Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Wanabodi,
Natanguliza samahani mbele ya haya nitakayo yasema kwa sababu sina hakika kama yamekwisha zungumziwa.
Moja ni kuhusiana na Prof Wangwe ambaye inaonyesha kabadilisha msimamo wake kuhusiana na kesi hii, limewatatiza wengi lakini wameshindwa kufahamu kwamba hata Vyombo vya Usalama kama Polisi wanaweza kubadilisha msimamo kulingana na ushahidi unavyo zidi kupatikana. Mkisiwa wa kwanza akawa huru, na mtu mwingine kabisa nje akavutwa ndani kama mhusika maadam file halijafungwa. Na hata kama limefungwa linaweza kufunguliwa upya na madai mapya kabisa yakatokea!. Hii haina maana Polisi ni wajinga kufikia uamuzi wa kwanza.

Nikirudi ktk sakata hili la wangwe nimesoma mahala wanabodi wakihoji hoja ya wangwe ambayo ilikuwa iwakilishwe bungeni.. Ukweli ni kwamba ninavyofahamu mimi mbunge yoyote anayetaka kuwakilisha hoja huipeleka kwa Spika ili apatiwe ruksa na hupitiwa kuangalia nafasi yake, uzito wake na kadhalika. Kisha mbunge hujulishwa kwamba hoja yake itasimama. kama mnakumbuka vizuri Dr. Slaa alipeleka hoja ya BoT bungeni ikakataliwa au kwa namna fulani alishtuka yeye kwamba haiwezi kukubaliwa. Zito pia (kama sikosei ama mbunge fulani) kuna sehemu kama nakumbuka vizuri alihoji kuhusiana na swala moja ambalo halikuwa ktk hoja yake ya awali (inayotambuliwa na spika) kiasi kwamba ilitolewa nje hali uzito wake ulikuwa mkubwa... sasa basi kama Wangwe alikuwa na hoja ambayo alitaka kuiwakilisha bungeni kuna uwezekano mkubwa kuwa spika ameisha ipata, lakini hapo hapo kwa kutumia njama CCM wanaweza kabisa kuibadilisha na kuweka hoja tofauti kwa sababu sio lazima Chadema wafahamu hoja ya Wangwe ambayo ilikuwa inawakilisha jimbo lake kama mbunge wa Tarime..Nasema hivi kwa sababu wapo wabunge wa CCM ambao huingiza hoja kuuliza viongozi wa wizara fulani bila viongozi hao kuwa na taarifa za hoja hiyo nje ya bunge.
Hakuna kiongozi wa CCM aliyejua kwamba mama Kilango angeuliza swali kuhusiana na Mafisadi wa EPA kabla ya bunge kuanza ila kuna uwezekano watu wa karibu naye iwe ndani ya CCM, ama marafiki wanaweza kuwa nataarifa hiyo kutokana na ukaribu wao kwa mtoa hoja...
Hofu yangu kubwa isije kuwa CCM wakaunda FITNA na kusema kwamba hoja ya Wangwe inahusiana na Mbowe wakati swala na matatizo ya ndani ya chama cha Chadema huwasilishwa kwa wanachama wa chama hicho wazee, ama viongozi wa chama na sio bungeni..
Kwa hiyo tuwe macho tuelewe kwamba hapa CCM wanaweza kusuka FITNA na dalili zimeshaanza kujitokeza kiasi kwamba mimi hapa najiuliza ilikuwaje CCM wawe na nakala za malalamiko ya Wangwe kuhusiana na viongozi wa Chadema hali marehemu alisema anapeleka kesi hiyo kwa wanachama na hata ikibidi kufika Mahakamani atakwenda kupata haki yake.. hapo hapo tunaelewa wazio kwamba laptop yake ilipotea ama kuibiwa!...
I mean guys kweli hapo kijijini kibaka aibe laptop na kuacha simu za mkono..Of all the thing -laptop ndio ya kwanza kuondoka na huyu Mallya mbali na msukosuko wa ajali aliweza kufahamu kwamba laptop imechukuliwa na vibaka..
Muda gani alikuwa nao kutazama vitu vilivyoibiwa na ashindwe hata kuwafukuza wezi kwa sababu hakuwa na jeraha, alitoka mzima hana hata vumbi!..
Guys something is very wrong!...Ndivyo hata FBI huunda kesi zao jamani tusifikirie tu kwamba hii ni ajali na Mungu ndiye aliyepanga....Basi kama ni kweli Mungu ndiye aliyepanga (mawazo yalifungana na Utumwa wa akili) inakuwaje Mungu huyo huyo amhukumu moto wa Jahanam muuaji hali ni yeye aliyepanga kifo hicho sio muuaji?..
Guys Mungu katupa uwezo wa kuchagua kati ya mema na mabaya.. ni uchaguzi wetu sisi wenyewe ktk kila matendo yetu.. na yeye hujalia mema au mabaya kutokana na maombi yetu wenyewe kufanikisha azma zetu..Shetani ambaye ni nafsi za ubaya wa binadamu hutuangamiza sisi wenyewe hakuna mkono wa Mungu ktk mema ama mabaya na ndio maana tutahukumiwa kwa kila tuliyoyafanya(if you believe in judgement day..).Hii ni imani yangu mimi binafsi..
 
Mkuu Waberoya,

Nakushauri upunguze matumizi ya rangi nyekundu katika posts zako; inaumiza macho kwa sisi tunaopenda kusoma word to word and between the lines. Asante!

Asante mkuu nimekupata nimeelewa na nitafanya vingine post zijazo
 
mkandara, niliposema watu waangalie mkono ule wa kushoto wa Deus ulioshika vitu kwangu mimi kilichonigusa ni specifity? Vitu viko mkononi ambavyo kwa hakika alitaka kuwa navyo mkononi. What does that mean?

a. Alikuwa na muda wa kutosha kukusanya vitu vyake
b. Vitu vyake havikuwa mbali naye baada ya ajali
c. Vitu vyake wakati wa ajali havikutawanyika; vilikuwa mfukoni akavitoa baada ya ajali why?
d. Kati ya vitu ambavyo watu hawakumbuki katika ajali ni wallets; vinotebook, n.k ni vitu ambavyo mtu mwingine anaweza kuviokota (ukizingatia ni usiku basi ni lazima mtu mwenye uwezo wa kumulika kutafuta).
e. Deus alikuwa na vitu vyote plus simu za wangwe;

Halafu inaonekana watu wamemiss alichosema Prof. Wangwe which to me tumeshagusia hapa:

a. Kichwa cha marehemu kilipasuka mara mbili; Ina maana kilijibamiza mahali fulani na mahali hapo lazima pawe pagumu kweli. Option nyingine, kupigwa na kitu kizito kinachoweza kufracture fuvu namna hiyo. Tukiangalia gari na kiti cha abiria naweza kusema kwa asilimia mia moja, kichwa hicho hakikuvunjika while Wangwe ameegama kwenye kiti hicho.

b. Amehoji kama ajali hiyo ilikuwa ni ya kupangwa na ya kuwa labda aliuawa sehemu nyingine na kuingizwa kwenye gari na kulazwa kiti cha nyuma (ambako wanakuta damu). Hii ina wezekana sana hasa kama (i) damu nyingi inakutwa kwenye kingo za kiti au karibu na madirisha.

c. Kiwango cha damu kinachokutwa ndani ya gari lazima kiwe consistent na nature of injury. Kama mtu akikatwa shingo, eneo hilo inatarajiwa kuwa na damu nyingi ukilinganisha na mtu aliyejitaka kidole. Hivyo kwa jinsi ambavyo wanasema ajali imetokea bila ya shaka ndani ya gari lile kungekuwa na damu nyingi, siyo tu kwenye eneo moja la kiti lakini hata sehemu nyingine za gari kwa sababu gari is presumed to have overturned several times. Ni sawa na mtu akifungulia chupa ya maji kwenye gari linalobingirika unatarajia kuona maji yamerushwa rushwa kwenye sehemu mbalimbali za gari. So far hata kwa macho ambayo ni untrained huwezi kuona.

I know I said two things...
 
Mwanakijiji,
niliposema watu waangalie mkono ule wa kushoto wa Deus ulioshika vitu kwangu mimi kilichonigusa ni specifity? Vitu viko mkononi ambavyo kwa hakika alitaka kuwa navyo mkononi. What does that mean?

a. Alikuwa na muda wa kutosha kukusanya vitu vyake
b. Vitu vyake havikuwa mbali naye baada ya ajali
c. Vitu vyake wakati wa ajali havikutawanyika; vilikuwa mfukoni akavitoa baada ya ajali why?
d. Kati ya vitu ambavyo watu hawakumbuki katika ajali ni wallets; vinotebook, n.k ni vitu ambavyo mtu mwingine anaweza kuviokota (ukizingatia ni usiku basi ni lazima mtu mwenye uwezo wa kumulika kutafuta).
e. Deus alikuwa na vitu vyote plus simu za wangwe;
Mkuu hii pia sikuiona!...duh kweli maneno yako ilikuwa usiku huyu dogo aliweza vipi kuona na kukusanya vitu hivyo kizani ikiwa kweli gari lilipinduka na kwa maneno yake mwenye ilikuwa vumbi zito (alitoka msafiii)... bila shaka alikuwa navyo sijui mfukoni ama?.. kisha alikuwa amelala kujipumzisha!..ghafla bin vuuu ajali hiyooo, dogo kawahi vilivyo vyake.. ama kweli dogo Comandoo..
 
Mwanakijiji,
Mkuu hii pia sikuiona!...duh kweli ilikuwa usiku huyu dogo aliweza vipi kukusanya vitu hivyo kizani ikiwa kweli gari lilipinduka na kwa maneno yake mwenye ilikuwa vumbi zito... bila shaka alikuwa navyo sijui mfukoni ama?.. kisha alikuwa amelala kujipumzisha!..ghfla bin vuuu ajali, dogo kawahi vilivyo vyake.. ama kweli dogo Comandoo..

Mimi sijawahi kupatwa na ajali (Mungu Epusha) lakini siwezi kuamini kama mtu unaweza kuwemo kwenye gari iliyopata ajali namna ile halafu ukatoka mzima na kuanza kuokota vitu vyako.!!!! Wandugu haya kweli ndiyo yaliyotokea au tunazidi kukuza uvushi. Sababu, iwapo haya ni kweli yalitokea basi naanza kushawishika kuwa Mallya pengine hata hakuwemo ndani ya hilo gari..!!!

Ajali kama ile ukitoka mzima, akili inakuwa na ganzi kwa masaa kadhaa kama sio siku kadhaa.
 
Duh flip and flopping...Anyways...Hapo kwenye amount ya damu kwenye eneo la tukio...This time ikiwa NDANI YA GARI... VS nature ya injury ni swali zuri pia.....Kuna amount ya damu unayoi expect kwenye scene kama hiyo provided majeraha yalikuwa makubwa kiasi hicho....Na pia the fact kuwa marehemu ali bleed to death right on the scene!

Pia kama kichwa kilipasuka ndani ya gari...Je kuna mabaki ya ubongo humo ndani?

Maana kusema kweli gari lilionekana kama staged...Kwani kimtizamo haraka haraka based on the pictures that they have provided us with ...Hatuoni damu nyingi kiasi cha kukubali kuwa huyu mtu alifia ama alipata majeraha yake kutokana na migongano ndani ya gari...Tena ukitilia maanani the fact kwamba mwanakijiji alimkuta akiwa na mkanda..Hivyo vitu vyenye ncha kali vilitoka wapi na wakati hata kioo cha mbele hakijavunjika na marehemu alikuwa amekaa mbele?

Honestly mimi naona kama ni time wasting kwani maswali tunayojiuliza hapa wao washajiuliza na wao si wajinga kiasi hiki...Kwani kuna mambo mengine wao wanayajuwa at the first hand na sisi ku speculate wakati facts hatuna zote ni UPUUZI TU.
 
Yebo Yebo,
iwapo haya ni kweli yalitokea basi naanza kushawishika kuwa Mallya pengine hata hakuwemo ndani ya hilo gari..!!!
..
Hicho ndicho niuolichofikiria hata mimi toka mwanzo wa michango yangu!...Hoja zangu zote zilitaka kuonyesha kuwa huyu kijana pamoja na uongo wote, haonekani kabisa kwamba alikuwa ktk ajali hiyo!.. mashaka yangu ya ajali hii yanaanzia kwa huyu kijana.. statement zake, vitendo vyake vyote vinapingana kabisa na kila suahidi unaotolewa kuhusiana na ajali hii..Na ndiye pekee aliyekuwa na marehemu, sisi wote pamoja na Polisi tunajaribu kuunganisha vitu lakini mwanzo wa kutatua tatizo hili ni lazima tumtazame sana huyu kijana....

Mwaka 1972, nilipata ajali nikitoka Kibara kuelekea Ukerewe sehemu inaitwa Nansimo... unaambiwa bus lilipinduka mimi nilijikuta niko kwa dereva.. Ukiitazama ajali ile huwezi kuamini alitoka mtu lakini kwa rehma zake Mungu sote tulitoka wazima. Nakumbuka mimi niliumia nyongani kidogo na majehara madogo ya mikwaruzo.. bus zima hakuna mtu aliyefunga mkanda hata dereva mwenyewe..wanadamu tulitoka poaaaa, bus nyang'anyang'a!.. halitamaniki.
Lakini pamoja na yote hayo, nilichoweza kukumbuka ni kwamba bus liliyumba kama vile kulikuwa na tetemeko la ardhi...nakumbuka kuna mwanamke alipiga kelele akisema - Mungu wangu weee tunakufa!.. that's it bob, kila kitu kilikuwa blank!..niliona kiza cha ghafla (hali ilikuwa mchana) kwa sekunde chache yaaani sikuwezai kuelezea hata robo ya kilichotokea wakati wa ajali yenyewe. Ni baada ya bus kutulia tu ndipo akili ilirudi na kuona ama kufahamu nilipokuwa.
Kitu cha Kwanza nilipotoka nje ilikuwa kujitazama kama mzima tena ajabu ni kwamba nilikimbia mbali na bus lenyewe nikaanza kujitazama kama mzima bila kuuunganisha kwamba kama niliweza kukimbia bila shaka nilikuwa na uzima fulani. Sikukumbuka hata sanduku langu wala rafiki yangu tuliyekuwa pamoja...Kwa nini nilikimbia mbali na hilo gari mkuu hadi leo sifahamu..Ni baada ya dakika fulani ndipo niliweza kurudi ktk bus hilo, kutazama kilichotokea haswa...
Ajali ya pili nimeipata hukuhuku majuu wakati wa snow, nilikuwa na mshikaji tunatoka mji mmoja,yeye akiendesha.. basi kama sinema vile tuliyumba kushoto akajaribu kulirudisha gari kulia ndio hapo tukavutwa na snow.... chanuu kichwa chini miguu juu..lakini pia the same experience ya kupoteza fahamu kwa sekunde fulani hivi wakati gari lipo ktk motion ya kupinduka. Bahati sote tulikuwa na mikanda..Na tuliulizana kama sote tuko salama baada ya gari kutulia machakani.. lakini hata hapo tulitoka bila vitu vyetu, vilibakia ndani ya gari hadi tulipopata usafiri wa pili...
Lakini huyu dogo mkuu kaonyesha U Komandoo wa nguvu yaani mzoefu sana wa ajali...
 
Mkandara,Yebo Yebo msichanganye mambo..Maana haswa huyo Yebo Yebo naona sijui anafanya makusudi ama ni kwamba haelewi...Yani hapo sijuwi.
Ila tuendelee kujadili issue kama wasomi wa kweli waliosoma wakaelimika.
 
wakubwa habari ndiyo hiyoo!
kila tunalowaza hapa linawezekana kabisa kuwa limefanyika, hii yote ni katika jitihada za kumtoa uhai mh. wangwe ambaye tayari wameshafanikiwa!
Je tunafanya nini kama jambo la msingi la kumkoma nyani giladi?
Nini mpango mahsusi ili tuweze kuweka haya mambo bayana kuwa mhusika ni Rostam Aziz, au Makamba au Mbowe?
Tutajadili hili mpaka lini? Mallya yupo, je kuna maendeleo yeyote toka kwake? Au tuendelee kuchonga tu hapa then keshokutwa tunaambiwa kuwa Mallya kafia Cello dodoma??
Nadhani swala la msingi tukate mzizi wa fitina, tusioneane aibu zaidi tutaumia tena na tena na tutaogopa hata kusema hapa tena!
Wangwe kutoa tamko hili kwa mara ya pili ni sawa kuamua sasa anawapatia uhuru wananchi waamue, ila wao kama familia wanaamini kuwa mh. aliandaliwa kifo! Na hii inaweza kuwa ndo yalikuwa makubaliano na siri kali siku ya uchunguzi wa maiti kwa mara ya pili, kwamba bwana pro. hapa ukisema mh. kapigwa risas utakuwa umewasha moto mubaya nchini, bora utumie diplomasia ili kunusuru balaa!
Sidhani kama hii inahitaji elimu ya M15, cha msingi tutajane tu mhisika ni fulani, na handler wa Mallya ni nani?? La sivyo tusishangae kusikia kuwa Mallya anaumwa kipindu pindu na anakufa baada ya masaa 3!
 
Duh jamani mmeisoma kwa makini hoja aliyoiangusha Mtanzania kutoka ktk magazeti yetu?..jamani mbona kazi ipo.. Sasa nakuombeni someni maelezo ya Baba mtoto, kisha maelezo ya mbunge Kilimba halafu malizia na haya hapa uone jinsi dogo huyu anavyochanganya watu akili...inasema hivi:-

SIKU moja baada ya viongozi watatu kutoka kambi ya upinzani kuibua madai mazito kuhusu Deus Mallya, anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, vijana waliosoma naye Libya wamejitokeza kumtetea.

Steve Mbogo, mmoja wa vijana wanaomfahamu Mallya na aliyewahi kuwa naye nchini Libya, alisema alikuwa na mtuhumiwa huyo nchini Libya kwa mafunzo tofauti, lakini si ya kijasusi.
Mbogo ambaye ni mratibu wa taasisi ya Tanzania Development Initiative (TADIP), alisema madai yaliyotolewa na wenyeviti wa upinzani si ya kweli, kwani yeye na Mallya walikuwa miongoni mwa wawakilishi 20 kutoka Tanzania waliokwenda Tripoli, Libya Juni mwaka jana.
Alisema walikwenda Libya kushiriki mkutano wa kutoa mapendekezo kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, uliokuwa ufanyike nchini Ghana mwaka jana, kujadili ajenda ya kuwa na serikali moja ya Afrika.
Akifafanua zaidi, alisema mkutano huo ulishirikisha nchi mbalimbali za Afrika, mbali na Tanzania, na uliandaliwa na Ubalozi wa Libya kwa kushirikiana na asasi ya Revolutionary Committee Movement (RCM), yenye makao yake makuu nchini Libya.

Alisema wawakilishi wa mkutano huo, walipatikana kwa utaratibu wa kutuma maombi kwa uongozi wa matawi na wakala wa RCM kutoka katika nchi shiriki.
Aliongeza kuwa madai yaliyotolewa na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Augustine Mrema (TLP) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), yanashangaza, kwani mkutano huo wa Libya, ulichukua siku 20, na muda wote huo, walilala chumba kimoja na Mallya, lakini hakuwahi kumwona akitoroka mkutanoni kwenda kupata mafunzo ya ujasusi, kama ilivyodaiwa na wanasiasa hao.
"Haiingii akilini kuwa Mallya alikuwa Libya kwa mafunzo ya ujasusi, kwani mkutano uliotupeleka huko, ulikuwa na wawakilishi wengine 19 kutoka Tanzania, wakiwamo Sheikh Mkuu, Shaaban Simba, Juma Kilimba (Mbunge wa Iramba) na Makongoro Nyerere, watu ambao hawajawahi kutuhumiwa kwa ujasusi," alisema.
Hata hivyo, alipoulizwa iwapo ana uhakika kuwa Mallya hakuwahi kuwa Libya kabla au baada ya mkutano huo, alisema kuwa hajui lolote kuhusu hilo.
Gazeti hili jana liliripoti tamko la wenyeviti wa CUF, NCCR-Mageuzi na TLP, ambao walidai kuwa wana ushahidi wa kutosha kwamba Mallya ni mmoja wa watu waliopata mafunzo makali ya kijasusi nchini Libya, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa, na ni mtaalamu wa hali ya juu wa kompyuta.
Viongozi hao walivitaka vyombo vya usalama kufanya utafiti wa kina juu ya suala hili, ili kubaini ukweli zaidi kuhusu Mallya, kwani inasemekana alikuwa dereva wa Wangwe, lakini wamebaini ni mtu aliyezoeana naye kwa muda mfupi sana, hali ambayo inaibua maswali mengi.
Utata kuhusu Mallya na nini kilitokea hata kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha Wangwe, ulisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimwandikie barua Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Said Mwema, kikitaka kufanyika uchunguzi wa kina.
CHADEMA pia ilimtaka IGP kuchunguza ukweli kuhusu maelezo ya Mallya na kujua ni wapi alikuwa amekaa wakati ajali ikitokea, na kuchukua hatua zinazopaswa, baada ya uchunguzi huo.
Wakuu mimi binafsi nimechokaa na sasa hivi nimechakaaa!.. yaani huyu Steve Mbogo kazidi kunivuruga..
1. Kwanza amedai walikwenda Libya kwa mafunzo mbali mbali lakini sio Ujasusi kisha ktk maelezo yake anasema walikwenda Libya ktk mkutano!... sasa Lipi ni lipi?..
2. Haya tunaona mbunge Kilimba akisema hamjui Mallya na alishangaa walikuwa pamoja ktk msafara huo, meaning hata baada ya mafunzo ama mkutano bado Kilimba hamfahamu Mallya isipokuwa anamkumbukia kiwanjani Zurich! - kuna uwezekano hawakuwa pamoja Libya kama alivyodai Steve Mbongo..
Huwezi kuwa ktk mafunzo ama mkutano na Mtanzania mwenzako kisha ushangae kaingia vipi ama amehusika vipi tofauti na jinsi huyu jamaa anavyotueleza UNLESS huyu Kilimba anaongopa! kama anaongopa WHY?....
Swali langu jingine je hata hao viongozi wetu alowatajwa nao waliomba kushiriki mafunzio/mkutano kupitia hiyo RCM?..Na iweje wawe na Mapendekezo wao kuhusiana na kuunganishwa kwa bara la Afrika!.. I mean huyu Mallya msanii wa fulana, fundi komputa ana CV gani kutoa ushauri juu la kuunda Afrika moja?
3. Katika taarifa inayomhusu Kilimba sasa hivi jina la mtu aliyekuwa kiongozi wa msafara na ambaye alimsaidia Mallya alipokwama Zurich limeondolewa.. nina hakika kuna report ya kwanza somewhere ndani ya hizi mada za wangwe nililiona jina la kiongozi aliyemsaidia Mallya kama kiongozi wa msafara. Imekuwaje habari zote za sasa hivi jina lake limeondolewa?...Nakumbuka Kilimba alisema mtu aliyemsaidia kijana huyu ni blaa blaa blaa, kiongozi wa msafara sio mimi!.. hilo jina limepotelea wapi?
Jamani hamuoni kuna tatizo hapa ama macho yangu mwenyewe!
 
nimejaribu kuanzia siku ya kwanza kuvishawishi vyombo vya nyumbani vya habari kuitisha Scotland Yard wao wameng'ang'ania Polisi wa Tanzania! Hawana nia ya kutafuta ukweli wao wamezama kwenye mchezo na malumbano ya Chadema na CCM na wanapoteza fact kuwa kuna mtu amekufa katika mazingira ya kutatanisha sana.

Kama taasisi na wanasiasa wangeacha kulililia jeshi la Polisi na wangetaka uchunguzu huru karibu wiki nzima iliyopita basi kungekuwa na dalili ya kupata ushahidi wa kweli. Kosa kubwa lilifanywa kama mazingaombwe.

Ili mazingaombwe yafanikiwe hasa yale ambayo mtu anatumia mikono tu, siri kubwa iko kwenye kutengeneza distraction. Ukiweza kuwafanya watu waangalia mkono wa kulia ukiwa unavingirisha kitu, huku wakisikiliza maneno yako mengi na vichekesho vyako vya mbwembwe wanachopoteza kuangalia ni mkono wako wa kushoto ambako mazingaombwe hasa yanafanyika. Ukirudisha mikono yote pamoja? wala njia anapeperuka na watu wanapigwa na mshangao "how did he do it?" wanajiuliza.

Kilipotokea kifo cha Wangwe, kulikuwa na pressure kubwa sana Dodoma. Wenye ujuvi wa mambo walihitaji sana kuondosha pressure Dodoma wakaamua kuihamishia Tarime. Siku ile ya Alhamisi ambayo nidyo ilikuwa siku nzuri kwa watu angalau kutulia na kufuatilia mambo Dodoma, watu (pamoja na TBC) wakajikuta wote wamepelekwa Tarima (Mkono wa kulia). Masikio na macho ya watu (vyombo vya habari) vyote vikawa vimeelekezwa Dodoma.

Na ili kutia chumvi mazingaombwe stori ikaanzishwa kwa njia ya sms kuwa "risasi mbili zimekutwa" na ndio mazingaombwe yakanoga hakuna mtu aliyekuwa anauliza "what was happening in Dodoma). Waandishi, wanasiasa, n.k wote wakawa wamenogewa na mazingaombwe ya Tarime. Wakati wote huo mazingaombwe hasa yalikuwa yanafanyika Dodoma, kwani walihitaji full day kubrief, na kuwekana sawa, n.k

Na siku hiyo ndipo kelele za kilichotokea Tarime ikawa Ijumaa asubuhi na watu wakasahau kabisa mambo ya Dodoma wakawa wametekwa na suala la Mbowe kufukuzwa na marungu na mishale. Meanwhile Dodoma wanamalizia mambo.

Na ilipotokea kuwa WAngwe anazikwa na sasa turudi Dodoma (kuunganisha mikono) mambo waaa! Kijana anafunguliwa mashtaka uchwara na habari zinakuja zinasema familia wamekubali, poleni wafiwa. Ndiyo imetoka hiyo. Hakuna aliyeuliza gari hilo likowapi, limesafishwa vipi, je eneo la ajali lilikuwa secured kwa kiasi gani, mtu yeyote aliyetaka kwenda kutengeneza alama za matairi au kitu chochote to tamper with the evidence alikuwa na zaidi ya masaa 24 kufanya hivyo.

Halafu mwishoni (leo) familia wamekumbuka ajali yenyewe wanarudi na kuwataka Polisi wafanye uchunguzi. Haloo??? Uchunguzi umeshafanyika na jibu ni jepesi, ilikuwa ni ajali mbaya sana iliyotokana na mwendo mkali, na huyu kijana alivyoelezea tumemwelewa kuwa alichanganyikwa na vitu vyake vilikusanywa na mtu asiyemkumbuka n. k n.k na kwa kweli ni msiba mzitoo sana bla bla bla. Kesi closed!

Makofiiii !!!!! mnabakia kujiuliza "how did they do that"?

Mnakaa mnasubiri onesho jingine!!
 
Mkandara miye nilipochoka na stori hiyo ni hapa:

Alisema walikwenda Libya kushiriki mkutano wa kutoa mapendekezo kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, uliokuwa ufanyike nchini Ghana mwaka jana, kujadili ajenda ya kuwa na serikali moja ya Afrika.

sasa nikajiuliza kati ya Watanzania wote ambao wangeweza kujadili suala zito na kubwa kama hili kiasi cha kutoa mapendekezo kwa wakuu wa nchi za Afrika, huyu Bw. Malya alikuwa na qualification gani ya kufanya hivyo? Anazungumza Kiingereza? anajua nini kuhusu historia ya AU, na malengo yake ya baadaye? Nakuambia mtu akimuuliza huyu kijana alienda LIbya kufanya nini atawaeleza kuhusu mkutano tofauti kabisa na huo na ukimuuliza alikuwa huko kwa siku ngapi hatakupa namba kamili!
 
Kijana inaelekea ni VERY SMART ila wamemtumia VIBAYA.
Umoja gani wa AFRIKA UNALETWA KWA NAMNA HIYO YA KUPONEA AJALI TUUU!
Swali langu kwako MKJJ...Hiyo agenda ya kuunganisha Afrika ilikuwa pushed na mataifa gani?
Je Tanzania ilikuwa na msimamo gani kwenye hilo?
Vipi kuhusu nchi nyingine zinazotuzunguka?
Vipi kuhusu nchi wafadhili? Ni zipi zilipinga mpango huo na zipi ziliusapoti? Mpango huo umefikia wapi? Nini VIKWAZO VYAKE?
Na je....Kuna mwingiliano wowote kuhusiana na hiyo hoja ya kuunga Afrika na madini?
Je nini msimamo wa East Afrika Gold Mine ambayo hata marehemu alishawahi kufanya kazi huko na kuacha mara moja na kujiunga na siasa?
Je kampuni hiyo ina uhisiaono wowote na hoja yake aliyokuwa akitaka kuitowa bungeni?
Je hoja ya kuundwa kwa serikali hiyo ya Afrika unafadhiliwa na nani?
 
nimejaribu kuanzia siku ya kwanza kuvishawishi vyombo vya nyumbani vya habari kuitisha Scotland Yard wao wameng'ang'ania Polisi wa Tanzania! Hawana nia ya kutafuta ukweli wao wamezama kwenye mchezo na malumbano ya Chadema na CCM na wanapoteza fact kuwa kuna mtu amekufa katika mazingira ya kutatanisha sana.

Kama taasisi na wanasiasa wangeacha kulililia jeshi la Polisi na wangetaka uchunguzu huru karibu wiki nzima iliyopita basi kungekuwa na dalili ya kupata ushahidi wa kweli. Kosa kubwa lilifanywa kama mazingaombwe.

Ili mazingaombwe yafanikiwe hasa yale ambayo mtu anatumia mikono tu, siri kubwa iko kwenye kutengeneza distraction. Ukiweza kuwafanya watu waangalia mkono wa kulia ukiwa unavingirisha kitu, huku wakisikiliza maneno yako mengi na vichekesho vyako vya mbwembwe wanachopoteza kuangalia ni mkono wako wa kushoto ambako mazingaombwe hasa yanafanyika. Ukirudisha mikono yote pamoja? wala njia anapeperuka na watu wanapigwa na mshangao "how did he do it?" wanajiuliza.

Kilipotokea kifo cha Wangwe, kulikuwa na pressure kubwa sana Dodoma. Wenye ujuvi wa mambo walihitaji sana kuondosha pressure Dodoma wakaamua kuihamishia Tarime. Siku ile ya Alhamisi ambayo nidyo ilikuwa siku nzuri kwa watu angalau kutulia na kufuatilia mambo Dodoma, watu (pamoja na TBC) wakajikuta wote wamepelekwa Tarima (Mkono wa kulia). Masikio na macho ya watu (vyombo vya habari) vyote vikawa vimeelekezwa Dodoma.

Na ili kutia chumvi mazingaombwe stori ikaanzishwa kwa njia ya sms kuwa "risasi mbili zimekutwa" na ndio mazingaombwe yakanoga hakuna mtu aliyekuwa anauliza "what was happening in Dodoma). Waandishi, wanasiasa, n.k wote wakawa wamenogewa na mazingaombwe ya Tarime. Wakati wote huo mazingaombwe hasa yalikuwa yanafanyika Dodoma, kwani walihitaji full day kubrief, na kuwekana sawa, n.k

Na siku hiyo ndipo kelele za kilichotokea Tarime ikawa Ijumaa asubuhi na watu wakasahau kabisa mambo ya Dodoma wakawa wametekwa na suala la Mbowe kufukuzwa na marungu na mishale. Meanwhile Dodoma wanamalizia mambo.

Na ilipotokea kuwa WAngwe anazikwa na sasa turudi Dodoma (kuunganisha mikono) mambo waaa! Kijana anafunguliwa mashtaka uchwara na habari zinakuja zinasema familia wamekubali, poleni wafiwa. Ndiyo imetoka hiyo. Hakuna aliyeuliza gari hilo likowapi, limesafishwa vipi, je eneo la ajali lilikuwa secured kwa kiasi gani, mtu yeyote aliyetaka kwenda kutengeneza alama za matairi au kitu chochote to tamper with the evidence alikuwa na zaidi ya masaa 24 kufanya hivyo.

Halafu mwishoni (leo) familia wamekumbuka ajali yenyewe wanarudi na kuwataka Polisi wafanye uchunguzi. Haloo??? Uchunguzi umeshafanyika na jibu ni jepesi, ilikuwa ni ajali mbaya sana iliyotokana na mwendo mkali, na huyu kijana alivyoelezea tumemwelewa kuwa alichanganyikwa na vitu vyake vilikusanywa na mtu asiyemkumbuka n. k n.k na kwa kweli ni msiba mzitoo sana bla bla bla. Kesi closed!

Makofiiii !!!!! mnabakia kujiuliza "how did they do that"?

Mnakaa mnasubiri onesho jingine!!

Nilisema hapo nyuma kwenye thread nyingine kuwa huyu mwanakijiji aliyekuwa wa kwanza kufika kwenye ajali alitibua kwa kiasi mtiririko wa ambacho sasa kinaenekana kama filamu ya Hollowood.

Naamini (by reasoning yangu) kuwa waliohusika kwenye tukio zima ni zaidi ya wawili na magari involved ni zaidi ya moja. Kupondeka kwa gari alikokutwa marehemu ilikuwa staged na hili gari lilikuwa liangamizwe kabisa baada ya ushahidi wowote ule kutolewa/kuchukuliwa.

Getaway car lililotorosha mhusika/wahusika mwingine/wengine haliongelewi kabisa kwa kuwa macho yote yalielekezwa Tarime. Huyu Malya anaonekana kama mtu aliyekuwa tayari kuingia mitini kama siyo kuwahi huo usafiri mwingine.

Sasa tusubiri na mengine, MAFISADI wameunda mtandao wa kiMAFIA na wengi wa viongozi wetu ni mateka, duh...........Ni analysis yangu tu.
 
Swali jingine pia ni hili...Ni watu wangapi zaidi ya Spika waliojuwa kuwa keshakabidhi hoja?
Maana nafikiri alimwuliza makamu spika na makamu spika akamwambia amsubiri spika six ili aweze kuikabidhi hoja yake hiyo...Sasa sijui sana kuhusu taratibu za hapo bungeni..Je kuna uwezekano wa kuvujishwa kwa habari ya yeye kumkabidhi spika hoja yake ama lilikuwa ni jambo la wazi lenye kujulikana na kila mbunge kuwa imeshakabidhiwa?
Je habari kwamba hoja imeshakabidhiwa ilitoka kabla ya kifo ama baada ya kifo?
 
Kazi lazima uwe nayo...Umesahau kifo cha Ballali?

Kweli unasahau mapema sana....Sasa mwajemi ni nani na shia ni nani...Unataka kufikiri mimi sijuwi Historia ya dunia...MKJJ....Hapa imelala!

Niambie kuhusu factions zote nitakupa the truth...Kwani hata Bush na wengineo walikuwa very WRONG...Na ndio maana dunia iko hapa ilipo!

Shida ni kwamba MUIRAN ana NGUVU KUBWA SANA NA SAPOTI YA MCHINA NA MRUSSIA IKO JUU.

Na kutokana na hilo...RA anapata nafasi ya kumbana JK...Kwani ni kweli WEST WASIPOKUWA MAKINI...WANAKWENDA CHINI.

Ila haina maana kuwa tuchaguwe mabwana pale inapokuja kwenye haki ya wananchi wa kawaida...HIYO NI LAZIMA ILINDWE....AMANI NI LAZIMA ILINDWE BY ANY MEANS AND COSTS!

Sasa kama RA asipoachana na siasa halafu nikasikia kuna mtu kafa tena huko kwasababu yake...Ama nikasikia kuwa ukabila na udini ume prevail kama anavyotaka kutugawa....UNAFIKIRI ETI NITAKAA TU?!

THUBUTU...NA MIMI NAMWAMBIA KABISA HUYO ROSTAM AZIZ KUWA....KAMA TONE JINGINE LIKIMWAGIKA KWASABABU YA MALIPIZANO YA TIT FOR TAT..AMA HATA PROPAGANDA HIZI ZIKIENDELEZWA NA MAGAZETI YAKE...Basi na mimi ni MJESHI WA TAIFA LANGU....NA I SWEAR TO GOD...NITALILINDA MPAKA KUFA!

Iran ananguvu sana? Just kwasababu ana support ya Russia na China?....... Basi pia Zimbabwe ananguvu sana maana pia ana support ya Russia na China.....Halafu whats the point of West going down?.... Dont you think they deserve so! They have been selfish and all what they think about ni wao wenyewe!....... Lakini hii siyo maada husika hapa!!

All what you saying, I wish you had evidence. It seems u and the guy, RA..... yaani ni personal hater!
Bring proofs.
 
Bring proof
 
usalama wa taifa uko wapi wakati nchi mmemkabidhi rostam aziz? yeye ndo usalma wa taifa, anaunda argument zake feki na kuweka kwenye magazeti eti vita izuke aonekane shujaa.

si mlishaandika hapa kuwa marehemu wangwe alikuwa anapeleka siri kwa za chadema kwa rostam? kwa nini isiwe hivi: baada ya rostam kuona kuwa siri anazopewa na wangwe hazina nguvu, akasuka dili la kumuua wangwe ili chedema waonekane wauaji?, nakwa kuwa rostam ni ponjoro mwenye shule wasiwasi akaamua kuwatumia akina balile na vikaragosi wengine

Proof please!....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom