"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...
I am not getting this one bit.Care to elucidate?
"Mpango huo wa Wangwe kufungua kesi ulikuwa unajulikana kabla na uongozi wa Chadema"...mwisho wa kunukuu...
Wewe ni laghai na mzushi sana, na uzushi wako unatisha mno! Ni mtu gani wa chadema alisema Chacha apigwe risasi? Hivi huu uzushi unamtumikia nani na kwa manufaa gani, au una-abuse anonymity yako hapa?
Unafikiri kwa kuwa unatumia jina bandia basi una uhuru wa kuropoka na kupayuka unavyotaka?
Kwa hiyo Mgagagigikoko unatakakusema jmushi ndiye Deus Mallya?Inawezekana sio JMUSHI ila mhusika mkuu aliposoma ushauri wa JMUSHI akaamua kuufanyia kazi. JMUSHI anaweza kuwa shahidi kwenye kesi hii na akajikuta anafungwa kwa kuuua bila kukusudia(Manslaughter).
na kauli zote kama vile SIWEZI KUFANYA KAZI NA WANGWE ukitizama sana zinaweza kuwaweka watu pabaya,kama Mwanakijiji alivyoishauri Polisi hivyo hivyo na MKAMAP anajaribu kuweka mawazo yake kama Mwanakijiji na baya zaidi pale Mwenyekiti aliposema kuwa Wangwe anashiriki kukihujumu chama kwa kutoa siri za chama nje. walimwita kwenye vikao vingi kumuonya asitoe siri,hakusikia na wakampa muda ajirekebishe, wanasema hakujirekebisha,hatuleti siasa ila kama sheria inafuatwa Chadema wana kubwa la kujibu.
Mazishi ya Mh. Chacha Wangwe, aliyekuwa Mbunge wa Tarime aliyefariki dunia kwa ajali ya gari majuzi huko Dodoma, yameshindwa kufanyika leo kijijini kwake Kamokorere baada ya kufumuka kwa vurugu kubwa ambapo wabunge na viongozi wa serikali na vyama vya siasa walohudhurian ilibidi watoke bomba kusalimisha maisha yao.
Vurugu hiyo ilianza dakika chache baada ya kuwasili kilioni hapo kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, katika kijiji cha Kemokorere kiasi cha kilomita 20 hivi toka mjini Tarime.
Hali ilipokuwa mbaya, ilibidi Mh. Mbowe na viongozi wote waliohudhuria mazishini waondolewe kilioni chini ya ulinzi mkali wa FFU ukiongozwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Afande Leberatus Barlow ambao walifanya kazi ya ziada kuepusha balaa.
Viongozi wengine waliohudhuria walikuwa ni pamoja na wenyeviti wa vyama vya upinzani Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Augustino Lyatonga Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Karatu Mh. Wilbroad Slaa pamoja na kiongozi wa upinzani bungeni, Mh. Hamad Rashid.
Wote hao walisindikizwa chini ya ulinzi mkali wa FFU kuondoka mahali hapo na kuelekea Musoma. Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Mh. Steven Wassira, na Manaibu Mawaziri ambao ni wabunge wa Kanda ya Ziwa, Dr. James Wanyacha na Gaudensia Kabaka nao ilibidi waondoke.
Ujumbe toka Kenya ulioongozwa na Dr Wilfred Machage ambaye ni mbunge wa jimbo la Kurya na pia Naibu Waziri katika serikali ya mseto ya Kenya pamoja na wakuu wa wilaya wawili nao walikuwepo na ilibidi waondoke kwa kuruka ukuta.
Tofauti na walivyoingia, itifaki haikuweza kufuata kama walipowasili wabunge 20 wakiongozwa na mbunge wa Bumburi Mh. William Lukindo vurugu hilo lilipoanza na ilibidi kila mmoja aondoke chini ya ulinzi mkali.
Maelfu ya waombolezaji, wengi wao wakiwa vijana waliobeba mabango yenye ujumbe mbalimbali unaohoji kifo cha Mh. Wangwe, walitawala hapo kilioni. Juhudi za Mkuu wa mkoa wa Mara Mh. Issa Machibya kuwatuliza hazikuzaa matunda.
Hata juhudi za kututuliza ghasia hizo za Wah. Zitto Kabwe na mmoja wa wanafamilia waandamizi kama vile Profesa Samwel Wangwe na Mkuu wa zamani wa Halmashauri ya Tarime Mh. Peter Wangwe pia hazikuambulia kitu.
Prof Wangwe aliwaambia waombolezaji hao wenye hasira kwamba familia ya Wangwe imeamua kumtafuta mtaalamu huru kuifanyia upya uchunguzi maiti ya hayati Chacha Wangwe ili kubaini alifariki kwa njia ipi.
Wengi ya waombolezaji wanatuhumu kwamba Mh. Wangwe hakufa kwa ajali ya gari. Mtu moja aliyekuwa na marehemu wakati wa ajali, Bw. Mallya, anahojiwa na polisi na uchunguzi wa kina unaendelea.
Hata mimi nahisi hivyo....Kwa hiyo Mgagagigikoko unatakakusema jmushi ndiye Deus Mallya?
mwili Wa Marehemu Ulipotolewa Dodoma Uliongopzana Na Ndugu Wa Marehemu Tuu Na Mtu Aliyepata Nafasi Ambaye Sio Ndugu Wa Marehemu Ni Mwenyekiti Wa Halimashauri Ya Wilaya Ya Tarime.
Ndege Hiyo Ilipangwa Ratiba Na Bunge Sasa Waulize Bunge Ni Kwanini Ujumbe Wa Wabunge Ulipangwa Kuwa Wanaenda Kwenye Msiba Leo?
Pili Wakati Msiba Unatokea Unajua Kuwa Mbowe Alikuwa Afrika Ya Kusini Akiongoza Ujumbe Wa Tcd Ambao Ni Muunganiko Wa Vyama Vya Ccm,cuf,chadema,na Tlp, Ulitaka Aweze Vipi Kuongozana Na Mwili Wakati Aliweza Kuingia Nchini Jana Mchana Baada Ya Kuahirisha Safari?
Fanya Kazi Nyingine Hii Unayofanya Inahitaji Watu Au Mtu Mwenye Iq Kubwa Sana ,sio Kama Ya Kwako,ashakumu Sio Matusi....
smart attempt... "watu wa chadema" waliodai "apigwe risasi" ni kina nani na wapi walifanya hivyo? Hii ni new information, kwa sababu ukiweza kuwaonesha hao "watu wa chadema" na mimi nitakuunga mkono.
VIONGOZI wa vyama vya NCCR Mageuzi, CUF na TLP wametoa tamko kuhusu msimamo wa familia ya Marehemu Chacha Wangwe, wakisema uchunguzi ni haki ya marehemu na kuipongeza kwa kuweka shinikizo hilo.
Viongozi hao, Augustine Mrema (TLP), Prof Ibrahim Lipumba (CUF), na James Mbatia (NCCR Mageuzi) ndiyo pekee waliosalia kutokana na viongozi wengi kukimbia vurugu nyumbani hapo kwa marehemu zilizozuka baada ya mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwasili.
Wa kwanza kuzungumza alikuwa Prof. Lipumba ambaye alisema marehemu Wangwe katika siasa alipata umaarufu kutokana na kuwa mpambanaji na mpiganaji kutetea haki za wanyonge.
Lipumba alisema hakuna njia nzuri ya kumuenzi marehemu zaidi ya kuhakikisha wananchi wa Tarime wanaendeleza mapambano dhidi ya uporaji wa raslimali ya nchi na wananchi kuendelea kunyanyasika.
''Marehemu alikuwa mpambanaji na mpiganaji, sasa njia pekee ya kumuenzi ni kuendeleza mapambano ya wanyonge dhidi ya uporaji wa raslimali,'' alisema na akaongeza kwamba wananchi wanapaswa kuwa na subira kuhusu uchunguzi wa familia.
Akizungumza kwa niaba ya chama chake, Mbatia alisema kuwa alivyomtambua na kumfahamu marehemu Wangwe alikuwa jasiri na hivyo kuwaomba wananchi nao kuendelea na ujasiri huo kudai haki hata ya marehemu.
''Huwezi kumnyang'anya mtu haki yake ya kuzaliwa wala kuishi, uhai ukitoweka huwezi kuulipa kwa kitu chochote, kuweni na subira, msiwe na itikadi katika msiba, hakuna itikadi, sasa msikubali kuteganishwa, tunangoja uchunguzi ufanyike watueleze nini kilimtokea na kama kuna watu walimuua tudai haki yetu na kwa aliyehusika basi sheria ifuatwe,? alisema na kushangiliwa na watu.
Mbatia alisema wakazi wa Tarime wamekuwa wakichukuliwa kama ni watu wenye vurugu, jambo ambalo ni kinyume kutokana na kuwa na msimamo wao unaopenda haki na kujali maslai ya wanyonge.
''Jamani Tarime siyo watu wa fujo, wamekuwa wakielewa hivyo, na kusema hivyo, lakini mimi najua Tarime ni haki na kuchukia kunyanyaswa kwa wanyonge, teteeni haki yenu,'' alieleza.
Naye Mrema ambaye alishangiliwa zaidi kuliko wote, alianza kwa kuwapongeza wananchi wa Tarime kwa kumchagua marehemu Wangwe.
''Nawapongeza kwa kumchangua Marehemu, lakini sasa ametutoka, hivi ukizaa mtoto akafa unaacha kuzaa tena? hapana unaendelea, Chacha amezaliwa Tarime na atazaliwa mwingine,'' alisema.
Alisema kifo cha marehemu kina utata kutoka Dodoma, lakini familia imesema 'no' (hapana) mpaka uchunguzi umefanyika jambo ambalo ameunga mkono.
''Kuna watu hawajui kama marehemu ana haki zake, na mimi siondoki hapa mpaka kieleweke, uchunguzi lazima ufanyike kisha naomba tumzike kwa heshima zote huyu ndugu yetu,'' alisema Mrema huku akishangiliwa.
Tatizo lako katika line of your thinking unashindwa kuuliza nani atanufaika sana na kifo cha Wangwe hasa katika mazingira hayo? Obviously siyo Chadema. Kwa sababu kwa wao walikuwa na uwezo wa kumfukuza uanachama na kumuondoa kwenye picha. Kuna mtu ambaye atanufaika na Chacha kutokuwa mbunge wa Tarime; and believe me, siyo Chadema. Think about it. Na inawezekana siyo CCM. Ukiondoa mawazo ya vyama vya kisiasa you might get real close na ukweli wenyewe. Haya mawazo ya Chadema na CCM yatapoteza muda sana.
Kwa maneno yako ni kuwa CHADEMA sio waliomuua kwani sasa watakosa hiyo ruzuku.Mwanakijiji elewa jambo moja Chadema walikuwa wakitaka ruzuku za Wangwe kupitia jimbo la Tarime, kwa vile priority ya Chadema ni RUZUKU NA UKABILA wasingeweza kumnyanganya uanachama,angekuwa si mwanachama wa Chadema nao makao makuu wangepata Ruzuku, kwa hiyo kilichokuwa kinambakiza Wangwe chadema ni lile kundi la Tarime linalizalisha Ruzuku Makao makuu.
Wangwe alibaki kuwa Mwanachama kwa ajili ya ruzuku si vinginevyo.