Pamoja na Prof Wangwe kusema wana wasiwasi na kifo cha marehemu kuna mambo nafikiria kiundani zaidi.
Prof Wangwe kuna uwezekano mkubwa ni CCM hata kama hajajitangaza wazi, hivyo basi kuna uwezekano baada ya YEYE mwenyewe kuwa msemaji wa familia na kukubali uchunguzi.Bado wameona kuna rumors nyingi ambazo wameshindwa kuzihandle na kila mpira unaangukia eneo la penati kwenye goli la CCM.ukianzia vyombo vya habari vilivyoripoti , na taarifa tatanishi za Deus Mallya.Ili kuzima na ionekane hata familia bado na wako against na hili basi nikusema kuwa wana wasiwasi, AMESEMA WANA WASIWASI LAKINI HAJASEMA WATAFANYA NINI! badala yake anataka watu wasiseme lolote mpaka polisi watakavyofanya uchunguzi.Uchunguzi upi huo? Deus amesema nini mpaka leo? mara ya kwanza kabla ya maziko akina nani walifanya uchunguzi wa maiti?.Hivi Prof siyo anatuzunguka kuna uwezekano kabisa marehemu aliuawa na mwili ulivyochunguzwa ulionyesha hivyo ila kwa sababu za kiusalama waliambiwa wasiseme lolote.
Haya leo mwili umezikwa endapo hao wataalamu watataka mwili ufanyiwe uchunguzi watafanyaje? maana uchunguzi yakinifu ni pamoja na kuona mwili may be!
Prof Wangwe anataka tuaminishe kuwa polisi wa Tanzania wanauwezo mkubwa? labda, lakini wakipata ukweli watautoa bila kificho pasipo kuuliza kwa mkuu wa taifa hili? na je kama taarifa mbaya itatoka?
Kama kwa level ya profesa unawaza hivi !!! naogopa! na kuwaambia watu wasispeculate unataka nini? Kama kweli amefikia kusema hivi bila hali yoyote basi ameweza tu kwa sababu za hisia ambazo hataki!!!
hakuna kitu chenye demokrasia kama mawazo ya mwanadamu anaweza akawaza lolote lile, hata asipolisema, wachache tunaweza waza na kusema kama kilivyo.Prof Wangwe hii yote siyo janja ya nyani? yaani wewe na wanafamilia wenzako mfikie kusema hivyo pasi kutoa suluhisho au kusema wachunguzi watoke nje ya nchi?
kama ni hivyo nashawishika kusema kuwa kuna swala limejificha nyuma ya kifo cha Wangwe si muda kila kitu kitafunuliwa.
Waberoya