Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
wewe naye!!!
Nipe jina mbunge wa mwaka 1990 ,mkuu wa wilaya wa mwaka 1996 na mkuu wa polisi wa mwaka 1998 na Mbunge kabla ya Chacha anatoka kijiji gani? maana nawasi wasi na wewe kidogo.

CHADEMA ndipo sehemu ya kuanzia kuchunguzwa.

1.CHACHA alikua ktk mchakato wa mwisho kukipeleka CHADEMA mahakamani ili waeleze na kuthibitisha waliyomzushia.

2. Wangwe alivuliwa umakamu na CHADEMA kwa kua ni mzigo na anayemega siri zao

3. MBOWE alisema hawezi fanya kazi na mtu kama CHACHA

4.CHACHA alikituhumu chdema kwa kufisadi fedha

5. Ktk uhai wake watu wa chadema walidai apigwe risasi na kweli dalili za mwanzo zinaonyesha CHACHA kapigwa RISASI mbili za kichwa.

Hata ktk hali ya kawaida mtu akikwambia aisii wewe subiri nitakuchoma kisu cha tako ,na baada ya siku kadhaa kweli ukachomwa kisu ,polisi wanakuja moja kwa moja kwa yule jamaa aliyetamka hakuna cha kujadiliana hapo.

Sehemu ya kuanzia ni CHADEMA ndio waende kwingine unless labda ajali hiyo ni ya kawaida kama ajali zingine.

Sehemu ya kuanzia ni humu JF ,kwani aliyesema kuwa apigwe risasi ni Jmushi ambaye tayari kaomba radhi, sasa naona mnatafuta kumhusisha Jmushi hivi huyu ndio Mallya? Huyu JMUSHI NDIO MALLYA?
 
Acha unafiki wako, kumuunga mkono Wangwe sio lazima uandike pumba zako mtandaoni. Kuna watu wanafanya vitendo zaidi ya maneno. Maneno yako ya chuki na dhihaka kwenye msiba huu yanaonesha jinsi gani usivyojali feelings za watu wa Tarime.

Heshima ni kitu cha bure, ungepungukiwa na nini kama ungesubiria siku chache tu wenzako tukaomboleza na kuzika ndio ulete unafiki na upuuzi wako hapa?
pumba unazo wewe, umesikia marehemu kafa unajifanya mtu wa karibu wa marehemu au unataka kuwadhulumu mirathi watoto wa Marehemu Wangwe?
ulikuwa wapi wakati anazomewa hapa hapa JF? au unataka ushike daftari la mchango wa marehemu?
 
Wewe ni laghai na mzushi sana, na uzushi wako unatisha mno! Ni mtu gani wa chadema alisema Chacha apigwe risasi? Hivi huu uzushi unamtumikia nani na kwa manufaa gani, au una-abuse anonymity yako hapa?

Unafikiri kwa kuwa unatumia jina bandia basi una uhuru wa kuropoka na kupayuka unavyotaka?

Amekasirika sana baada ya kuona aliyotaka yatokee Tarime hayakutokea. Yeye alitaka watu wa Tarime waanzishe ugomvi dhidi ya wachaga na wanachadema lakini mambo yamekuwa tofauti kwani viongozi wa upinzani wote wamepokelewa vizuri sana.

yeye alitaka watu wa-Tarime waonekane kuwa ni wapenda fujo kwa mgawanyiko wa kikoo - wanyabasi dhidi ya watimbaru au koo zingine lakini watu wa Tarime wote wameungana na kuwa kitu kimoja wakati huu wa majonzi makubwa.

Aibu sana kuwa Tanzania ina watu kama Mkamap wanaotaka kupata pointi za kisiasa kwenye misiba ya wenzao.
 
5. Ktk uhai wake watu wa chadema walidai apigwe risasi na kweli dalili za mwanzo zinaonyesha CHACHA kapigwa RISASI mbili za kichwa.

.

smart attempt... "watu wa chadema" waliodai "apigwe risasi" ni kina nani na wapi walifanya hivyo? Hii ni new information, kwa sababu ukiweza kuwaonesha hao "watu wa chadema" na mimi nitakuunga mkono.
 
Sehemu ya kuanzia ni humu JF ,kwani aliyesema kuwa apigwe risasi ni Jmushi ambaye tayari kaomba radhi, sasa naona mnatafuta kumhusisha Jmushi hivi huyu ndio Mallya? Huyu JMUSHI NDIO MALLYA?

Heheh!! Mkuu angalia usijefanya watu wakose usingizi!!
 
smart attempt... "watu wa chadema" waliodai "apigwe risasi" ni kina nani na wapi walifanya hivyo? Hii ni new information, kwa sababu ukiweza kuwaonesha hao "watu wa chadema" na mimi nitakuunga mkono.[/QUOTE

Ana ugomvi na jmushi, kwani ndio aliandika na kashaomba radhi tangia awali,wametumwa hawa.
 
Sehemu ya kuanzia ni humu JF ,kwani aliyesema kuwa apigwe risasi ni Jmushi ambaye tayari kaomba radhi, sasa naona mnatafuta kumhusisha Jmushi hivi huyu ndio Mallya? Huyu JMUSHI NDIO MALLYA?

Inawezekana sio JMUSHI ila mhusika mkuu aliposoma ushauri wa JMUSHI akaamua kuufanyia kazi. JMUSHI anaweza kuwa shahidi kwenye kesi hii na akajikuta anafungwa kwa kuuua bila kukusudia(Manslaughter).

na kauli zote kama vile SIWEZI KUFANYA KAZI NA WANGWE ukitizama sana zinaweza kuwaweka watu pabaya,kama Mwanakijiji alivyoishauri Polisi hivyo hivyo na MKAMAP anajaribu kuweka mawazo yake kama Mwanakijiji na baya zaidi pale Mwenyekiti aliposema kuwa Wangwe anashiriki kukihujumu chama kwa kutoa siri za chama nje. walimwita kwenye vikao vingi kumuonya asitoe siri,hakusikia na wakampa muda ajirekebishe, wanasema hakujirekebisha,hatuleti siasa ila kama sheria inafuatwa Chadema wana kubwa la kujibu.
 
pumba unazo wewe, umesikia marehemu kafa unajifanya mtu wa karibu wa marehemu au unataka kuwadhulumu mirathi watoto wa Marehemu Wangwe?
ulikuwa wapi wakati anazomewa hapa hapa JF? au unataka ushike daftari la mchango wa marehemu?

Sio lazima uongee hapa JF ili uonekane mtu wa karibu na Wangwe. Mimi na Wangwe ni marafiki wakubwa sana na tunajuana kwa muda mrefu. Kuongea mambo ya uchochezi kama yako ni sababu moja au zaidi inayofanya watu wengine kutoongea hapa JF.

Ninajaribu kuelezea ukweli kuhusu Tarime ambao watu wengi kama wewe na kwenye media mnataka kuigawa na kupanda chuki kwa wakazi wake. Michango ya marehemu itanisaidia nini maishani? Mimi ni mtu ninayetumia jina langu hapa na hiyo inafanya nia yangu kujulikana wazi.

Labda watu wakuulize wewe unayeonyesha dharau kubwa kwa watu wa Tarime hapa mtandaoni kwa kutumia jina la bandia kuwa utafaidika na nini?
 
CCM wateta

2008-07-31 17:59:56
Na Mwandishi wetu, Jijini

Kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Tarime Bw. Chacha Wangwe, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelazimika kuteta na hatimaye kutoa salamu zake kuhusiana na kifo hicho.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, ikitolewa na Katibu Mkuu wake, Bw. Yusuf Makamba, chama hicho kimeelezea kusikitishwa kwake na msiba wa Mhe. Wangwe na kueleza kuwa mbunge huyo ameacha pengo kubwa kwa wapenzi wa demokrasia nchini.

Source: Alasiri
 
Inawezekana sio JMUSHI ila mhusika mkuu aliposoma ushauri wa JMUSHI akaamua kuufanyia kazi. JMUSHI anaweza kuwa shahidi kwenye kesi hii na akajikuta anafungwa kwa kuuua bila kukusudia(Manslaughter).

na kauli zote kama vile SIWEZI KUFANYA KAZI NA WANGWE ukitizama sana zinaweza kuwaweka watu pabaya,kama Mwanakijiji alivyoishauri Polisi hivyo hivyo na MKAMAP anajaribu kuweka mawazo yake kama Mwanakijiji na baya zaidi pale Mwenyekiti aliposema kuwa Wangwe anashiriki kukihujumu chama kwa kutoa siri za chama nje. walimwita kwenye vikao vingi kumuonya asitoe siri,hakusikia na wakampa muda ajirekebishe, wanasema hakujirekebisha,hatuleti siasa ila kama sheria inafuatwa Chadema wana kubwa la kujibu.

Nakushauri ndugu yangu kwa mara nyingine uachane na unafiki na upuuzi wako hapa wakati wengine tuko kwenye msiba. Mbowe na viongozi walikuwa kwenye msiba Tarime na watu wa Tarime hawakuwa na tatizo lolote na uwepo wao huko.

Kama mnajaribu kubadilisha ukweli kwenye hili huku mkitaka kuanzisha fujo na vurugu Tarime mmenoa. Wakazi wa Tarime ni smart kuliko watu wenye bias kama wewe mnayofikiria.
 
sio Lazima Uongee Hapa Jf Ili Uonekane Mtu Wa Karibu Na Wangwe. Mimi Na Wangwe Ni Marafiki Wakubwa Sana Na Tunajuana Kwa Muda Mrefu. Kuongea Mambo Ya Uchochezi Kama Yako Ni Sababu Moja Au Zaidi Inayofanya Watu Wengine Kutoongea Hapa Jf.

Ninajaribu Kuelezea Ukweli Kuhusu Tarime Ambao Watu Wengi Kama Wewe Na Kwenye Media Mnataka Kuigawa Na Kupanda Chuki Kwa Wakazi Wake. Michango Ya Marehemu Itanisaidia Nini Maishani? Mimi Ni Mtu Ninayetumia Jina Langu Hapa Na Hiyo Inafanya Nia Yangu Kujulikana Wazi.

Labda Watu Wakuulize Wewe Unayeonyesha Dharau Kubwa Kwa Watu Wa Tarime Hapa Mtandaoni Kwa Kutumia Jina La Bandia Kuwa Utafaidika Na Nini?
Umekuwa Karibu Na Marehemu Leo? Alipokuwa Hai Ulikuwa Wapi?
Nitumie Simu Yako Kwenye Pm Tuongee Ili Nijue Ulikuwa Na Ukaribu Upo Na Marehemu.
 
Nitakuwa Kemakorere kesho,Nitaenda Nyanungu baadae,nitaelekeza nguvu zanu Nyandoto, Hatimaye nitaenda kukutana na ndugu zangu kule Mwema hawa ni Waryanchoka na Wanchare, nitaendelea na safari mpaka Pemba kabla sijaingia Sirari na ntalala hapo.

Keshokutwa nitaenda Bumera, hatimaye nitaendelea na safari mpaka Tarime mjini nami hapo ama nitalala La Kairo ama A M hoteli kabla ya kuendelea na maombolezo yangu hadi machimboni .

Hawa wanaojifanya wanapajua Tarime waseme wanajua wapi .
 
Nakushauri ndugu yangu kwa mara nyingine uachane na unafiki na upuuzi wako hapa wakati wengine tuko kwenye msiba. Mbowe na viongozi walikuwa kwenye msiba Tarime na watu wa Tarime hawakuwa na tatizo lolote na uwepo wao huko.

Kama mnajaribu kubadilisha ukweli kwenye hili huku mkitaka kuanzisha fujo na vurugu Tarime mmenoa. Wakazi wa Tarime ni smart kuliko watu wenye bias kama wewe mnayofikiria.
mbowe,Zitto na Slaa hata Mnyika waliongozana na maiti toka Dodoma hadi MUsoma? msiba wa mwenyekiti wa mkoa,mbunge na aliyekuwa makamu mwenyekiti unajiongoza wenyewe? kweli Marehemu aliheshimwa? jibu swali hilo mnafiki mkubwa unayedai ulikuwa karibu na marehemu.
 
Umekuwa Karibu Na Marehemu Leo? Alipokuwa Hai Ulikuwa Wapi?
Nitumie Simu Yako Kwenye Pm Tuongee Ili Nijue Ulikuwa Na Ukaribu Upo Na Marehemu.

Sina muda wa kuongea na watu wanafiki na wanaoleta mambo ya upuuzi kwenye misiba ya wenzao kama wewe. Wakazi wa Tarime tumeamua kuwa hatutagawanywa kwa misingi ya ukabila, vyama, au koo. Kwa sasa sisi ni kitu kimoja na tunaungana na watanzania wote wa vyama vyote na makabila na koo zote kuhuzunika na kuomboleza kifo cha mbunge wetu.

Nimekuomba tu usubiri hata siku mbili au tatu zipite ili uchunguzi ufanyike na watu wa Tarime tumzike mbunge na ndugu yetu lakini inaonekana wewe una lako jambo.

Ona aibu wewe.
 
Hii misiba ambayo inasimamiwa na serikali na kuzuia wafiwa wasimkague ndugu wao ninakuwa na mashaka nayo toka alipouliwa Dr.Omar ALi Juma nasema aliuliwa kwani serikali ilikataza mtu yeyote kumfunua au kumkagua na hata alipopelekwa Pemba Ndugu zake hawakuruhusiwa kuagana nae alipelekwa kaburini moja kwa moja na walihusika kuuzika mwili huwa ni usalama wa taifa kama majeshi au polisi ndio haohao,wahusika walitakiwa kukaa mbali na maiti eti wanazika kitaifa hadi hii leo nasikia kaburi lake kuna gadi ,kwani serikali inaamini watu wanaweza kwenda kulifukua ili kujua kama walizika mtu au gogo,ni utata mtupu lakini kweli itajulikana tunangojea kuanguka kwa CCM kila kitu kitaanikwa uwanjani na wahusika kama kufa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria labda wawahi kufa ,lakini hili litazuka tu kama wanasikia yule wa mauaji ya Sebrenika Bosnia yupo kizimbani akijibu masuala basi na hawa waache wachelewe kufa tuone ,hii itakuwa ishu ya kisiasa uhai ukiwepo.
Huu ni uongo mwingine,jamani mbona mnapaka kinyesi kwenye jamvi letu.
 
NImewahi kusikia suggestive messages... hii ya leo ni kilele. mmh! TBC imepata documents zinazoonesha kuwa katika safari yake ya kwenda Dar Wangwe alikuwa afungue kesi dhidi ya Chadema kwa kumsimamisha nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.

"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...
 
Kumbe wewe ni mwongo na mzushi namna hii, sikukujua. Kwa taarifa yako CHADEMA inaongoza halmashauri tatu, acha uvivu tafuta na hizo zingine mbili-achana kuandika mambo kwa hisia!

utasema mwongo kwa sababu sina std mbili.Kwa vile nasema CHADEMA ichunguzwe ndio waja juu sishangai hili ni tatizo la wana CHADEMA wengi.

Naheshimu Michango yako mingi lakini kwa hili lazima tutatofautiana tu maana na wewe yawezekana una nafasi ama unaiwania CHADEMA na hili ndilo TATIZO la sisi wtz.

Mfano ccm likitokea jambo hua wanaitana kuwekana sawa waje na msimamo wanaoujua wao mara nyingi ni wa kishetani na si kumtetea mwananchi ila wanalazimika kufanya hivyo kwa vile wanaabudu matumbo yao.

Ndivyo hivyo CHADEMA hakuna tofauti yaleyale wakishutumiwa nao wanawekana sawa ili iweje?

kama mtu uko msafi mtu kakutuhumu kua wewe ni mvuta bangi kwanza wewe ndio inabidi uwe wa kwanza kufanya iniatives za uchunguzi kitalaam ili umuumbue yule jamaa. Sasa tunaposema uchunguzi huru uchukuliwe na uanzie CHADEMA kama uko safi unaogopa nini?? mi nadhani ndio mda wakuchukua ujiko yani usafi wako machoni kwa watu.

Mtu ukiona anapinga kufanyiwa uchunguzi huru jua kuna jambo.Mtu akikutuhumu kwako ndani kuna gongo na wachunguzi huru wakaja kukagua ndani mwako kama kuna pombe ya gongo na kama wewe ni msafi na gongo hiyo haimo ndani utachekelea na kuwakaribisha kwa furaha.

Ok hizo halimashauri kuna nyingine kama sikosei ni ya ZITO ,nyingine sijui
 
Something is coming ama ndio mbinu za kujipanga kwa system? Mallya hakufa na akifa kabla ya kuhojiwa tutajua kuwa kumbe ni mkakati wa kiserikali kummaliza Wangwe ili kupunguza nguvu za CHADEMA.
 
NImewahi kusikia suggestive messages... hii ya leo ni kilele. mmh! TBC imepata documents zinazoonesha kuwa katika safari yake ya kwenda Dar Wangwe alikuwa afungue kesi dhidi ya Chadema kwa kumsimamisha nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.

"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...

Atakuwa na documents kwani yeye wakili?ama alikuwa anatengenezewa na wakili wa Serikali huko Dodoma?kama ni hivyo basi inawezekana kabisa kuwa kulikuwa na mpango wa kiserikali kummaliza.

CHADEMA lazima mfanye mapema kujua huyo wakili aliyetengeneza kama anaishi Dodoma ama laa ,na kama sio ni kwanini hizo document ziwe Dodoma?
 
NImewahi kusikia suggestive messages... hii ya leo ni kilele. mmh! TBC imepata documents zinazoonesha kuwa katika safari yake ya kwenda Dar Wangwe alikuwa afungue kesi dhidi ya Chadema kwa kumsimamisha nafasi ya Umakamu Mwenyekiti.

"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...
Wewe nawe hueleweki......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom