Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mushi,
Hili la uarabu wa mke wa marehemu kulihusisha na uarabu wa mume aliyeachana naye sidhani kama ni issue. Binafsi nashindwa kuamini kuwa huyu Mariam alikuwa hafahamiani na huyu Malya. Mariam ndiye mke aliyekuwa karibu na marehemu, na kwa mujibu wa kijana mkubwa wa marehemu kuwa Malya alikuwa akifanya kazi fulani na marehemu, bila shaka Mariam anaifahamu hiyo kazi waliyokuwa wakiifanya kwa ubia. Huyu mama anafahamu mengi sana tatizo ni kuwa, akitakiwa kueleza yote anayoyafahamu atakuwa tayari? Naanza kuhofia usalama wake.

Na ndio maana nikasema inaweza kuhamia kwenye Uislam na ukristo...Na pia nilitowa msisitizo kuwa Deus Mallya sijui ni kivipi alikubaliwa na mke wa KATI.
Na ni nani alimuunganishia marehemu na mke huyo mwarabu?
Maana mh Rais na yeye si ana mke mwarabu?
Ndugu zangu USALAMA WA TAIFA HAUPO TENA...Na ninasema kuwa kama hakuna wazalendo wa kweli ambao hawataki kuliingilia hili swala kati...Basi kuna shida!
Ni wazi usalama umegawanyika kama nilivyosema awali na inawezekana group baya la wanausalama mafisadi limemtumia agent wao ili kufifisha juhudi za wale wanausalama safi.

Shida iko hapo....TUNAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA SANA KWENYE USALAMA WETU WA TAIFA!
Hii si njia sahihi kabisa....Mwiran,mchina na mrusi vs m west....Kazi iko!

Watakaolikomboa Taifa ni TRUE BANTU...WAKISHIRIKIANA NA WALE WENYE NIA NZURI BILA KUJALI RANGI ZAO WALA DINI ZAO!

Rastafarianism nayo naona itapata UMAARUFU SANA...Kwani wao hawataki kugawanya na mwarabu wala mzungu!
 
duh.. nina kazi!

Kazi lazima uwe nayo...Umesahau kifo cha Ballali?

Kweli unasahau mapema sana....Sasa mwajemi ni nani na shia ni nani...Unataka kufikiri mimi sijuwi Historia ya dunia...MKJJ....Hapa imelala!

Niambie kuhusu factions zote nitakupa the truth...Kwani hata Bush na wengineo walikuwa very WRONG...Na ndio maana dunia iko hapa ilipo!

Shida ni kwamba MUIRAN ana NGUVU KUBWA SANA NA SAPOTI YA MCHINA NA MRUSSIA IKO JUU.

Na kutokana na hilo...RA anapata nafasi ya kumbana JK...Kwani ni kweli WEST WASIPOKUWA MAKINI...WANAKWENDA CHINI.

Ila haina maana kuwa tuchaguwe mabwana pale inapokuja kwenye haki ya wananchi wa kawaida...HIYO NI LAZIMA ILINDWE....AMANI NI LAZIMA ILINDWE BY ANY MEANS AND COSTS!

Sasa kama RA asipoachana na siasa halafu nikasikia kuna mtu kafa tena huko kwasababu yake...Ama nikasikia kuwa ukabila na udini ume prevail kama anavyotaka kutugawa....UNAFIKIRI ETI NITAKAA TU?!

THUBUTU...NA MIMI NAMWAMBIA KABISA HUYO ROSTAM AZIZ KUWA....KAMA TONE JINGINE LIKIMWAGIKA KWASABABU YA MALIPIZANO YA TIT FOR TAT..AMA HATA PROPAGANDA HIZI ZIKIENDELEZWA NA MAGAZETI YAKE...Basi na mimi ni MJESHI WA TAIFA LANGU....NA I SWEAR TO GOD...NITALILINDA MPAKA KUFA!
 
kwa nini uchanganye kabila zima kwa ajili ya kasoro ya mtu mmoja? kama damu itamwagika nchi hii kwa ajili ya vita ya kikabila, basi mwanzilishi na mfadhili wa hii vita ni rostam azizi kupitia magazeti yake ya new habari corporation, na fedha za wizi alizoiba. pia kupitia vikaragosi kama wewe na akina balile

MKUU Mwikimbi,

I salute you! Umenena maneno mazito sana mkuu.Chukua zako tano.Kwa kweli Gembe kachemsha kukubali kuwa part of ethnic comflict huku akijdai kuwa bonge la msomi na kukandia wengine hadi anafikia hatua ya kum-quote mtu bila kujua hata historia ya mtu mwenyewe.

Leo hii likimwagika hata tone moja la damu hapa nchini kwa sababu ya watu wenye tamaa za fisi kama akina RA akishirikiana na WASALITI wakubwa wa Taifa letu basi yatakayowapata wao na familia zao ni bora yasisemwe hapa maanke hawatakua salama hata kidogo.Ni kwa nini watu wakubali kueneza chuki against ndugu zao just because of cheap gains?

Leo hii Chama Tawala pia kimedhihirisha kuwa na maslahi makubwa na Kifo cha Mhe.Chacha Wangwe na ikiwezekana na hata yale yaliyotokea tarime kwa kuanza kujianika hadharani wao wenyewe na mkakakti wao ambao kimsingi inawezekana ni kujipongeza kisiri kwa kufanikisha mkakati wao.

Haina logic yoyote wao waamue kusambaza waraka ule halafu wakane kujihusisha na mgogoro wa Chadema,kwani kama Mbowe anatuhumiwa kwa kuhusika na yaliyompata Wange,Basi Chanzo kikuuu cha mgogoro wao NI CCM.Wanastahili kubeba lawama zote kwani,kama kweli walikua na nia ya Dhati na Chadema au na Demokrasia ya taifa letu,basi wasingejiingiza ndani kuuubomoa au kuleta mafarakano ndani ya opposition camp.Ndio maana nikasema CHADEMA nao waache sasa kucheza fair Game maanake the opponents are still playing unfairly
 
usalama wa taifa uko wapi wakati nchi mmemkabidhi rostam aziz? yeye ndo usalma wa taifa, anaunda argument zake feki na kuweka kwenye magazeti eti vita izuke aonekane shujaa.

si mlishaandika hapa kuwa marehemu wangwe alikuwa anapeleka siri kwa za chadema kwa rostam? kwa nini isiwe hivi: baada ya rostam kuona kuwa siri anazopewa na wangwe hazina nguvu, akasuka dili la kumuua wangwe ili chedema waonekane wauaji?, nakwa kuwa rostam ni ponjoro mwenye shule wasiwasi akaamua kuwatumia akina balile na vikaragosi wengine
 
usalama wa taifa uko wapi wakati nchi mmemkabidhi rostam aziz? yeye ndo usalma wa taifa, anaunda argument zake feki na kuweka kwenye magazeti eti vita izuke aonekane shujaa.

si mlishaandika hapa kuwa marehemu wangwe alikuwa anapeleka siri kwa za chadema kwa rostam? kwa nini isiwe hivi: baada ya rostam kuona kuwa siri anazopewa na wangwe hazina nguvu, akasuka dili la kumuua wangwe ili chedema waonekane wauaji?, nakwa kuwa rostam ni ponjoro mwenye shule wasiwasi akaamua kuwatumia akina balile na vikaragosi wengine
 
Mengine yote nakubaliana na wewe 100%, lakini nililo-bold hapo juu!!! nasita kusema kumbe tayari mnafanya vizuri sana... kumbe tuna makengeza wengine... mimi nilidhani ndio munahitaji kusimama imara kumbe already ndio muko imara...

Oooh... maskini nchi yangu.

Kwani umeona mapungufu gani yaliyotokana na weakness za ndani? Wao kama opposition wanatekeleza wajibu wao hadi wanafikia hatua ya kutangaza mafisadi hadharani lakini hii serikali ILIYOSHINDWA haichukui hatua zozote.

Serikali yako ndiyo inasababisha hayo yanayokupigisha butwaa au huoni?
 
Mimi nafikiri tumechanganya mambo mengi kwa sababu wengi wetu tumechangua upande. Ukitaka kuwa objective utagundua mambo haya:

  1. Ni wazi kwamba kulikuwa na tafrani kwenye msiba kutokana na ukweli kwamba kifo cha marehemu kilikuwa na utata mwingi. Ningeshangaa sana mimi kama msiba huu ungekuwa wa amani kama misiba mingine.
  2. Hata hivyo, kwa sababu za kisiasa, tafrani zilizotokea zimekuzwa ili kuonyesha kwamba kulikuwa na fujo, na fujo hizi zilielekezwa kwa chadema.
  3. Kwa sasa kuna kila dalili kwamba CCM watatumia msiba huu kama njia ya kutokea, maana kwa kweli wamebanwa sana.
  4. Sababu za chadema kunyoshewa kidole katika msiba huu zinaeleweka na zinapaswa kutarajiwa: i) ndio chama kinachotishia uhai wa CCM kwa sasa, ii) mbunge aliyefariki alikuwa ni mbunge wa chadema na hivyo wapinzani wa chadema wangependa kutumia msiba huu kuhakikisha kwamba chadema haichaguliwi tena huko Tarime iii) marehemu alikuwa na mgogoro na viongozi wake, na kwa kiasi kikubwa alijaribu kuonyesha kwamba mgogoro huu ulikuwa kati yake na Mwenyekiti wa chadema.
  5. Kwa maoni yangu, maelezo ya Zitto kwamba hapakuwa na fujo huko Tarime yalilenga zaidi kukanusha madai kwamba hasira za wananchi zilielekezwa kwa Mwenyekiti Mbowe, na kwamba hapakuwa na mapanga wala mishale. Pengine alichokosea Zitto ni kukanusha madai ya fujo kwa jumla jumla. Angeweza kukiri kwamba, yes, kulikuwa na aina fulani ya tafrani au fujo lakini sio kweli kwamba fujo hizi zilielekezwa kwa mwenyekiti Mbowe, na wala sio kweli kwamba fujo hizi zilifikia kiwango cha wananchi kubeba mapanga, mishale kama ilivyoripotiwa. Nafikiri ile kamati ya wahariri itaweza kufafanua hili vizuri. Nahisi kwamba kamati itakiri kuwepo kwa aina fulani ya fujo, ambayo inaeleweka kutokana na mazingira ya kifo na umaarufu wenyewe wa marehemu. Lakini nahisi pia kwamba kamati itakanusha madai ya kufanyiwa fujo kwa Mweneyikiti Mbowe, na wala wananchi kubeba mapanga na mishale.

Ni wazi kwamba CHADEMA tumetikiswa. Ama tutaanguka au la, itategemea tutakavyo-handle matukio baada ya msiba huu. Kwa maoni yangu njia pekee ya kusimama ni kuwa wa kweli, na inabidi tuwe wa kweli katika mambo makubwa manne yafuatayo:

(a) Tukiri kwamba, yes, kulikuwa na mgogoro kati ya marehemu na viongozi wenzake katika chama. Baada ya uchunguzi uliofanyika, Kamati Kuu ya CHADEMA iliona kwamba marehemu alikuwa amekiuka baadhi ya kanuni za chama ,na hivyo ikaona ni vyema kumsimamisha uongozi

(b) Tukiri kwamba, yes, baada ya kusimamishwa, marehemu hakuridhika na maamuzi yale, na alikuwa akifanya utaratibu wa kukata rufaa katika vikao vya chama, na hata mahakamani

(c) Tukiri kwamba, yes, baada ya msiba huu, wapinzani wetu, na hasa CCM, wamekuwa wakijaribu kuhusisha kifo cha marehemu na mgogoro huu ili ionekane kwamba kifo cha marehemu kimetokana na mgogoro huu.

(d) Tukemee njia chafu wanazotumia CCM kujaribu kufifisha nguvu za upinzani na kujipatia umaarufu kupitia kifo cha marehemu. Tuweke wazi kwamba huu ni ushetani, na sio jadi ya watanzania kutumia msiba wa mwenzako katika kujipatia umaarufu. Na wala sio jadi ya watanzania kujaribu kumjeruhi ng'ombe aliyekwishajeruhiwa. Katika hali ya kawaida ya utanzania wetu, ilitarajiwa kwamba CCM wangekuwa wanawapa CHADEMA pole na rubani kwa kufiwa na mwanachama, kiongozi na mbunge wa chama chao. Badala yake hawa wenzetu wapo busy kujaribu kutumia msiba huu kujinufaisha kisiasa. Kwa maoni yangu tukijenga hoja hii vizuri kwa wananchi, ndio itakuwa mwisho wa ghiliba za CCM kuendelea kutumia msiba huu kama njia ya kutokea. Hili jambo halihitaji danadana.


I like Mwl Kitila
yote uliyosema ni sahihi kabisa ,lakini aliyebugi step mimi naona ni Ndg yangu Mnyika.
Manyika ndio alibugi step kwa miono yangu ,Ile kuandika barua kwamba Ajali ichunguzwe hapo ktk hali ya ubinadamu tayari alikua anwatuhumu CCM,sasa Mnyika yeye alikua amebeba SMG wataalamu wakasitukia dili wakaibuka na ma B52.

hilo swala la uchunguzi mimi nahisi ilikua ni familia kutoa tamko na si chama,maana tamko la Mnyika lilikua limebeba zana kuu mbili.
1.CCM wamehusika ktk kifo hicho AMA
2,CHADEMA wamehusika ktk kifo hicho ila wanataka kujiwekea kinga mapema.
 
Kwani waarabu na waajemi si wasilam?
Ama wakisema wakristo humaanisha ni wazungu tu?

Mushi bwana saa nyingine mambo yako ya ajabu sana! Sio kila mwarabu ni muislamu, waajemi si waarabu, sio kila muajemu ni muislamu....kuna waarabu wengi tu ambao ni wakristo hasa Lebanon, Egpty, Palestine na sehemu za Syria!! Pia waajemi kuna kundi la kutosha wana dini yao inaitwa Bah'ai. Anywayz hiyo ni issue nyingine kwa wakti mwine....tatizo langu kule juu sehemu nimeona una-introduce udini ktk sakata hili!! ati, "wakristo v/s waslam."!! kwanini? kwanini Mushi? Ushindwe na ulegee.

bado ni rafiki yangu, though..

eazy.
 
Myika alichemsha kama kawa...Kama alivyomwita Sina MSALITI...Ndivyo hivyo hivyo alijitayarisha kusema Deus ni msaliti...Kwasababu Deus sijui atakuwa kamsaliti nani...Kwani yuko chadema na ccm kama ilivyokuwa kwa marehemu Wangwe.
Yeye baada ya kuona TBC1 wamei politisize issue na yeye aka jump kwenye bandwagon ya Tit for Tat...
Alchotakiwa kusema ni siasa zisihusishwe na kama ukweli ukitakiwa ni uchunguzi ufanyike.
Sasa kwasababu kuna wana chadema waliokuwa wakifurahia issue ya ukabila na kuifumbia macho ama kuipalilia kwa kumfukuza wangwe...Then sioni ajabu wakiendelea na trend ile ile..Kwani bado kuna chadema wenye uhusiano na ccm...Tena chadema viongozi wakubwa kama marehemu mwenyewe...Hivyo na wao wawe makini.
TAIFA KWELI LIKO HATARINI.
 
Oooh... maskini Kasheshe
Mimi nakuonea huruma maana mambo naona yanakupita kushoto. Udhaniavyo sivyo. Mbowe ndiye kiboko ya sisisemu sasa na mikakati ya sisiemu inajulikana dhahiri.
Binafsi sintaamini propaganda kuhusu upinzani maana nazo propaganda ni upinzani
 
Mushi bwana saa nyingine mambo yako ya ajabu sana! Sio kila mwarabu ni muislamu, waajemi si waarabu, sio kila muajemu ni muislamu....kuna waarabu wengi tu ambao ni wakristo hasa Lebanon, Egpty, Palestine na sehemu za Syria!! Pia waajemi kuna kundi la kutosha wana dini yao inaitwa Bah'ai. Anywayz hiyo ni issue nyingie..tatizo langu kule juu sehemu nimeona una-introduce udini ktk sakata hili!! Ushindwe na ulegee.

bado ni rafiki yangu, though..

eazy.

Mkuu tuko kwenye defining moment hapa duniani.
Mmarekani alifanikiwa kuwagawa washia na wa suni...Sasa kama wakirudi pamoja in the name of uislam na wakisaidiwa na mrusi na mchina si ni HATARI HII?

Ok...Naona umesahahu kuwa agenda hapa ama toka mwanzo ilikuwa kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini ama ukabila...UMESHASAHAU YA Mtikila na Kwaya ya Kinondoni.

Naomba sana mnisamehe kama RA si muislam basi naomba msamaha RASMI kwa kumuhusisha na uislam...Kwani mimi siamini kabisa UBAGUZI...NA mimi binafsi nakiri wazi kuwa wenye msimamo mkali...Either walokole ama wasilam...Hawa watu wajiangalie sana..Kwani dunia hii ni ya kuishi pamoja....Na pia tusisahahu kuwa too much of anything is harmfull.

Ila BANTU...Kaeni makini naona hamjafuatilia historia yetu ya Afrika!
Sisi sote ni ndugu kabla hata mwarabu hajaja kutukamata na kutuuza kwa Mzungu!
 
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza kwenye mjadala huu, na haswa baada ya Kiranja kuweka post zake ,naona kuna baadhi ya watu wameloose control mpaka inafika mahali wanajitambulisha kuwa wao sio A bali ni B wakati siku zote walikuwa wanajionyesha kama ni Neutral.

Heri walio upande fulani na maandishi yao yanasema hivyo kuliko walio upande fulani halafu wanaona aibu kutetea misimamo yao, naamini kuwa baada ya siku zinavyokwenda patachorwa mstari na nani ni nani kujulikana ama kwa matendo au kwa maandishi yake.

Huo mstari nani atauchora?? Hakuna atakaye chora mstari huo kwa kizazi hiki cha nyoka .Labda Mbiguni tu.

Kizazi hiki cha faa kuangamizwa kabisa maana chote ni cha kinafiki na kikifuata sera za yule MWOVU.
Mwanasiasa aliyevaa hilizi kiuononi ama kua na kababu akiamini ndio mlinzi wake ama vibuyu ktk kona ya nyumba zake AMINI NA KUAMBIA KAMWE hatachora mstari wa haki BALI atachora mstari wa dhuluma ,unyanganyi,UONGO,WIVU,UZINIFU,UUWAJI,UTAPELI,UFITINISHI.
 
Huo mstari nani atauchora?? Hakuna atakaye chora mstari huo kwa kizazi hiki cha nyoka .Labda Mbiguni tu.

Kizazi hiki cha faa kuangamizwa kabisa maana chote ni cha kinafiki na kikifuata sera za yule MWOVU.
Mwanasia aliyevaa hilizi kiuononi ama kua na kababu akiamini ndio mlinzi wake ama vibuyu ktk kona ya nyumba zake AMINI NA KUAMBIA KAMWE hatachora mstari wa haki BALI atachora mstari wa dhuluma ,unyanganyi,UONGO,WIVU,UZINIFU,UUWAJI,UTAPELI,UFITINISHI.

MKAMAP inakuwaje leo tunakubaliana...Ama kweli this issue ni very serious...Lakini i am OPIMISTIC.
 
Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kujitokeza wazi kusambaza waraka wa Chadema, ikiacha maswali kama ilipewa waraka huo na Wangwe au ndiyo ilikuwa ikishirikiana naye katika kuendesha harakati zake ndani ya chama hicho cha upinzani.
Hapa tayari kuna jibu kuwa yawezekana marehemu alikuwa na kadi mbili. Ya Chadema na ya sisiemu.
Na ndiyo sababu hata wao sisiemu wamepata pigo. Kwanai hujashangaa kwamba hata wana sisiemu walifurika katika msiba huu kana vile aliyekufa ni mbunge wa ccm?
Mungu amemuumbua mnafiki!
 
Alipofariki Wangwe nilichangia katika thread iliyohusu kifo chake kwa kuandika misitari miwili tu, na baada ya hapo sikuchangia tena kwa sababu my gut feeling was telling me that the man was assassinated!

Mistari miwili pekee niliyochangia katika kifo cha Marehemu Wangwe ni hii hapa na baada ya hapo nilifumba mdomo wangu:

1. RIP Wangwe.

2. Police should thoroughly investigate the cause of the eccident.

Kutokana na hali inavyoendelea, ambapo sisiem na chadema wanaonekana kutoa kauli mbalimbali za ama kuchafuana au kujisafisha, ninalazimika kusema kitu kimoja tu nacho ni kwamba: kama ni kweli kwamba kifo cha wangwe kina mkono wa mtu basi huo mkono lazima uwe umetoka ama csiemu au chademo. Na ndomaana wanatumia muda mwingi kujisafisha na kuchafuana.

Nataka nimalizie kwa kusema hivi: Kujisafisha au kuchafuana kunakoendelea, kuhusiana na kifo cha Wangwe ni kazi bure! Kwani it is just the matter of time before tanzanians can know what real is behind Wangwe's death or assassination if proved! Kila kitu kitakuwa wazi. Tusubili muda, ukifika either csiemu or chadema wataumbuka. Believe me they won't get away with it! Hakika Mungu atawaumbua!

RIP Wangwe.

Kunguru maneno haya ni MAZITO...Ila usisahau kuwa UKABILA NA CHUKI DHIDI YA KABILA JINGINE...Chuki ya namna moja ama nyingine inaweza kutupeleka pabaya!
Kila kabila lina watu wasio wazuri bila kujali tofauti za kabila hizo...Kuna watu prejudice na watu wazalendo...WABANTU HALISI WALIOPATA ELIMU YA UASILIA WAO WA AFRIKA!
Ambao hawana mabwana waarabu wala wazungu...Bali wenye kujali UTU,UBINADAMU NA HESHMA YA MWAFRIKA..WENYE KUJALI MAENDELEO YA BINADAMU KWA KUSHIRIKIANA NA BINADAMU WENZAKE BILA KUJALI UTOFAUTI WA RANGI,DINI WALA KABILA....HAO NI "THE CITIZENS OF THE WORLD!"
 
Tunaomba pia tuwekewe na taarifa walizozitowa siku daktari wao alipofanya upasuaji na familia pamoja na mwakilishi wa chadema kutowa kauli kuwa ilikuwa ni ajali na hakuna risasi...Hizi ni siasa ama serious issue?

Nini kinawafanya watu wanabadili mawazo haraka haraka hivyo wakati marehemu keshazikwa kama si siasa hizi?

Ama amebadilishwa mawazo na forum hii?

Je wanataka uchunguzi HURU WA NJE? Maana si waliridhika walipoambiwa kuwa daktari wa nje hawezi kuruhusiwa?

Maana hata mimi nilishangazwa sana na kuridhika kwa familia hiyo juu a mazingira yote a kifo hicho.

Kaazi kweli kweli....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom