Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kamaliza kozi gani?ile BBA ya jioni?

Natolea Mfano mmoja tu,kama leo Mnyika akifukuzwa CHADEMA tafanya nini??Je elimu aliyonayo itamsaidia nini?sababu hajawahi kuifanyia kazi..?mie nina uhakika leo ukimwambia mhe. Mnyika aelezee chochote kuhsu Macro Economix hataweza.

Mie namuona Mnyika kama Mwanasiasa ambaye anaweza kufanikwa kama kwanza akijiendeleza na shule ili apate exposure,wewe unadhani ni jambo la kumwadikia SMS RA ni siasa za kisasa au ni mambo ya kushangaza,huku ni kushindwa kwa hoja,

Do you know why Mkapa seems to be better than Muungwana in terms of implimentation of different Projects..achilia mbali mapungufu yake,

Hata JF Sr & Premium Member nao huwa wanachemka. Siamini kama Mnyika atakosa kazi Bongo nje ya siasa kwa sababu ka-graduate Mlimani. Katika jamii yoyote duniani kuna mgawanyo wa kazi. Hata kama Mnyika angekuwa fundi wa viatu still ni kazi. Kuna watu bado wana fikra kuwa unakwenda shule ili upate kazi. Mtu unakwenda shule ili uelimike, kazi ni matokeo ya usomi wako hata kama ni kuunga baiskeli. Hivyo kama Mnyika aliamua kufuata siasa, huo ulikuwa ni utashi wake kwa maslahi ya chama chake pamoja na taifa lake. Dr. Slaa, Lipumba hawa si wana PIHECHIDII mbona ni wanasiasa?
 
Kamaliza kozi gani?ile BBA ya jioni?

Natolea Mfano mmoja tu,kama leo Mnyika akifukuzwa CHADEMA tafanya nini??Je elimu aliyonayo itamsaidia nini?sababu hajawahi kuifanyia kazi..?mie nina uhakika leo ukimwambia mhe. Mnyika aelezee chochote kuhsu Macro Economix hataweza.

Mie namuona Mnyika kama Mwanasiasa ambaye anaweza kufanikwa kama kwanza akijiendeleza na shule ili apate exposure,wewe unadhani ni jambo la kumwadikia SMS RA ni siasa za kisasa au ni mambo ya kushangaza,huku ni kushindwa kwa hoja,

Gembe, bado hujajibu swali. kwanza kubali au kanusha kwamba Mnyika ni graduate wa UDSM, either alikuwa full-time au part-time si hoja, zipo njia mbalimbali za kupata elimu na mojawapo ni hiyo inayowawezesha watu wanaofanya kazi kusoma huku wakiendelea na kazi zao kama kawaida na ndio maana ya mpango wa part-time na upo dunia nzima na elimu ni ileile, tofauti ni muda wa kumaliza (duration).

Tupe uchambuzi wako binafsi what is "to have a good education", hilo ndilo unatakiwa utueleze.
 
Last edited:
Yaani huyu mkuu sijui anamaanisha nini kuanzisha uzushi tu.Sijui ni kwa maslahi ya nani maanake there is no logic at all.
 
Hapa naona tumeacha kujadili maudhui ya kauli za mzee Shelukindo ,pamoja na jinsi waandishi walivyoweza kuripoti tukio hilo sasa tuanajadili degree ya Mnyika ,na PHD za wengine.

Naamini kuwa waandishi walienda mno mbali, na walikuwa wanamlenga Mbowe specific, na mpango huo huenda ulisukwa na watu wenye nia zao na hila zao dhidi ya Mbowe na CHADEMA kwa ujumla wake.

Taarifa rasmi ndio hiyo,japo hata leo ukisoma gazeti mojawapo limeanza kusema kuwa wananchi wanamtaka Zitto awaombe radhi kwani alivishushia hadhi vyombo vya habari na haswa magazeti husika,sasa naona kuwa huu mjadala utaenda mbali sana .

Tuendelee kuijenga nchi ,na kufuatilia kwa kina msiba huu kwani inawezekana tukaona ni kawaida kesho inaweza ikawa ni zamu ya mwingine hivyo lazima tuwe soba na kujiridhisha kuwa kifo hiki ni cha ajali ama laa.
 
Nipo kwenye Trainning za ORACLE and mambo yanayohusu Advanced Ethicial Hacker and Information Systems Security.

Hao waandishi walioko huku nimekutana nao na nina wafahamu sana sababu nilikutana nao Mlimani wakati namaliza Masters Yangu wao wakiwa wadoo zangu na kwa kuwa mmoja wao tumetoka sehemu moja ilikuwa rahisi mie kuwapa ushauri wa maisha,wewe ulitaka nani awasomeshe?Mie nimewasifu kwa mbinu yao ya kujipatia Elimu kwa ujanja.ulitaka waje kwako uwasaidie au?acheni wivu wa kijinga kwa vijana hawa na waacheni watafute maisha.

Mie niko tayari kutoa pesa ili Mnyika ajiendeleze na Shule,sababu namkubali
Gembe,
Sipo hapa kujisifu. Nimekaa nje ya Tanzania miaka mingi. Nimekuja kugundua kitu kimoja. Watu wengi huenda kusoma na kurudi Tanzania huku wakijiona wasomi. Wakati mwingine masomo hayo wangeliweza kuyasoma Tanzania ila nchi iliwapeleka nje. Sasa hapo swali, kwa nini kumpeleka mtu nje?
Unapokuwa nje, usisome tu shule na kufaulu na kurudi nyumbani. Nenda pia huko kwa wanyeji ukajifunze jinsi wanavyoishi, mila zao, utamaduni wao na angalia jambo gani utaweza kulichukua na kulileta NYUMBANI.
Katika kukaa nje, nimejifunza kuwa, elimu unayopata mitaani kwa wenyeji, ni kubwa sana kuliko unayopata darasani. Hivyo, kama uko SA tafadhali angalia na kuchunguza sana, hasa Wazungu maisha yao yakoje. Ukirudi na kwenda kuishi sehemu chafu, maji ya choo yanapita mbele ya nyumba yako nk, ujuwe hiyo shule yako SA haikukusaidia. Ukiwa huko ufumbuke macho. Usiwe mbele kumtetea RA kwa kila jambo hata kama jamaa kachemsha. Mtakuja aibika nyie watu vibaraka wa RA. Ukioana mambo mazito SI KUWA BUBU?
Jambo kubwa maishani nimejifunza ni hili:- KAMA WATANZANIA tungelikuwa na walau NUSU ya ushirikiano wa WAYAHUDI ..................

NB: Hivi Rais Reagan na Arnold Schwarzenegger ELIMU YAO imekaa kaaje?
Mandela pia ni nshomile hadi wapi?
Kama una pesa na unataka kusaidia watu wasome, tafuta watto yatima na msaidia mmoja mwenye uwezo hadi UDSM. Na Mungu atakubariki.
 
Hapa naona tumeacha kujadili maudhui ya kauli za mzee Shelukindo ,pamoja na jinsi waandishi walivyoweza kuripoti tukio hilo sasa tuanajadili degree ya Mnyika ,na PHD za wengine.

Naamini kuwa waandishi walienda mno mbali, na walikuwa wanamlenga Mbowe specific, na mpango huo huenda ulisukwa na watu wenye nia zao na hila zao dhidi ya Mbowe na CHADEMA kwa ujumla wake.

Taarifa rasmi ndio hiyo,japo hata leo ukisoma gazeti mojawapo limeanza kusema kuwa wananchi wanamtaka Zitto awaombe radhi kwani alivishushia hadhi vyombo vya habari na haswa magazeti husika,sasa naona kuwa huu mjadala utaenda mbali sana .

Tuendelee kuijenga nchi ,na kufuatilia kwa kina msiba huu kwani inawezekana tukaona ni kawaida kesho inaweza ikawa ni zamu ya mwingine hivyo lazima tuwe soba na kujiridhisha kuwa kifo hiki ni cha ajali ama laa.


Mkuu Wangu,

Hapa ilikua kuwekana sawa kwanza maanake kitendo alichofanya Gembe hakitofautiani sana na cha hao akina RA na manazi wengine.Tukiwa njiani kujadili maudhui wa hiyo ripoti tayari mabo yanayofanana na hayo tunayoyalaani yameshatokea hapa hapa.Lazima kuikemea na ama kudadisi ni nini madhumuni ya wenzetu hawa ili kubaini tatizo liko wapi.

CCM nao ni watu wa ajabu sana yaani ni watu waliokosa uzalendo na ubinadamu kwani wako radhi kuona damu inamwagika kwa kueneza propaganda,nakubali si cCM wote wako hivyo lakini kuna yale Magugu ambayo hatakiwi katika harakati za kulistawisha taifa letu.

Btw: Hii ripoti imeonyesha kweli kulikua na vurugu.Lakini sasa kama Mbowe ndiye alifukuzwa hao wengine wakiwemo viongozi wa cCM walikimbia nini sasa au nao walikua wanaji-feel guilty tu? Kuna mtu mwingine mpuuzi mpuuzi anetaka kuwa-manipulate watanzania huyu Paul Kyara.Yeye anakurupuka na kuropoka maneno ambayo hana hawezi kutufanya tumuamini manake hajaweza kututhibitishia aliyotamka kwenye gazeti la majira leo hii.Yaani sijui CHADEMA ikifa leo hii ata-achieve nini.

CHADEMA sasa pia inabidi kubadili mbinu na mkakati wa kukabiliana na CCM,tuache siasa za kidiplomasia.Huu ni mkakati ulioshindwa.Na ninyi tumieni siasa za kuwarudishia kibao kwenye shavu lao la karibu.Wao kila siku wawaonee na kuwafanyia umafia halafu muwaache tu,huu uvumilivu umevuka mpaka hadi Raia wa kigeni(Iran) anakuja kutuletea mgawanyo wa kikabila.No it is too much
 
swala hili linazidi kuwa tata mno, habari nilizozipata punde zinaeleza pia kuwa Marehemu alioa mke wa mtu, huyo Mariam (Mke mdogo)alikuwa mke wa mwarabu mmoja Tabora anaetoka kwenye familia Tajiri, huyo mariam alikuwa akiendesha Hotel moja maarufu Mjini Tabora iliuyoitwa Bambino Hotel inayotazama na TMP book shop kwa sasa ni Meyor Hotel, mumewe na Mariam kwa wakati nadhani hadi sasa alikuwa akijishughulisha na biashara ya kuuza mashine za kusaga na spea zake, nazidi kuthibitishiwa kuwa mtu yeyote alikuwepo Tabora miaka minne mitano iliyopita anamfahamu vizuri Mariam Bambino kama mke wa mwarabu aliyezaa nae watoto nadhani watatu wenye wajihi wa kiarabu kabisa tofauti na mtoto aliyezaa na wangwe kwa sasa( pure black) nadhani si vibaya pia tukiendelea kuutazama upande wa pili wa shilingi kama Mwarabu aliponyang'anywa mke na marehemu Wangwe alifurahia au la. lastly, this is not uzushi coz mariam amekuwa maarufu sana Tabora kwa ku tengeneza chakula cha sherehe, keki n.k


Mke wa Wangwe Mariam kutaka familia iamini kuwa CHADEMA inahusika ,huku akiwa yeye ndio alikuwa anaenda kukutana na wakina Rostam Azizi haswa pale Kempinsik kwa ajili ya kufanya mipango na hata kumfanya mumewe kuwa na ukaribu na MAFISADI HAO.
Mariam amekuwa sasa na mkakati wa kuhakikisha kuwa mtoto wa marehemu yule wa kiume mkubwa Zakayo anatumika kisawasawa kutoa kauli kuwa CHADEMA wanahusika ,japo watu wengine kwenye familia hiyo wamekuwa wakipingana na mawazo hayo,na haswa baada ya kujua na kuona mbinu na hila za huyu mke mdogo ambaye alikutana na Wangwe baada ya kuwa Mbunge na hata kumfanya Wangwe kuishi naye.

Familia mpaka sasa wanaugomvi na huyu mke mdogo kwani wanataka kujua mali za marehemu kama vile nyumba na shamba la ekari sita lililonunuliwa huko Dodoma liko wapi na hati zake ziko kwa nani ,hii ilipelekea juzi usiku kukaa kikao mpaka asubuhi.

Mke mdogo akishirikiana na mke wa kwanza wameamua kumtenga mke wa kati yaani yule wa pili ,sasa huyu ndio alikuwa na marehemu wakati wote wa kampeni na hata alipokuwa amefungwa huyu alikuwa naye bega kwa bega.
Interesting.....
 
Hapana bwana Mbowe hakumchezea rafu marehemu; uamuzi wa kumsimamisha ulifanywa na kikao halali kabisa cha CHADEMA kwa mujibu wa katiba. Mbowe anabeba lawama nyingi, ambayo ni sawa, kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa chama, lazima abeba dhamana hiyo.Kwa hiyo binafsi sioni ajabu kwa Mbowe kubebeshwa msalaba kwa niaba ya chama kwa sababu kwa sasa ndiye kiongozi, tena kiongozi ambaye CCM wanamhara, kama vile ambavyo amekuwa akichukua sifa pale ambapo CHADEMA inafanya vizuri.
Ni kama vile ambavyo JK inabidi abeba dhamana ya madhira yote yanayotokea sasa hivi katika nchi yetu, lajikini haina maana kwamba madhira haya anayafanya peke yake, mengine wala sio yeye, ni ya akina Makamba, Kisumo na vilaza wengine katika CCM!



Mengine yote nakubaliana na wewe 100%, lakini nililo-bold hapo juu!!! nasita kusema kumbe tayari mnafanya vizuri sana... kumbe tuna makengeza wengine... mimi nilidhani ndio munahitaji kusimama imara kumbe already ndio muko imara...

Oooh... maskini nchi yangu.
 
Babake mzazi wa Mallya azidi kuchanganya mambo

Francis Matey Mallya, baba mzazi wa Deus Mallya akiwa katika ofisi za Mwananchi, mjini Moshi kumtetea mwanae jana.
Na Daniel Mjema, Moshi

BABA mzazi wa kijana aliyekuwa na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe (Chadema) kwenye gari lililosababisha kifo chake, amezidi kuchanganya mambo baada ya kueleza kwamba, mwanaye hakuwahi kusoma sekondari Nairobi, nchini Kenya, kama mwanaye huyo alivyodai.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili mjini hapa jana, Francis Matey Mallya, ambaye ni baba mzazi wa Deus Mallya, alisema mwanaye hakuwahi kabisa kujiunga na shule yoyote ya sekondari ndani au nje ya nchi kwa vile hakuwa na uwezo wa kumsomesha masomo hayo.

Kijana huyo (27), ambaye ameshitakiwa kwa tuhuma za kuendesha gari bila leseni na kwa mwendo kasi uliosababisha kifo cha Wangwe, wiki iliyopita, alikaririwa na gazeti hili akidai kwamba, ana fani ya usanifu aliyoipata Nairobi katika Chuo cha Mtakatifu Hubert baada ya kumaliza sekondari kidato cha nne.

Hata hivyo, katika maelezo yake aliyoyatoa jana, Francis alisema anakumbuka kwamba, mwanaye alizaliwa mwaka 1983 katika Kijiji cha Kichare na kubatizwa kisha kusoma shule ya msingi Umbwe hadi darasa la saba.

“Kwa sababu mimi sikuwa na uwezo wa kumpeleka sekondari aliendelea kujisomea akawa ananunua vitabu vya kujisomea, lakini baadae akaondoka kwenda Dar es Salaam alikojifunza kozi ya kompyuta,” alisema Francis.

Francis alisema mwanaye alipita tu Nairobi alipokuwa akirejea kutoka nchini Libya, ambako hadi sasa hafahamu hasa shughuli iliyompeleka huko (Libya).

Mzee huyo, alisema aliporejea kutoka Libya, alishukia Nairobi ambako alikutana na rafiki yake waliorejea wote jijini Dar es Salaam.

Alisema anachofahamu ni kwamba kulikuwa na mtu ambaye hamfahamu, ambaye alikuwa akiwasiliana na mwanae kwa ajili ya kwenda Libya na alipokwenda hakufikisha wiki alirejea nchini.

Francis alisema mwanae aliweza kumudu vyema mafunzo ya kompyuta baada ya kupata mtu wa kumfundisha na baada ya kumudu mafunzo hayo alijishughulisha na kazi ya kutengeneza fulana, ambayo anaendelea kuifanya hadi sasa.

Alishutumu mwelekeo unaoanza kujitokeza wa kutaka kuhalalisha kuhusika kwa mwanae na kifo cha Wangwe.

“Kumuita mtoto wangu ni jasusi bila kumpa nafasi ya kumsikiliza wala vyombo vya dola havijathibitisha hilo ni kumhukumu, jambo ambalo ni kinyume cha katiba…wanamhukumu vipi kwa hisia?,” alihoji Francis.

Alidai kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ya kumuita mwanae ni jasusi, ina lengo la kuushawishi umma uamini mwanae anahusika na kifo cha Wangwe.

Francis ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Kichare katika kijiji cha Umbwe Sinde alisisitiza kilichotokea ni ajali kama ajali nyingine na suala hilo sasa liachiwe mahakama ambayo itachambua ushahidi na kujua lipi la kweli na lipi halina ukweli.

“Kwa muelekeo huu ninaouona, naomba taasisi zinazotoa msaada wa kisheria zisaidie kulinda haki ya mwanangu, ambaye tangu akamatwe hatuna mawasiliano naye na ndugu wamezuiwa kuonana naye,” alidai.

Akielezea tabia ya mwanae, alisema anamfahamu vyema na kwamba hajawahi kushika bunduki wala kisu achilia mbali kutembea na wahuni, bali alikuwa akifuata maadili mema ya Kanisa Katoliki.

Alisema anamfahamu mwanae kama mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchapisha maandishi na picha kwenye fulana na kazi hiyo ndio ambayo amekuwa akiifanya kwa ajili ya shule, makanisa na vyama vya siasa.

Alifafanua kuwa mara tu baada ya ajali, mwanae alimpigia simu akimuarifu kuwa alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam akiwa na mbunge mmoja, lakini kwa bahati mbaya gari imepata ajali na mbunge amefariki dunia.

“Aliniambia kuwa gari imepinduka mara sita na kujikuta nje ya gari akiwa hana simu yake ya mkononi huku akiwa na majeraha miguuni na kichwani na mbunge alifariki dunia papo hapo,” alidai Francis.

Aliendelea kusema kuwa: ”Alinitaka nisiwe na wasiwasi sana kwani hajaumia sana ila masikitiko yake ni kwamba mbunge amefariki…nilimuuliza nani alikuwa anaendesha gari akasema ni mbunge mwenyewe.”

Kwa mujibu wa Francis, hata wakati anakwenda kwake Dodoma mwanae alimpigia simu na kumjulisha kuwa anakwenda huko kikazi kwa wiki moja na baadae atarejea Dar es Salaam kabla ya kwenda tena Dodoma kwa kazi ya fulana.

Katika hatua nyingine, Ramadhan Semtawa anaripoti kutoka Dodoma kuwa Deus Mallya anayedaiwa kuwa dereva wa marehemu Wangwe, amezidi kugonganisha vichwa vya watu baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Juma Kilimba, kusema hamjui wala hana urafiki na kijana huyo.

Kauli hiyo ya Kilimba inapingana na ile aliyotoa Mallya kwamba anafahamiana vema na mbunge huyo kwani walikuwa wote katika safari yao ya kwenda Libya mwaka jana.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili nje ya viwanja vya Bunge mjini hapa jana, Kilimba alisema licha ya kutomfahamu pia alishangaa na hadi sasa hajui kijana huyo aliingiaje katika msafara wao wa kwenda Libya hapo mwaka jana.

Kilimba alifafanua kwamba, alisikia Mallya kwamba anamfahamu yeye (Kilimba), alishangaa na kuongeza kwamba: “Siyo urafiki tu, simjui na sijawahi kuwa na ukaribu naye.”

Hata hivyo, Kilimba aliongeza kwamba baada ya kusikia taarifa hizo alikumbuka kwamba wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Zurich, Uswisi, katika safari hiyo kuelekea Libya mwaka jana, kijana huyo aliwahi kusahau hati yake ya kusafiria kwenye ndege.

Alisema kwa kuwa walikuwa katika msafara mmoja, yeye (Kilimba), alishauri asaidiwe baada ya kuzuka tafrani ndipo kiongozi aliyeshughulikia safari hiyo akamsadidia kijana huyo na wala si yeye.

“Niliposikia huyo kijana ana nifahamu mimi, kwanza sikuwa na fikra kabisa kwamba kuna kijana kama huyo aliwahi kuwa rafiki yangu au namfahamu, nikakumbuka kumbe ahaa, ni yule ambaye aliwahi kusahau pasi ya safari yake ndani ya ndege tukiwa Zurich,”alisema Kilimba na akaongeza:

''Mimi nilikuwa Bussines Class yeye alikuwa Economy, sikuwa nikimfahamu, nilishangaa hata mimi pale Zurich kumuona yuko katika msafara, nilihoji na hadi sasa sijajua, aliingiaje katika msafara ule, ndiyo maana nakwambia simfahamu kabisa zaidi ya kuonana pale.''

Aliongeza kwamba, watu aliokuwa nao na aliowafahamu ni pamoja na Makongoro Nyerere ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mamuya, Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Simba, Shehe Seleman Kilemile na Hebron Mwakagenda, ambaye ni kutoka Leadership Forum.

Mallya alifunguliwa kesi namba TR 103/08, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa, kwa makosa ya kuvunja sheria za usalama barabarani, ambayo ni kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo cha Wangwe na kuendesha gari bila lesen
 
Nadhani hapa tunachanganya maada, Wangwe alikuwa jasiri kwa ujasiri unaoufahamu wewe.Lakini yeye kuwa shujaa haimaanishi ndio alielewana na kukubaliana na kila mtu.Kila mtu ana mapungufu yake na nguvu zake.Nguvu zake na uzuri wake havikuwa kinga ya yeye kutokutofautiana na wengine katika mambo mengine.uzungumzamvyo ni kana kwamba mlijua kuwa Wangwe atafariki kwa hiyo mlikuwa mnamtetea au kukubaliana na mawazo yake kwa sababu mlijua kuwa atakufa muda si mrefu! Haiwaletei wala hamtakuwa washindi kwa sababu mlikuwa upande wa Wangwe, lakini hii haimpi kushindwa au kuonekana mbumbumbu bwana Mbowe.

Yale aliyoaacha ni mazuri kwa Mbowe kuyafanyia kazi , maana sifa ya kiongozi ni kubadilika na kukubaliana na ukweli.Lakini pia si kwa sababu Wangwe allikuwa vile tunavyomfahamu ndio aonekane alikuwa sahihi kwa kila kitu.Hata baba wa kwanza wa TZ nae alikuwa na mambo mengi ambayo hakuelewana na wenzake.Kutokuelewana au kuelewana katika swala moja havipelekei ukawa dhaifu au na nguvu katika swala lingine.Narudia uzuri wa Wangwe haupelekei au haumkingi kuwa hakuwa na udhaifu katika maswala mengine.Hali kadhalika Mbowe kukosea sehemu moja haimaanishi kuwa ni dhaifu kiasi hicho, na wala haipelekei kuwa wewe nawe huko sahihi sana kiasi cha kuwa mawazo yako ni final!

If i were you, ningempa break Mbowe atafakari kipindi hiki kigumu kwake-ubinadamu uwepo.Kama unaona unaweza ukaandika chochote kwenye internet ili mradi kuandika tu, with your status in JF!.Yaani wewe mwenzetu vifo vyote unatoa rambirambi! yaani unataka mpaka mume aliyefiwa mkewe atoe rambirambi usikie wakati msiba nae unamhusu, kipimo cha upendo kwako wewe ni kutoa rambirambi wala sio hata kutoa hela ya Sanda,fedha za kula na kuitunza familia ya marehemu.Unataka aende redioni aseme ndio ufurahi-Hapa nimekudevalue

Give me a break


"The breath of accusation kills an innocent name, and leaves for lame acquittal the poor life, which is a mask without it" Percy Bysshe Shelley



Waberoya


Mkuu Waberoya,

Nakushauri upunguze matumizi ya rangi nyekundu katika posts zako; inaumiza macho kwa sisi tunaopenda kusoma word to word and between the lines. Asante!
 
Kwa muhistasari unasema kwa nini Mbowe? Jibu ni kwa sababu alimchezea rafu Marehemu. Chacha wangwe kwenye chama kabla ya kifo chacke na wala sio sababu nyingine yoyote.

Mtu mwenye akili yoyote akiona fujo zitatokea hata za kibaka anajiondoa kwa sababu hajui baada ya kibaka kupiga what next... wote waliojiondoa walijiondoa kwa sababu hiyo...

Swali lingine rahisi sana... kwani suspect mkubwa wa kifo cha Mh. Wangwe ni nani? Kwa vyovyote walikuwa wale waliokuwa na bifu naye... na sikumbuki kama serikali au bunge au CUF, TLP, NCCR walikuwa na bifu naye?

Safi Mkuu, lakini kama aliyekuwa na bifu ni Mbowe, na wananchi wakamlenga Mbowe, wale viongozi wengine walikimbia nini?
 
Kamaliza kozi gani?ile BBA ya jioni?

Natolea Mfano mmoja tu,kama leo Mnyika akifukuzwa CHADEMA tafanya nini??Je elimu aliyonayo itamsaidia nini?sababu hajawahi kuifanyia kazi..?mie nina uhakika leo ukimwambia mhe. Mnyika aelezee chochote kuhsu Macro Economix hataweza.

Mie namuona Mnyika kama Mwanasiasa ambaye anaweza kufanikwa kama kwanza akijiendeleza na shule ili apate exposure,wewe unadhani ni jambo la kumwadikia SMS RA ni siasa za kisasa au ni mambo ya kushangaza,huku ni kushindwa kwa hoja,

Do you know why Mkapa seems to be better than Muungwana in terms of implimentation of different Projects..achilia mbali mapungufu yake,

Kaka kweni Kikwete aliwahi fanyia kazi Dgree yake wapi kaka! Na sasa ndo Rais wako! Mbona unajichanganya mkuu!
 
Vijana wamtetea Deus Mallya




na Edward Kinabo



SIKU moja baada ya viongozi watatu kutoka kambi ya upinzani kuibua madai mazito kuhusu Deus Mallya, anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, vijana waliosoma naye Libya wamejitokeza kumtetea.

Steve Mbogo, mmoja wa vijana wanaomfahamu Mallya na aliyewahi kuwa naye nchini Libya, alisema alikuwa na mtuhumiwa huyo nchini Libya kwa mafunzo tofauti, lakini si ya kijasusi.

Mbogo ambaye ni mratibu wa taasisi ya Tanzania Development Initiative (TADIP), alisema madai yaliyotolewa na wenyeviti wa upinzani si ya kweli, kwani yeye na Mallya walikuwa miongoni mwa wawakilishi 20 kutoka Tanzania waliokwenda Tripoli, Libya Juni mwaka jana.

Alisema walikwenda Libya kushiriki mkutano wa kutoa mapendekezo kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, uliokuwa ufanyike nchini Ghana mwaka jana, kujadili ajenda ya kuwa na serikali moja ya Afrika.

Akifafanua zaidi, alisema mkutano huo ulishirikisha nchi mbalimbali za Afrika, mbali na Tanzania, na uliandaliwa na Ubalozi wa Libya kwa kushirikiana na asasi ya Revolutionary Committee Movement (RCM), yenye makao yake makuu nchini Libya.

Alisema wawakilishi wa mkutano huo, walipatikana kwa utaratibu wa kutuma maombi kwa uongozi wa matawi na wakala wa RCM kutoka katika nchi shiriki.

Aliongeza kuwa madai yaliyotolewa na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Augustine Mrema (TLP) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), yanashangaza, kwani mkutano huo wa Libya, ulichukua siku 20, na muda wote huo, walilala chumba kimoja na Mallya, lakini hakuwahi kumwona akitoroka mkutanoni kwenda kupata mafunzo ya ujasusi, kama ilivyodaiwa na wanasiasa hao.

“Haiingii akilini kuwa Mallya alikuwa Libya kwa mafunzo ya ujasusi, kwani mkutano uliotupeleka huko, ulikuwa na wawakilishi wengine 19 kutoka Tanzania, wakiwamo Sheikh Mkuu, Shaaban Simba, Juma Kilimba (Mbunge wa Iramba) na Makongoro Nyerere, watu ambao hawajawahi kutuhumiwa kwa ujasusi,” alisema.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo ana uhakika kuwa Mallya hakuwahi kuwa Libya kabla au baada ya mkutano huo, alisema kuwa hajui lolote kuhusu hilo.

Gazeti hili jana liliripoti tamko la wenyeviti wa CUF, NCCR-Mageuzi na TLP, ambao walidai kuwa wana ushahidi wa kutosha kwamba Mallya ni mmoja wa watu waliopata mafunzo makali ya kijasusi nchini Libya, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa, na ni mtaalamu wa hali ya juu wa kompyuta.

Viongozi hao walivitaka vyombo vya usalama kufanya utafiti wa kina juu ya suala hili, ili kubaini ukweli zaidi kuhusu Mallya, kwani inasemekana alikuwa dereva wa Wangwe, lakini wamebaini ni mtu aliyezoeana naye kwa muda mfupi sana, hali ambayo inaibua maswali mengi.

Utata kuhusu Mallya na nini kilitokea hata kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha Wangwe, ulisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimwandikie barua Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Said Mwema, kikitaka kufanyika uchunguzi wa kina.

CHADEMA pia ilimtaka IGP kuchunguza ukweli kuhusu maelezo ya Mallya na kujua ni wapi alikuwa amekaa wakati ajali ikitokea, na kuchukua hatua zinazopaswa, baada ya uchunguzi huo.

Mh! haya mambo naona yanazidi kujichanganya. Mzee wake anasema hakumaliza wiki Libya, huyu anasema ziara ilichukua siku ishirini. Which is which!!!!!!!!!!
 
Nimegundua,
Nimegundua kuwa KASHESHE na GEMBE ni watu wa Rostam Aziz. Mwanzo nilikuwa na shida sana kufahamu kuwa FMes anawajuaje watu wa RA? Kumbe ukisoma sana unakuja kufahamu msimamo wa mtu na maono yake. Ni vema na safi sana kuwa na watu kama hawa maana maishani ni lazima uwe na challenge. At least si wote tunakubaliana kwa kila kitu. Hii ni nzuri sana. Inafanya watu wawe wanafikiri mara mbili kabla ya kuandika. Mnafanya kazi nzuri sana anyway. Keep up. Nafikiri siku zinavyokwenda, nitaendelea kuwafahamu wengine.
 
baba yake hajui mtoto kasoma wapi....kisha tunaambiwa mtu wa kawaida!
 
haabri za mwanzo zilisema kuwa malya alisema alikaa Libya siku NNE tu! hapa tunaambiwa siku 20! ....something is wrong here.
 
Hivi CCM wana masilahi gani kwenye mgogoro wa CHADEMA? Kuna kitu gani kinaendelea hapa ?hebu someni habari hii ya Gazeti la Mwananchi la leo.


Date::8/4/2008
CCM yasambaza waraka wa Wangwe kuhusu mtafaruku wa Chadema
Frederick Katulanda, Mwanza

WAKATI kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Zakayo Wangwe, aliyefariki kwa ajali gari Julai 28 mwaka huu kinazidi kuleta utata, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamekuwa wakisambaza waraka wake wenye kurasa sita ukielezea jaribio la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kutaka kumvua wadhifa wake na uanachama.


Waraka huo umekuwa ukisambazwa kwa viongozi mbalimbali wa CCM ili kuwapatia ufahamu viongozi wake kujua kwa kina mgogoro huo wa Chadema ambao umekuwa ukihusishwa kama ndiyo chanzo cha sababu ya kifo cha mbunge huyo.


Waraka huo unaodaiwa kuwa umeandikwa na marehemu Wangwe mwenyewe, ingawa muda ambao alikuwa anakusudia kuutoa hadharani kwa wananchi na wanachama wa chama hicho kama sehemu ya kufafanua tuhuma ambazo anadaiwa kuhusika nazo na hata kuvuliwa wadhifa wake, hauainishwi.


Katika nakala ya waraka huo ukurasa wa nne, unaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza ulitumwa kutoka Dodoma Julai 27 mwaka huu majira ya saa 9:42 alasiri toka namba (026) 2322965 ambayo imeonyesha Kusajili kwa jina la ‘KATIBU MKUU CCM DOD' tarehe ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Wangwe kilichotokea akienda Dar es Salaam.


Kwa maana hiyo waraka huo ulianza kusambazwa mikoani kwa viongozi wa CCM siku moja kabla ya kifo cha Wangwe.


Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kwamba baada waraka huo kufika Dar es Salaam, ulianza kusambazwa kutoka Dar es Salaam kwa namba za faksi 2667457 iliyotanguliwa na kodi namba ya mkoa (022) ikimaanisha kutumwa kutoka Dar es Salaam Julai 31 mwaka huu majira ya saa 11:50 asubuhi mwenye kumiliki namba hiyo akitambuliwa kama SIGMA ICT.


Gazeti hili pia limebaini kuwa waraka huo umetumwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM mikoani, wakiwemo makatibu wa mikoa na wilaya pamoja na wengine ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaonyesha kwa kina mgogoro wa Chadema ulivyo.


Katika tamko hilo imeelezwa kuwa sababu zote zilizotolewa na kumvua wadhifa marehemu ni za uzushi na kwamba hata kikao kilichoketi kumjadili kilikuwa na jumla ya wajumbe 31 ambao nusu yake walikuwa wajumbe wasio na uhalali wa kupiga kura, lakini kati yao 24 walipiga kura kinyume cha Katiba ya Chadema.


Marehemu Wangwe ameeleza katika waraka huo kwamba, chama hicho kikiwa chini wa uongozi wa Mbowe na wafuasi wake kati ya Sh 374milioni zilizopatikana kama ruzuku kati ya Januari Mosi na Juni 30, mwaka huu Sh 350milioni zilitumika makao makuu ya chama na Sh25m tu ndizo zilizokwenda wilayani kuimarisha chama na kueleza mgao huo umekuwa ukitukuza chama makao makuu na kukidhalilisha chama nchi nzima.


''Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama dola za Kimarekani181,949.00 sawa na Sh 218,338,546 na mpaka sasa chama kimemlipa Sh175milioni. Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha wilayani na makao makuu, niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku, kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa

usimamizi wa pesa za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikali.


''Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibitishie pesa hizo anazodai alikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya Chadema kupitia hundi ipi na lini?'' ilieleza sehemu ya waraka huo.


Waraka huo pia umegusia suala lingine la uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum kwa kueleza kuwa Mbowe na wafuasi wake walighushi orodha ya majina badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


''Siyo siri, naamini hata Mbowe atakubaliana nami kuwa hili si moja ya siri anazodai nimevujisha,'' ilieleza sehemu ya waraka huo unaodaiwa kuwa wa marehemu Wange na kwamba chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa ubabe na misingi ya kikabila jambo ambalo alieleza litasababisha kukosa wananchama.


Katika hitimisho la waraka huo umeeleza kuwa: ''Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote kati ya hayo (yaliyoelezwa juu) nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mbowe na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli, kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na au vyombo vya habari, sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji kutoka makao makuu.''


Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kujitokeza wazi kusambaza waraka wa Chadema, ikiacha maswali kama ilipewa waraka huo na Wangwe au ndiyo ilikuwa ikishirikiana naye katika kuendesha harakati zake ndani ya chama hicho cha upinzani.

Source ;Mwananchi.
 
Gembe,
Sipo hapa kujisifu. Nimekaa nje ya Tanzania miaka mingi. Nimekuja kugundua kitu kimoja. Watu wengi huenda kusoma na kurudi Tanzania huku wakijiona wasomi. Wakati mwingine masomo hayo wangeliweza kuyasoma Tanzania ila nchi iliwapeleka nje. Sasa hapo swali, kwa nini kumpeleka mtu nje?
Unapokuwa nje, usisome tu shule na kufaulu na kurudi nyumbani. Nenda pia huko kwa wanyeji ukajifunze jinsi wanavyoishi, mila zao, utamaduni wao na angalia jambo gani utaweza kulichukua na kulileta NYUMBANI.
Katika kukaa nje, nimejifunza kuwa, elimu unayopata mitaani kwa wenyeji, ni kubwa sana kuliko unayopata darasani. Hivyo, kama uko SA tafadhali angalia na kuchunguza sana, hasa Wazungu maisha yao yakoje. Ukirudi na kwenda kuishi sehemu chafu, maji ya choo yanapita mbele ya nyumba yako nk, ujuwe hiyo shule yako SA haikukusaidia. Ukiwa huko ufumbuke macho. Usiwe mbele kumtetea RA kwa kila jambo hata kama jamaa kachemsha. Mtakuja aibika nyie watu vibaraka wa RA. Ukioana mambo mazito SI KUWA BUBU?
Jambo kubwa maishani nimejifunza ni hili:- KAMA WATANZANIA tungelikuwa na walau NUSU ya ushirikiano wa WAYAHUDI ..................

NB: Hivi Rais Reagan na Arnold Schwarzenegger ELIMU YAO imekaa kaaje?
Mandela pia ni nshomile hadi wapi?
Kama una pesa na unataka kusaidia watu wasome, tafuta watto yatima na msaidia mmoja mwenye uwezo hadi UDSM. Na Mungu atakubariki.

Ndugu yangu Sikonge maneno hayo hapo juu ni mazito sana...Kusema ukweli tutafutane ndugu yangu...Wewe ni mtu mwenye akili mingi sana wanafiki hawataki.

Watu wenye mawazo mazuri hawapewi kipaumbele Si unajuwa haufahamiki hapa na hukutokea sijui wapi?

Mimi nimepunguza kasi ya kuchangia lakini kwenye mijadala sivuki posting yako hata siku moja.

Moja tu ulighafilika kuhusu wachagga...Lakini OVERALL umeonyesha balance ya hali ya juu na MAPENZI DHABITI YA TAIFA LAKO...Na ni kweli huwezi kusema umetoka Ulaya kusoma halafu ukaenda kueendekeza mambo yasiyolenga kuiendeleza jamii na kuikwamua...Na badala yake kujidai wamesoma na mivyeti yao ya kutundika ukutani kama alivyosema Shalom....Licha ya kwamba Mnyika bado namsubiri kwa kauli yake ya kuhusu mashujaa...Hili halina maana kuwa machango wake Ushushwe na watu wenye chuki mbaya kama Gembe.
 
Nimegundua,
Nimegundua kuwa KASHESHE na GEMBE ni watu wa Rostam Aziz. Mwanzo nilikuwa na shida sana kufahamu kuwa FMes anawajuaje watu wa RA?

Kwa taarifa yako tu,

Yeye FMES anawajua watu wa RA?Nimekuja kujibu yale ambayo ni ya uongo mkubwa.

Mie siyo mtu wa Rostam na wala sijawahi kupewa pesa wala kutumika kumtetea RA.RA ni mtu wa kawaida sana kwangu na ndiyo maana wakati mwingine huwa nampinga kwa baadhi ya mambo ambayo yana maslahi ya kitaifa.

Ila la kumzushia Rostam jambo la uongo lazima nimtete,na hata wakati wa suala la kanisa nilisimama kidete sababu najua wajibu wa kanisa kwa watu wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom