Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mambo ya kijana mallya, eti baba yake hajui Libya alienda kufanya nini, hajui kwamba mtoto wake kasoma Nairobi kama anavyo dai mallya. Kazi ipo.

Date::8/4/2008
Babake mzazi wa Mallya azidi kuchanganya mambo
Francis Matey Mallya, baba mzazi wa Deus Mallya akiwa katika ofisi za Mwananchi, mjini Moshi kumtetea mwanae jana.
Na Daniel Mjema, Moshi

BABA mzazi wa kijana aliyekuwa na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe (Chadema) kwenye gari lililosababisha kifo chake, amezidi kuchanganya mambo baada ya kueleza kwamba, mwanaye hakuwahi kusoma sekondari Nairobi, nchini Kenya, kama mwanaye huyo alivyodai.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili mjini hapa jana, Francis Matey Mallya, ambaye ni baba mzazi wa Deus Mallya, alisema mwanaye hakuwahi kabisa kujiunga na shule yoyote ya sekondari ndani au nje ya nchi kwa vile hakuwa na uwezo wa kumsomesha masomo hayo.

Kijana huyo (27), ambaye ameshitakiwa kwa tuhuma za kuendesha gari bila leseni na kwa mwendo kasi uliosababisha kifo cha Wangwe, wiki iliyopita, alikaririwa na gazeti hili akidai kwamba, ana fani ya usanifu aliyoipata Nairobi katika Chuo cha Mtakatifu Hubert baada ya kumaliza sekondari kidato cha nne.

Hata hivyo, katika maelezo yake aliyoyatoa jana, Francis alisema anakumbuka kwamba, mwanaye alizaliwa mwaka 1983 katika Kijiji cha Kichare na kubatizwa kisha kusoma shule ya msingi Umbwe hadi darasa la saba.

"Kwa sababu mimi sikuwa na uwezo wa kumpeleka sekondari aliendelea kujisomea akawa ananunua vitabu vya kujisomea, lakini baadae akaondoka kwenda Dar es Salaam alikojifunza kozi ya kompyuta," alisema Francis.

Francis alisema mwanaye alipita tu Nairobi alipokuwa akirejea kutoka nchini Libya, ambako hadi sasa hafahamu hasa shughuli iliyompeleka huko (Libya).

Mzee huyo, alisema aliporejea kutoka Libya, alishukia Nairobi ambako alikutana na rafiki yake waliorejea wote jijini Dar es Salaam.

Alisema anachofahamu ni kwamba kulikuwa na mtu ambaye hamfahamu, ambaye alikuwa akiwasiliana na mwanae kwa ajili ya kwenda Libya na alipokwenda hakufikisha wiki alirejea nchini.

Francis alisema mwanae aliweza kumudu vyema mafunzo ya kompyuta baada ya kupata mtu wa kumfundisha na baada ya kumudu mafunzo hayo alijishughulisha na kazi ya kutengeneza fulana, ambayo anaendelea kuifanya hadi sasa.

Alishutumu mwelekeo unaoanza kujitokeza wa kutaka kuhalalisha kuhusika kwa mwanae na kifo cha Wangwe.

"Kumuita mtoto wangu ni jasusi bila kumpa nafasi ya kumsikiliza wala vyombo vya dola havijathibitisha hilo ni kumhukumu, jambo ambalo ni kinyume cha katiba…wanamhukumu vipi kwa hisia?," alihoji Francis.

Alidai kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ya kumuita mwanae ni jasusi, ina lengo la kuushawishi umma uamini mwanae anahusika na kifo cha Wangwe.

Francis ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Kichare katika kijiji cha Umbwe Sinde alisisitiza kilichotokea ni ajali kama ajali nyingine na suala hilo sasa liachiwe mahakama ambayo itachambua ushahidi na kujua lipi la kweli na lipi halina ukweli.

"Kwa muelekeo huu ninaouona, naomba taasisi zinazotoa msaada wa kisheria zisaidie kulinda haki ya mwanangu, ambaye tangu akamatwe hatuna mawasiliano naye na ndugu wamezuiwa kuonana naye," alidai.

Akielezea tabia ya mwanae, alisema anamfahamu vyema na kwamba hajawahi kushika bunduki wala kisu achilia mbali kutembea na wahuni, bali alikuwa akifuata maadili mema ya Kanisa Katoliki.

Alisema anamfahamu mwanae kama mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchapisha maandishi na picha kwenye fulana na kazi hiyo ndio ambayo amekuwa akiifanya kwa ajili ya shule, makanisa na vyama vya siasa.

Alifafanua kuwa mara tu baada ya ajali, mwanae alimpigia simu akimuarifu kuwa alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam akiwa na mbunge mmoja, lakini kwa bahati mbaya gari imepata ajali na mbunge amefariki dunia.

"Aliniambia kuwa gari imepinduka mara sita na kujikuta nje ya gari akiwa hana simu yake ya mkononi huku akiwa na majeraha miguuni na kichwani na mbunge alifariki dunia papo hapo," alidai Francis.

Aliendelea kusema kuwa: "Alinitaka nisiwe na wasiwasi sana kwani hajaumia sana ila masikitiko yake ni kwamba mbunge amefariki…nilimuuliza nani alikuwa anaendesha gari akasema ni mbunge mwenyewe."

Kwa mujibu wa Francis, hata wakati anakwenda kwake Dodoma mwanae alimpigia simu na kumjulisha kuwa anakwenda huko kikazi kwa wiki moja na baadae atarejea Dar es Salaam kabla ya kwenda tena Dodoma kwa kazi ya fulana.

Katika hatua nyingine, Ramadhan Semtawa anaripoti kutoka Dodoma kuwa Deus Mallya anayedaiwa kuwa dereva wa marehemu Wangwe, amezidi kugonganisha vichwa vya watu baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Juma Kilimba, kusema hamjui wala hana urafiki na kijana huyo.

Kauli hiyo ya Kilimba inapingana na ile aliyotoa Mallya kwamba anafahamiana vema na mbunge huyo kwani walikuwa wote katika safari yao ya kwenda Libya mwaka jana.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili nje ya viwanja vya Bunge mjini hapa jana, Kilimba alisema licha ya kutomfahamu pia alishangaa na hadi sasa hajui kijana huyo aliingiaje katika msafara wao wa kwenda Libya hapo mwaka jana.

Kilimba alifafanua kwamba, alisikia Mallya kwamba anamfahamu yeye (Kilimba), alishangaa na kuongeza kwamba: "Siyo urafiki tu, simjui na sijawahi kuwa na ukaribu naye."

Hata hivyo, Kilimba aliongeza kwamba baada ya kusikia taarifa hizo alikumbuka kwamba wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Zurich, Uswisi, katika safari hiyo kuelekea Libya mwaka jana, kijana huyo aliwahi kusahau hati yake ya kusafiria kwenye ndege.

Alisema kwa kuwa walikuwa katika msafara mmoja, yeye (Kilimba), alishauri asaidiwe baada ya kuzuka tafrani ndipo kiongozi aliyeshughulikia safari hiyo akamsadidia kijana huyo na wala si yeye.

"Niliposikia huyo kijana ana nifahamu mimi, kwanza sikuwa na fikra kabisa kwamba kuna kijana kama huyo aliwahi kuwa rafiki yangu au namfahamu, nikakumbuka kumbe ahaa, ni yule ambaye aliwahi kusahau pasi ya safari yake ndani ya ndege tukiwa Zurich,"alisema Kilimba na akaongeza:

''Mimi nilikuwa Bussines Class yeye alikuwa Economy, sikuwa nikimfahamu, nilishangaa hata mimi pale Zurich kumuona yuko katika msafara, nilihoji na hadi sasa sijajua, aliingiaje katika msafara ule, ndiyo maana nakwambia simfahamu kabisa zaidi ya kuonana pale.''

Aliongeza kwamba, watu aliokuwa nao na aliowafahamu ni pamoja na Makongoro Nyerere ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mamuya, Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Simba, Shehe Seleman Kilemile na Hebron Mwakagenda, ambaye ni kutoka Leadership Forum.

Mallya alifunguliwa kesi namba TR 103/08, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa, kwa makosa ya kuvunja sheria za usalama barabarani, ambayo ni kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo cha Wangwe na kuendesha gari bila leseni.

Source: Mwananchi
 
Dr. Slaa yupo Nchini,maanda haongelei kabisa suala la Mbowe,wamemuachia Zitto na Mnyika.Na hapa natoa ujumbe kwa mnyika,kama jana alisikiliza hotuba ya Mzee Mandela hapa SA nilipo kwa sasa katika kituo cha kulelea Yatima Basi atakuwa ameupata vizuri.Without Education you can not be a good leader..Rudi shule na ujiendeleze kwanza na ambao mengine baadaye,ungana kina Kitila Mkumbo

Gembe, kwa mawazo yako ni kwamba JK na Mkapa hawakuwa na elimu ndo maana si au hawakuwa viongozi bora? By education, in your own perspective, what do you mean and or understand?

We all know (sic!) that Mnyika is a University of Dar es salaam graduate, what do you want to tell us. Kwa mtazamo wako mandela alikuwa anamaanisha a good education is to have a PhD? Tupe uchambuzi wako hususu hii haya maneno"Good Education".
 
Kwanini wamuogope Mbowe,Na hiki kitu kwa sisi wakruya huwa hatukitaki,na ndiyo maana walimchukia Chacha Wangwe sababu hakutaka kubeba mambo ya ukabila.

Kwa hili la kifo cha wangwe niilishatoa onyo zamani sana,ole wao CHADEMA....

Dr. Slaa yupo Nchini,maanda haongelei kabisa suala la Mbowe,wamemuachia Zitto na Mnyika.Na hapa natoa ujumbe kwa mnyika,kama jana alisikiliza hotuba ya Mzee Mandela hapa SA nilipo kwa sasa katika kituo cha kulelea Yatima Basi atakuwa ameupata vizuri.Without Education you can not be a good leader..Rudi shule na ujiendeleze kwanza na ambao mengine baadaye,ungana kina Kitila Mkumbo

Huu msiba wa Wangwe umetufanya tuwajue wakury wengi sana
 
We all know (sic!) that Mnyika is a University of Dar es salaam graduate, what do you want to tell us. Kwa mtazamo wako mandela alikuwa anamaanisha a good education is to have a PhD? Tupe uchambuzi wako hususu hii haya maneno"Good Education".

Kamaliza kozi gani?ile BBA ya jioni?

Natolea Mfano mmoja tu,kama leo Mnyika akifukuzwa CHADEMA tafanya nini??Je elimu aliyonayo itamsaidia nini?sababu hajawahi kuifanyia kazi..?mie nina uhakika leo ukimwambia mhe. Mnyika aelezee chochote kuhsu Macro Economix hataweza.

Mie namuona Mnyika kama Mwanasiasa ambaye anaweza kufanikwa kama kwanza akijiendeleza na shule ili apate exposure,wewe unadhani ni jambo la kumwadikia SMS RA ni siasa za kisasa au ni mambo ya kushangaza,huku ni kushindwa kwa hoja,

Do you know why Mkapa seems to be better than Muungwana in terms of implimentation of different Projects..achilia mbali mapungufu yake,
 
Mkuu MK,

Kwanini kama Mbowe hakutishiwa kukatwa mapanga na kukatwa mapanga,kuna tatizo gani?Je inampunguzia nini Mh. Mbowe?Hoja imekuwa mbowe hakutishiwa kukatwa mapanga,kwa kuwa wanampenda sana au?

Kama wanampenda,

1.Kwanini hakuhudhuria Mazishi kama ilivyo kwa Mhe. Kabwe na viongozi wengine?

2.Mhe. Shelukindo mtu mzima na ndiyo maana kasema haya kwa kifupi,Suala la Mbowe kutishiwa kukatwa Mapanga siyo suala la kitaifa,liko kichama zaidi ndiyo maana kwenyeripoti yake hakusema ammbo ya CCM wala CHADEMA

Uandishi wa habari ni taaluma adhimu lakini HATARI SANA. Hoja hapa ambayo haihitaji ushabiki wa kisiasa ni UKWELI na ukweli ambao haupaswi kutiwa chumvi. Hali haikuwa shwari, huo ni ukweli ambao hata Zitto ameukubali, jambo lenye utata hapa ni mapanga, na silaha za jadi, ambazo zilionyeshwa kwa Mbowe peke yake. Hapa suala si Mbowe, wala Lipumba na Mrema. Ukimsikiliza Mrema na Mbatia utaona wanasema wote walitimuliwa na wanasema kulikua na sialaha za jadi. Japo bado kuna utata, hata kama kina Mrema walikua sahihi, hebu soma story zote zinazolalamikiwa (zilizofanana) kama zilieleza kwamba viongozi wote walitishiwa maisha, wote walisema Mbowe tu, ndiye aliyetimuliwa na kuokolewa na polisi. Hawakuwaona kina Mrema na kina Shelukondo kama kweli kulikuwa na silaha? Hebu tusijadili kwa jazba ama ushabiki, tuwe makini na kuwaandaa waandishi wetu wasijione Miungu watu, kulinda maadili, ili baadaye tusije kujilaumu. Ni media ndiyo iliyotupa tunachohangaika nacho sasa na hatutasahau MILELE
 
Kwanini tusikubali yaishe?

tumeacha kujadili vikao vya bajeti,huko watu wanapumua tu huku siye tukihangaika kumsafisha Mbowe tu.Kwanini alikimbia kemakorere.??haya mie nakubaliana na Halisi kwamba walimshangilia mbowe kw akumuita Rais rais..he he he,Rais akakimbia kbala ya mazishi..you guys mnachekesha sana!

Nakubaliana na Nyani Ngabu,

Hivyo ndivyo tulivyo.Mie sijadili tena maada hii!
 
Good Halisi, you made it clear!

Hata binafsi nilivo wasikia kina Lipumba na Mrema wakiongea walisema hali haikuwa shwari wakapitia mlango wa chumba kilicho kuwa na mwili wa marehemu, na walitishika wote including akina Wasira na Kina Kabaka ambao nao waliruka ukuta!
Sasa hii swala la kwamba Mbowe peke yake ndo alitaka katwa mapanga naona lina makusudi maalumu kupotosha ukweli period!
 
mkuu Mk,

Kwanini Kama Mbowe Hakutishiwa Kukatwa Mapanga Na Kukatwa Mapanga,kuna Tatizo Gani?je Inampunguzia Nini Mh. Mbowe?hoja Imekuwa Mbowe Hakutishiwa Kukatwa Mapanga,kwa Kuwa Wanampenda Sana Au?

Kama Wanampenda,

1.kwanini Hakuhudhuria Mazishi Kama Ilivyo Kwa Mhe. Kabwe Na Viongozi Wengine?

2.mhe. Shelukindo Mtu Mzima Na Ndiyo Maana Kasema Haya Kwa Kifupi,suala La Mbowe Kutishiwa Kukatwa Mapanga Siyo Suala La Kitaifa,liko Kichama Zaidi Ndiyo Maana Kwenyeripoti Yake Hakusema Ammbo Ya Ccm Wala Chadema

Maneno Ya Busara Haya!!!
 
Mimi nafikiri tumechanganya mambo mengi kwa sababu wengi wetu tumechangua upande. Ukitaka kuwa objective utagundua mambo haya:

  1. Ni wazi kwamba kulikuwa na tafrani kwenye msiba kutokana na ukweli kwamba kifo cha marehemu kilikuwa na utata mwingi. Ningeshangaa sana mimi kama msiba huu ungekuwa wa amani kama misiba mingine.
  2. Hata hivyo, kwa sababu za kisiasa, tafrani zilizotokea zimekuzwa ili kuonyesha kwamba kulikuwa na fujo, na fujo hizi zilielekezwa kwa chadema.
  3. Kwa sasa kuna kila dalili kwamba CCM watatumia msiba huu kama njia ya kutokea, maana kwa kweli wamebanwa sana.
  4. Sababu za chadema kunyoshewa kidole katika msiba huu zinaeleweka na zinapaswa kutarajiwa: i) ndio chama kinachotishia uhai wa CCM kwa sasa, ii) mbunge aliyefariki alikuwa ni mbunge wa chadema na hivyo wapinzani wa chadema wangependa kutumia msiba huu kuhakikisha kwamba chadema haichaguliwi tena huko Tarime iii) marehemu alikuwa na mgogoro na viongozi wake, na kwa kiasi kikubwa alijaribu kuonyesha kwamba mgogoro huu ulikuwa kati yake na Mwenyekiti wa chadema.
  5. Kwa maoni yangu, maelezo ya Zitto kwamba hapakuwa na fujo huko Tarime yalilenga zaidi kukanusha madai kwamba hasira za wananchi zilielekezwa kwa Mwenyekiti Mbowe, na kwamba hapakuwa na mapanga wala mishale. Pengine alichokosea Zitto ni kukanusha madai ya fujo kwa jumla jumla. Angeweza kukiri kwamba, yes, kulikuwa na aina fulani ya tafrani au fujo lakini sio kweli kwamba fujo hizi zilielekezwa kwa mwenyekiti Mbowe, na wala sio kweli kwamba fujo hizi zilifikia kiwango cha wananchi kubeba mapanga, mishale kama ilivyoripotiwa. Nafikiri ile kamati ya wahariri itaweza kufafanua hili vizuri. Nahisi kwamba kamati itakiri kuwepo kwa aina fulani ya fujo, ambayo inaeleweka kutokana na mazingira ya kifo na umaarufu wenyewe wa marehemu. Lakini nahisi pia kwamba kamati itakanusha madai ya kufanyiwa fujo kwa Mweneyikiti Mbowe, na wala wananchi kubeba mapanga na mishale.

Ni wazi kwamba CHADEMA tumetikiswa. Ama tutaanguka au la, itategemea tutakavyo-handle matukio baada ya msiba huu. Kwa maoni yangu njia pekee ya kusimama ni kuwa wa kweli, na inabidi tuwe wa kweli katika mambo makubwa manne yafuatayo:

(a) Tukiri kwamba, yes, kulikuwa na mgogoro kati ya marehemu na viongozi wenzake katika chama. Baada ya uchunguzi uliofanyika, Kamati Kuu ya CHADEMA iliona kwamba marehemu alikuwa amekiuka baadhi ya kanuni za chama ,na hivyo ikaona ni vyema kumsimamisha uongozi

(b) Tukiri kwamba, yes, baada ya kusimamishwa, marehemu hakuridhika na maamuzi yale, na alikuwa akifanya utaratibu wa kukata rufaa katika vikao vya chama, na hata mahakamani

(c) Tukiri kwamba, yes, baada ya msiba huu, wapinzani wetu, na hasa CCM, wamekuwa wakijaribu kuhusisha kifo cha marehemu na mgogoro huu ili ionekane kwamba kifo cha marehemu kimetokana na mgogoro huu.

(d) Tukemee njia chafu wanazotumia CCM kujaribu kufifisha nguvu za upinzani na kujipatia umaarufu kupitia kifo cha marehemu. Tuweke wazi kwamba huu ni ushetani, na sio jadi ya watanzania kutumia msiba wa mwenzako katika kujipatia umaarufu. Na wala sio jadi ya watanzania kujaribu kumjeruhi ng'ombe aliyekwishajeruhiwa. Katika hali ya kawaida ya utanzania wetu, ilitarajiwa kwamba CCM wangekuwa wanawapa CHADEMA pole na rubani kwa kufiwa na mwanachama, kiongozi na mbunge wa chama chao. Badala yake hawa wenzetu wapo busy kujaribu kutumia msiba huu kujinufaisha kisiasa. Kwa maoni yangu tukijenga hoja hii vizuri kwa wananchi, ndio itakuwa mwisho wa ghiliba za CCM kuendelea kutumia msiba huu kama njia ya kutokea. Hili jambo halihitaji danadana.
 
Kwanini tusikubali yaishe?

tumeacha kujadili vikao vya bajeti,huko watu wanapumua tu huku siye tukihangaika kumsafisha Mbowe tu.Kwanini alikimbia kemakorere.??haya mie nakubaliana na Halisi kwamba walimshangilia mbowe kw akumuita Rais rais..he he he,Rais akakimbia kbala ya mazishi..you guys mnachekesha sana!

Nakubaliana na Nyani Ngabu,

Hivyo ndivyo tulivyo.Mie sijadili tena maada hii!

Haya wewe msomi tueleze umeisaidiaje nchi yako japo kidogo na hizo degree zako au nyie ndiyo wale mnaopamba degree zenu ukutani? Ukiwa huru unang'aa hata ufanye nini watu wanakuona na kukusikia tu tu ila ukitumwa unakuwa kama wewe presha kibao
 
I love Tanzania:

Nakumbuka kipindi fulani Mh. Basil Mramba aliwahi kusema yeye sasa ni bubu! hivyo akawa haongei...

Sikumbuki kwamba Mh. Mbowe naye kama ametangaza kitu cha namna hii... mimi namuheshimu sana lakini mpaka sasa najiuliza hivi tangu lini Mh. Mbowe akawa na uwezo wa subra kama ule wa Mh. Malecela kiasi kwamba hata vitu ambavyo anatakiwa aseme au aongee mwenyewe inabidi asemewe na akina Mh. Zitto, Mnyika, Kitila etc.?

Hivi si ndio vyama vya upinzani siku vyote vinataka mtu aseme mwenyewe... vyombo vya habari vina kawaida ya kufanya watu fulani hawagushwi kwa wakati fulani kwa masilahi fulani...

I love Tanzania
 
Was a normal accident, then what are the possible causes, may be mechanical falts or alcohol influence.

Mkulu inawezekana na wewe unajaribu kuficha kitu hebu tupe majibu ya maswali yafuatayo.
  • Nani alikuwa dereva wakati wa hajari, Wangwe au Mallya?
  • Kama ni mallya kwanini anakataa kusema ukweli kuwa yeye alikuwa dereva pamoja na ushaidi wa kutosha kuwa alikuwa dereva
  • Kwanini kiti cha abiria tu ndo kilikuwa na damu wakati aliyekuwa alikuwa kiti cha dereva?
  • Huyu kijana ana elimu gani?
  • Je safari ya Libya alikwenda kama nani kwenye msafara wa key figures kwenye nchi yetu?
  • Je inawezekana ukaacha passport yako kwenye ndege nchi ya kigeni halafu wakakuruhusu kuendelea na safari?
  • Vitambulisho vingi vilikuwa vya nini?
  • Je aliwahi kuishi Nairobi kama anavyosema au sio kweli kama baba yake anavyosema kuwa hajawahi kuishi Nairobi?

Nafikiri tukipata majibu ya maswali haya tunaweza kulidhika na tusiulize tena.

Mimi nina wasiwasi wamemtumia sasa wanataka kumkaanga mbele ya jamii kabla hajakwenda kwa pilato ambako hata akinyeshewa mvua ya maisha hakuna atayemsaidia.
 
Kwanini tusikubali yaishe?

tumeacha kujadili vikao vya bajeti,huko watu wanapumua tu huku siye tukihangaika kumsafisha Mbowe tu.Kwanini alikimbia kemakorere.??haya mie nakubaliana na Halisi kwamba walimshangilia mbowe kw akumuita Rais rais..he he he,Rais akakimbia kbala ya mazishi..you guys mnachekesha sana!

Nakubaliana na Nyani Ngabu,

Hivyo ndivyo tulivyo.Mie sijadili tena maada hii!

Sijakuelewa!! Yaishe tuache waandishi wetu waendelee kutulisha sumu? Ajuu tuache yaishe wanasiasa waendelee kupinga habari ya kweli iliyoripotiwa na vyombo vya habari? Kwisha ni kujua ukweli, tena ukweli wa dhati. Nimeshasema, kama kulikua na fujo na kama kulikua na silaha (japo hata TBC1 walionyesha hapakuwa na mapanga), viongozi walioondoka wakiwa na salam na rambirambi za serikali na Bunge, nao walikimbia nini? Mbona ni Mbowe tu anayehojiwa kwanini alikimbia? Mrema, Mbatia, Lipumba hawana mguso wowote pale Tarime naamini walionekana kama watu wa kawaida tu. Walioonekana ni wawakilishi wa Bunge wakiongozwa na Shelukindo wakiwa wamekodishiwa ndege mbili kwa fedha za walipa kodi na Mbowe ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chenye wafuasi wengi Tarime na baada ya mgogoro na Chacha ni chama pia chenye maadui wengi kikitanguliwa na CCM
 
Vijana wamtetea Deus Mallya

na Edward Kinabo

SIKU moja baada ya viongozi watatu kutoka kambi ya upinzani kuibua madai mazito kuhusu Deus Mallya, anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, vijana waliosoma naye Libya wamejitokeza kumtetea.

Steve Mbogo, mmoja wa vijana wanaomfahamu Mallya na aliyewahi kuwa naye nchini Libya, alisema alikuwa na mtuhumiwa huyo nchini Libya kwa mafunzo tofauti, lakini si ya kijasusi.

Mbogo ambaye ni mratibu wa taasisi ya Tanzania Development Initiative (TADIP), alisema madai yaliyotolewa na wenyeviti wa upinzani si ya kweli, kwani yeye na Mallya walikuwa miongoni mwa wawakilishi 20 kutoka Tanzania waliokwenda Tripoli, Libya Juni mwaka jana.

Alisema walikwenda Libya kushiriki mkutano wa kutoa mapendekezo kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, uliokuwa ufanyike nchini Ghana mwaka jana, kujadili ajenda ya kuwa na serikali moja ya Afrika.

Akifafanua zaidi, alisema mkutano huo ulishirikisha nchi mbalimbali za Afrika, mbali na Tanzania, na uliandaliwa na Ubalozi wa Libya kwa kushirikiana na asasi ya Revolutionary Committee Movement (RCM), yenye makao yake makuu nchini Libya.

Alisema wawakilishi wa mkutano huo, walipatikana kwa utaratibu wa kutuma maombi kwa uongozi wa matawi na wakala wa RCM kutoka katika nchi shiriki.

Aliongeza kuwa madai yaliyotolewa na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Augustine Mrema (TLP) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), yanashangaza, kwani mkutano huo wa Libya, ulichukua siku 20, na muda wote huo, walilala chumba kimoja na Mallya, lakini hakuwahi kumwona akitoroka mkutanoni kwenda kupata mafunzo ya ujasusi, kama ilivyodaiwa na wanasiasa hao.

"Haiingii akilini kuwa Mallya alikuwa Libya kwa mafunzo ya ujasusi, kwani mkutano uliotupeleka huko, ulikuwa na wawakilishi wengine 19 kutoka Tanzania, wakiwamo Sheikh Mkuu, Shaaban Simba, Juma Kilimba (Mbunge wa Iramba) na Makongoro Nyerere, watu ambao hawajawahi kutuhumiwa kwa ujasusi," alisema.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo ana uhakika kuwa Mallya hakuwahi kuwa Libya kabla au baada ya mkutano huo, alisema kuwa hajui lolote kuhusu hilo.

Gazeti hili jana liliripoti tamko la wenyeviti wa CUF, NCCR-Mageuzi na TLP, ambao walidai kuwa wana ushahidi wa kutosha kwamba Mallya ni mmoja wa watu waliopata mafunzo makali ya kijasusi nchini Libya, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa, na ni mtaalamu wa hali ya juu wa kompyuta.

Viongozi hao walivitaka vyombo vya usalama kufanya utafiti wa kina juu ya suala hili, ili kubaini ukweli zaidi kuhusu Mallya, kwani inasemekana alikuwa dereva wa Wangwe, lakini wamebaini ni mtu aliyezoeana naye kwa muda mfupi sana, hali ambayo inaibua maswali mengi.

Utata kuhusu Mallya na nini kilitokea hata kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha Wangwe, ulisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimwandikie barua Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Said Mwema, kikitaka kufanyika uchunguzi wa kina.

CHADEMA pia ilimtaka IGP kuchunguza ukweli kuhusu maelezo ya Mallya na kujua ni wapi alikuwa amekaa wakati ajali ikitokea, na kuchukua hatua zinazopaswa, baada ya uchunguzi huo.
 
Sijakuelewa!! Yaishe tuache waandishi wetu waendelee kutulisha sumu? Ajuu tuache yaishe wanasiasa waendelee kupinga habari ya kweli iliyoripotiwa na vyombo vya habari? Kwisha ni kujua ukweli, tena ukweli wa dhati. Nimeshasema, kama kulikua na fujo na kama kulikua na silaha (japo hata TBC1 walionyesha hapakuwa na mapanga), viongozi walioondoka wakiwa na salam na rambirambi za serikali na Bunge, nao walikimbia nini? Mbona ni Mbowe tu anayehojiwa kwanini alikimbia? Mrema, Mbatia, Lipumba hawana mguso wowote pale Tarime naamini walionekana kama watu wa kawaida tu. Walioonekana ni wawakilishi wa Bunge wakiongozwa na Shelukindo wakiwa wamekodishiwa ndege mbili kwa fedha za walipa kodi na Mbowe ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chenye wafuasi wengi Tarime na baada ya mgogoro na Chacha ni chama pia chenye maadui wengi kikitanguliwa na CCM

Kwa muhistasari unasema kwa nini Mbowe? Jibu ni kwa sababu alimchezea rafu Marehemu. Chacha wangwe kwenye chama kabla ya kifo chacke na wala sio sababu nyingine yoyote.

Mtu mwenye akili yoyote akiona fujo zitatokea hata za kibaka anajiondoa kwa sababu hajui baada ya kibaka kupiga what next... wote waliojiondoa walijiondoa kwa sababu hiyo...

Swali lingine rahisi sana... kwani suspect mkubwa wa kifo cha Mh. Wangwe ni nani? Kwa vyovyote walikuwa wale waliokuwa na bifu naye... na sikumbuki kama serikali au bunge au CUF, TLP, NCCR walikuwa na bifu naye?
 
Mimi nafikiri tumechanganya mambo mengi kwa sababu wengi wetu tumechangua upande. Ukitaka kuwa objective utagundua mambo haya:

  1. Ni wazi kwamba kulikuwa na tafrani kwenye msiba kutokana na ukweli kwamba kifo cha marehemu kilikuwa na utata mwingi. Ningeshangaa sana mimi kama msiba huu ungekuwa wa amani kama misiba mingine.
  2. Hata hivyo, kwa sababu za kisiasa, tafrani zilizotokea zimekuzwa ili kuonyesha kwamba kulikuwa na fujo, na fujo hizi zilielekezwa kwa chadema.
  3. Kwa sasa kuna kila dalili kwamba CCM watatumia msiba huu kama njia ya kutokea, maana kwa kweli wamebanwa sana.
  4. Sababu za chadema kunyoshewa kidole katika msiba huu zinaeleweka na zinapaswa kutarajiwa: i) ndio chama kinachotishia uhai wa CCM kwa sasa, ii) mbunge aliyefariki alikuwa ni mbunge wa chadema na hivyo wapinzani wa chadema wangependa kutumia msiba huu kuhakikisha kwamba chadema haichaguliwi tena huko Tarime iii) marehemu alikuwa na mgogoro na viongozi wake, na kwa kiasi kikubwa alijaribu kuonyesha kwamba mgogoro huu ulikuwa kati yake na Mwenyekiti wa chadema.
  5. Kwa maoni yangu, maelezo ya Zitto kwamba hapakuwa na fujo huko Tarime yalilenga zaidi kukanusha madai kwamba hasira za wananchi zilielekezwa kwa Mwenyekiti Mbowe, na kwamba hapakuwa na mapanga wala mishale. Pengine alichokosea Zitto ni kukanusha madai ya fujo kwa jumla jumla. Angeweza kukiri kwamba, yes, kulikuwa na aina fulani ya tafrani au fujo lakini sio kweli kwamba fujo hizi zilielekezwa kwa mwenyekiti Mbowe, na wala sio kweli kwamba fujo hizi zilifikia kiwango cha wananchi kubeba mapanga, mishale kama ilivyoripotiwa. Nafikiri ile kamati ya wahariri itaweza kufafanua hili vizuri. Nahisi kwamba kamati itakiri kuwepo kwa aina fulani ya fujo, ambayo inaeleweka kutokana na mazingira ya kifo na umaarufu wenyewe wa marehemu. Lakini nahisi pia kwamba kamati itakanusha madai ya kufanyiwa fujo kwa Mweneyikiti Mbowe, na wala wananchi kubeba mapanga na mishale.

Ni wazi kwamba CHADEMA tumetikiswa. Ama tutaanguka au la, itategemea tutakavyo-handle matukio baada ya msiba huu. Kwa maoni yangu njia pekee ya kusimama ni kuwa wa kweli, na inabidi tuwe wa kweli katika mambo makubwa manne yafuatayo:

(a) Tukiri kwamba, yes, kulikuwa na mgogoro kati ya marehemu na viongozi wenzake katika chama. Baada ya uchunguzi uliofanyika, Kamati Kuu ya CHADEMA iliona kwamba marehemu alikuwa amekiuka baadhi ya kanuni za chama ,na hivyo ikaona ni vyema kumsimamisha uongozi

(b) Tukiri kwamba, yes, baada ya kusimamishwa, marehemu hakuridhika na maamuzi yale, na alikuwa akifanya utaratibu wa kukata rufaa katika vikao vya chama, na hata mahakamani

(c) Tukiri kwamba, yes, baada ya msiba huu, wapinzani wetu, na hasa CCM, wamekuwa wakijaribu kuhusisha kifo cha marehemu na mgogoro huu ili ionekane kwamba kifo cha marehemu kimetokana na mgogoro huu.

(d) Tukemee njia chafu wanazotumia CCM kujaribu kufifisha nguvu za upinzani na kujipatia umaarufu kupitia kifo cha marehemu. Tuweke wazi kwamba huu ni ushetani, na sio jadi ya watanzania kutumia msiba wa mwenzako katika kujipatia umaarufu. Na wala sio jadi ya watanzania kujaribu kumjeruhi ng'ombe aliyekwishajeruhiwa. Katika hali ya kawaida ya utanzania wetu, ilitarajiwa kwamba CCM wangekuwa wanawapa CHADEMA pole na rubani kwa kufiwa na mwanachama, kiongozi na mbunge wa chama chao. Badala yake hawa wenzetu wapo busy kujaribu kutumia msiba huu kujinufaisha kisiasa. Kwa maoni yangu tukijenga hoja hii vizuri kwa wananchi, ndio itakuwa mwisho wa ghiliba za CCM kuendelea kutumia msiba huu kama njia ya kutokea. Hili jambo halihitaji danadana.

Mkuu Kitila,

CHADEMA wangelikuwa na watu kama wewe kama 10 hivi, naamini kwa matatizo ya sasa ya CCM mungeweza kuitikisa mno CCM.

Nachelea kukusifia sana ili tembo lisije ongezewa maji ila tu kwa uchunguzi wangu usio wa kisayansi najua vyama vyetu hasa vya upinzani vina matatizo ya kukosa watu wenye uwezo wa kuviongoza. Vinaweza kuwa na watu watatu au wanne wazuri, lakini hiyo namba haitoshi, lazima muvute vijana wengine ili kusaidia gurudumu.

Bahati mbaya kwa haya yanayoendelea ni ngumu sana watu wenye mawazo huru kuamua
waende wapi maana risk inaonekana kubwa na sio kila mtu yuko tayari kubeba risks kubwa kwenye maisha yake. Ukikosana na wakubwa na ukatimuliwa, jua wamekumaliza kisiasa, labda uwe na nguvu sana.

Mnahitaji hata washauri tu, sio lazima wawe Tanzania na sio lazima wawe wanachama damu damu wa CHADEMA. Ushauri mzuri ni ule unaotaka kwa mtu huru na wala sio yule ambaye mkate wake unategemea kwa huyo anayemshauri.

Nawatakia mafanikio mema kwa mwaka 2010.
 
Kwa muhistasari unasema kwa nini Mbowe? Jibu ni kwa sababu alimchezea rafu Marehemu. Chacha wangwe kwenye chama kabla ya kifo chacke na wala sio sababu nyingine yoyote.

Hapana bwana Mbowe hakumchezea rafu marehemu; uamuzi wa kumsimamisha ulifanywa na kikao halali kabisa cha CHADEMA kwa mujibu wa katiba. Mbowe anabeba lawama nyingi, ambayo ni sawa, kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa chama, lazima abeba dhamana hiyo.Kwa hiyo binafsi sioni ajabu kwa Mbowe kubebeshwa msalaba kwa niaba ya chama kwa sababu kwa sasa ndiye kiongozi, tena kiongozi ambaye CCM wanamhara, kama vile ambavyo amekuwa akichukua sifa pale ambapo CHADEMA inafanya vizuri.

Ni kama vile ambavyo JK inabidi abeba dhamana ya madhira yote yanayotokea sasa hivi katika nchi yetu, lajikini haina maana kwamba madhira haya anayafanya peke yake, mengine wala sio yeye, ni ya akina Makamba, Kisumo na vilaza wengine katika CCM!
 
swala hili linazidi kuwa tata mno, habari nilizozipata punde zinaeleza pia kuwa Marehemu alioa mke wa mtu, huyo Mariam (Mke mdogo)alikuwa mke wa mwarabu mmoja Tabora anaetoka kwenye familia Tajiri, huyo mariam alikuwa akiendesha Hotel moja maarufu Mjini Tabora iliuyoitwa Bambino Hotel inayotazama na TMP book shop kwa sasa ni Meyor Hotel, mumewe na Mariam kwa wakati nadhani hadi sasa alikuwa akijishughulisha na biashara ya kuuza mashine za kusaga na spea zake, nazidi kuthibitishiwa kuwa mtu yeyote alikuwepo Tabora miaka minne mitano iliyopita anamfahamu vizuri Mariam Bambino kama mke wa mwarabu aliyezaa nae watoto nadhani watatu wenye wajihi wa kiarabu kabisa tofauti na mtoto aliyezaa na wangwe kwa sasa( pure black) nadhani si vibaya pia tukiendelea kuutazama upande wa pili wa shilingi kama Mwarabu aliponyang'anywa mke na marehemu Wangwe alifurahia au la. lastly, this is not uzushi coz mariam amekuwa maarufu sana Tabora kwa ku tengeneza chakula cha sherehe, keki n.k
 
Kiranja,

Nadhani wewe ni kiranaja wa sehemu ulipo,suala la mimi kulipiwa na mtu yeyote ambaye ni muajiri wangu wewe alikuhusu kabisa.

Kama una ugomvi na Kijana kuhama Mwananchi na kwenda RAI,is up to you lakini kaaa ukijua kila mtu anatafuta maisha na suala la kuhama gazeti moja kwenda lingine ni mpango wa mtu.

Kwanini unataka kila mtu aishi kama wewe utakavyo,hiyo ni tabia ya ubinafsi na watu wengi wenye tabia hiyo ni wachaga.Suala la kujitambulisha mie halinihusu.

Mkuu Gembe,

Kumbe wewe nawe una ukabila namna hii? Naona hapo juu kuna mahali umejitangaza kwamba umesoma masters Degree na kumkandia mbaya Mh. Mnyika,lakini mi naona hata bora huyo ndugu ambae unadharau BBA yake ya jioni lakini ukiangalia vitu alivyo-accomplish na mchango wake kwa taifa letu ,he is far better than you.

Sioni mantiki ya mtu mwenye master's Degree kueneza chuki za kikabila huku akijua madhara yake.Hata kama ni mtu wa kidato cha Tatu tayari anajua madhara ya ukabila,sasa nakushangaa hapa unasema wewe ni msomi but still huonyeshi usomi huo katika kunena na kutenda.

Naona ulikua unamnukuu vibaya Mzee madiba maanake hata yeye alisoma correspondence,afadhali hata Mnika anapata hata lecture.Je,mandela hakuweza kuwakomboa watu wake? Kimsingi sipingi elimu au kujiendeleza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom