ndugu zangu wa chadema,
kwanza poleni sana kwa dhahama ambalo limewakuta maana katika dunia tunayoishi ni vigumu sana kuamini kama nyinyi leo mnaweza kuuliza maswali kama haya huku jamii ikijua wazi kuwa majibu mnayo.
kwa mshangao wa upeo wangu, maswali ambayo mh. mnyika ameomba serikali kupitia jeshi lake la polisi liyajibu, yanaleta utata mwengine hasa nikiangalia kwamba uelewa wake au kamati iliyokaa kujadili kuweka haya maandishi chini. kwa nini nasema hivyo........
ngoja niwaambieni ndgu zangua jamaa zangu, kifo ni kifo tu. mallya kwa maelezo yake alikuwa rafiki wa siku nyingi wa mh.chacha na hata kusema kuwa alikutana naye kwa mara ya kwanza makao makuu ya chadema pale kinondoni..(sijui kama ofisi zipo kinondoni) kwa hiyo ni aibu kuwa hamumjui huyu kijana ambaye ana fika sehemu ya hata kuingia gari moja na makamu mwenyekiti. kwa upande mwengine nashawishika kuamini kuwa huyu ni mtu aliyekuwa na umuhimu fulani katika maisha ya makamu mwenyekiti, mjumbe wa kamati kuu ya chama.
pamoja na hayo, tujikumbushe siku za mwisho za marehemu. kabla mahuti hayajamkuta bwana wangwe, kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara ndani ya chama. ambayo kwa namna moja au nyengine inatokana na siasa za ukanda zinazotawala maendeleo ya chama. sintoshangaa watu wakija juu na kusema kuwa chadema au kundi la wanasiasa wa upande fualani wamemuuwa chacha.ni jambo la kawaida ambalo mnatakiwa kulikabili.
polisi kwa upande wao kama wafanya kazi wa sekta hii lazima watafanya uchunguzi wao. kuweka ripoti adharani au kutoweka ni juu yao. wewe unataka ripoti iwekwe hadharani kwa jambo gani haswa. unafikiri hii ndiyo njia ya kujisafisha? ndugu yangu angalia maana unaweza kuja tafuta njia ya kukimbilia maana jamii inataka maelezo zaidi maana hawata elewa kusikia kwamba hamjahusika. wangwe alikuwa akiongelea sauti ya umoja. alikuwa anaubiri siasa ya ukweli ambayo kwa ushujaa wake aliweza isimamia, sio tu ndani ya chadema bali pia bungeni. alipenda sana kupanua wigo wa siasa.
ZITTO ZUBERI KABWELUKA...........kaka pole sana. maana umepoteza mpiganaji aliyekuwa anakupa raha na uelekeo katika mitizamo. ni imani yangu umepwaya ndani ya harakati zako. umepoteza muhubiri wa mtazamo wako wa kutanua demokrasia ndani ya chadema, toka machame hadi tanzania. usikonde mungu atakusaidia. mnyika ni hajui alitendalo.
mwisho elewa maswali kama haya haustahili kuuliza...ongea na watu wa karibu watakuambieni.najua mnataka kuanzisha kuwa huyu mallya alitumwa na mtu fulani. hapana naibu katibu....endelea fanya kazi zako na achana na haya.
sijui alienda dodoma kufanya nini....ina maana yeye ndiye alimwambia chacha twende dar kuzika au unafikiri ni rahisi kwa mtu ambaye hamjui kumpa gari alipeleke garage. haiwezekani bro.huyu ni mtu aliyeaminiwa na chacha na ndiyo maana hata alisafiri naye.
mungu ibariki tanzania.