Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
Nakubaliana kabisaa na Invisible,
Dawa ya Mtikila ni kumpeleka mahakamani ambako kuna mwisho wa kila jambo kuliko kumuacha aendelee kumwaga sumu yake. Hao wanaosema eti waandishi waachane naye tu ndio dawa, wanaota ndoto za mchana maana sio kila gazeti/redio/TV wenye nia ya kuibeba Chadema. Kama akina Dr. Slaa wanataka Mtikila asiendelee kuwachongea kwa wananchi, basi watumie taratibu zinazoeleweka, ambayo sidhani kuna zaidi ya mahakama.
Nakubaliana na wewe kuhusu suala hili kupelekwa mahakamani, lakini kwa kawaida mahakamani ndio nyumbani kwa Mtikila. Amesema kuhusu Kolimba, hakuwa na ushahidi na ameshinda kesi. Alisema ya Mkapa, hakuwa na ushahidi Mkapa bado ni raia wa Tanzania, lakini kaachiwa hana hatia. Alisema ya Sumaye hana ushahidi lakini ameachiwa. Mahakamani atakwenda kuendeleza na itakuwa kuendeleza kuchafua aliokusudia kuwachafua.
Lakini pia suala la timing, yeye analenga uchaguzi wa Tarime kwa hiyo mahakamani kwa sasa ni kumpa ushindi Mtikila maana Tundu Lissu ni mwanasheria lakini ni mtu anayeheshimika sana kule Tarime, kwa hiyo kumfanya Lissu aache kusaidia ushindi wa Chadema Tarime aje Mahakamani ni kupunguza nguvu ya Chadema. Hata sasa huu mjadala unalenga kubadili mwelekeo wa kampeni za Tarime.
Nadhani suala la kumfikisha Mtikila mahakamani ni suala la wakati lakini ni LAZIMA ili kuweka kumbukumbu sahihi. Mtikila hasimami peke yake na hiyo inajulikana.