Ochu
Platinum Member
- May 13, 2008
- 976
- 50
Mtikila kuhojiwa na polisi
JESHI la Polisi limesema litamhoji Mchungaji Christopher Mtikila kutokana na madai yake kuwa kuna vigogo wamemuua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, marehemu Chacha Zakayo Wangwe.
Akizungumza na mwandishi wetu jana Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba alisema Mtikila atahojiwa kama atatoa ushirikiano kuhusu ushahidi alionao wa madai ya kuuawa kwa Wangwe.
"Ikiwa atathibitisha hayo madai ya kuuawa kwa Wangwe sisi kama jeshi la polisi tutashughulikia, tutamuomba tu aoneshe ushirikiano," alisema Manumba.
Juzi Jumapili Mchungaji Mtikila aliwaambia waandishi wa habari jijini Dare s Salaam kuwa, Wangwe aliuawa na watu kutoka Kenya kwa operesheni maalum iliyosukwa na vigogo (majina tunayahifadhi).
Alisema ana ushahidi wa kutosha wa jinsi vigogo hao walivyoshiriki kutekeleza mauaji hayo aliyoyaita ya kinyama.
Alimuomba Rais Jakaya Kikwete kukiajiri Kikosi Maalum cha Upelelezi cha Uingereza cha Scotland Yard kufanya uchunguzi wa kifo hicho kwa madai kuwa Wangwe alikuwa kiongozi wa kitaifa.