akilimtindi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 421
- 83
Asante sana, huyu hawezi kuwa tofauti na wao akapewa majukumu aliyopewa. Ni mmoja wao. Hata hivyo simaanishi alishiriki kum-kolimba kaka yake kama mtandao wao utakuwa unahusika.Huyo ni mtaalamu wa mambo ya uchumi, zamani kidogo alikuwa mwenyekiti wa bodi ya madirectore wa ESRF, kisha akateuliwa kuwa mwenyekiti wa kuongoza tume ya kuratibu maoni ya watanzania kuhusu kuharakishwa kwa shirikisho la afrika mashariki, of which watanzania waliukataa huo mchakato, na nadhani ile tume inafahamika zaidi kama tume ya Wangwe...walau kwa juu juu
Lakini si mtu mdogo kitaaluma yuko juu sana...sina hakika kama naye si mmoja wao.
Hata hivyo kidogo kuna utata pale inaposemekana Prof. Samwel Wangwe anaandaliwa kuchukua jimbo badala ya ndugu yake aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha.