Faith
Member
- Jul 9, 2008
- 52
- 12
Kifo cha Wangwe: Shuhuda atoa taarifa mpya polisi
* Adai Mbunge Wangwe hakuendesha gari lililopata ajali
Na Faraja Jube, Dodoma
UTATA umejitokeza iwapo marehemu Chacha Wangwe aliyefariki katika ajali ya gari Jumatatu usiku alikuwa akiendesha gari hilo ama la.
Kwa mujibu wa mtu aliyefika katika eneo la tukio dakika chache baada ya ajali hiyo, Mwiguni George, alimkuta marehemu Wangwe akiwa katika kiti cha mbele cha abiria huku sehemu ya kichwa chaki kikiwa kimebanwa ubavuni mwa kiti hicho na mlango wa nyuma.
Akizungumza juzi mbele ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishina Msaidizi wa Polisi, Peter Kivuyo, Kamanda wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Dodoma, Vitus Nikata na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kongwa, Ramadhan Kalowa, Georgr alieleza kwamba alikuta mwili wa marehemu Wangwe ukiwa umebanwa ubavuni mwa kiti na mlango wa nyuma huku mkanda wa usalama katika gari hilo ukiwa bado upo mwilini mwake.
''Nilikuwa nyumbani nasikiliza kipindi cha michezo, muda ya saa mbili na nusu usiku, nikasikia kishindo kikubwa, nikakimbilia eneo la ajali. Nilipofika katika eneo la ajali nilimkuta kijana mmoja akiwa analizunguka gari huku akipiga kelele za kuomba msaada,'' alieleza George.
Hata hivyo, mtu huyo alieleza mashaka yake kuwa kulikuwa na watu watatu katika gari hilo na siyo wawili kamba ambavyo ilitangazwa katika vyombo vya habari.
Juzi Deus Francis Mallya alikaririwa mara mwili wa marehemu ulipofikishwa katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma, akisema kwamba walikuwapo wawili katika safari hiyo na kwamba marehemu Wangwe ndiye aliyekuwa akiendesha gari.
''Nilisikia katika taarifa ya habari kuwa walikuwa wawili. Marehemu ndiye aliyekuwa akiendesha gari na kwamba mmoja amepona. Mimi nina mashaka, kwani nahisi kuwa na mtu wa tatu na kwamba marehemu hakuwa anaendesha gari wakati wa tukio,'' alisema George na kuongeza.
''Nilipofika katika eneo la ajali kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akiwatawanya watu walioanza kufika kwa ajili ya kutoa msaada wasilikaribie gari. Hata hivyo, tulianza kuutoa mwili wa marehemu uliokuwa katika kiti cha abiria upande wa mbele,'' alieleza George.
''Nilimvua mkanda wa usalama katika gari ambao bado ulikuwapo mwilini mwake, kisha tukamtoa kupitia mlango wa dereva kwani mlango upande aliokuwa amekaa haukuweza kufunguka,'' alisema.
Kwa mujibu wa Goerge, mtu huyo wa tatu alielekeza kutolewa kwa fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya mfuko wa koti, jambo ambalo lilimfanya shuhuda huyo kuhisi kuwa alikuwa pamoja nao.
''Tulianza kutoa vitu vya marehemu na mtu huyo alielekeza kuwa kuna fedha ndani ya mfuko wa koti,'' alieleza na kuhoji: ''Sasa mie nikajiuliza kama hakuwa nao alijuaje kuwa marehemu aliweka fedha ndani ya mfuko wa koti?''
Hata hivyo, shuhuda huyo alieleza kuwa wakati pilikapilika zilipokuwa zikiendelea, hakuweza tena kumuona mtu huyo wa tatu, ambaye alitoweka.
Maelezo hayo ya George yalipelekea Kamanda Kivuyo kuagiza askari waliokuwapo katika eneo hilo kuchukua maeleo ya shuhuda huyo kwa
ukamilifu.
''Kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako na moyo wa kizalendo wa kutoa msaada kwa marehemu,'' Kamanda Kivuyo alimweleza shuhuda huyo.
Maelezo hayo yanaleta mkanganyiko kutokana na taarifa za awali kuwa marehemu Wangwe alikuwa akiendesha gari na kwamba walikuwapo watu wawili katika gari hilo.
source:MWANANCHI
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6189
sasa hapo inabidi uchunguuzi ufanyike tupate ukweli juu ya kifo chake