Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kwanini wamuogope Mbowe,Na hiki kitu kwa sisi wakruya huwa hatukitaki,na ndiyo maana walimchukia Chacha Wangwe sababu hakutaka kubeba mambo ya ukabila.

Kwa hili la kifo cha wangwe niilishatoa onyo zamani sana,ole wao CHADEMA....

Dr. Slaa yupo Nchini,maanda haongelei kabisa suala la Mbowe,wamemuachia Zitto na Mnyika.Na hapa natoa ujumbe kwa mnyika,kama jana alisikiliza hotuba ya Mzee Mandela hapa SA nilipo kwa sasa katika kituo cha kulelea Yatima Basi atakuwa ameupata vizuri.Without Education you can not be a good leader..Rudi shule na ujiendeleze kwanza na ambao mengine baadaye,ungana kina Kitila Mkumbo

Kama wewe kweli upo S A , Naanza kupata wasiwasi juu yako , hivi wewe ni miongoni mwa wale waandishi wa RAI waliopelekwa shule kwa ajili ya kuliandikia gazeti lao na unaandaliwa kuwa mhariri wa mtandao 2010?

Naomba japo kujua,
 
Vikao vya Marehemu Chacha Wangwe na Katibu Mkuu wa CCM luteni ussu Yusuph Rajabu Makamba, haswa pale Wangwe alipoenda ili kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya kazi za kukiumiza CHADEMA, ILA NINAJUA KUWA ALIPEWA ASSIGNMENT FULANI KABLA YA KUPEWA FEDHA HIZO.

Wangwe alikutana na Mawaziri mbalimbali nyumbani kwao usiku na kupanga hatua za kuchukua.

Kitendo cha CCM kuanza kuusambaza waraka wa Wangwe kwenda mikoani siku moja kabla ya ajali husika kutokea ,hili linapaswa kuchunguzwa kwani waraka huo umekuwa ukitumwa kutokea Lumumba na Makao makuu ya CCM huko Dodoma.

Kitendo cha CCM kupanga kumdhalilisha Mbowe akiwa huko Tarime kiliposhindwa magazeti yakawa tayari yameshaandika kuhusiana na suala hilo.

RA kupiga simju yake ya kwanza ndani ya dk 15 baada ya ajali ya Marehemu hili linapaswa kufanyiwa kazi na kufuatioliwa kwa kina sana , kwani alikuwa yupo nje ya Nchi na bila kutafuna maneno huyu alikuwa Jijini Nairobi Kenya.

RA kusambaza milioni moja kwa baadhi ya wahariri waliopotosha habari ile , nasema kwa uhakika kuwa alisambaza milioni moja kwa kila mhariri ama mhariri wa habari aliyeweza kuwepo kwenye kikao chake na wengine ilibidi wakapelekewa fedha hizo wakiwa news room.

Kitendo cha numba za FAX ZA CCM kutumika kusambaza waraka unaoitwa wa WANGWE kwenda nchi nzima na mpaka ngazi za chini ,kinaonyesha kuwa kuna jambo lilikuwa limeandaliwa mahususi na kwa makakati maalum.

Mpango kazi uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya Wangwe kufanya ziara nchi nzima kuanzia mwezi September na bajeti yake ambayo tayari ilikuwa imeshaanza kuandaliwa, mpango kazi huo utachapishwa na gazeti mojawapo kama makala ,ila utalipiwa na mtu mmoja ambaye amekuwa akifadhili mkakati mzima.

Mke wa Wangwe Mariam kutaka familia iamini kuwa CHADEMA inahusika ,huku akiwa yeye ndio alikuwa anaenda kukutana na wakina Rostam Azizi haswa pale Kempinsik kwa ajili ya kufanya mipango na hata kumfanya mumewe kuwa na ukaribu na MAFISADI HAO.
Mariam amekuwa sasa na mkakati wa kuhakikisha kuwa mtoto wa marehemu yule wa kiume mkubwa Zakayo anatumika kisawasawa kutoa kauli kuwa CHADEMA wanahusika ,japo watu wengine kwenye familia hiyo wamekuwa wakipingana na mawazo hayo,na haswa baada ya kujua na kuona mbinu na hila za huyu mke mdogo ambaye alikutana na Wangwe baada ya kuwa Mbunge na hata kumfanya Wangwe kuishi naye.

Familia mpaka sasa wanaugomvi na huyu mke mdogo kwani wanataka kujua mali za marehemu kama vile nyumba na shamba la ekari sita lililonunuliwa huko Dodoma liko wapi na hati zake ziko kwa nani ,hii ilipelekea juzi usiku kukaa kikao mpaka asubuhi.

Mke mdogo akishirikiana na mke wa kwanza wameamua kumtenga mke wa kati yaani yule wa pili ,sasa huyu ndio alikuwa na marehemu wakati wote wa kampeni na hata alipokuwa amefungwa huyu alikuwa naye bega kwa bega.

Namalizia hapa kwa leo.

Mkuu,

Unaona mkiipa familia ya Wangwe peace? Sasa mnaanza kumwingiza hata mke na mtoto?

Familia wakifiwa wanasema mambo mengi sana, wapeni nafasi waomboleze na baadaye
watakuja kuamini kwenye ukweli kwamba hiyo ilikuwa ni ajali tu.

Hapo mtatupia lawama watu wengine wote isipokuwa CHADEMA, hapo ndipo mnapokosea mno kwenye hili la Wangwe. Ni bora kuamini kwamba ni ajali, mkiamza ya mkono wa mtu basi kwenye list juu kabisa baadhi ya viongozi wa CHADEM lazima muwaweke kama suspects. Huwezi ukasema mkono wa mtu na bado ukaiondoa CHADEMA kabisa juu ya hili maana theory nzima inakufa labda mpaka siku mmepata ushahidi kamili nani alihusika.

Mimi kwenye hili naamini ilikuwa ni ajali tu na hakuna mkono wa mtu yeyote zaidi ya uendeshaji mbaya wa Mallya.

Mimi naamini kuna watu ndani ya CHADEMA walipanic waliposikia kifo cha Wangwe, walijua wataambiwa wamehusika, na hivyo kutoa haraka haraka tamko la Mnyika kama njia ya kujiondoa wao. Hapo bila kujua walikuwa wanafungulia gates za kutuhumiana na kuingiza siasa kwenye msiba. CCM nao kama kawaida, hawakubaki nyuma, akina RA na wenzake wakajipanga na kuanza kuwapanga baadhi ya wahariri wao.

Siasa mchezo mchafu sana, hasa kama unachezwa kwenye nchi maskini na ambayo watu wake wengi bado hawajaelemika na wana umaskini wa kutupwa.
 
Mkuu,

Unaona mkiipa familia ya Wangwe peace? Sasa mnaanza kumwingiza hata mke na mtoto?

Familia wakifiwa wanasema mambo mengi sana, wapeni nafasi waomboleze na baadaye
watakuja kuamini kwenye ukweli kwamba hiyo ilikuwa ni ajali tu.

Hapo mtatupia lawama watu wengine wote isipokuwa CHADEMA, hapo ndipo mnapokosea mno kwenye hili la Wangwe. Ni bora kuamini kwamba ni ajali, mkiamza ya mkono wa mtu basi kwenye list juu kabisa baadhi ya viongozi wa CHADEMA lazima muwaweke kama suspects. Huwezi ukasema mkono wa mtu na bado ukaiondoa CHADEMA kabisa juu ya hili maana theory nzima inakufa labda mpaka siku mmepata ushahidi kamili nani alihusika.

Siku zote nimekuwa nikiandika baada ya kufanya kazi ya utafiti, na kumbuka siku ya kwanza kuandika humu kwa mwaka huu niliandika kuhusu waandishi kisha ukaniuliza kama nina ushahidi nikasema ndio ,na kesho yake yalitokea.

Pili, sio kila anayeandika kuhusiana na Rostam basi huyu ni CHADEMA la hasha , jitahidi kusoma kwenye mistari na uelewa naandika kitu gani sio kuandika kwa hisia , mimi nimewapo taarifa juu ya kile kinachoendelea na cha uhakika,sasa hapo wewe unaanza kunilaumu ,kuwa focused sio kuwa biased.

Nitaendelea kuandika ukweli halisi ,na nilisema tangu siku ya kwanza kuwa nitaweka ukweli bayana .

Nawatakia kazi njema ,naenda kuendelea na utafiti wangu na mwisho wa siku nitaweka hapa na kujitambulisha hata kama itanigharimu ajira yangu pamoja na marafiki zangu .
 
Kama kuna mtu anamfaamu vizuri huyu kijana atuwekee hapa maana i can smell something fishy, huyu jamaa Libya alikwenda kufanya nini, alifuatana na akina nani je walikuwa mission moja au alikuwa na mission tofauti.

Nahisi kuna siri ambayo haitafichuliwa hapa bila kupata associate wa huyu kijana kwa ufasaha.
 
Kama wewe kweli upo S A , Naanza kupata wasiwasi juu yako , hivi wewe ni miongoni mwa wale waandishi wa RAI waliopelekwa shule kwa ajili ya kuliandikia gazeti lao na unaandaliwa kuwa mhariri wa mtandao 2010?

Naomba japo kujua,
Nipo kwenye Trainning za ORACLE and mambo yanayohusu Advanced Ethicial Hacker and Information Systems Security.

Hao waandishi walioko huku nimekutana nao na nina wafahamu sana sababu nilikutana nao Mlimani wakati namaliza Masters Yangu wao wakiwa wadoo zangu na kwa kuwa mmoja wao tumetoka sehemu moja ilikuwa rahisi mie kuwapa ushauri wa maisha,wewe ulitaka nani awasomeshe?Mie nimewasifu kwa mbinu yao ya kujipatia Elimu kwa ujanja.ulitaka waje kwako uwasaidie au?acheni wivu wa kijinga kwa vijana hawa na waacheni watafute maisha.

Mie niko tayari kutoa pesa ili Mnyika ajiendeleze na Shule,sababu namkubali
 
•Mbaya wa Wangwe aanikwa

*Lipumba, wenzake wajipanga kumwona IGP
*Wadau wa habari wamjia juu Zitto Kabwe

Na Gladness Mboma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezidi kukabwa koo na baadhi ya wanasiasa kwa kudaiwa kuhusika kwa namna fulani na kifo cha Mbunge wa Tarime, Bw. Chacha Wangwe, kutokana na kumsimamisha umakamu Mwenyekiti.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha Sauti ya Umma (SAU), Dkt. Paul Kyara, alisema tangu CHADEMA ilipomsimamisha Bw. Wangwe umakamu alikuwa hatulii bungeni.

"Tunaweza kusema kuwa kifo hicho kimesababishwa na CHADEMA kwa sababu ya kumsimamisha umakamu mwenyekiti Bw. Wangwe

"Ingekuwa si hivyo, Wangwe asingekuwa na pilikapilika za kukimbiakimbia huku na kule, angetulia bungeni na hivyo asingepatwa na ajali kwa kuwa angekuwa na amani, angetulia, CHADEMA wamechangia pamoja na kuwa ni ajali," alisema Dkt. Kyara.

Alisema kwa muda mfupi aliokaa na Bw. Wangwe baada ya kumtembelea ofisini kwake kumwomba ushauri kuhusiana na kusimamishwa umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA, simu zake za mkononi zilikuwa zinaingia kutoka sehemu mbalimbali kama vile alikuwa opareta wa simu.

Dkt. Kyara alidai kuwa kaka wa mtuhumiwa wa ajali iliyosababisha kifo cha Bw. Wangwe, mfanyabiashara Bw. Deus Mallya ambaye alikuwa na marehemu Bw. Wangwe ni rafiki mkubwa wa kigogo mmoja ndani ya CHADEMA.

Aliendelea kudai kwamba kigogo huyo wa CHADEMA amekuwa akifanya shughuli za kibiashara na kaka wa Bw. Mallya kwa siku nyingi na kudai kuwapo kwa umuhimu wa kumchunguza.

"Haiwezekani kijana mdogo kama huyo kuwa na urafiki na mtu mkubwa kama marehemu Wangwe, eti amekwenda Dodoma kumwandikia marehemu kitabu cha umaarufu wake, haiwezekani hata kidogo, huyu alikwenda huko kwa lengo fulani," alisisitiza Dkt. Kyara akikariri maelezo ya Bw. Mallya kama alivyokaririwa katika gazeti la Mtanzania la jana.

Alisema mara ya mwisho wakati Bw. Wangwe anakwenda Dodoma alipita ofisini kwake akiongozana na mkewe na watoto wake wawili wakitokea Muhimbili kumwona Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, ambaye alikuwa amelazwa.

"Nilimuuliza hali ya mgonjwa, licha ya kwamba alikuwa akimtukana wakati akiwa Tanga, hapo ndipo nilipojua kuwa Bw. Wangwe alikuwa na moyo ya utu licha ya kutukanwa lakini alikwenda hospitali kumwona," alisema Dkt. Kyara.

Alisema yeye alimkabidhi Bw. Wangwe habari ya kwenda kuchapisha katika vyombo vya habari na kumsihi pia kufikisha suala la kufutiwa uanachama mahakamani, kwani alimweleza kuwa akifukuzwa uanachama 'biashara imekwisha'.

Dkt. Kyara alisema marehemu alimweleza kuwa alikuwa amekwishapata Mwanasheria ambaye alitaka sh. milioni 12 gharama ambayo alimweleza kuwa ni kubwa, na alimshauri atafute wakili mwingine.

Alisema alimshauri marehemu amtafute mwanasheria mwingine licha ya kwamba anasimamia kesi dhidi ya CHADEMA na CCM na aliegemea sana upande wa CCM.

"Nilimwambia ajaribu kwenda kumwona na amweleze kuwa mimi ndiye niliyemtuma na angempa mawazo mazuri na kama akishindwa, nilimwambia amwone Mwanasheria Mathew Kakamba kwa kuwa naye ni Mwanasheria mzuri," alisema Dkt. Kyara.

Alisema marehemu aliishia kwa Bw. Kakamba na kwamba inavyoelekea, walikwishakubaliana na siku ya ajali alikuwa anakwenda Dar es Salaam kusimamia kesi yake kutokana na kuiacha CHADEMA 'uchi' na hivyo kutaka kumfukuza uanachama.

Dkt. Kyara alisema wameshindwa kumwelewa Bw. Kabwe kwa madai yake aliyoyatoa kwamba hakukuwa na fujo wala vurugu katika msiba wa marehemu wangwe.

"Mimi nilikuwa nawasiliana kila baada ya muda na watu wa Tarime, walinieleza kuwa vurugu na fujo kubwa zilizotokea kwenye msiba wa Mbunge wa Tarime, Bw. Wangwe, hazijawahi kutokea kwa msiba wa kiongozi yeyote hapa nchini.

"Na fujo hizo ziliibuka mara baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, kuwasili msibani hapo, wanachama wakalazimika kumtoa kwa mlango wa uani, sasa Bw. Zitto anakanusha nini wakati kitu kilikuwa wazi?," alihoji Dkt. Kyara.

Alisema Bw. Kabwe kudai kuwa hakukuwa na fujo wanashindwa kumwelewa alikuwa na maana gani, wakati yeye alikuwa ni mmoja wa viongozi waliokuwa wakituliza fujo.

Mwenyekiti huyo alisema kiongozi anayeaminika kitaifa na katika jamii, hatakiwi kusema uongo hata kidogo.

Alisema kutokana na kifo cha Bw. Wangwe, CHADEMA wasitarajie kupata tena jimbo la Tarime "ni dhahiri kuwa jimbo hilo wamelipoteza ikiwa ni pamoja na ruzuku kupungua na hilo halina mjadala".

Juzi wenyeviti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba; TLP Bw. Augustino Mrema na Bw. James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, walikutana Dar es Salaam na kushangaa kauli ya Bw. Kabwe, kwa wahariri wa vyombo vya habari ikikanusha kuwapo kwa vurugu katika msiba wa Bw. Wangwe kijijini Kemokerere, Tarime.

Naye Said Mwishehe, anaripoti kwamba Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema siku yoyote kuanzia leo watapeleka ushahidi wao kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema ambao utasaidia katika uchunguzi wa ajali ya gari iliyosababisha kifo cha Bw. Wangwe.

Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati Majira lilipotaka kujua ni lini watapeleka ushahidi wao kwa IGP baada ya kusema kwamba kifo cha mbunge huyo kimezua maswali mengi.

Alisema kwa sasa wanaendelea vizuri juu ya suala hilo na watahakikisha wana kila kitu ambacho wanaamini kitalisaidia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo.

"Tunakwenda vizuri katika hili na nimeacha wenzangu wanaendelea kuweka mambo sawa na siku yoyote kuanzia kesho (leo) tutapeleka kila kitu ambacho kitasaidia Polisi kuchunguza vizuri tukio hilo la kifo," alisema Profesa Lipumba.

Alisema kwa kweli kifo cha Bw. Wangwe bado kimejaa mambo magumu na lazima kitaendelea kujadiliwa na hata familia ya marehemu naamini watalizungumzia hilo.

Alipoulizwa kuhusu kulaumiwa kwa vyombo vya habari na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kuhusiana na jinsi waandishi walivyoripoti mazishi ya marehemu Wangwe, alisema suala hilo atalitafutia siku yake kwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Naye Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Bw. Kabwe, akizungumzia taarifa zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa upinzani kuhusu mazishi ya marehemu Wangwe, alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa tayari malalamiko yao yanashughulikiwa na Jukwaa la Wahariri.

"Kwa upande wetu tulishatoa malalamiko yetu kuhusu tukio zima la mazishi ya marehemu Wangwe na jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti, hivyo kwa sasa hatuna cha kusema lolote kama kuna kiongozi amekuja na hoja yake, atakuwa shahidi mzuri kwa kulisaidia Jukwaa la Wahariri kufanya kazi yao vizuri," alisema Bw. Kabwe.

Kutoka Shinyanga, Suleiman Abeid, anaripoti kwamba baadhi ya wadau wa habari mjini humo wamemtaka Bw. Kabwe kuwaomba radhi waandishi wa habari kutokana na hatua yake ya kuwatuhumu kuwa waliandika habari za uongo kuhusu kufanyiwa vurugu kwa Bw. Mbowe kwenye mazishi ya marehemu Wangwe.

Hatua hiyo inatokana na kukanushwa kwa madai hayo na viongozi wakuu watatu wa vyama vya upinzani nchini juzi, ambao walithibitisha kuwapo kwa vurugu katika mazishi hayo ambapo pia Bw. Mbowe na wao wenyewe walikabiliana na vurugu hizo.

Wadau hao walisema kutokana na kubainika ukweli wa habari hizo zilizoandikwa na waandishi kuwa viongozi mbalimbali walifanyiwa vurugu ni vizuri sasa Bw. Kabwe akawaomba radhi waandishi hao.

Mmoja wa wadau hao, Bw. Juma Burhani, mkazi wa Lubaga mjini humo, alisema mashambulizi ya Bw. Kabwe dhidi ya waandishi yalivuka kiwango na bahati mbaya madai yake hayakuwa na ukweli.

Alisema ni vizuri kabla ya kukanusha habari hizo za waandishi kufanya utafiti wa kina ili kujua ukweli wake, badala ya kuwapaka matope.

"Wengi tulianza kuingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kitendo hicho, kuona ni vipi waandishi waamue kututangazia habari za uongo tena karibu kila chombo cha habari, lakini tukashangaa kumsikia Bw. Kabwe akikanusha kuwa hapakuwa na tukio hilo, sasa ukweli umebainika, kwa nini asiombe radhi?," alihoji.

Alisema bila ushuhuda uliotolewa na viongozi watatu wa vyama vya upinzani, Bw. Mrema, Bw. Mbatia na Bw. Lipumba, umma wote wa Watanzania ungewadharau kwa kiasi kikubwa waandishi wa habari wa nchini hasa wa mikoani.

Bw. Mohab Dominick mwandishi wa magazeti ya Nipashe, alisema Bw. Kabwe alikurupuka kuwashutumu waandishi na kwamba hakufanya subira kuchunguza ukweli wa habari alizozikanusha.

"Sasa wenzake wameweka mambo hadharani, ni kweli katika mazishi ya Bw. Wangwe kulikuwa na vurugu kubwa, kiasi cha viongozi wa vyama vya upinzani kulazimika kuokolewa na Polisi, lakini Kabwe anadai kuwa hapakuwa na vurugu zozote na amani ilitawala, sijui baada ya maelezo ya wenzake ataueleza nini umma wa Watanzania?," alihoji Bw. Dominick.
 
Mtanzania ,naona uko kwenye kazi maalum sasa endelea na ntakuja kukujibu siku moja ,nipo bize kwa sasa.

Kumbuka watu watatu waliokutana na RA jana usiku na kukaa 4 hrs.
 
Nipo kwenye Trainning za ORACLE and mambo yanayohusu Advanced Ethicial Hacker and Information Systems Security.

Hao waandishi walioko huku nimekutana nao na nina wafahamu sana sababu nilikutana nao Mlimani wakati namaliza Masters Yangu wao wakiwa wadoo zangu na kwa kuwa mmoja wao tumetoka sehemu moja ilikuwa rahisi mie kuwapa ushauri wa maisha,wewe ulitaka nani awasomeshe?Mie nimewasifu kwa mbinu yao ya kujipatia Elimu kwa ujanja.ulitaka waje kwako uwasaidie au?acheni wivu wa kijinga kwa vijana hawa na waacheni watafute maisha.

Mie niko tayari kutoa pesa ili Mnyika ajiendeleze na Shule,sababu namkubali

Acha matusi kaka, sasa kuwa Cape town si unalipiwa na RA ? alikufanya ukahama media house inayoheshimika sasa ona unatetea hata visivyofaa kutetewa kaka, please linda masilahi nya taifa lako kwani hapa tulipo tuko kwenye wakati mgumu sana kama taifa ,na kama watanzania wachache wasipoamua kusimama na kusema tutaenda kuangamia sote, jiunge na upande wa ukweli na haki hata kama itakugharimu maisha yako, shule yako, ajira yako kwa masilahi ya wananchi masikini wa Taifa hili.

Sintoendelea kusema sana ndugu ,ila nitajitambulisha soon kwa jina halisi la kwangu .
 
Halafu tunaambiwa tuisuse VODACOM ambako RA ana hisa tu huku RAI ni MMILIKI!
 
Mtanzania ,naona uko kwenye kazi maalum sasa endelea na ntakuja kukujibu siku moja ,nipo bize kwa sasa.

Kumbuka watu watatu waliokutana na RA jana usiku na kukaa 4 hrs.

wewe ndiyo huyo huyo uliyesema kwamba RA aliongea na Chacha Wangwe na leo unatuambia kakutana na wengine Dodoma,tuambie alikutana na kina nani hapo Dodoma na waliongea nini...Na hizi ni Fact za kijinga sana,kila RA akikutana na mtu basi kuna jambo.

Nawashauri CHADEMA ,badili siasa zenu na msipoangalia chama mnakipeleka kubaya,mmekuwa walinzi wa watu na kuacha kulinda sera za chama chenu.Mpaka sasa mmeweza vipi kuelezea sera zenu?

we are tired of Spculation and Rostam is not concerned with this issues
 
Mtanzania ,naona uko kwenye kazi maalum sasa endelea na ntakuja kukujibu siku moja ,nipo bize kwa sasa.

Kumbuka watu watatu waliokutana na RA jana usiku na kukaa 4 hrs.

Kiranja,

Ha haaa!!! nalipwa pesa nyingi sana na RA kwahiyo kazi maalum. I hope utafurahisha moyo ukisikia Mtanzania ni FISADI.

Mtaishia kuita kila asiyekubaliana na nyie fisadi. Mimi nabeba mabox na napata clean money, sihitaji hata senti moja ya kuibia maskini.
 
wewe ndiyo huyo huyo uliyesema kwamba RA aliongea na Chacha Wangwe na leo unatuambia kakutana na wengine Dodoma,tuambie alikutana na kina nani hapo Dodoma na waliongea nini...Na hizi ni Fact za kijinga sana,kila RA akikutana na mtu basi kuna jambo.

Nawashauri CHADEMA ,badili siasa zenu na msipoangalia chama mnakipeleka kubaya,mmekuwa walinzi wa watu na kuacha kulinda sera za chama chenu.Mpaka sasa mmeweza vipi kuelezea sera zenu?

we are tired of Spculation and Rostam is not concerned with this issues

Mhh,nasema kuwa wengine tupo kwa ajili ya masilahi ya taifa sio ya vyama ,tuko juu ya siasa za vyama .

Sijataja Dodoma ,hayo umesema wewe inamaana unajua hata yuko wapi kwani aliyetaja kuhusu Dodoma ni wewe na sio mimi.

Kumbe yuko Dodoma ,sikulijua hilo ila nilitaka baadhi yenu mjue kuwa wengine tupo kila mahali ndio maana naweza kukupa habari zilizo sahihi na ntaendelea kukupa habari hizo.
 
Acha matusi kaka, sasa kuwa Cape town si unalipiwa na RA ? alikufanya ukahama media house inayoheshimika sasa ona unatetea hata visivyofaa kutetewa kaka, please linda masilahi nya taifa lako kwani hapa tulipo tuko kwenye wakati mgumu sana kama taifa ,na kama watanzania wachache wasipoamua kusimama na kusema tutaenda kuangamia sote, jiunge na upande wa ukweli na haki hata kama itakugharimu maisha yako, shule yako, ajira yako kwa masilahi ya wananchi masikini wa Taifa hili.

Sintoendelea kusema sana ndugu ,ila nitajitambulisha soon kwa jina halisi la kwangu .

Kiranja,

Nadhani wewe ni kiranaja wa sehemu ulipo,suala la mimi kulipiwa na mtu yeyote ambaye ni muajiri wangu wewe alikuhusu kabisa.

Kama una ugomvi na Kijana kuhama Mwananchi na kwenda RAI,is up to you lakini kaaa ukijua kila mtu anatafuta maisha na suala la kuhama gazeti moja kwenda lingine ni mpango wa mtu.

Kwanini unataka kila mtu aishi kama wewe utakavyo,hiyo ni tabia ya ubinafsi na watu wengi wenye tabia hiyo ni wachaga.Suala la kujitambulisha mie halinihusu.
 
You know Mhache,
Hakika uchunguzi wowote huwezi kumrejesha wangwe but its good that we know more about mallya for its not clear of his relationship with the late Wangwe.

Allegations made by opposition parties are very strong and in my opinion, terrorist actions are also a threat to the nation.

ITS BETTER WE MAKE FOLLOW UP and if the allegations are true the govt should act on the matter.Am telling you, this is not a private matter, it is a national matter.

We have been spending alot of our resources in useless things, at least this one is useful, in my opinion.
 
Kwanini wamuogope Mbowe,Na hiki kitu kwa sisi wakruya huwa hatukitaki,na ndiyo maana walimchukia Chacha Wangwe sababu hakutaka kubeba mambo ya ukabila.

Kwa hili la kifo cha wangwe niilishatoa onyo zamani sana,ole wao CHADEMA....

Dr. Slaa yupo Nchini,maanda haongelei kabisa suala la Mbowe,wamemuachia Zitto na Mnyika.Na hapa natoa ujumbe kwa mnyika,kama jana alisikiliza hotuba ya Mzee Mandela hapa SA nilipo kwa sasa katika kituo cha kulelea Yatima Basi atakuwa ameupata vizuri.Without Education you can not be a good leader..Rudi shule na ujiendeleze kwanza na ambao mengine baadaye,ungana kina Kitila Mkumbo

Wale waleee. Hebu onyesha mfano jinsi shule inavyokusaidia. Mandela alilenga mazingira haya, sio hayo ya kwako kaka
 
Mhh,nasema kuwa wengine tupo kwa ajili ya masilahi ya taifa sio ya vyama ,tuko juu ya siasa za vyama .

Sijataja Dodoma ,hayo umesema wewe inamaana unajua hata yuko wapi kwani aliyetaja kuhusu Dodoma ni wewe na sio mimi.

Kumbe yuko Dodoma ,sikulijua hilo ila nilitaka baadhi yenu mjue kuwa wengine tupo kila mahali ndio maana naweza kukupa habari zilizo sahihi na ntaendelea kukupa habari hizo.
umeshindwa kwa hoja,sasa unaleta viroja..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom