Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Jakaya Kikwete, Rostam Aziz na wenzenu.... mnaipeleka Tanzania pabaya. Huu mpango wa kutumia fedha ili kuwadhoofisha watu/vyama vinavyoonekana kukubalika kwa wananchi utakuja kuwatokea puani... kama sio ninyi ni watoto wenu. Nchi haiendishwi hivyo. Huwezi kuuondoa "ugonjwa unakusumbua" kwa kuwafanya wenzio nao wawe wagonjwa... Mmeingia dili na Mtikila mkamhonga fedha na kumfutia kesi iliyokuwa inamkabili ili aichafue chadema.... LAKINI KUMBUKENI WATANZANIA WANAENDELEA KUSUMBUKA NA KUFA KWA UFISADFI WENU...OLE WAKO KIKWETE.. OLE WAKO ROSTAM...
 
Dr Slaa una ushahidi kuwa Makamba kampa 50m? Mh tunakuheshimu sana mambo ya kuokoteza udaku kwa mtu calibre yako sio mazuri kabisa
Je, Dr Slaa anao ushahidi kuwa hela za EPA zilikwapuliwa benki kuu? Mbona hilo haumwuulizi?
 
Magabe hujatulia wewe...! 🙂

Huyu jamaa hajatulia kabisa teh teh teh teh teh

Ajibu hoja ama tuhuma.

Chama kisicho na SERA ni chadema .Wewe utaendaje kuuza SERA zako kwa kusema hivi "msichague chama cha mafisadi" na kisipochakuliwa NEXT ???.

Na CHAMA cha wabishi ni CHADEMA .Na kibaya zaidi wanabisha wakiwa wametia masikio Pamba .

Eti Mr INVISIBLE Mimi nadhani hiyo kauli ingekua Kikorobwezo ambacho umeshakikorobweza na wakorobwezeka wemisha kwisha korobwezeka au sio?
 
Hivi mbona polisi hawajaenda kuwakata waliotajwa kuhusika na kifo cha Wangwe, pamoja na Mtikila mwenyewe kwa mahojiano ya kipolisi zaidi?

Mtikila anatakiwa achukuliwe na polisi aende akatoe maelezo ya kutosha, kisha ndipo hao watuhumiwa wanaweza kuhojiwa pia. Ni nani anaweza kukurupuka kwenda kubishana kwenye vyombo vya habari?

Lengo la Mtikila ni kuwafanya CHADEMA wawe na mambo mawili kwa wakati mmoja, kesi mahakamani, na uchaguzi Tarime. Dawa ni kumwacha tu, kama polisi wanamwamwini, waende wakawakamate watuhumiwa.

Hivi mwanaume mzima kutoka nyumbani kwake akiwa na akili timamu anyway, aseme utumbo kama huo, polisi wamchukue? nadhani tutawaonea sana polisi.

Kwa nini mtikila anaongea hivi sasa? huo ushahidi uko wapi? in my opinion huyu mtu ni hatari kama Ukimwi!

Tutawapa kazi ngumu polisi wakamate hata vichaa, wakimwacha kama alivyo, jamii ikaka kimya. Atajiona mjinga!

Waberoya
 
Huyu jamaa hajatulia kabisa teh teh teh teh teh

Ajibu hoja ama tuhuma.

Chama kisicho na SERA ni chadema .Wewe utaendaje kuuza SERA zako kwa kusema hivi "msichague chama cha mafisadi" na kisipochakuliwa NEXT ???.

Na CHAMA cha wabishi ni CHADEMA .Na kibaya zaidi wanabisha wakiwa wametia masikio Pamba .

Eti Mr INVISIBLE Mimi nadhani hiyo kauli ingekua Kikorobwezo ambacho umeshakikorobweza na wakorobwezeka wemisha kwisha korobwezeka au sio?

Haya wakwetu (poti) umeshinda mkuu
 
Lengo la Mtikila ni kuwafanya CHADEMA wawe na mambo mawili kwa wakati mmoja, kesi mahakamani, na uchaguzi Tarime. Dawa ni kumwacha tu, kama polisi wanamwamwini, waende wakawakamate watuhumiwa.


Mkuu Masaki,
Sidhani kesi mahakamani ni kazi ya kukifanya Chadema kipoteze mwelekeo Tarime. Kama hawataweza jambo dogo kama hilo la matamshi ya Rev., wanategemea wataweza kushughulikia vipi nchi nzima yenye majukumu kibao?

Mimi bado nafikiri ni vema kwa Chadema kumfikisha Mtikila mbele ya sheria ili ukweli uweze kujulikana, kinyume na hapo ni kukubali shutuma za Mtikila.
 
Haya wakwetu (poti) umeshinda mkuu

Hatushindani tunataka tunagonganisha hoja hapa.

Waika
Nipe SERA ya CHADEMA waliyoenda nayo huko kwenye kampeni,Maana nimejitahidi kufuatilia naona hizo password tu za kifisadi.
 
Hatushindani tunataka tunagonganisha hoja hapa.

Waika
Nipe SERA ya CHADEMA waliyoenda nayo huko kwenye kampeni,Maana nimejitahidi kufuatilia naona hizo password tu za kifisadi.
Mkamap,
Hivi CCM wana sera gani vile?
 
Mtikila hili sasa umelikoroga,itabidi ulinywe!

Tatizo sio kwa Mtikila tu kunywa alichokoroga, kimeongezeka tena kingine cha yeye kuingia kwenye kundi la wale wanaopanga mabaya dhidi ya Tarime kwa kutumia vyombo vya habari (TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi).

Haya mengine ya kutaka watu kwenda mahakamani kumshitaki Mtikila na blah blah zingine zote ni side show za kitoto ambazo wana Tarime walishazishtukia zamani sana.

Serikali na vyombo vya usalama vilikataa kufanya uchunguzi huru wa kifo cha Wangwe ili kufikisha hili jambo kwenye mwisho wake wakati hii issue ikiwa hot, leo hii wanaleta polisi kwa mamia Tarime huku Mtikila naye akija na hii press conference yake. Wenye kujua kinachoendelea hapa wanaendelea kutambua namna huu mchezo wa kuleta vita na machafuko Tarime unavyoandaliwa na unavyoendelezwa.

Bahati mbaya kwao ni kuwa, wana Tarime tuna akili zetu na hatutaruhusu ujinga kama huu utugawe na kuharibu wilaya yetu.
 
Mtikila hili sasa umelikoroga,itabidi ulinywe!

Tuwe wakweli lakini

Mimi naona humu ukumbini Mtikila angekua shujaa kama angemtaja RA,Lowasa na CCM ama wewe unaona je?

Na kulikoroga kwake ni kutotaja hao waliotakiwa kutajwa ama wewe unaona je?
 
Mi sifungamani na chama chochote,napenda kuwajulisha wote kuwa sasa hivi huyo Mtikila hana 'CREDIBILITY' yoyote huku mitaani na watanzania wengi tunamchukulia kama cartoon character flani.Chadema wakibishana nae nao watajishusha kwenye level yake.Kuna hakimu kisutu miaka ya nyuma alipropose akapimwe akili muhimbili sikumbuki kama agizo lilitekelezwa?
 
Hatushindani tunataka tunagonganisha hoja hapa.

Waika
Nipe SERA ya CHADEMA waliyoenda nayo huko kwenye kampeni,Maana nimejitahidi kufuatilia naona hizo password tu za kifisadi.

Nani amekwambia kuwa mimi ni mwakilishi au msemaji wa CHADEMA hapa? Umeona chochote kwenye maandishi yangu kilichoonyesha kuwa ninaiwakilisha CHADEMA hapa?

Usiingize siasa kwenye mambo makubwa kama hili la kifo cha Wangwe. Maisha ya watu yako kwenye very high stake hapa na wanatarime wamezungukwa sasa hivi na mamia ya askari ambao wamekuja "kutuliza fujo" ambazo no body so far amezithibitisha.

Ukitaka kuongelea siasa za CHADEMA na vyama vingine, unaweza kuanzisha thread nyingine hapa na ukaanza kuleta sera za CCM kabla ya kuwauliza wengine walete za vyama vyao.

Kuwa serious kidogo poti, maisha ya watu wengi wa Tarime yako kwenye line hapa na hizi propaganda zako hazimsaidii yeyote yule.
 
JF,
Siyo fedha za Rostam tu. Taarifa zinazotufikia ni kuwa ana 50 za Makamba pia. Amepewa kwa jukumu pekee la kuimaliza Chadema kama prelude ya Kampeni za Tarime. Amechelewa tu kwenda kule baada ya kuona kuna mvua ya mawe kwa wanaoichafua Chadema. Logic ya kuomba Scotland Yard ieleweke kwa msingi huo. Haitaitwa,na ataendelea kwa kisingizio hicho kukataa kutoa ushahidi. Hata hivyo, sina sababu ya kujibizana na Mtikila, mwisho umma hautajua kichaa ni nani.

Dr.W.Slaa,
Maneno yako yatakuwa na maana pale tu utakapotoa ushahidi juu ya madai yako vinginevyo huna sababu yeyote ya kumshutumu Mtikila.

Hapa JF tunamkoma nyani mchana kweupe, kama huna ushahidi don't waste your time here.

Lete ushahidi, hatutaki siasa zenu.
 
Mtikila belongs in a mental institution....restrained!! The man is suffering from recurrent verbal diarrhoea. Does he have to comment on everything? He certainly has an attention seeking personality which is fueled by the press! Journalists should start ignoring him!!
 
Kampani za kumrithi Chacha wangwe hizo. mtikila kishavuta uchache wake sasa anafanya kazi yake aliyotumwa na Mabwana zake. Huyu jamaa ni mjanja sana yaani anaishi mjini kwa kazi kama hizi. Na usikute deni kasemehewa na kaongezwa nyingine kama 10 hivi. Kwa nini asitoe ushahidi baada ya kifo anasubiri Kampeni za uchguzi zimeanza?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom