Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Wandugu,

Mzee wa Kiraracha anasema anayesema mapanga hayakuwepo... na kwamba kulikuwa na usalama 100% ni mwongo... hata yeye alificha kwa muda karibu na mwili wa marehemu kwa dakika 5.... source TBC1... mzee mwenyewe wa Kiraracha aliongea.
 
Kupondeka kwa gari hakutegemei ardhi peke yake...Huko majangwani kwenye mchanga gari hupondeka pale zinapopinduka. The factor here is speed! Hivi hujajiuliza kama ile rolling haikuanzia kwenye tarmac na kuishia pembeni? Au conspiracy theories zina cloud your reasoning?

Wangwe alikuwa nyuma na wengi wanapokaa nyuma hawafungi mkanda. Mallya na mtu mwingine (aliyetoka baruti baada ya ajali) walikuwa mbele na wengi wa mbele hufunga mikanda.

Usipofunga mkanda unarushwa huku na kule gari linapobingirika na kichwa ni sehemu mojawapo itakayojigonga.

OUTSIDE THE BOX...

Mallya tried to save his skin by telling a lie on who was behind the steering. He knew, dead men don't talk.

The key is the third person as, why would Wangwe sit behind if there was no third person? Unless he was very sick and decided to sleep in the back seat in that case the issue of him not having put on seat belt is self explanatory.

Insurgent,

Nakubaliana na theory yako. Naamini Mallya alikuwa anaendesha gari na Wangwe alikuwa kiti cha nyuma na most likely hakufunga mkanda. Atakuwa alichoka na kuamua kujipumzisha.
Kuumia alikoumia ni dalili ya mtu ambaye hakufunga mkanda. Ukifunga mkanda ni ngumu sana kupasuka kichwa labda ugonge mwamba au mti.

Duniani kote, wanaosababisha ajali husingizia waliokufa. Siamini kwamba kulikuwa na mtu wa tatu.
 
Hapana bwana; inategemea na wakati. Kama ni wakati wa vita sawa, huogopi kifo. Kama ni wakati wa mapinduzi, sawa huogopi kifo. Lakini katika hali ya kawaida, ya amani ambapo tunatarajia kuendesha mapambano haya kwa njia ya demokrasia na nguvu ya wananchi, mwanasiasa, kama binadamu mwingine yeyote, lazima aliweka swala la usalama wa maisha yake juu kabisa. Yeye ni binadamu kama binadamu mwingine, ana familia, watoto na wengi wa kumtegemea. Kama kuwa mwanasiasa ni kutokujali maisha yako, hapo wengi siasa itawashinda!

Lakini kuna kitu kikubwa zaidi hasa kwa mtu kama wewe ambaye ni mtetezi wa sheria na utaratibu, kwa kadri ninavyokuelewa katika post zako hapa. Mwenyekiti Mbowe, kiongozi mwenye dhamana ya chama na nchi yake, ameshauriwa na usalama wa taifa na vyombo vya usalama kwamba asibaki kwenye msiba kwa sababu usalama wake utakuwa hatarini, halafu akatae kufuata huo ushauri, huyu atakuwa ni kiongozi kweli? Akibaki halafu lolote likatokea, hata kama litafanywa na vyombo hivyohivyo, atakayelaumiwa hapo ni nani?

Mkuu Kitila,

Kushauriwa na usalama wa taifa sio kufuata sheria, huo ni ushauri tu ambao unaweza kuufuata au kuupuza. Hata angekataa angelikuwa hajavunja sheria yoyote ya nchi. Ingelikuwa polisi wakamwambia wamempiga marufuku kuhudhuria mazishi hapo ningeelewa.

Mkuu Kitila tuache siasa, mahali popote pale Tanzania ambayo ninaijua mimi, Mbowe angepata wakati mgumu kuhudhuria yale mazishi. Ingelikuwa kule kwetu ile kufika tu asingelirudi salama.

Hayo mambo yanatokea kila siku, wananchi wakijua tu jamaa alikuwa na ugomvi na aliyekufa na anaenda kwenye mazishi hutokea kasheshe. Hata kwenye familia, wakiachana na kugombana, akifa mmoja, huyo mwenza kwenda inakuwa kasheshe. Sasa mnataka kutuambia Mbowe angepokelewa kwa mikono miwili kule Tarime baada ya hayo yote yaliyotokea kati yake na Wangwe? Siami kabisa mkuu, hiyo itakuwa sio Tanzania ninayoijua mimi.
 
Mzee wa Kijiji,
Nimesoma article yako ya leo kwenye Tanzania Daima. Ilikuwa kama nasoma novel ya Agatha Christie! Hongera. Enzi zetu tukisoma hizo detective stories kuna kitu kinaitwa 'lie detector'. Sasa hako kajamaa kanakoitwa Deus Mallya bila shaka kakiwekewa hiyo lie detector kakahojiwa juu ya yote haya tunayoyasikia na kusoma, itadhihirika kirahisi sana wapi kanadanganya na kutuwezesha kuondoa mkanganyiko na hisia zinazotusumbua.

Kutokana na yote yanayotokea nchini mwetu hivi sasa, akina sie wa mwaka 47 tunabaki midomo wazi kuona jinsi nchi inavyobadilika! Mwenyezi Mungu atunusuru na majanga.
 
amesema kuwa kuna mtu yeyote alifukuzwa na mapanga? na yeye aliona mapanga mangapi... kuna mtu yeyote mwenye picha ya mapanga hayo? TBC waliokuwa kule wameonesha video ya mapanga au wamemhoji tu.
 
Habari hii kuhusu Mallya anadaiwa kumuendesha Marehemu Wangwe ni Jasusi inatoka kwa viongozi wa Vyama vya upinzani kama ilivyo katika gazeti la Tanzania Daima hapa chini......

‘Mallya ni jasusi’

na Kulwa Karedia

VIONGOZI watatu kutoka kambi ya upinzani, wameibua madai mengine mazito yanayoonyesha kuwa mtu anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, ni jasusi aliyefuzu mafunzo hayo na ni mtaalamu wa hali ya juu wa kompyuta.

Viongozi hao na vyama vyao kwenye mabano ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia (NCCR – Mageuzi) na Augustine Mrema (TLP).

Waliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya NCCR- Mageuzi, Dar es Salaam jana kuwa, Mallya ni mmoja wa watu wanaoonekana kupata mafunzo makali ya kijasusi, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa.

Aliyeanza kuzungumza katika mkutano huo ni Profesa Lipumba, ambaye alidai kuwa Mallya aliwahi kupata mafunzo hayo nchini Libya, jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na vyombo vya usalama ili kubaini ukweli zaidi.

“Huyu tunaambiwa alikuwa dereva wa Wangwe, lakini tunaambiwa kwamba ni mtu ambaye alizoeana naye kwa muda mfupi sana, hali ambayo inaibua maswali mengi …lakini tunaambiwa aliwahi kuishi Libya, sasa huku alikuwa anafanya nini?” alihoji Profesa Lipumba.

Alisema mbali ya Mallya kuwa na mafunzo hayo, pia katika upekuzi alikuwa na vitambulisho vingi ambavyo vilikuwa na maandishi mbalimbali yakiwamo ya Kiarabu.

“Mbali ya kuishi Libya kijana huyo, alikutwa na vitambulisho vingi mno, tena vikiwa katika lugha mbalimbali, vikiwemo vyenye maandishi ya Kiarabu, ndiyo maana tunasema huyu ni jasusi na mtu mwenye mafunzo makali,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema Mallya anaweza kuwa na maelezo mengi kama akihojiwa vizuri jinsi alivyoweza kumfahamu marehemu Wangwe na mazingira mazima ya ajali ilivyotokea,” alisema Profesa Lipumba.

Kuhusu hali ya vurugu iliyotokea wilayani Tarime wakati wa mazishi ya Wangwe, Profesa Lipumba alikiri kuwapo hali hiyo, jambo ambalo alisema liliwatia shaka viongozi wote waliohudhuria mazishi hayo.

“Unajua pale Tarime wananchi walionekana kuwa na munkari sana, huku wakionyesha kutoamini kwamba Wangwe kafariki kwa ajali ya gari…lakini baada ya uchunguzi na maelezo yaliyotolewa na kaka yake, Profesa Samwel Wangwe, ulionyesha kuwa alikufa kwa ajali iliyosababisha fuvu la kichwa kupasuka,” alisema Profesa Lipumba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, Mbatia, alisema mazingira waliyoyakuta Tarime yalikuwa ya hatari na kumpongeza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Lebaratus Lyimo na Mkuu wa mkoa huo, Kanali mstaafu, Issa Machibya, kwa kuhakikisha hali ya utulivu na amani inakuwapo.

Alisema mbali ya hali hiyo, kifo cha Wangwe bado kimewatia mashaka wapinzani, kwani inaonyesha kuna mtandao wa uhalifu unaotishia usalama wa taifa.

“Tumegundua kuwa hivi sasa kunaonyesha wazi kwamba kuna mtandao wa uhalifu, uharamia unaotishia usalama wa taifa letu, kwa moyo mweupe nasema lazima tujitolee ili kuhakikisha hali hii haitokei kabisa,” alisema Mbatia.

Alisema wamepata taarifa nyeti kwamba Mallya amepata mafunzo makali ya kijasusi, ikiwamo kupindua magari, na kwamba hiyo inawalazimu kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, kwa ajili ya kumweleza ukweli wa mambo hayo.

“Kutokana na ukweli wa mambo haya, sasa tunajiandaa kukutana na IGP Mwema kwa ajili ya kumweleza ukweli kuhusu kijana huyu Mallya… tupo hapa kwa masilahi ya taifa letu,” alisema Mbatia.

“Tunasema uhalifu huu lazima ukomeshwe, taifa haliko salama, niko tayari kumweleza ukweli wa mambo kuhusu suala hili, hatupaswi kuficha, tutatoa ushirikiano wa kila aina kutokomeza uhalifu huu na kwamba tunataka jambo hili liwekwe hadharani,” alisema Mbatia.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Mrema, alisema kambi ya upinzani imepata pigo kubwa kwa kupoteza kiongozi shupavu na mtetea haki za watu wake.

“Kwa mara ya kwanza kambi ya upinzani tumepata pigo kubwa ambalo halijawahi kututokea…tumezoea kuyaona kwa wenzetu, sasa kazi iliyoko mbele yetu ni kupambana na tatizo hili ili kuona nchi yetu inabaki salama,” alisema Mrema.

Alisema mtandao wa kijana huyo umesambaa nchini na kuitaka polisi kutopuuzia madai hayo, kwa lengo la kuhakikisha hali ya ulinzi na utulivu inaendelea kuwapo nchini.

Akizungumzia ilivyokuwa Tarime, Mrema alilipongeza Jeshi la Polisi wilayani humo kwa kutotumia nguvu ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye mazishi hayo.

“Kama polisi wangetumia nguvu kubwa pale msibani, hali ingekuwa mbaya, lakini walitumia busara iliyowezesha hata sisi kuendelea kubaki pale… hali ya usalama haikuwa nzuri sana, mpaka viongozi wote tulipitishwa kwenye mlango ambao mwili wa marehemu ulikuwa umewekwa,” alisema Mrema.

Alisema katika mazishi hayo, baadhi ya T-shirt zilizokuwa zimeandaliwa na bendera zilichomwa moto, kitendo kinachoashiria kuwapo kwa vurugu zilizotokana na ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wa Wangwe, kutaka kujua sababu ya kifo cha Wangwe.

Alisema hasira ya wananchi wa Tarime haikutokana na ujio wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Wakati wapinzani wakitoa tuhuma hizo nzito dhidi ya Mallya (27), tayari kijana huyo amefunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, akidawa kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo, kumekuwa na maswali mengi kuhusu ni nani hasa alikuwa akiendesha gari lililosababisha kifo cha Wangwe, baada ya maelezo ya watu mbalimbali kuonyesha kuwa Mallya ndiye aliyekuwa dereva, tofauti na maelezo ambayo amekuwa akiyatoa kwa siku kadhaa sasa.

Katika mahojiano ya ana kwa ana aliyofanya na Tanzania Daima kwa nyakati mbili tofauti, Mallya alifikia hatua ya kudai kwamba alikuwa hajawahi kuendesha gari na kwamba alikuwa hana utaalamu wowote wa udereva.

“Mimi sijui kuendesha gari na wala sina utaalamu wowote wa kuendesha magari, nimeshangazwa sana na taarifa za watoto wa marehemu zilizopo magazetini kwamba tulipotoka nyumbani nilikuwa namuendesha baba yao.

“Ninayaogopa sana magari, lakini niliwahi kujifunza mwaka 2004, nikiwa Nairobi, yupo rafiki yangu mmoja alinishawishi kujifunza, lakini niliacha, wakati najifunza niligonga ukuta, nikaumia vibaya na sikujifunza tena mpaka leo, hivyo sijui kabisa kuendesha,” alisema Mallya wakati alipohojiwa na Tanzania Daima siku mbili tu baada ya ajali.

Kauli hiyo ya Mallya ilikuwa ikitofautiana na ile iliyotolewa na watoto wawili wa marehemu Wangwe, Zakayo na Bob, ambao wote walisema wakati wakiondoka nyumbani siku hiyo ya Jumatatu wiki iliyopita, kijana huyo ndiye aliyekuwa akiendesha gari.

Aidha, maelezo yaliyotolewa na mkazi mmoja wa Pandambili aliyekuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika eneo la tukio kuhusu nani aliyekuwa akiendesha gari hilo, nayo yanaonyesha picha tofauti na ile iliyokuwa ikielezwa na Mallya.

Katika mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima, mkazi huyo wa Pandambili, George Mwigunde, alieleza kuwa, walimkuta marehemu akiwa amekaa katika kiti cha mbele cha abiria cha mkono wa kushoto wakati ajali hiyo ilipotokea.

Mwigunde ambaye alijitambulisha kuwa ni mkulima wa kijiji hicho, alisema kabla ya kumtoa marehemu Wangwe, alilazimika kumfungua mkanda wa gari kutoka katika kiti chake hicho alipokuwa ameketi.

Utata huo kuhusu nini kilitokea hata kumsababishia mauti Wangwe, ulisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilazimike kuandika barua kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kikitaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina.

CHADEMA katika tamko lake hilo ilisema imefikia uamuzi huo kutokana na kuwapo kwa taarifa zinazoonyesha kuwapo kwa utata katika tukio zima.

Chama hicho kilimtaka IGP kumchunguza Mallya na kubainisha ni mtu wa namna gani, ikiwa pamoja na kufuatilia shughuli zake na uhusiano aliokuwa nao na marehemu Wangwe.

CHADEMA pia ilimtaka IGP kuchunguza ukweli kuhusu maelezo ya Mallya na kujua ni wapi alikuwa amekaa wakati ajali ikitokea na kuchukua hatua zinazopaswa baada ya uchunguzi huo.
 
amesema kuwa kuna mtu yeyote alifukuzwa na mapanga? na yeye aliona mapanga mangapi... kuna mtu yeyote mwenye picha ya mapanga hayo? TBC waliokuwa kule wameonesha video ya mapanga au wamemhoji tu.

You know, kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba: kwa wakurya (esp. in rural areas) kutembea na silaha za jadi kama rugu, panga, sime, bakora ni kitu cha kawaida kabisa. Ni kitu cha kawaida kwasababu ya nature ya maisha yao (ufugaji/uwindaji/ukulima) inayo demand wao kutembea na silaha hizo za jadi at any time. Kama ilivyo kwa wazaramo kushindia vijiweni na vikombe vya kahawa na kashata (most of the time), wakurya nao kutembea na paga/sime/rugu/bakora muda wote (walioko vijijini hususani) is a part of who they are. So, hata kama hayo mapanga yalikuwepo msibani (na hukuna aliyeripotiwa kujeruhiwa), then sioni point ya kulishikia bango suala hili. Besides, Wangwe alikuwa anapendwa sana! So you can see kwanini damu za watu/wakurya zilikuwa zina boil-up siku ya mazishi.
 
Last edited:
Aisee BongoTZ ambae kashikilia suala la mapanga kuwepo au kutokuwepo ni Zito Kabwe. Yaani safari hii wanaogopa na wameona kifo cha Chacha Wangwe kimewaharibia kisiasa. Angalia hata Dr Slaa hasikiki ilhali alikuwa huko na alionekana kwenye TV amejaa hofu na woga wa kucharazwa mapnga na waombolezaji. Lakini kwa kuwa yeye ni bingwa wa kuhonga waandishi wa magazeti hakuna ambacho wamekiandika juu yake. Sisi tuliohudhuria tunajua Slaa na Mbowe mzimu wa Chacha Wangwe utaendelea kuwasuta. Hamkuuona unafiki wao baada ya kifo chake. Ni kama wiki 3 zilizopita walimfukuza umakamu wenyekiti. Leo yule dogo Mnyika ambaye Slaa kuijanja kaona eti awe Kaimu Katibu Mkuu, ndiyo anasema Chacha alikuwa Vice Chairman wao na blah blah. Kweli unafiki huo ulinitia kichefuchefu. Hawana lolote. Wanafiki wakubwa. Wakae wakijua by election ijayo hicho kiti wamekipoteza. Ndiyo maana kama umesoma gazeti la Tanzania Daima jana utaona jitihada ya kumsafisha Mbowe. Naye huyo Datoo eti kaunda tume ya kuchunguza. Nothing but cheap propaganda.
 
chadema inataka kujisafisha sana kwenye hili, kwa sababu wanaogopa isije ikawa ndio sababu ya kuanguka kwa chama chao.

yes, walikuwa na mgogoro na wangwe, hilo halifutiki....na pia halisababishi wao kuwa wameingiza mkono kwenye kifo chake.

ila sishangai kutoshangaa kusikia kikundi kidogo kilikuwa na hasira na hakikutaka kumuona mbowe msibani hapo.

yaweza kuwa mbowe hakufukuzwa kwa mapanga, ila mapanga yalikuwepo kama anavyosema mrema. na si mbowe tu aliyeingia hofu kwa kuona mapanga hayo, hata mrema labda na viongozi wengine walishtuka, licha ya kuwa mapanga hayo hayakuelekezwa kwao moja kwa moja.
 
Hivi jamani mbona sioni hoja za msingi? Mapanga, mawe, mishale, bunduki, risasi na kadhalika. Mbowe, Slaa na kadhalika sawa. Hivi niwangapi hamjawahi kukosana na marehemu (yaani yeyote aliepoteza maisha)? Hivi kweli kabisa mgogoro wa chadema na wangwe umepelekea huku? tumekuwa wavivu wa kusurubiri au kufikiri? hivi hapa tunajadili nini? tumesahau usifadi wa kila siku? mtu wakishindwa kueelewana bahati mbaya au makusudi akatutoka tunaanza hivi? ama kweli tumepoteza mwelekeo!

Kwaherini
 
Kama ni kweli basi haya mambo yanazidi kupanuka na mwisho tutapata habari za kusikitisha zaidi. Soma hii kutoka gazeti la Tanzania Daima.

‘Mallya ni jasusi’

na Kulwa Karedia

VIONGOZI watatu kutoka kambi ya upinzani, wameibua madai mengine mazito yanayoonyesha kuwa mtu anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, ni jasusi aliyefuzu mafunzo hayo na ni mtaalamu wa hali ya juu wa kompyuta.

Viongozi hao na vyama vyao kwenye mabano ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia (NCCR – Mageuzi) na Augustine Mrema (TLP).

Waliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya NCCR- Mageuzi, Dar es Salaam jana kuwa, Mallya ni mmoja wa watu wanaoonekana kupata mafunzo makali ya kijasusi, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa.

Aliyeanza kuzungumza katika mkutano huo ni Profesa Lipumba, ambaye alidai kuwa Mallya aliwahi kupata mafunzo hayo nchini Libya, jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na vyombo vya usalama ili kubaini ukweli zaidi.

“Huyu tunaambiwa alikuwa dereva wa Wangwe, lakini tunaambiwa kwamba ni mtu ambaye alizoeana naye kwa muda mfupi sana, hali ambayo inaibua maswali mengi …lakini tunaambiwa aliwahi kuishi Libya, sasa huku alikuwa anafanya nini?” alihoji Profesa Lipumba.

Alisema mbali ya Mallya kuwa na mafunzo hayo, pia katika upekuzi alikuwa na vitambulisho vingi ambavyo vilikuwa na maandishi mbalimbali yakiwamo ya Kiarabu.

“Mbali ya kuishi Libya kijana huyo, alikutwa na vitambulisho vingi mno, tena vikiwa katika lugha mbalimbali, vikiwemo vyenye maandishi ya Kiarabu, ndiyo maana tunasema huyu ni jasusi na mtu mwenye mafunzo makali,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema Mallya anaweza kuwa na maelezo mengi kama akihojiwa vizuri jinsi alivyoweza kumfahamu marehemu Wangwe na mazingira mazima ya ajali ilivyotokea,” alisema Profesa Lipumba.

Kuhusu hali ya vurugu iliyotokea wilayani Tarime wakati wa mazishi ya Wangwe, Profesa Lipumba alikiri kuwapo hali hiyo, jambo ambalo alisema liliwatia shaka viongozi wote waliohudhuria mazishi hayo.

“Unajua pale Tarime wananchi walionekana kuwa na munkari sana, huku wakionyesha kutoamini kwamba Wangwe kafariki kwa ajali ya gari…lakini baada ya uchunguzi na maelezo yaliyotolewa na kaka yake, Profesa Samwel Wangwe, ulionyesha kuwa alikufa kwa ajali iliyosababisha fuvu la kichwa kupasuka,” alisema Profesa Lipumba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, Mbatia, alisema mazingira waliyoyakuta Tarime yalikuwa ya hatari na kumpongeza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Lebaratus Lyimo na Mkuu wa mkoa huo, Kanali mstaafu, Issa Machibya, kwa kuhakikisha hali ya utulivu na amani inakuwapo.

Alisema mbali ya hali hiyo, kifo cha Wangwe bado kimewatia mashaka wapinzani, kwani inaonyesha kuna mtandao wa uhalifu unaotishia usalama wa taifa.

“Tumegundua kuwa hivi sasa kunaonyesha wazi kwamba kuna mtandao wa uhalifu, uharamia unaotishia usalama wa taifa letu, kwa moyo mweupe nasema lazima tujitolee ili kuhakikisha hali hii haitokei kabisa,” alisema Mbatia.

Alisema wamepata taarifa nyeti kwamba Mallya amepata mafunzo makali ya kijasusi, ikiwamo kupindua magari, na kwamba hiyo inawalazimu kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, kwa ajili ya kumweleza ukweli wa mambo hayo.

“Kutokana na ukweli wa mambo haya, sasa tunajiandaa kukutana na IGP Mwema kwa ajili ya kumweleza ukweli kuhusu kijana huyu Mallya… tupo hapa kwa masilahi ya taifa letu,” alisema Mbatia.

“Tunasema uhalifu huu lazima ukomeshwe, taifa haliko salama, niko tayari kumweleza ukweli wa mambo kuhusu suala hili, hatupaswi kuficha, tutatoa ushirikiano wa kila aina kutokomeza uhalifu huu na kwamba tunataka jambo hili liwekwe hadharani,” alisema Mbatia.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Mrema, alisema kambi ya upinzani imepata pigo kubwa kwa kupoteza kiongozi shupavu na mtetea haki za watu wake.

“Kwa mara ya kwanza kambi ya upinzani tumepata pigo kubwa ambalo halijawahi kututokea…tumezoea kuyaona kwa wenzetu, sasa kazi iliyoko mbele yetu ni kupambana na tatizo hili ili kuona nchi yetu inabaki salama,” alisema Mrema.

Alisema mtandao wa kijana huyo umesambaa nchini na kuitaka polisi kutopuuzia madai hayo, kwa lengo la kuhakikisha hali ya ulinzi na utulivu inaendelea kuwapo nchini.

Akizungumzia ilivyokuwa Tarime, Mrema alilipongeza Jeshi la Polisi wilayani humo kwa kutotumia nguvu ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye mazishi hayo.

“Kama polisi wangetumia nguvu kubwa pale msibani, hali ingekuwa mbaya, lakini walitumia busara iliyowezesha hata sisi kuendelea kubaki pale… hali ya usalama haikuwa nzuri sana, mpaka viongozi wote tulipitishwa kwenye mlango ambao mwili wa marehemu ulikuwa umewekwa,” alisema Mrema.

Alisema katika mazishi hayo, baadhi ya T-shirt zilizokuwa zimeandaliwa na bendera zilichomwa moto, kitendo kinachoashiria kuwapo kwa vurugu zilizotokana na ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wa Wangwe, kutaka kujua sababu ya kifo cha Wangwe.

Alisema hasira ya wananchi wa Tarime haikutokana na ujio wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Wakati wapinzani wakitoa tuhuma hizo nzito dhidi ya Mallya (27), tayari kijana huyo amefunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, akidawa kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo, kumekuwa na maswali mengi kuhusu ni nani hasa alikuwa akiendesha gari lililosababisha kifo cha Wangwe, baada ya maelezo ya watu mbalimbali kuonyesha kuwa Mallya ndiye aliyekuwa dereva, tofauti na maelezo ambayo amekuwa akiyatoa kwa siku kadhaa sasa.

Katika mahojiano ya ana kwa ana aliyofanya na Tanzania Daima kwa nyakati mbili tofauti, Mallya alifikia hatua ya kudai kwamba alikuwa hajawahi kuendesha gari na kwamba alikuwa hana utaalamu wowote wa udereva.

“Mimi sijui kuendesha gari na wala sina utaalamu wowote wa kuendesha magari, nimeshangazwa sana na taarifa za watoto wa marehemu zilizopo magazetini kwamba tulipotoka nyumbani nilikuwa namuendesha baba yao.

“Ninayaogopa sana magari, lakini niliwahi kujifunza mwaka 2004, nikiwa Nairobi, yupo rafiki yangu mmoja alinishawishi kujifunza, lakini niliacha, wakati najifunza niligonga ukuta, nikaumia vibaya na sikujifunza tena mpaka leo, hivyo sijui kabisa kuendesha,” alisema Mallya wakati alipohojiwa na Tanzania Daima siku mbili tu baada ya ajali.

Kauli hiyo ya Mallya ilikuwa ikitofautiana na ile iliyotolewa na watoto wawili wa marehemu Wangwe, Zakayo na Bob, ambao wote walisema wakati wakiondoka nyumbani siku hiyo ya Jumatatu wiki iliyopita, kijana huyo ndiye aliyekuwa akiendesha gari.

Aidha, maelezo yaliyotolewa na mkazi mmoja wa Pandambili aliyekuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika eneo la tukio kuhusu nani aliyekuwa akiendesha gari hilo, nayo yanaonyesha picha tofauti na ile iliyokuwa ikielezwa na Mallya.

Katika mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima, mkazi huyo wa Pandambili, George Mwigunde, alieleza kuwa, walimkuta marehemu akiwa amekaa katika kiti cha mbele cha abiria cha mkono wa kushoto wakati ajali hiyo ilipotokea.

Mwigunde ambaye alijitambulisha kuwa ni mkulima wa kijiji hicho, alisema kabla ya kumtoa marehemu Wangwe, alilazimika kumfungua mkanda wa gari kutoka katika kiti chake hicho alipokuwa ameketi.

Utata huo kuhusu nini kilitokea hata kumsababishia mauti Wangwe, ulisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilazimike kuandika barua kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kikitaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina.

CHADEMA katika tamko lake hilo ilisema imefikia uamuzi huo kutokana na kuwapo kwa taarifa zinazoonyesha kuwapo kwa utata katika tukio zima.

Chama hicho kilimtaka IGP kumchunguza Mallya na kubainisha ni mtu wa namna gani, ikiwa pamoja na kufuatilia shughuli zake na uhusiano aliokuwa nao na marehemu Wangwe.

CHADEMA pia ilimtaka IGP kuchunguza ukweli kuhusu maelezo ya Mallya na kujua ni wapi alikuwa amekaa wakati ajali ikitokea na kuchukua hatua zinazopaswa baada ya uchunguzi huo.
 
SILAHA JADI YA WAKURYA..NIWAULIZE KUNA ATAKAYESHANGAA SILAHA KWA MASAI AU ZULLU?...NA DEFINATTELY PENYE SILAHA HAKUNA USALAMA 100%.......ILA SI BUSARA KU CAPITALIZE..KWENYE UBEBAJI WA JADI WA SILAHA....

WAPINZANI NAONA SASA WANA MIX WENYEWE....KAMPENI ZA UBUNGE ZIMEANZA????....nasikia hawa nccr na tlp...walijaribu kumshawishi kaka yake chacha mmoja ajiunge nao agombee ..hawajafanikiwa hadi sasa......suala la mgombea mmoja mwaka 2010 litawezekana?????

wapinzani wajitahidi kuwa na hoja za pamoja...naona statement ya chadema iliwahi sana ...au baada ya chadema kuongea UMOJA haukutakiwa tena kuongea....makosa wangerekebishana wenyewe..
 
Profesa Lipumba ameongea Pumba bila kujijua. Kitendo cha kumuuta Mallya jasusi ni kumkuza kupindukia. Kwa habari za kipaparazi ni kuwa Mallya alikwenda Libya kwenye mkutano wa siku tatu na alikwenda pamoja na mufti shaban simba na wabunge wa CCM. ulikuwa mkutano wa kujadili kuunganisha Afrika tu.

Habari zinaeleza zaidi kuwa Mallya anajua kompyuta lakini ni graphics tu, yaani kubuni michoro kwa kutumia kompyuta. Ni mtu wa sanaa.

Nitafuatilia zaidi kujua nini kimewafanya viongozi watatu wa upinzani waliobaki wenyewe Tarime kuja na hadithi hiyo. Viongozi wa CHADEMA watueleze hapa, kwanini hawakuwepo kwenye hiyo press conference? Kwa nini tamko halikuwa kwenye maandishi yaliyotiwa saini na vyama vinne kama ilivyo kawaida?

Je, ushirikiano wa upinzani umevunjika sababu ya msiba wa Chacha Wangwe? Niliwaeleza hapa siku chache zilizopita kwamba kuna kiongozi wa upinzani atahusishwa kwenye vikao na Rostam kumjibu Zitto Kabwe. Ngoja nipate taarifa kamili kama kilifanyika. Nitawajulisha

PM
 
Viongozi hao pia walithibitisha habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuwa vurugu zilizotokea siku ya yalipoahirishwa maziko ya Wangwe zilisababisha baadhi ya viongozi kuamriwa na Polisi kuondoka eneo hilo. "Hali ilikuwa mbaya sisi wenyewe tuliingizwa kwenye chumba cha maiti kuhemea humo tukakaa dakika 10 na akina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) ndipo tukaondoka katika eneo hilo," alisema Mrema.

Naye Mbatia alikiri kuwa vijana walikuwa wamebeba silaha za jadi na kama isingekuwa busara ya Polisi na ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, kulikuwa na uwezekano wa kutokea vurugu. Alisema viongozi wengi wakiwamo wabunge na mawaziri waliruka uzio kutokana na hali kuwa tete kwenye msiba na hiyo inatokana na utata wa kifo cha Wangwe.

Alisema hata fulana zilizoandaliwa kwa heshima ya marehemu zilichomwa moto pamoja na bendera za baadhi ya vyama vya siasa. Hata hivyo hakutaja vyama ambavyo bendera zake zilichomwa moto. Juzi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alikanusha habari zilizoandikwa na vyombo vya habari kuhusiana na vurugu hizo. Alizielezea habari hizo kuwa zilikuwa za uzushi zenye lengo la kukiua chama cha Chadema.

Habari yote hii hapa;

ikumbukwe kwamba wanazi wa chama fulani walisema hakupakuwa na tatizo lolote.
 
Wandugu,

Mzee wa Kiraracha anasema anayesema mapanga hayakuwepo... na kwamba kulikuwa na usalama 100% ni mwongo... hata yeye alificha kwa muda karibu na mwili wa marehemu kwa dakika 5.... source TBC1... mzee mwenyewe wa Kiraracha aliongea.

Mrema alisema, "Waandishi wa habari walikuwepo toka asubuhi. Labda waliyaona mapanga. Sasa kama mapanga yalionekana. Halafu watu wanakuja baadaye kuimba hatoki mtu bila chacha wangwe. Kuna usalama kweli?"

Nilitaka kumuuliza Mrema, umeyaona mapanga kwa macho yako au umesikia? Kama umesikia tu. Nini kimekutuma uthibitishe?

Niltaka kumuuliza pia, CHADEMA wameonyesha wahariri mkanda ambao hauna mapanga na mikuki una watu wakiimba nyimbo za kumsifu Chacha na kuhoji kifo chake. Tena kwa sehemu kubwa wakifurahia. Vijana, wakizunguka zunguka huko na huko na mabango. Je, yeye anaweza kuonyesha mkanda kuwa kulikuwa na mapanga, mikuki nk?

Je, yuko tayari kutoa ushahidi akiitwa na Jukwaa la Wahariri kuthibitisha kwamba kulikuwa na mapanga, mikuki nk?

PM
 
sikubaliani na umoja wa wapinzani, kwani kila chama kina sera zake na endapo wataungana kama wanavyosema basi msishangae yanayomtokea KIBAKI na chama chake cha PNU yatakuwa ndo life style.
Pili, kuungana kwa wapinzani ni dalili ya uroho wa madaraka maana endapo wanapenda kuungana basi wanejiunga ktk chama wanachoamini kina sera wanazokubaliana nazo ili kutoa nguvu ya ushindi.
Thus nasema kuondokewa na mpambanaji (WANGWE) ni pigo kwa chadema na wajipange kuweka mambo sawa ili safari iendelee....
Hebu tuchukue mfano, endapo chama changu (CCM) kitashindwa uchaguzi mkuu, je kitaungana na chama au vyama vyengine vya upinzani kuitoa CHADEMA madarakani???? nasisitiza kila chama kijipange kama timu za ligu kuuu au la viwe tayari kununua mechi (UFISADI) ili vipate kushinda au walau nafasi za juu....
 
we cant rule out anything......
mallya anahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina mno. .....
historia yake ina utata na anaonyesha ni msemaji uongo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom