzisha movement ambayo nchi haijawahi kuishuhudia hata siku zile za kudai uhuru. Who said case closed???
ALUTA CONTINUA
 
Mwanakijiji angalia kile kipengele kinachosema baada ya kuona hayo,maafisa usalama.........ndio utaona hadi koma zipo sehemu moja.
Unaporipoti tukio unaliripoti kutoka na mtitiriko ulivyokuwa.ikiwa sikukuu ya uhuru kama kuna magazeti yameandika kitatofautiana kichwa cha habari tu lakini habari itakuwa kama ilivyokuwa.
ukiripoti mpira kama goli alifunga DROGBA kila gazeti litaandika kuwa ni DROGBA.
Huwezi kuumuliza mwanakjj kwani sio EXPERT wa Journalism, wala huwezi kuyakosoa magazeti ambayo yameajiri watalaam wa fani hiyo ya habari.
 
Mhh!! Hapa kuna kazi kweli kweli.

Enzi zile pale Mlimani tulikuwa tunaita KuDessa.
Yaani kuwa na list ndefu ya possibles na kuzikariri kwa moyo wako wote kabla ya mtihani.
Waandishi wetu wa habari au wana pigwa Imla na Mfisadi fulani au wana Dessa kutoka kwa mwandishi wanaye dhani anamajibu ya kila kitu.
Kifo cha Wangwe kitawaibua na kuwaweka wazi Vibaraka na wababaishaji wote katika fani ya uandishi.
 
Habari za ndani kabisa zinasema kuwa maamuzi ya familia yanaelekea kwenye kuzika mwili ili yaishe. Keba na Samuel (Prof) Wangwe wanajulikana Tarime kwa kutopenda maneno mengi na mwelekeo hapa ni kuwaambia wana Tarime kuwa yamekwisha na watu wazike, walie, waomboleze, na kisha kuendelea na kazi zao za maendeleo.

Katika hili, inaonekana chochote kile kitakachoonekana kwenda kinyume na yale yanayotakiwa kufanyika kitakumbana na vikwazo na usumbufu mwingi huku pia watu wa Tarime tukiwekwa hostage na kuamshwa emotions zetu kiaina kwa propaganda bab kubwa inayoendeshwa na TBC1 na magazeti yote ya Rostam Azizi na wapambe wake.

Katika hili, ukweli utajulikana mioyoni mwetu no matter what they do. Sisi sio wajinga na watu wa Tarime sio wanyama kama wengine wanavyotuonyesha hapa. Thanks GOD hakuna ugomvi au mapigano yaliyotokea kama wengine wenye nia mbaya na Tarime walivyotaka. MUNGU ashukuriwe kwa kuwalinda na kuwatunza watu wote wa Tarime.

Chacha Wangwe, umepigania mengi sana kwa maisha ya wana Tarime. Kwa miaka zaidi ya 15 umekuwa mstari wa mbele kutusaidia watu wa Tarime kwa kila kitu - kuanzia sheria batili za ulinzi wa sungusungu hadi kwenye sheria onevu za watoza kodi wa halmashauri ya Tarime. Umekuwa mstari wa mbele kwa sana kuwaunganisha wamiliki wadogowadogo wa machimbo ya madini kupambana na makampuni makubwa ya kifisadi ambayo sasa yatafurahia kuondoka kwako.

Chacha umekuwa mstari wa mbele kujaribu kusuluhisha migogoro ya ardhi Tarime hata pale ambapo serikali ilionekana kupuuzia. Nakumbuka nilipokuwa shule ya upili ulianzisha kampeni ya kuondoa adhabu zisizo na maana kwa watoto wa shule, kampeni ambayo ilikuchukua karibu miaka kumi kufanikiwa. Chacha Wangwe - rastafarian, nakumbuka ulinifundisha maneno halisi ya nyimbo za Bob Marley na Dube na kuniambia tafsiri yake nikiwa kinda tu.

Chacha Wangwe, watu wa Tarime tutakukumbuka milele kwa yote mema uliyofanya na tutasahau milele zile tofauti za kawaida za kibinadamu ambazo zimeweza kuwa zimetokea.

MUNGU wa mbinguni ailinde familia yako na ndugu zako. Kuna watakaodhani kuwa wameshinda kwa yaliyotokea lakini MUNGU wa mbinguni ataleta Chacha mwingine kutoka kwa jamii ya wakurya wa Tarime ambaye atafanya yote yale uliyotaka yafanyike na kuendeleza mazuri zaidi. Kuna wanaodhani kuwa huu msiba wako ndio utamaliza upinzani Tanzania. Hata kama Chadema na NCCR - vyama ambavyo ulivihamasisha sana Tarime vitakufa, bado ari na nia ya kuwa na serikali bora Tarime na Tanzania itaendelea kuwa mioyoni mwa wana Tarime forever and ever.

Kwaheri Wangwe, kwa heri rasta man, kwa heri mpambanaji, kwa heri murra, kwa .....inhi inhi inhi hiiiiiiiiiiiiiiiii inhi .... uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ENOKWE ikuhituke naghukuha ahasi ha kumunya hano YESO aricha.

Amen

I dedicated this song for u RASTA CHACHA

Verse 1
I love to see my people living in love
I hate to see them fighting and swimming in blood
Nuff neglect the farming, scourning the mud
Yet they wanna be the first to reap the food as it bud
Oh, dem fill the earth wid prison, church, and whorehouse
Love the rum-bar, yet dem hate the pure-house
Dem tek di micro-chip, and now a wrath go pour out
Less food, more drought and more mouth

Chorus
Oy, rasta tell dem all di while
Stop war and go till di soil
Stop fighting for land and oil
Fi di coil, so many go defile
Slavemaster spit inna dem face, dem tek dat wid a smile
The banks of the Nile, so mild and so fertile
Acres mores than a zillion mile
People acting vile, pick up cannibal style
Waan devour mama, papa, and child

Verse 2
Oh, sew thy seed and let it buss earth
Dem say dem ting deh tek too long fi grow and start to cuss earth
I couldn’t trust none a those as how I trust earth
Such is life, dem say a just earth
High Tikasha Heights, weh dem call this spot a land
Some say fi government, some say fi Mattaland
Still no waan share although dem got a lot a land
Dem waan fi turn inna gun range and shotta land

Chorus

Verse 3
Politician a talk, certain ting dem nah mention
Say a drugs and gun di people tax money spend pon
Come wid plastic smile and dem wicked intention
Inna yuh hand, a weh dem put dem evil invention
Turn gun model, seeking attention
See it deh now yuh dead and death is no redemption
Parents a wonder where to get the first cent from
To bury di dead, dem not even got pension

RIP RASTA CHACHA
 
Rest In Peace Chacha Wangwe.

Habari lazima zifanane sababu zinazungumzia tukio moja, lazima kuna maneno mengi ya kufanana.

kama magazeti yote yamesema habari inayofanana isipokuwa gazeti la MBOWE(Tanzania Daima) basi tufuate magazeti mengi kuliko kufuata gazeti la Mbowe ambalo haliwezi kutueleza jinsi MBOWE alivyokoswakoswa kuuawa.

CCM na Rostam hawawezi kumuua Wangwe wala kutumia nguvu za namna hiyo, chama kikuu cha upinzani ni CUF na ndio wamekuwa wakiisumbua CCM toka 1992 kama wana uwezo huo wangewaua watu wa CUFambao wameipaka matope serikali na CCM hadi umoja wa mataifa na nchi nyingi za ulaya,

Chadema hawana kubwa walilofanya kiasi cha Wangwe kupotezwa maisha yake na CCM.

baada ya kifo cha Wangwe watu wa chadema hasa Mwanakijiji wamekuwa wakitumia mitandao na kupeleka maoni kwenye magazeti kama Tanzania Daima la jumatano kuwa CCM wanahusika na hilo la Wangwe,kwanini ghafla wawe na mapenzi na Wangwe?

kuna sehemu Mwanakijiji ameandika kuwa simu ya WAngwe haikukutwa na number ya MBOWE,swali jepesi kwa wote inajulikana Wangwe alikuwa hasemi na Mbowe,sababu ipi itapelekea aisave kwenye simu yake namba ya hasimu wake?
lakini walipokufa kina Chifupa na mtoto wa Malecela wachawi walitafutwa ndani ya CCM, vipi kifo cha Wangwe mchawi atafutwe nje ya Chadema?
polisi wafuatilie ugomvi mkubwa kati ya Mbowe na kundi lake dhidi ya Wangwe wanaweza kupata ushahidi mzuri sana.

Acha mchezo wako wa kumtete ROSTAM KWENYE hili, jana alifanya kitu gani?subirini watu tumechoka na huyu jamaa RA tutaweka taarifa zake kwenye hili zote zote na kwa ushahidi wote.

Aseme jana kwanini alifanya alichofanya?
 
Unaporipoti tukio unaliripoti kutoka na mtitiriko ulivyokuwa.ikiwa sikukuu ya uhuru kama kuna magazeti yameandika kitatofautiana kichwa cha habari tu lakini habari itakuwa kama ilivyokuwa.
ukiripoti mpira kama goli alifunga DROGBA kila gazeti litaandika kuwa ni DROGBA.
Huwezi kuumuliza mwanakjj kwani sio EXPERT wa Journalism, wala huwezi kuyakosoa magazeti ambayo yameajiri watalaam wa fani hiyo ya habari.

huwezi kukosea hadi jina la Mbatia. Haiwezekani magazeti yote haya yakakosea jina la Mbatia. Kwenye mtiririko nakubaliana nawe lakini kwenye jina la Mbatia hapo inayonyesha kabisa kuwa mwandishi wa hiyo habari ni mmoja. Swali la kujiuliza ni kuwa, imekuwaje magazeti yote haya ambayo inasemekana kuwa yana wamiliki tofauti na ambayo yanadai kuwa yalikuwa na waandishi wao Tarime kuchapisha habari toka kwa mwandishi mmoja? Nia hapa ni nini?
 
Rest In Peace Chacha Wangwe.

Habari lazima zifanane sababu zinazungumzia tukio moja, lazima kuna maneno mengi ya kufanana.

kama magazeti yote yamesema habari inayofanana isipokuwa gazeti la MBOWE(Tanzania Daima) basi tufuate magazeti mengi kuliko kufuata gazeti la Mbowe ambalo haliwezi kutueleza jinsi MBOWE alivyokoswakoswa kuuawa.

CCM na Rostam hawawezi kumuua Wangwe wala kutumia nguvu za namna hiyo, chama kikuu cha upinzani ni CUF na ndio wamekuwa wakiisumbua CCM toka 1992 kama wana uwezo huo wangewaua watu wa CUFambao wameipaka matope serikali na CCM hadi umoja wa mataifa na nchi nyingi za ulaya,

Chadema hawana kubwa walilofanya kiasi cha Wangwe kupotezwa maisha yake na CCM.

baada ya kifo cha Wangwe watu wa chadema hasa Mwanakijiji wamekuwa wakitumia mitandao na kupeleka maoni kwenye magazeti kama Tanzania Daima la jumatano kuwa CCM wanahusika na hilo la Wangwe,kwanini ghafla wawe na mapenzi na Wangwe?

kuna sehemu Mwanakijiji ameandika kuwa simu ya WAngwe haikukutwa na number ya MBOWE,swali jepesi kwa wote inajulikana Wangwe alikuwa hasemi na Mbowe,sababu ipi itapelekea aisave kwenye simu yake namba ya hasimu wake?
lakini walipokufa kina Chifupa na mtoto wa Malecela wachawi walitafutwa ndani ya CCM, vipi kifo cha Wangwe mchawi atafutwe nje ya Chadema?
polisi wafuatilie ugomvi mkubwa kati ya Mbowe na kundi lake dhidi ya Wangwe wanaweza kupata ushahidi mzuri sana.

Dunia ya Tanganyika mtu hafi hivi hivi tu ila kwa mazingara.
 
Jambo kubwa na ambalo ningetaka wenzangu humu mulijadili kwa kina na kuangalia kinachoendelea ni kuwa ukisoma magazeti yote ya leo isipokuwa Tanzania daima na Mwananchi ambayo yaliripoti taarifa hiyo utaona ya kuwa mwandishi wa habari hiyo alikuwa ni mtu mmoja.

Ukianza kusoma Nipashe,majira,mtanzania,kulikoni,uhuru na habari leo utaona hiki ninachosema ,kwani kuna paragrafu tatu zinafanana kila sentensi na ni zile zinazohusiana na Mbowe jinsi alivyowasili Kemakorere.

Nimefanya uchunguzi wangu tangu asubuhi leo na nimeweza kujua kuwa habari hiyo ilitumwa na Mwandishi mmoja ambaye naomba kumtaja baadae huyu mwandishi ni mwandishi wa IPP Media,na yuko based Mkoa wa Mara.

Nowashuri muweze kusoma hicho ninachosema kwenye magazeti niliyotaja ,na kisha mtaweza kuupata ukweli wenyewe jinsi ulivyo, haiwezekani waandishi tofauti wakaandika kitu kile kile kwa maneno yaleyale na paragrafu zilezile,na kila penye koma,nukta na hata mkato pakawa ni pale pale.

Nimegundua kuwa Rostam Aziz jana amekutana na wahariri na wale ambao hawakwenda aliwapigia simu kuanzia saa tisa na dakika 26 jioni na kuanza kufanya kazi yake,na ilipofikia jioni akakutana na wahariri wa habari na kuwapa bahasha maalum kwa ajili ya kuitumia story hiyo, na kuwaahidi kuwapatia donge nono na hizi nina uhakika nazo nasubiri muda wa kuziweka hadharani .

Tatu, waandishi ambao majina yao yametumika kwenye magazeti niliyotaja hawapo na kwa vile vyombo vilivyoandika majina ni majina ya kutungwa kwani waliokuwepo huko leo wamekaa na kutoa msimamo kuwa ni kwanini habari zao hazikutumika kama walivyotuma .

Prof. Wangwe anategemewa kutoa tamko jioni hii kuhusiana na habari zilizoandikwa kuhusiana na Mbowe kutimuliwa kwa mapanga,marungu n.k. ila alikuwa anashauriwa na watu watatu waliokuwa naye kuwa asifanye hivyo ila yeye anaonekana kuwa na msimamo wa kutaka kusema kilichojiri na kutoa tamko rasmi la familia .

Naenda tena kupata habari nyingine za kina kwani imebidi nikaweka watu maalum huko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa napata habari za kweli na kuna siku nitajitambulisha rasmi kuwa mimi ni nani ,na haya maandishi yangu yataendelea kuwa ni ukweli, nakumbuka jana niliandika na kuna mtu aliniuliza humu kama ninayoandika kuhusiana na magazeti yataripoti nini kama ni ukweli nami nilimjibu kuwa ni ukweli..Ndugu,Mtanzania unakumbuka ni wewe uliniuliza jana majira ya mchana saa za huku ila ilikuwa majira ya jioni huko nyumbani kama sio usiku.

Hii nayo ni habari inayopaswa kufuatiliwa kwa ukaribu na kutafitiwa haswa. MCT na MOT lazima wa-act upo this ili kufuta ile dhana ya Ukanjanja; Wamiliki na BAraza la Habari wachunguze na kuvalia njuga suala hili na kama ni kweli hatua kali zichukuliwe dhidi ya Mwandishi (Waandishi?) huyo Kanjanja.
 
nA JIMBO LA TARIME CCM MLISAHAU KABISA HADI YESU AJE, HISTORY ITAWAHUKUMU MILELE
 
Eti alipigwa risasi mdomoni ikatokea kisogoni- je mwuuaji ni deus mallya? kama ndio je alikuwa peke yake? aliwezaje kumshikia bastola na marehemu asifurukute? Ni nani wahusika hasa?

Nafunga msiba huu nikiwa na maswali mengi kuliko majibu.
R.I.P
Am out of here
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom