Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Dr Slaa una ushahidi kuwa Makamba kampa 50m? Mh tunakuheshimu sana mambo ya kuokoteza udaku kwa mtu calibre yako sio mazuri kabisa

Wewe mwenyewe una ushahidi kwamba Dr. Slaa hana ushahidi kabla ya kumuita muokota udaku au unamuita majina kwa vile tu una uhuru wa kupiga madongo kutoka nyuma ya screen ya Komputa ?
 
Na wewe ushahidi wako wa kuwa dokta Masau hakusomea upasuaji moyo uko wapi?
 
This fake reverend is surely an id1ot of the highest degree. His credibility is sinking by a minute. He deserves the title of fisadi, like CCM fisadis.
 
Point ni z rl chadema wameshiriki? Na kama ndio 2pewe huo ushahidi na kama siyo je mtikila katoa wapi hayo maneno,.
Najua chadema wapo na mpango wakukisafisha chama na fitna znazoendelea sasa niwakate wenu kutupa ukwel wenu
mpaka hapo ni kwel wangwe kauwawa sasa who z the killer? N lazma 2mjue
 
Wakuu,

Hivi Mtikila hawezi kusema jambo bila kuambiwa anatumiwa na mtu?

Hivi Tanzania mtu hawezi kufa bila kuwepo mkono wa mtu?

Hivi JF mtu hawezi kuwa na mawazo yake pekee bila kuambiwa kibaraka wa mafisadi?

Hivi Mtikila anawezaje kuja na madai makubwa namna hiyo bila hata kutoa ushahidi wowote wa maana?

Inakuwaje waandishi wanamsikiliza na kuandika habari nzito kama hiyo bila kumbana atoe ushahidi?

Dr. Slaa anawezaje kuandika hapa kwamba Mtikila kapewa 50m za makamba bila ushahidi wowote?

Hivi sisi Watanzania tunaenda wapi? Tunawezaje kupakana matope kiasi hicho bila kudirika angalau hata kidogo kutoa ushahidi (data)?

Ninachokiona kwenye huu mjadala hakitii tumaini juu ya viongozi wetu wa sasa na baadaye. Watu kama mnataka kuwa wapiga ramli nendeni huko, ila kuanza kuja na tuhuma kubwa kubwa bila data sio dalili nzuri kabisa.

Mtanzania,
In all fairness, Mtikila angekuwa hajakutana kwa siri na Rostum na kuomba na kupokea mkopo kwake, ambao mpaka sasa hatujui ameurudisha, na mimi ningekuwa upande wako katika haya maswali uliyouliza. Lakini kwa kukubali kukopa kwa fisadi wakati vita dhidi ya mafisadi inapamba moto Mtikila kisha- compromise credibility yake. It is that simple. Huenda kweli hajatumwa, lakini kadhalika uwezekano kuwa anatumiwa ni mkubwa. BTW, haijakushtua kuwa katika suala la mafisadi ukimya wa Mtikila umekuwa na kishindo?
 
Jasusi,

Nyerere na kuwatukana IMF na WB bado aliendelea kwenda kukopa huko, sioni unashangaa nini kwenye hilo la Mtikila? Mwenye njaa hachagui mlo, ndio maana ni muhimu mno kwa mtu au taifa kuwa na uwezo wa kujitegemea.

Lakini je ushahidi uko wapi kwamba Mtikila kalipwa 50m na Makamba?

Je ushahidi uko wapi kwamba akina Mbowe wamehusika kumwua Wangwe?

Bado maswali yangu yako pale pale, tunajenga genge la wanasiasa wapiga ramli. Wengine ni wasomi na wanajua umuhimu wa data (facts) kabla ya conclusion lakini bado bila hata
aibu wanakuja na statements kubwa kubwa ambazo haziwi backed na data zozote. Hii mimi naliona ni hatari mno huko tunakoenda. Tutaishia kujenga taifa la waropokaji.
 
Huko mwanza kuna bomu lolote wamelitoa Chadema...???

CCM wamefanikiwa kufanya Divide n Rule kwa upinzani...Tayari chadema hawaoni umuhim wa kukutana na wenzao..Kuna wakati nilimwuliza Dr. Slaa kuwa wao wameshindwa vipi kuwaita wapinzani wenzao kujadili kwa pamoja kwa Yaliyotokea Huko kwa Wangwe, then kujadili mustakbali wa Tarime....lkn hapakuwa na majibu...may be Chadema washajua ndani ya Muungano kuna pandikizi....

Nami naungana na wengine.Mtikila afikishwe Mahakamani kwa tuhuma zake...si vema chadema kumjibu ktk media...au wanaweza mjibu thru Media, baada ya kumpandisha Mahakamani...
 
Last edited:
Mkuu Rwabu,
Kumuacha Rev. aendelee kutoa sumu ni njia mojawapo ya kukwepa hoja zake, kama hakuna watakaomsikiliza Rev. Kama atapata audience, basi inaweza ikawa shida kwa Chadema hasa wakati huu wa uchaguzi. Ndio maana nikasema, kama Dr. Slaa na wenzake hawana wanalotaka kuficha, basi wampe Mtikila kipigo mahakamani kitakachomfanya asirudie tena kuwashambulia. Unaweza kuachana tu na Mtikila kama hatapata wanaomsikiliza, otherwise leaving him is at your own peril, you need to hit him the hardest.

Kubwajinga,

Naelewa kwa nini hili swali umelivalia njuga maana hata Rev. mwenyewe ameomba kwa Mungu watu kama wewe, na unaoshabiiana nao kwa akili na jina, mjitokeze na kulivalia njuga. Lakini wenye common sense wameamua kulipuuza na huu ukweli unawapa taabu sana na kuwanyima usingizi. Kwa kuhesabu post zako kuhusiana na hii habari ni wazi hayo mafungu yamewafikia wengi na mafungu yana masharti.

Huu ni wakati wa Kampeni na nawaomba wote wanaoitakia mema nchi yetu kama bado mpo mlaani kwa nguvu zote hizi mbinu chafu zinazofadhiliwa na MAFISADI. Kama wameweza kumnasa hata Rev., bila shaka kuwafikia kubwajinga na kundi lake ni jambo dogo sana.
 
Kwa kweli nchi imefikia mahali pabaya sana. Kwa sasa nchi inayumba na wahusika wanahakikisha hakuna chama mbadala cha kuweza kuchukua madaraka na hayo yanafanyika kwa gharama kubwa na kwa kutumia kodi zetu.

Kuna kila sababu ya kila Mtanzania ukiwamo ndugu yangu Mtanzania wa hapa JF kulijua hilo na kwa kulijua hilo tutakua makini na kuangalia Tanzania Yetu iliyo njema kama alivyo ndugu yangu Tanzania Njema.

Tunahitaji mikakati mahususi ili angalau serikali iwe na woga wa kuwasaliti Watanzania kama si kuondolewa kabisa na kuingia wale wenye nia njema na nchi hii.

Kwa utangulizi huo, na kwa historia ya Mtikila ambayo si ngeni kwetu; na kwa mazingira na wakati (timing) ya taarifa ya Mtikila (akisema wazi anaweka mgombea Tarime), haihitaji mtaalamu kung'amua kinachoendelea.

Hawa jamaa wameingia gharama kubwa kufanya kila wawezalo kutimiza malengo yao na kuhakikisha wanafikishwa wanakokusudia. Kwa bahati mbaya sana tuna ombwe (vacum) kubwa la utawala na ombwe hilo tusipoangalia litazibwa na kafara ambayo niliwahi kuizungumzia. Kwa kawaida nchi nyingi zimeweza kuendelea baada ya kutoa kafara (umwagaji damu) kwa 'mizimu inayokalia' mali zilizopo ardhini na baharini. Kwa wanaoelewa nchi sasa imekidhi sehemu kubwa kama si kupitiliza vigezo vinavyoweza kusababisha nchi iingie katika machafuko.

Huhitaji ushahidi kuona kwamba Mtikila ameingia katika kazi kama aliyoifanya mara kadhaa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000 na baadaye kabla na wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.

MUNGU anatupa mwanga kila kukicha na tuliweza kuona na kumfahamu Mtikila ni mtu wa aina gani kama ambayo sasa tunaona Mhariri Mkuu wa gazeti la Majira ni mtu wa aina gani.
 
mag3,
Kama kila anayeikosoa Chadema au viongozi wake anakuwa amepewa kitu kidogo na RA, basi sio ajabu tuko wengi TZ wenye hivyo vimilioni.

Lakini huu ujinga uliopo JF, ambao na wewe inaelekea umeuvaa, wa kukubali kila lisemwalo na MChadema, utaniwia radhi maana wengine hatunao.

Suala hapa ni very simple, Mtikila katoa sumu hadharani na ushahidi wa aliyosema hata kwenye video upo, sasa Dr. Slaa na wenzake wengine walioshutumiwa kwa nini wasichukue hatua za kisheria?

Dr. Slaa ni msomi kama tulivyo wengi wetu, anaelewa wazi kuwa hakuna njia iliyo rahisi ya kutengeneza pesa kwenye common law system kama kumshitaki mtu anayekuchafulia jina. Angmshitaki ili azivune hizo 50m alizopewa na Makamba.

Dr. Slaa anayo haki ya kutuelezea au hata kupiga propaganda ya kwa nini Chadema wamekataa kuungana na wapinzani wenzao, lakini asitumie maneno ya Mtikila kufumbia ubinafsi waliojijengea ambao marehemu Wangwe alikuwa anaupinga.
 
Jasusi,

Nyerere na kuwatukana IMF na WB bado aliendelea kwenda kukopa huko, sioni unashangaa nini kwenye hilo la Mtikila? Mwenye njaa hachagui mlo, ndio maana ni muhimu mno kwa mtu au taifa kuwa na uwezo wa kujitegemea.

Lakini je ushahidi uko wapi kwamba Mtikila kalipwa 50m na Makamba?

Je ushahidi uko wapi kwamba akina Mbowe wamehusika kumwua Wangwe?

Bado maswali yangu yako pale pale, tunajenga genge la wanasiasa wapiga ramli. Wengine ni wasomi na wanajua umuhimu wa data (facts) kabla ya conclusion lakini bado bila hata
aibu wanakuja na statements kubwa kubwa ambazo haziwi backed na data zozote. Hii mimi naliona ni hatari mno huko tunakoenda. Tutaishia kujenga taifa la waropokaji.

Mtanzania,
Juu ya ushahidi wa Mtikila kupewa hela na Makamba Mheshimiwa Dr. Slaa amesema wanao ushahidi huo. Nina hakika watautoa wakati muafaka. Tumsubiri. Juu ya ushahidi wa kuhusika kwa akina Mbowe katika kifo cha Wangwe ni Mtikila mwenyewe aliyedai kuwa anao. Na kuhusu Nyerere kukopa IMF na WB hakuwa na jinsi lakini yeye aligombana nao kwa kupinga masharti waliyokuwa wanaziwekea nchi ndogo zinazoendelea. Na hilo hata viongozi wa IMF na WB walikuja kuliona baadaye na ndio mara kwa mara katika safari zake hapa Washington walikuwa hawakosi kumtafuta na kupata nasaha zake. Nyerere hakupinga mikopo ya IMF per se bali masharti na sera walizokuwa wanalazimishia nchi zinazoendelea. Kuna tofauti. Nyerere hakuziona IMF na WB kama mafisadi. Hapana.
 
Mtikila hawezi kuisaidia Polisi katika haya anayosema ili mashtaka ya Mallya kule Dodoma yabadilishwe?
 
Dr Slaa anashauriwa na Kubwa jinga kuwa hakuna njia iliyo rahisi ya kutengeneza pesa kwenye common law system kama kumshitaki mtu anayekuchafulia jina hivyo Slaa amshitaki Mtikila ili avune hizo 50m za Mtikila. Hii dhana ya kutengeneza pesa kwa njia rahisi ndiyo umetufikisha hapa tulipo leo. Kwa wengine njia rahisi ni kuchinja mazeru zeru, kwa walio juu imekuwa mikataba ya maangamizi nk. Kwa wengi njia ya kutenegeneza pesa si kuafanya kazi tena bali ujanja ujanja. Nitamshangaa sana Slaa kama atakimbilia mahakamani ili avune hizo 50m.
 
Kwa kweli nchi imefikia mahali pabaya sana. Kwa sasa nchi inayumba na wahusika wanahakikisha hakuna chama mbadala cha kuweza kuchukua madaraka na hayo yanafanyika kwa gharama kubwa na kwa kutumia kodi zetu.

Kuna kila sababu ya kila Mtanzania ukiwamo ndugu yangu Mtanzania wa hapa JF kulijua hilo na kwa kulijua hilo tutakua makini na kuangalia Tanzania Yetu iliyo njema kama alivyo ndugu yangu Tanzania Njema.

Tunahitaji mikakati mahususi ili angalau serikali iwe na woga wa kuwasaliti Watanzania kama si kuondolewa kabisa na kuingia wale wenye nia njema na nchi hii.

Kwa utangulizi huo, na kwa historia ya Mtikila ambayo si ngeni kwetu; na kwa mazingira na wakati (timing) ya taarifa ya Mtikila (akisema wazi anaweka mgombea Tarime), haihitaji mtaalamu kung'amua kinachoendelea.

Hawa jamaa wameingia gharama kubwa kufanya kila wawezalo kutimiza malengo yao na kuhakikisha wanafikishwa wanakokusudia. Kwa bahati mbaya sana tuna ombwe (vacum) kubwa la utawala na ombwe hilo tusipoangalia litazibwa na kafara ambayo niliwahi kuizungumzia. Kwa kawaida nchi nyingi zimeweza kuendelea baada ya kutoa kafara (umwagaji damu) kwa 'mizimu inayokalia' mali zilizopo ardhini na baharini. Kwa wanaoelewa nchi sasa imekidhi sehemu kubwa kama si kupitiliza vigezo vinavyoweza kusababisha nchi iingie katika machafuko.

Huhitaji ushahidi kuona kwamba Mtikila ameingia katika kazi kama aliyoifanya mara kadhaa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000 na baadaye kabla na wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.

MUNGU anatupa mwanga kila kukicha na tuliweza kuona na kumfahamu Mtikila ni mtu wa aina gani kama ambayo sasa tunaona Mhariri Mkuu wa gazeti la Majira ni mtu wa aina gani.

Men! You are so good, I salute you!

icon14.gif

.
 
Chama chenye kiburi kuliko vyote Tz ni CCM.

Na chama cha ubishi kuliko vyote ni CHADEMA .

Chama kisicho na SERA kuliko vyote ni CHADEMA eti kwenye kampeni za kuuza SERA wao wanauza SERA zao hivi MSICHAGUE chama cha mafisadi.hii ni hatari na nusu

Hivyo ndg zangu huko Tarime akili ni nywere.

Kama sera nzuri za chama zingekuwa ndo utendaji wa chama basi CCM ingekuwa the best chama ever in the world! But alas!! look at what is happening in our beloved mother land Tanzania under the good sera of CCM for over 40 yrs!!!!

Kama akili ni nywere basi watanzania tuamke na tuzichane nywere zetu!
 
Wewe mwenyewe una ushahidi kwamba Dr. Slaa hana ushahidi kabla ya kumuita muokota udaku au unamuita majina kwa vile tu una uhuru wa kupiga madongo kutoka nyuma ya screen ya Komputa ?

Na wewe una ushahidi gani kuwa sina ushahidi kuhusu Dr Slaa au kwa vile una uhuru wa kuuliza kutoka kwenye nyuma ya screen yako ya kompyuta?
 
Last edited:
mag3,
Kama kila anayeikosoa Chadema au viongozi wake anakuwa amepewa kitu kidogo na RA, basi sio ajabu tuko wengi TZ wenye hivyo vimilioni.

Lakini huu ujinga uliopo JF, ambao na wewe inaelekea umeuvaa, wa kukubali kila lisemwalo na MChadema, utaniwia radhi maana wengine hatunao.

Suala hapa ni very simple, Mtikila katoa sumu hadharani na ushahidi wa aliyosema hata kwenye video upo, sasa Dr. Slaa na wenzake wengine walioshutumiwa kwa nini wasichukue hatua za kisheria?

Dr. Slaa ni msomi kama tulivyo wengi wetu, anaelewa wazi kuwa hakuna njia iliyo rahisi ya kutengeneza pesa kwenye common law system kama kumshitaki mtu anayekuchafulia jina. Angmshitaki ili azivune hizo 50m alizopewa na Makamba.

Dr. Slaa anayo haki ya kutuelezea au hata kupiga propaganda ya kwa nini Chadema wamekataa kuungana na wapinzani wenzao, lakini asitumie maneno ya Mtikila kufumbia ubinafsi waliojijengea ambao marehemu Wangwe alikuwa anaupinga.

Hiyo hela Mtikila atazilipa toka wapi? May be toka kwa hao mafisadi! Lakini hiyo kesi itaisha lini? Mafisadi wakiona mnapenda sana kushitaki, kila kukicha watakuwa wanaleta watu kama Mtikila ili muishie kushinda mahakamani! Mtikila aachwe/apuuzwe, siasa iendelee mbele. Na kama Mtikila ana hoja ndio yeye azipeleke polisi nk. Naamini Chadema ni chama kidogo hakihitaji kupoteza hela zaidi mahakamani badala ya kuzitumia kukikuza!

Naunga mkono hoja ya bwana mmoja aliyesema press isimpe publicity sana huyu Mtikila. Hii ni habari cheap sana kuiweka front page! Mtu hawezi kuita press na kusema chochote kikaandikwa! Fanyeni uchunguzi fuatilia hilo kanisa lake anaendesha vipi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom