Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Nimegundua,
Nimegundua kuwa KASHESHE na GEMBE ni watu wa Rostam Aziz. Mwanzo nilikuwa na shida sana kufahamu kuwa FMes anawajuaje watu wa RA? Kumbe ukisoma sana unakuja kufahamu msimamo wa mtu na maono yake. Ni vema na safi sana kuwa na watu kama hawa maana maishani ni lazima uwe na challenge. At least si wote tunakubaliana kwa kila kitu. Hii ni nzuri sana. Inafanya watu wawe wanafikiri mara mbili kabla ya kuandika. Mnafanya kazi nzuri sana anyway. Keep up. Nafikiri siku zinavyokwenda, nitaendelea kuwafahamu wengine.

Nakuunga mkono Sikonge...Naona mgagagigikoko anavuta pumzi yeye...Mimi licha a kutokuelewana na chadema...Bado niko HURU...Hawa mafisadi hawataruhusiwa kuviangusha vyama vya kisiasa na pia kununuwa UHURU WETU.
Ndio maana nilitabiri toka mwanzo kuwa uwezekano wa kupigia debe mgombea binafsi ni mkubwa sana na watanzania wajiandae na maswali ya kuwa mtu watakayempa Urais awe na sifa gani...Ikifika karibia na wakati huo...Basi nitaanzisha mada ya SIFA ZA RAIS WA TANZANIA 2010...Sifa ambazo ni jf peke yake watakaozijadili ili tupate mtu safi asiye FISADI.
 
Kwa taarifa yako tu,

Mie siyo mtu wa Rostama ila ni mtu wa CCM

Wewe si tu kuwa una mwelekeo wa kifsadi...Hata hiyo picha yako hapo juu inatupa tabu wengine kwani ni picha yenye kuamsha HASIRA DHIDI MIZIMU YA UFISADI AMBAYO imeli HUNT TAIFA LETU KIASI CHA MWALIMU KUANDIKA KITABU CHA UONGOZI WA JK NA HATMA YA TZ!
Wewe Gembe ni KICHEFU CHEFU!
 
dah kweli kazi,field marshal alisema hii forum ina vichwa na pia ina vilaza,kwakuongezea tu pia tuna watu wasio na msimamo katika maamuzi yao.Alidai hatochangia tena mjadala huu kwasababu anazozijua yeye ghafra huyo karudi,tuwe na misimamo jamani na sio kukurupa tu
 
Gembe mimi nimerudi kwasababu yako maana nimeshatapika MARA MBILI kwasababu yako!
Na ili nisiendelee KUTAPIKA...Itanibidi niache kusoma jf...Na nikiacha kusoma jf nitasoma nini?
Majira?
 
Jamani hapo alicho nena mkuu wa msafala kipo wazi kabisa inadhihilisha kabisa wao walilakiwa na mabango na si malungu.mishare na sime hivi TBC walirusha hawa vijana wakiwa wamebeba marungu na hizo silaha za jadi?
Mabango waliyo yakuta waheshimiwa yaliwaogofya na si sime wengi wanavyo dai,kama kungalikuwa na hizo siraha za jadi huyu kiongozi wa msafara si angesema...!kwa hiyo kuna watu wachache ndo wanapotosha uhalisia wa mambo yalivyo kuwa kule.
 
dah kweli kazi,field marshal alisema hii forum ina vichwa na pia ina vilaza,kwakuongezea tu pia tuna watu wasio na msimamo katika maamuzi yao.Alidai hatochangia tena mjadala huu kwasababu anazozijua yeye ghafra huyo karudi,tuwe na misimamo jamani na sio kukurupa tu

Kiroboto unasema NILIDAI SITACHANGIA TENA?

Kwi kwi kwi...Kumbe ndio maana mlitaka kunifungia?

JMUSHI HANA CHAMA...JMUSHI IS FREE!

Cha kunishangaza kuna wana ccm ambao wanakubaliana sana na chadema wakati huu...And vice versa...Hii inaonyesha kuna mapandikizi both sides...Ama pia kifo kinataka kutumiwa na both sides kwa sababu za KISIASA...

Kujitowa kwangu ni baada ya mwelekeo wa UKABILA ambao tumeushinda...

Sasa tunataka mweleko mwingine..Mwelekeo wa HAKI NA UKWELI....

Mwelekeo wa KISAYANSI KUHUSIANA NA VIFO TATA NA REALITY NA SI PROPAGANDA ZA KISIASA...YOU SOUND LIKE A RAT MAN!

You is A RAT RACE?

MIMI NI BANTU MAN....Rasta and AFRIKA IS ONE!

UPO?
 
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza kwenye mjadala huu, na haswa baada ya Kiranja kuweka post zake ,naona kuna baadhi ya watu wameloose control mpaka inafika mahali wanajitambulisha kuwa wao sio A bali ni B wakati siku zote walikuwa wanajionyesha kama ni Neutral.

Heri walio upande fulani na maandishi yao yanasema hivyo kuliko walio upande fulani halafu wanaona aibu kutetea misimamo yao, naamini kuwa baada ya siku zinavyokwenda patachorwa mstari na nani ni nani kujulikana ama kwa matendo au kwa maandishi yake.
 
cha kushangaza kuna chadema na ccm wanaoshirikiana kusema ni mpango wa Mungu na ni ajali.

Halafu kuna chadema wanaosema ni ccm na RA.

Pia kuna ccm wanaosema ni Mbowe na chadema.

HALAFU KUNA WATU HURU KAMA SISI AMBAO TUNASEMA UKWELI UKO KWENYE UCHUNGUZI HURU....NA SHAHIDI WA KUTOWA MAELEZO HAYO NI KIJANA HUYO MWENYE UHUSIANO NA BOTH chadema na ccm....Kwa mtizamo wangu...Mtu huru ni yule ambaye hakuwa na uhusiano na BOTH PARTIES....Na ambaye HAKI KWAKE SI KUKIRIDHISHA CHAMA CHOCHOTE KILE CHA KISIASA.

TUNASUBIRIA NA HAKIKA HAPATAHARIBIKA KITU...UNLESS NIFUNGIWE, JF IFUNGIWE, AMA NISIWEPO DUNIANI.

ZAIDI YA HAPO...ALUTA CONTINUA FOR THE FREEDOM CAUSE!

God willing...WE THE PEOPLE...WE WILL BE VICTORIOUS!
 
Date::8/4/2008
CCM yasambaza waraka wa Wangwe kuhusu mtafaruku wa Chadema
Frederick Katulanda, Mwanza
Mwananchi

WAKATI kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Zakayo Wangwe, aliyefariki kwa ajali gari Julai 28 mwaka huu kinazidi kuleta utata, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamekuwa wakisambaza waraka wake wenye kurasa sita ukielezea jaribio la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kutaka kumvua wadhifa wake na uanachama.

Waraka huo umekuwa ukisambazwa kwa viongozi mbalimbali wa CCM ili kuwapatia ufahamu viongozi wake kujua kwa kina mgogoro huo wa Chadema ambao umekuwa ukihusishwa kama ndiyo chanzo cha sababu ya kifo cha mbunge huyo.

Waraka huo unaodaiwa kuwa umeandikwa na marehemu Wangwe mwenyewe, ingawa muda ambao alikuwa anakusudia kuutoa hadharani kwa wananchi na wanachama wa chama hicho kama sehemu ya kufafanua tuhuma ambazo anadaiwa kuhusika nazo na hata kuvuliwa wadhifa wake, hauainishwi.

Katika nakala ya waraka huo ukurasa wa nne, unaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza ulitumwa kutoka Dodoma Julai 27 mwaka huu majira ya saa 9:42 alasiri toka namba (026) 2322965 ambayo imeonyesha Kusajili kwa jina la ‘KATIBU MKUU CCM DOD’ tarehe ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Wangwe kilichotokea akienda Dar es Salaam.

Kwa maana hiyo waraka huo ulianza kusambazwa mikoani kwa viongozi wa CCM siku moja kabla ya kifo cha Wangwe.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kwamba baada waraka huo kufika Dar es Salaam, ulianza kusambazwa kutoka Dar es Salaam kwa namba za faksi 2667457 iliyotanguliwa na kodi namba ya mkoa (022) ikimaanisha kutumwa kutoka Dar es Salaam Julai 31 mwaka huu majira ya saa 11:50 asubuhi mwenye kumiliki namba hiyo akitambuliwa kama SIGMA ICT.

Gazeti hili pia limebaini kuwa waraka huo umetumwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM mikoani, wakiwemo makatibu wa mikoa na wilaya pamoja na wengine ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaonyesha kwa kina mgogoro wa Chadema ulivyo.

Katika tamko hilo imeelezwa kuwa sababu zote zilizotolewa na kumvua wadhifa marehemu ni za uzushi na kwamba hata kikao kilichoketi kumjadili kilikuwa na jumla ya wajumbe 31 ambao nusu yake walikuwa wajumbe wasio na uhalali wa kupiga kura, lakini kati yao 24 walipiga kura kinyume cha Katiba ya Chadema.

Marehemu Wangwe ameeleza katika waraka huo kwamba, chama hicho kikiwa chini wa uongozi wa Mbowe na wafuasi wake kati ya Sh 374milioni zilizopatikana kama ruzuku kati ya Januari Mosi na Juni 30, mwaka huu Sh 350milioni zilitumika makao makuu ya chama na Sh25m tu ndizo zilizokwenda wilayani kuimarisha chama na kueleza mgao huo umekuwa ukitukuza chama makao makuu na kukidhalilisha chama nchi nzima.

''Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama dola za Kimarekani181,949.00 sawa na Sh 218,338,546 na mpaka sasa chama kimemlipa Sh175milioni. Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha wilayani na makao makuu, niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku, kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa pesa za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikali.

''Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibitishie pesa hizo anazodai alikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya Chadema kupitia hundi ipi na lini?'' ilieleza sehemu ya waraka huo.

Waraka huo pia umegusia suala lingine la uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum kwa kueleza kuwa Mbowe na wafuasi wake walighushi orodha ya majina badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

''Siyo siri, naamini hata Mbowe atakubaliana nami kuwa hili si moja ya siri anazodai nimevujisha,'' ilieleza sehemu ya waraka huo unaodaiwa kuwa wa marehemu Wange na kwamba chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa ubabe na misingi ya kikabila jambo ambalo alieleza litasababisha kukosa wananchama.

Katika hitimisho la waraka huo umeeleza kuwa: ''Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote kati ya hayo (yaliyoelezwa juu) nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mbowe na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli, kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na au vyombo vya habari, sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji kutoka makao makuu.''

Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kujitokeza wazi kusambaza waraka wa Chadema, ikiacha maswali kama ilipewa waraka huo na Wangwe au ndiyo ilikuwa ikishirikiana naye katika kuendesha harakati zake ndani ya chama hicho cha upinzani.
 
cha kushangaza kuna chadema na ccm wanaoshirikiana kusema ni mpango wa Mungu na ni ajali.

Halafu kuna chadema wanaosema ni ccm na RA.

Pia kuna ccm wanaosema ni Mbowe na chadema.

HALAFU KUNA WATU HURU KAMA SISI AMBAO TUNASEMA UKWELI UKO KWENYE UCHUNGUZI HURU....NA SHAHIDI WA KUTOWA MAELEZO HAYO NI KIJANA HUYO MWENYE UHUSIANO NA BOTH chadema na ccm....Kwa mtizamo wangu...Mtu huru ni yule ambaye hakuwa na uhusiano na BOTH PARTIES....Na ambaye HAKI KWAKE SI KUKIRIDHISHA CHAMA CHOCHOTE KILE CHA KISIASA.

TUNASUBIRIA NA HAKIKA HAPATAHARIBIKA KITU...UNLESS NIFUNGIWE, JF IFUNGIWE, AMA NISIWEPO DUNIANI.

ZAIDI YA HAPO...ALUTA CONTINUA FOR THE FREEDOM CAUSE!

God willing...WE THE PEOPLE...WE WILL BE VICTORIOUS!

Hivi wewe asee Mushi ni chama gani???????
 
Date::8/4/2008
Babake mzazi wa Mallya azidi kuchanganya mambo

Na Daniel Mjema, Moshi
Mwananchi

BABA mzazi wa kijana aliyekuwa na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe (Chadema) kwenye gari lililosababisha kifo chake, amezidi kuchanganya mambo baada ya kueleza kwamba, mwanaye hakuwahi kusoma sekondari Nairobi, nchini Kenya, kama mwanaye huyo alivyodai.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili mjini hapa jana, Francis Matey Mallya, ambaye ni baba mzazi wa Deus Mallya, alisema mwanaye hakuwahi kabisa kujiunga na shule yoyote ya sekondari ndani au nje ya nchi kwa vile hakuwa na uwezo wa kumsomesha masomo hayo.

Kijana huyo (27), ambaye ameshitakiwa kwa tuhuma za kuendesha gari bila leseni na kwa mwendo kasi uliosababisha kifo cha Wangwe, wiki iliyopita, alikaririwa na gazeti hili akidai kwamba, ana fani ya usanifu aliyoipata Nairobi katika Chuo cha Mtakatifu Hubert baada ya kumaliza sekondari kidato cha nne.

Hata hivyo, katika maelezo yake aliyoyatoa jana, Francis alisema anakumbuka kwamba, mwanaye alizaliwa mwaka 1983 katika Kijiji cha Kichare na kubatizwa kisha kusoma shule ya msingi Umbwe hadi darasa la saba.

"Kwa sababu mimi sikuwa na uwezo wa kumpeleka sekondari aliendelea kujisomea akawa ananunua vitabu vya kujisomea, lakini baadae akaondoka kwenda Dar es Salaam alikojifunza kozi ya kompyuta," alisema Francis.

Francis alisema mwanaye alipita tu Nairobi alipokuwa akirejea kutoka nchini Libya, ambako hadi sasa hafahamu hasa shughuli iliyompeleka huko (Libya).

Mzee huyo, alisema aliporejea kutoka Libya, alishukia Nairobi ambako alikutana na rafiki yake waliorejea wote jijini Dar es Salaam.

Alisema anachofahamu ni kwamba kulikuwa na mtu ambaye hamfahamu, ambaye alikuwa akiwasiliana na mwanae kwa ajili ya kwenda Libya na alipokwenda hakufikisha wiki alirejea nchini.

Francis alisema mwanae aliweza kumudu vyema mafunzo ya kompyuta baada ya kupata mtu wa kumfundisha na baada ya kumudu mafunzo hayo alijishughulisha na kazi ya kutengeneza fulana, ambayo anaendelea kuifanya hadi sasa.

Alishutumu mwelekeo unaoanza kujitokeza wa kutaka kuhalalisha kuhusika kwa mwanae na kifo cha Wangwe.

"Kumuita mtoto wangu ni jasusi bila kumpa nafasi ya kumsikiliza wala vyombo vya dola havijathibitisha hilo ni kumhukumu, jambo ambalo ni kinyume cha katiba…wanamhukumu vipi kwa hisia?," alihoji Francis.

Alidai kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ya kumuita mwanae ni jasusi, ina lengo la kuushawishi umma uamini mwanae anahusika na kifo cha Wangwe.

Francis ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Kichare katika kijiji cha Umbwe Sinde alisisitiza kilichotokea ni ajali kama ajali nyingine na suala hilo sasa liachiwe mahakama ambayo itachambua ushahidi na kujua lipi la kweli na lipi halina ukweli.

"Kwa muelekeo huu ninaouona, naomba taasisi zinazotoa msaada wa kisheria zisaidie kulinda haki ya mwanangu, ambaye tangu akamatwe hatuna mawasiliano naye na ndugu wamezuiwa kuonana naye," alidai.

Akielezea tabia ya mwanae, alisema anamfahamu vyema na kwamba hajawahi kushika bunduki wala kisu achilia mbali kutembea na wahuni, bali alikuwa akifuata maadili mema ya Kanisa Katoliki.

Alisema anamfahamu mwanae kama mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchapisha maandishi na picha kwenye fulana na kazi hiyo ndio ambayo amekuwa akiifanya kwa ajili ya shule, makanisa na vyama vya siasa.

Alifafanua kuwa mara tu baada ya ajali, mwanae alimpigia simu akimuarifu kuwa alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam akiwa na mbunge mmoja, lakini kwa bahati mbaya gari imepata ajali na mbunge amefariki dunia.

"Aliniambia kuwa gari imepinduka mara sita na kujikuta nje ya gari akiwa hana simu yake ya mkononi huku akiwa na majeraha miguuni na kichwani na mbunge alifariki dunia papo hapo," alidai Francis.

Aliendelea kusema kuwa: "Alinitaka nisiwe na wasiwasi sana kwani hajaumia sana ila masikitiko yake ni kwamba mbunge amefariki…nilimuuliza nani alikuwa anaendesha gari akasema ni mbunge mwenyewe."

Kwa mujibu wa Francis, hata wakati anakwenda kwake Dodoma mwanae alimpigia simu na kumjulisha kuwa anakwenda huko kikazi kwa wiki moja na baadae atarejea Dar es Salaam kabla ya kwenda tena Dodoma kwa kazi ya fulana.

Katika hatua nyingine, Ramadhan Semtawa anaripoti kutoka Dodoma kuwa Deus Mallya anayedaiwa kuwa dereva wa marehemu Wangwe, amezidi kugonganisha vichwa vya watu baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Juma Kilimba, kusema hamjui wala hana urafiki na kijana huyo.

Kauli hiyo ya Kilimba inapingana na ile aliyotoa Mallya kwamba anafahamiana vema na mbunge huyo kwani walikuwa wote katika safari yao ya kwenda Libya mwaka jana.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili nje ya viwanja vya Bunge mjini hapa jana, Kilimba alisema licha ya kutomfahamu pia alishangaa na hadi sasa hajui kijana huyo aliingiaje katika msafara wao wa kwenda Libya hapo mwaka jana.

Kilimba alifafanua kwamba, alisikia Mallya kwamba anamfahamu yeye (Kilimba), alishangaa na kuongeza kwamba: "Siyo urafiki tu, simjui na sijawahi kuwa na ukaribu naye."

Hata hivyo, Kilimba aliongeza kwamba baada ya kusikia taarifa hizo alikumbuka kwamba wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Zurich, Uswisi, katika safari hiyo kuelekea Libya mwaka jana, kijana huyo aliwahi kusahau hati yake ya kusafiria kwenye ndege.

Alisema kwa kuwa walikuwa katika msafara mmoja, yeye (Kilimba), alishauri asaidiwe baada ya kuzuka tafrani ndipo kiongozi aliyeshughulikia safari hiyo akamsadidia kijana huyo na wala si yeye.

"Niliposikia huyo kijana ana nifahamu mimi, kwanza sikuwa na fikra kabisa kwamba kuna kijana kama huyo aliwahi kuwa rafiki yangu au namfahamu, nikakumbuka kumbe ahaa, ni yule ambaye aliwahi kusahau pasi ya safari yake ndani ya ndege tukiwa Zurich,"alisema Kilimba na akaongeza:

''Mimi nilikuwa Bussines Class yeye alikuwa Economy, sikuwa nikimfahamu, nilishangaa hata mimi pale Zurich kumuona yuko katika msafara, nilihoji na hadi sasa sijajua, aliingiaje katika msafara ule, ndiyo maana nakwambia simfahamu kabisa zaidi ya kuonana pale.''

Aliongeza kwamba, watu aliokuwa nao na aliowafahamu ni pamoja na Makongoro Nyerere ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mamuya, Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Simba, Shehe Seleman Kilemile na Hebron Mwakagenda, ambaye ni kutoka Leadership Forum.

Mallya alifunguliwa kesi namba TR 103/08, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa, kwa makosa ya kuvunja sheria za usalama barabarani, ambayo ni kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo cha Wangwe na kuendesha gari bila leseni.
 
Kifo hiki kweli cha kisiasa...Na kama kweli kauwawa...Basi ni muhimu sana kumjuwa muuwaji kwani ana nia mbaya sana na TAIFA LETU!

Na pia nashangazwa na sisi kuendelea kupingana na familia ya marehemu...Kwani Ballali si alisababishwa nikatukanwa hapa na ndugu zake kwa kujidai kukomalia kifo chake?

Sasa kwanini uamuzi wa ndugu zake marehemu Wangwe hauheshimiwi kama ule wa ndugu za Ballali akiwemo mke wake Anna Muganda Ballali kuheshimiwa?

DOUBLE STANDARD NI MBAYA KWASABABU YA SIASA NA TAMAA ZA MADARAKA!

Kama ndugu na baadhi ya viongozi wa chadema walishasema ni ajali ya kawaida...Then siasa ambazo zinachochewa na vyama vyote viwili zina mpango gani?

chadema walitia shaka sana pale waliposhindwa namna ya kudeal na issue ya Wangwe...Sasa migogoro ya Kitaifa wataiwezea wapi kama kifo cha mwanachama wao ama hata vurugu zake na madai yake ya kisiasa hayakuweza kufanyiwa kazi?

Binafsi mimi naona kuna baadhi ya viongozi wa chadema wanataka chama kianguke kwasababu ya tamaa za madaral...madaraka si sababu ya kubaguana kiasi hicho...Sijuwi utofauti wa Wangwe na viongozi hao wa ccm/chadema ulisababishwa na nini...Na kama issue yake ya ukabila haikuwa na nguvu...Kwanini issue ya kifo chake iwe na nguzu za kukiangusha chama na kuwa HUNT KIASI HIKI?

Ukweli wa Ballali utafunuwa mengi sana.
 
Kuna kitu kikubwa sana kitakuja kufahamika siku za usoni kwani kitendo cha kusamabaza waraka huo siku moja kabla ya kifo cha marehemu kuna mkono wa mtu kama nilivyosema hapo awali.

Pili Nilisema na nitaendelea kusema kuwa kwenye hili RA hawezi kuepuka kuhusika kwake,pia kuna mkono wa Makamba na haswa baada ya Wangwe kukutana na Makamba na kuandaa mkakati husika.

Huu waraka ni wa kupikwa kwani hauna saini ya Wangwe japo alishiriki kwenye kuuandaa ila hajausaini, nawashauri CHADEMA waende mahakamani na kulishitaki gazeti la majira ili ukweli uweze kupatikana kuwa huu waraka aliuandaa nani na kwa masilahi ya nani.

Mbowe anapaswa kuwa makini zaidi kwani mkakati wote huu ni kukidhoofisha chama chake ,na hata yeye pia,

Mbatia ajiepushe kutumbukia kule alikotumbukia Mtikila na haswa alipokuwa anaandikia gazeti la HOJA na kujifanya kuwa yeye ni Paul Kyara , na kama ilivyotokea wiki iliyopita Makala moja iliandikwa na mwandishi wa habari wa TBC Taifa ,chini ilionyesha jina lake ila juu ilionyesha jina la Kyara, fuatilieni haya mambo kwani makakati ni mkubwa na mbaya dhidi ya CHADEMA.
 
Kwa taarifa yako tu,

Yeye FMES anawajua watu wa RA?Nimekuja kujibu yale ambayo ni ya uongo mkubwa.

Mie siyo mtu wa Rostam na wala sijawahi kupewa pesa wala kutumika kumtetea RA.RA ni mtu wa kawaida sana kwangu na ndiyo maana wakati mwingine huwa nampinga kwa baadhi ya mambo ambayo yana maslahi ya kitaifa.

Ila la kumzushia Rostam jambo la uongo lazima nimtete,na hata wakati wa suala la kanisa nilisimama kidete sababu najua wajibu wa kanisa kwa watu wake.

Sawa tusihukumu ila hilo la usomi umetia aibu kubwa. Kama ni msomi wa mlimani unashindwa kujua tanzania yako! sasa usomi wa nani? kujua SA na USA? Umefilisika kifikra kaka. Pole sana, kwani hujui syllabus za vyuo zinatofautina? sababu unaijua? Please check then utanieleza.

Hili ulisema uwongo nalo lisemee kaka
 
mmh ...ccm kweli kiboko! nia yamaendeleo kwa wananchi haipo akili mwao kabisa.....tutafika kweli wajameni?
 
Date::8/4/2008
Kifo cha Wangwe usiwe mtaji wa kisiasa
Mwananchi

MLOLONGO wa mambo unaotokea hivi sasa baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe, unatoa picha moja ya wazi kwa wanasiasa, kwamba wanataka kutumia kifo hicho kupandisha umaarufu wao wa kisiasa.

Wapo wanasiasa wanaotumia kifo hicho kwa nia ya kuchafuana, wapo wengine ambao wanaamini kwamba sasa wamepata kitu cha kuzungumza, kwa sababu kwao siasa ni mikutano na waandishi wa habari, hata kama wameshindwa kuendesha siasa kwa maana ya kusaka wanachama na kutafuta nafasi za kuchanguliwa na wananchi.

Kwa kifupi, wanasiasa wetu wanatia aibu. Wanadhani kwamba kuzusha mambo, kuwapakazia wenzao katika majonzi haya watakuwa wamejiinua kisiasa na hivyo kupata kukubalika zaidi machoni mwa wananchi.

Tunaamini kwamba, kama kweli wanasiasa hawa ambao kila mmoja ameibukia kuwa mtaalam wa kumfahamu vilivyo Deus Mallya, dereva aliyekuwa anaendesha gari iliyopata ajali na kumuua Wangwe na kama kweli wangekuwa na taarifa za maana kuhusu kijana huyu ambaye tayari amekwisha kufunguliwa mashitaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, wangekuwa ama wametoa taarifa hizo kwa polisi au hadharani kupitia kwenye vyombo vya habari.

Lakini la muhimu zaidi, wanasiasa hawa kusubiri hadi vyombo vya habari vifanye kazi yake kwa kufuatilia na kubaini kwamba Mallya ndiye aliyeendesha gari lililomuua Wangwe, pamoja na taarifa nyingine za kina ambazo zimekwisha kutolewa na magazeti yapata wiki sasa ndipo wajitokeze, ni kudandia mambo ambayo hayawezi kutuongezea tija katika kupambana na uhalifu nchini.

Yapo mambo ya msingi ambayo viongozi wa vyama vya siasa wanapaswa kuwaongoza wananchi kudai kutoka kwa watawala, mathalan, suala la watuhumiwa wa ufisadi kuendelea kutesa, mbona wanasiasa hawa hawaonekani kuchukua dhima ya kuwaunganisha wananchi ili wadai uwajibikaji kutoka serikalini juu ya hili?

Tunaheshimu na kutambua mchango wa wanasiasa katika kushinikiza mabadiliko ndani ya serikali kwa kutaka kuwako kwa uwajibikaji zaidi, lakini katika msiba wa Wangwe tunadhani wanataka kutafuta mtaji mahali ambapo haupatikani. Kama kuna mwenye ushahidi wowote unaoweza kuisadia polisi waupeleke sasa, mbwembwe za mikutano na waandishi wa habari haziwezi kutuvusha.
 
Kwa taarifa yako tu,

Yeye FMES anawajua watu wa RA?Nimekuja kujibu yale ambayo ni ya uongo mkubwa.

Mie siyo mtu wa Rostam na wala sijawahi kupewa pesa wala kutumika kumtetea RA.RA ni mtu wa kawaida sana kwangu na ndiyo maana wakati mwingine huwa nampinga kwa baadhi ya mambo ambayo yana maslahi ya kitaifa.

Ila la kumzushia Rostam jambo la uongo lazima nimtete,na hata wakati wa suala la kanisa nilisimama kidete sababu najua wajibu wa kanisa kwa watu wake.


Acha kusema sema sana, huwezi kujinasua eti hujawahi kupewa pesa wakati huko uliko Cape umeenda kwa nguvu za huyo huyo RA, na hili ndio tatizo la vijana wetu kuwa hawataki kusema ukweli kwa masilahi ya taifa ila wanasema kujiridhisha wao binafsi.
 
Interesting.....

Duh!
Mke wa KATI wamarehemu naye PANDIKIZI?
Maana kama na yeye alikuwa akiishi naye...Kwanini alimkaribisha NYOKA nyumbani kama alikuwa hamjui?
Nani alianza kumjuwa Nyoka kati ya marehemu na mkewe wa KATI?
Kaazi kweli kweli...Maana maslahi ni mengi na wake ni wengi..Sasa hata huto tujimali twa marehemu nato tuko kwenye kasheshe...Sasa usikute mke mdogo anajuwa ya RA na labda mali hizo ni za KUHONGWA..HAPO HATAKUBALI KUZIACHIA!
Kazi ipo.
 
Tutapona kweli mwaka huu?kama hali ndio hii na mambo yenyewe ndio haya,kama wanaweza kusambaza waraka inadvance......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom