Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
MKUU mwita...WAAFRIKA WAKWELI WENYE NIA NZURI NA AFRIKA MNAWAJUWA...Nyie msibaki kwenye propaganda za vyama kabisa na msisikilize propaganda zenye kujali maslahi ya chama cha kisiasa...Na ndio maana ni muhimu mpiganie wagombea binafsi...Kwani inawezekana wakawa na mawazo mazuri toka BOTH parties kwasababu UHURU WAO HAUTAWABANA NA MASLAHI YA CHAMA!

Mkuu Mwita...Ni lazima msiwe wafuata mkumbo ama mashabiki tu.

Wekeni sifa za kiongozi ajaye na yale tunayotaka viongozi wetu watufanyie...Baada ya hapo ni rahisi sana kutafuta yule anaye fit kwenye hizo qualifications zetu tutakazozijadili za UZALENDO.

Jmush1,
Sasa kwa kuanzia tuanzie wapi kama humu kwenye vyama ni pumba mtupu? lakini usisahau kuwa ccm ndiyo wanazidi kuiuza nchi!
 
++bado

Mwana wasu,
Sijakuelewa, unataka kusema bado hatumpata yesu wetu? ama unamaanisha nini?

YEEEH mwana wasu kamaa kazi !!!

Wengi watakuja na Kusema mimi ndiye mkombozi wa Taifa hili na watawafanyia miujiza mingi ili mpate kuamini yakua wao ndio.Lakini mmetahadharishwa mjiepushe nayo maana siku ile watawalalua kama kifaru.
 
Tutawajuaje? kwani rangi zao zaonekana kuwa njema sijui tutawatambuaje,
 
Ndio tunachofanya hapa...Kama kiongozi akikubaliwa na jf...TANURU HILI LA MOTO....Basi atakuwa chuma cha puwa chenye kustahili kuliongoza Taifa...Maana hapa jf kuna watu wenye uwezo wa kuwatetea wananchi zaidi hata ya wabunge UCHWARA.....Basi ni wazi akijadiliwa kiongozi hapa na kupitishwa...HUYO NI LAZIMA ATAKUWA MTEULE...Kwasababu uzito wa jf unajulikana na ndio maana ilifungiwa kwa madai ya UGAIDI!
Kila kitu kiko hapa na kuchaguwa kiongozi mzuri kutaanzia hapa!

Jmushi ni kweli kabisa
Mgombea binafsi kuna viashiria vya kuleta tija

Samahani Mwl Kitila kwa kukutolea mfano
Mwl Kitila ana uwezo na miono mizuri ila ila ila Tatizo lake amefungamana na chama.
Nafikiri huyu akisimama kama mgombea Binafsi ataleta tija kwa watanzania

Yupo pia Mtanzania
Naye ana maono yakuleta tija japo hana chama ,lakini akiungana na chama lazima watamgeuza kimawazo.
 
Tutawajuaje? kwani rangi zao zaonekana kuwa njema sijui tutawatambuaje,

tumepewa macho ya kuona,masikio ya kusikia na akili ya kutambua mema na mabaya.
Nakumbuka hakuna neno wala jambo ambalo laweza tokea kwa ajali ama bahati mbaya mambo yote huruhusiwa na BWana ili yapate kutokea na kwake kondoo wapate kujifunza.
 
Ni wazi kwamba CHADEMA tumetikiswa. Ama tutaanguka au la, itategemea tutakavyo-handle matukio baada ya msiba huu. Kwa maoni yangu njia pekee ya kusimama ni kuwa wa kweli, na inabidi tuwe wa kweli katika mambo makubwa manne yafuatayo:

Mkuu Kitila,

Maneno mazito sana, ninaomba kuongeza kidogo kwamba ufike wakati Chadema, waamke na kuona kwa macho mawili kwamba as long as huu mjadala wa Wangwe unaendelea kati yao na CCM, ni advantage kubwa sana kwa CCM, kwa sababu kwa mara ya kwanza Chadema nayo inaanza kuwekewa mashaka na wananchi, kitu ambacho ni kawaida kwa CCM,

It is about time sasa, Chadema wakatafuta a new subject ya kuiondoa hii ya Wangwe, kwa sababu the more inasimama na wao kujiingiza kurushiana maneno ya propaganda na CCM, ni the more wana-sink kwenye Public Opinion na ni kwa sababu moja nzito sana ya kumsimamisha Makamu Wa Mwenyekiti wao, in only seven months toka achaguliwe, na hasa kitendo cha baadhi ya viongozi wao wa juu kujiingiza kwenye vita vya propaganda na marehemu, alipokuwa hai, wananchi hupenda the under dog hiyo ni sheria ya siasa na michezo dunia nzima, ingawa hufuraia sana the top dog akishinda, lakini hufurahi zaidi the underdog akishinda, hapa the under dog Wangwe ameshia kutangulia kwenye haki, sasa the top dog viongozi wa juu wa Chadema wamebaki, Wangwe hakuwa na ishus na CCM, bali Chadema, sasa wanashindaje the Public Opinion kwa kurushiana maneno na CCM, kwa ajili ya marehemu the under dog waliyekuwa wamemsimamisha uanachama?

Only kama Chadema wataweza kutoa ushaidi mzito kuwa hawahusiki na kifo cha Wangwe, na kutoa ushahidi mzito wa wanaohusika na hicho kifo kama wapo, otherwise ni kufukuza hewa kushindana na CCM on this ishu, na believe me kuwa kuna wajinga flani ndani ya CCM ambao are having a lot of fun na hii topic,

Chadema, please change the subject now kabla haijawa too late!

Ushauri wa bure na wa binafsi, kwa sababu can you imagine our national politics bila ya Chadema?
 
Kwa kifupi tukubali na kusikiliza ushauri wa Professa Wangwe kuwa tuachane na UVUMI NA UZUSHI NA TUWAACHIE POLISI KAZI YAO.
Binafsi nimekubaliana na ushauri huo na sitochangia tena kuhusiana na UVUMI...Only kwenye maswali kama alivyotaka professa.
Ni busara nzuri kaitumia.
 
............MIGODI MIGODI...hawa ni watu ambao wana uwezo wa kupindua au kufadhili uasi kwenye serikali nyingi za afrika etc..ie angalia BLOOD DIAMOND MOVIE..................sembuse kumuondoa mtu mmoja???

..nashauri hoja ya wangwe aliyokuwa aiwasilishe bungeni ambayo pamoja na mengi ilikuwa iwatetee wana tarime walioamishwa kwa nguvu ili kupisha ujenzi wa mgodi ..watu wa CHADEMA wangalie namna ya kuiwasilkisha bungeni ndani ya kikao hichi ili kumuenzi marehemu....
 
PM.. kwa mtazamo wangu hiyo hoja haiwezi kutolewa tena na Chadema isipokuwa CCM. It seems kuwa CCM wana nyaraka za Wangwe. Na ukiangalia utaona kuwa hakuna mtu yeyote anayedai kuwa ana nakala ya hoja ya Wangwe. TBC??
 
Duh!
Mke wa KATI wamarehemu naye PANDIKIZI?
Maana kama na yeye alikuwa akiishi naye...Kwanini alimkaribisha NYOKA nyumbani kama alikuwa hamjui?
Nani alianza kumjuwa Nyoka kati ya marehemu na mkewe wa KATI?
Kaazi kweli kweli...Maana maslahi ni mengi na wake ni wengi..Sasa hata huto tujimali twa marehemu nato tuko kwenye kasheshe...Sasa usikute mke mdogo anajuwa ya RA na labda mali hizo ni za KUHONGWA..HAPO HATAKUBALI KUZIACHIA!
Kazi ipo.
Kwa Taarifa tu...
Miriam Wandwe (Warden) ni mke mdogo, Mke wa kati aliwekwa kando baada ya Marehemu kuwa Mh.
 
Kwani hawa wabunge huwa wanatayarisha hizi hoja kwa taratibu zao binafsi au kupitia ofisi za vyama vyao. Wabunge huwa wana ofisi zao tofauti na za vyama vyao, kabla wabunge hawajawasilisha hoja bungeni huwa haipitiwi kwanza katika vikao vya vyama vyao??

Nashindwa kujua kwa nini Marehemu tu ndie awe na nakala ya hiyo hoja iwapo hoja ilishakamilika na ilikuwa itolewe bungeni siku ile??
 
Nakubaliana na Profesa Wangwe. Kusema kwamba tumeridhika ni ajali ya kawaida ni kurahisha mambo na kujaribu kufunika kombe mwanaharamu apite. Inatakiwa kila jiwe ligeuziwe hadi ukweli ujulikane.

Tatizo ni kwamba ni nani huyo mwenye kutafuta ukweli na nani huyo wa kuuweka huo ukweli nje? Tumezoea kufunikafunika ili mambo yaishe, na tunaendelea na mambo mengine. Tumepiga kelele wee kuhusu "kifo" cha Balali hadi mambo yameisha na imetoka hiyo, hadi mhuni mmoja atakapojitokeza aseme "nimekutana" na Balali Minneapolis ndipo tutaanza tena kelele na kujaza thread kwa thread!

Sasa Profesa angetuambia baada ya kutoridhika huko, wao kama familia wamechukua hatua gani ili kujua ukweli. Haya, huyo Mallya mwenyewe ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari bila leseni, wala polisi hawajaona tatizo la yeye kuwadanganya kwamba alikuwa haendeshi gari. Yaani kwetu perveting the course of justice sio issue kabisa!

At the end of the day, "mchawi" wetu mkuu ni vyombo vya dola, ambavyo kwa uzembe, ujinga, kutokujua mambo au kwa makusudi, na kwa sababu ya kukubali kutumiwa na kutumikia wanasiasa badala ya nchi, wamekuwa wakifunika ukweli wa mambo badala ya kuyafunua. Matokeo yake wananchi tunazidi kukosa imani na vyombo hivi. Na hakuna hatari kwa nchi kama wananchi kukosa imani na vyombo vya dola na sheria.

Tungekuwa na vyombo imara vya dola vya kusimamia sheria na haki tungekuwa tunapewa updates za uchunguzi wa kifo cha Wangwe, na tungekuwa hatuna sababu za ku-speculate. Lakini wapi, sasa hivi tupo kwenye giza, tumebaki kupiga soga mitaani na kwenye internet. Kwa sababu ya udhaifu wa vyombo vyetu vya dola tumejikuta kila mtu ni msengenyaji na mmbea; tumekuwa watu wa kuishi kwa hisia, na tumejikuta tunapoteza muda mwingi wa kazi na kujadili mambo mengine ya maana.

Ungeniuliza nitaje failure moja kubwa ya uongozi wa JK, ningekwambia sio ufisadi; ningekwambia ni kitendo chake cha kuendesha nchi ki-uswahili-tatizo ambalo limesababisha vyombo vya dola kuacha kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, bali kwa matakwa na maslahi ya kisiasa ya kikundi fulani katika serikali na chama tawala. It is pathetic, and we're doomed. Ni aibu!
 
Binafsi naamini kuwa Polisi hawafai kuchunguza kesi hii kwani wao ni sehemu ya mashahidi.
 
PM.. kwa mtazamo wangu hiyo hoja haiwezi kutolewa tena na Chadema isipokuwa CCM. It seems kuwa CCM wana nyaraka za Wangwe. Na ukiangalia utaona kuwa hakuna mtu yeyote anayedai kuwa ana nakala ya hoja ya Wangwe. TBC??

.taarifa nilizonazo mjj...ni kuwa hii hoja ya wangwe ilikuwa na madai mazito ya ardhi na fidia kwa wana tarime ..kutokana na ardhi yao kuchukuliwa na wawekezaji..ilhali wao wana shida ya ardhi kwa kilimo na uchimbaji mdogo...habari zinazidi kusema kuwa madai ya chacha kwa hawa watu wa madini na serikali yalikuwa yanafikia dola milioni 800...

katika siku za karobuni baada ya serikali kufanikiwa kupata nakala za hiyo hoja[labda kwa kumtumia mallya]...juhudi kubwa zilikuwa ziikifanyika kumbembeleza asilete hoja au apunguze ukali wa hoja...najuwa hakukubali kuitupa hoja yake...ila sijui kama alikubali kupunguza ukali......

NI KWELI INAWEZEKANA KABISA CHADEMA WAKAWA HAWANA COPY YA HIYO HOJA KWANI .....HATA MKUU WA UPINZANI BUNGENI ALISHAWEKA WAZI KUWA CHACHA ALIKUWA AMEANZA TABIA YA KUTOWASHIRIKISHA WAPINZANI WENZAKE KWENYE HOJA ZAKE BUNGENI.....NAKUBALI KUWA UWEZEKANO MKUBWA UPO KWA CCM KUWA NA HIYO HOJA AU SPIKA ....

KILIO CHA SPIKA BUNGENI....kuna wabunge wengi wamepata kufa ..na spika wetu ni jasiri..sijapata kumuona akidondosha japo chozi...zaidi ya kwa wangwe...sijui haya machozi ya spika tunayachambuaje???.....je kuna jambo la hatari ambalo spika angeweza kumuepusha wangwe na akashindwa,,,au kuna nini hapa>..kumbuka alikuwa amemuahidi ruhusa ya kuwasilisha hoja baada ya kutoka dar es salaam..kuzika...spika ndio pekee alijua anasafiri.

KUIBIWA KWA LAPTOP YA MAREHEMU ...kunaweza kuwa kumepoteza nyaraka zote za kuwasilisha hiiyo hoja..kwa nini haijapatikana hadi leo...kama ingekuwa imeibiwa na mwanakijiji ..angeshindwa kuiuza ,itakuwa imechukuliwa na waelewa......

UKIANGALIA YOTE HAPO JUU na kitendo cha KATIBU MKUU WA CCM kutuma nyaraka za mgogoro wa CHADEMA mikoa yote ..masaa machache kabla ya msiba as if walikuwa wakitegemea BIG NEWS..inazidi kukita mawazo yetu kufikiria zaidi..katibu mkuu alijuaje kuwa hoja ya wangwe dhidi ya wana chadema wenzake..ilikuwa inakaribia kuwa mtaji wa kisiasa???

bado tunahitaji kuchunguza...
 
Huyu nae Prof mzima anachemsha big time, just a days ago the same old fashioned Prof amekaririwa akisema "wameridhika" Wangwe kafa kwa ajali ya kawaida all over suddenly comes this spectacular u turn. If this crap could come from Prof then sijuii tutegemee nini kutoka kwa the like Mnyika...

Kweli ndio tulivyo....

Not all professors give crap. For example professor Kapuya....Not even all the Mnyikas are hopeless leaders. For example Mr Stephen Wasira....
 
.taarifa nilizonazo mjj...ni kuwa hii hoja ya wangwe ilikuwa na madai mazito ya ardhi na fidia kwa wana tarime ..kutokana na ardhi yao kuchukuliwa na wawekezaji..ilhali wao wana shida ya ardhi kwa kilimo na uchimbaji mdogo...habari zinazidi kusema kuwa madai ya chacha kwa hawa watu wa madini na serikali yalikuwa yanafikia dola milioni 800...

katika siku za karobuni baada ya serikali kufanikiwa kupata nakala za hiyo hoja[labda kwa kumtumia mallya]...juhudi kubwa zilikuwa ziikifanyika kumbembeleza asilete hoja au apunguze ukali wa hoja...najuwa hakukubali kuitupa hoja yake...ila sijui kama alikubali kupunguza ukali......

NI KWELI INAWEZEKANA KABISA CHADEMA WAKAWA HAWANA COPY YA HIYO HOJA KWANI .....HATA MKUU WA UPINZANI BUNGENI ALISHAWEKA WAZI KUWA CHACHA ALIKUWA AMEANZA TABIA YA KUTOWASHIRIKISHA WAPINZANI WENZAKE KWENYE HOJA ZAKE BUNGENI.....NAKUBALI KUWA UWEZEKANO MKUBWA UPO KWA CCM KUWA NA HIYO HOJA AU SPIKA ....

KILIO CHA SPIKA BUNGENI....kuna wabunge wengi wamepata kufa ..na spika wetu ni jasiri..sijapata kumuona akidondosha japo chozi...zaidi ya kwa wangwe...sijui haya machozi ya spika tunayachambuaje???.....je kuna jambo la hatari ambalo spika angeweza kumuepusha wangwe na akashindwa,,,au kuna nini hapa>..kumbuka alikuwa amemuahidi ruhusa ya kuwasilisha hoja baada ya kutoka dar es salaam..kuzika...spika ndio pekee alijua anasafiri.

KUIBIWA KWA LAPTOP YA MAREHEMU ...kunaweza kuwa kumepoteza nyaraka zote za kuwasilisha hiiyo hoja..kwa nini haijapatikana hadi leo...kama ingekuwa imeibiwa na mwanakijiji ..angeshindwa kuiuza ,itakuwa imechukuliwa na waelewa......

UKIANGALIA YOTE HAPO JUU na kitendo cha KATIBU MKUU WA CCM kutuma nyaraka za mgogoro wa CHADEMA mikoa yote ..masaa machache kabla ya msiba as if walikuwa wakitegemea BIG NEWS..inazidi kukita mawazo yetu kufikiria zaidi..katibu mkuu alijuaje kuwa hoja ya wangwe dhidi ya wana chadema wenzake..ilikuwa inakaribia kuwa mtaji wa kisiasa???

bado tunahitaji kuchunguza...

Kuna ile breaking news that I never made... lakini you almost nailed it.
 
Polisi ni kitengo cha CCM ndiyo maana wameshindwa kuchukua hatua zozote zile dhidi ya mafisadi kwa sababu katika wizi wa BoT, CCM wanahusika. Hivyo hawatakuwa na ubavu wa kumgusa fisadi Makamba.

Date::8/5/2008
Chadema yamshtaki Makamba polisi kuhusu waraka wa Wangwe
Na Kizitto Noya
Mwananchi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, kumhoji Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema jana kuwa, chama chake kina wasiwasi na jinsi CCM ilivyopata waraka wa marehemu kuhusu mgogoro wake na Chadema na kuanza kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake.

Alisema, Makamba anapaswa kuhojiwa ili aeleze uhusiano wake na marehemu ambaye alikuwa Mbunge Chadema, hata akapata nyaraka hizo za siri katika kipindi kifupi kabla ya kifo chake na kuzisambaza.

''Hatutaki kuhitimisha kwa sababu sisi ni wanademokrasia, ila tunataka IGP sambamba na maombi yangu ya awali ya kumhoji Mkurugenzi wa TBC1, amhoji Makamba ili tujue uhusiano wake na marehemu na jinsi alivyopata waraka huo na kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake,'' alisema Kabwe na kuongeza:

''Waraka huo ulipotolewa kwa mara ya kwanza na TBC1, mimi (Kabwe) nilikuwa na mashaka na Jumamosi iliyopita, niliwasiliana na IGP na Mkuu wa Usalama wa Taifa kuwataka wamhoji Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya umma. Lakini leo (jana) tumefumbuliwa macho kwamba waraka huo ulianzia CCM na ikabidi niwasiliane naye (IGP), tena ili zoezi hilo limguse pia Makamba,'' alisema.

Alisema Makamba anapaswa kueleza alikopata waraka huo na sababu za kutumwa kwake muda mfupi kabla ya kifo cha marehemu ikiwa ni pamoja na msukumo uliomfanya ausambaze kwa viongozi wa CCM.

Kwa mujibu wa Kabwe, sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1996 inatambua ndugu wa marehemu kuwa wamiliki wa mali na taarifa muhimu zinazomhusu marehemu, hivyo ni ajabu CCM kumiliki waraka huo wakati haina uhusiano wa kindugu wala kiitikadi na marehemu Wangwe.

''Hivi CCM ina uhusiano gani na mbunge wa Chadema au ndugu wa marehemu hata ikahalalisha kumiliki waraka huo na kuusambaza bila woga?'' alihoji Kabwe na kusisitiza kuwa Chadema haijauona waraka huo na wala kuambiwa na ndugu wa marehemu.

Akizungumzia suala hilo, Makamba alikanusha kuhusika na waraka huo na kueleza kuwa, CCM haina haja wala sababu ya kuwa nao na kuusambaza.

Alisema CCM haihusiki na waraka huo na kubainisha kuwa wanaofanya hivyo ni watu wanaomwunga mkono marehemu Wangwe katika migogoro yake na chama chake.

''Mimi sijauona waraka wenyewe na sina taarifa nao, lakini kwa nini CCM iusambaze, ina shida gani na Chadema?'' alihoji na kuongeza:

"Chadema sisi hatuiogopi, tuliishinda Jimbo la Kiteto na tutaishinda mwaka 2010, hatuna haja nayo wala haitusumbui."

Kauli za Makamba na Zitto zimefuatia taarifa kwamba, CCM imekuwa ikisambaza waraka wa marehemu Wangwe wenye kurasa sita unaoelezea jaribio la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutaka kumvua wadhifa wake na uanachama.

Waraka huo unadaiwa kusambazwa kwa viongozi wa CCM kwa lengo la kuwafahamisha mgogoro wa Chadema ambao umekuwa ukihusishwa na chanzo cha kifo cha mbunge huyo.

Ukurasa wa nne wa nakala ya waraka huo unaonyesha kwamba, kwa mara ya kwanza ulitumwa kutoka Dodoma Julai 27 mwaka huu majira ya saa 9:42 alasiri toka namba (026) 2322965 ambayo imeonyesha kusajili kwa jina la ‘KATIBU MKUU CCM DOM' tarehe ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Wangwe.

Uchunguzi umebaini kuwa waraka huo ulianza kusambazwa kutoka Dar es Salaam kwa namba za faksi 2667457 iliyotanguliwa na kodi namba ya mkoa (022) ikimaanisha kutumwa kutoka Dar es Salaam Julai 31, mwaka huu saa 5:50 asubuhi na mmiliki wa namba hiyo akitambuliwa kama SIGMA ICT.

Waraka huo, umetumwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM mikoani, wakiwemo Makatibu wa Mikoa na Wilaya na wengine ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaonyesha kwa kina mgogoro wa Chadema ulivyo.

''Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama dola za Kimarekani 181,949.00, sawa na Sh 218,338,546 na mpaka sasa chama kimemlipa Sh175 milioni.

''Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha wilayani na makao makuu, niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku, kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa pesa za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikali.

''Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo, basi atuthibitishie pesa hizo anazodai alikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya Chadema kupitia hundi ipi na lini?'' ilieleza sehemu ya waraka huo.
 
Kwani hawa wabunge huwa wanatayarisha hizi hoja kwa taratibu zao binafsi au kupitia ofisi za vyama vyao. Wabunge huwa wana ofisi zao tofauti na za vyama vyao, kabla wabunge hawajawasilisha hoja bungeni huwa haipitiwi kwanza katika vikao vya vyama vyao??

Nashindwa kujua kwa nini Marehemu tu ndie awe na nakala ya hiyo hoja iwapo hoja ilishakamilika na ilikuwa itolewe bungeni siku ile??

Safi sana Yebo Yebo...Hapa ndio kwenye mzizi wa FITNA HAPA...Hoja nani anayo kati ya chadema na ccm?
HAPO.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom