Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Madela wa Madilu,
Mkuu kama impact ingetokea mbele ni lazima kioo cha mbele kingevunjika ama kumomonyoka kuelekea mbele..lakini badala yake tunaona kioo cha nyuma ndicho kimeondoka kisha basi cha mbele kinaonyesha kimelalia nyuma baada ya kutoka kwenye frame yake..nguvu ya msukumo ilikuwa nyuma hata kiti cha abiria kimefyatuka kurudi nyuma sio mbele..
Na ikiwa Marehemu alipata majeraha kisogoni ina maanisha zaidi kuwa alivutwa nyuma wakati wa impact na sio mbele..
 
Kichuguu na wengine,

Inaonekana kuna kazi nzito kuirudisha nchi kwenye mstari sio rahisi kama watu tunavyofikiria. Kama mtu anahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kutungwa tu, kwa sababu watu fulani wametaka iwe hivyo kwa maslahi yao ....we have a long way to go.
 
Wana JF,
Chacha Wangwe amefariki kwa ajali na wala si vinginevyo.

Dereva wa gari alikuwa Mallya, na gari ilikuwa inakwenda mwendo wa kasi, ikamshinda nguvu huyu kijana na kuanza kutoka nje ya barabara. Mallya akaona isiwe shida akaachia kila kitu na kuruka. Gari likaviringika na kujipiga kwenye miti ama mawe upande wa nyuma. Wangwe alikaa kiti cha mbele na hakufunga mkanda hivyo alijibamiza kichwa kwenye nguzo ya gari ama mti na ndipo umati ulipomfika.

Theory butu kabisa hii hasa kwa vile:

(a) Mzee George anasema alipofika pale shughuli kubwa ilikuwa ni kumfungulia mkanda marehemu Wangwa.

(b) Kama gari likuwa spidi kubwa iliyomshinda Mallya hadi akaamua kuruka nje ya gari ni lazima naye angekuwa ameumia sana. Afterall magari mengi ya siku huwa milango yake haifuguki wakati yakiwa kwenye mwendo wa kuzidi kiasi fulani.

(c) Binafsi simchukulii huyu Mallya kuwa hajui kuendesha gari kabisa kama serikali inavyojaribu kufanya tuamini.
 
Lakini pamoja na moyo wote wa Wangwe kwa wananchi hakuwa na bahati kwani huko Chadema ndio kapata masimango mengi toka kwa Mbowe aliyesema kuwa hawezi kufanya kazi na Wangwe, Kitila Mkumbo alisema kuwa Wangwe ni mzigo mkubwa ndani ya Chadema na hana INTERPERSONAL SKILLS, swali kama hakuwa na INTERPERSONAL SKILLS aliweza vipi kukubalika na wananchi wake?

Misukosuko waliyompa Wangwe hawa jamaaa wa Chadema ni mingi sana, na cha ajabu Mwenyekiti wa Chadema hajatuma wala kuandaa salamu za rambirambi kwa familia au wanachadema, pia wazee wa Chadema hakuna aliyekwenda kuzika kama Mtei,Ndesamburo,ngaiza,baregu,wabunge wanawake wa chadema hawakwenda kuzika.

Mbowe alituma barua nyingi wakati wa Wangwe kusimamishwa lakini kwenye msiba hajatuma salamu za rambi rambi wala pole kwa wana Chadema wala ndugu wa Wangwe ameshindwa kupeleka hata ubani kwa wafiwa.
 
Mgagagigikoko,
Mkuu kuna sehemu nakubaliana na wewe lakini hili tena mkuu wangu umevuka mpaka!.. Hivi kweli wewe unaweza kusimama hapa na kuyasema yote hayo kwa moyo ulikuwa huru na majonzi ya msiba huu ama unafanya utani?..
Hivi kweili kuna haja kubwa ya Kikwete apeleke barua ya rambirambi ktk familia za kina Mbatia na wengineo kupitia vyombo vya habari wakati ameweza kwenda yeye mwenyewe?..Hivi kweli ni lazima mtu ajitangaze ktk vyombo vya habari anapotoa fedha za ubani na usipotoa ina maana wewe una matatizo na marehemu!..come on now!
Mkuu tafadhari acha uhuni nadhani sasa unaingia kubaya, binafsi siwezi hata siku moja kumtazama Mkapa (mbaya wangu) kwa mabaya yake kutokana na jinsi anavyojishirikisha ktk vifo vya watu...Labda moja tu pale alipoonekana akicheka sana na Lowassa ktk msiba wa mzee Munanka hali watu wote wanaonekana wana majonzi..Hata hivyo nilihukumu kitendo cha wao kucheka ktk hali ile pamoja na kwamba walihudhuria mazishi na pengine kukata kisu kikubwa.
 
Ndiyo maana ni vyema tunafanya discussion. Mi nimejifunza information nyeti hapa. Inawezekana kuwa actually Mallya ni jasusi aliyespecialize katika assasination. Kumbukeni Libya ilikuwa terrorist state na wamesamahewa kwa sababu ya pesa nyingi waliyolipa wazungu na also kwa sababu ya mafuta. Lakini fact ni kwamba wanatoa training ya hali ya juu ya kijasusi.
Hiyo travel itinerary niliyosoma ya Mkandara aliyoipata kwa kweli inaonyesha moja kwa moja ya kuwa Mallya si mtu wa kawaida maana in this time of post 9/11 si rahisi kusafiri bila pasi na kudandia misafara. Kijana kama huyu alitoa wapi finances za kusafiri? Pia kuna mtu amepost earlier ya kuwa anamdai Mallya na pia anamfahamu na Mallya alitamba kuwa anamjua Gadaffi. Sasa tunaweza kupuuza but sometimes the most incredible things are true! Jamani endeleeni kuweka hapa data tuendelee kupata pieces of the jigsaw puzzle.
 
Hivi kuna waatu mpaka sasa hivi wanaamini kuwa wachunguzi wetu wameshindwa kujua nani alikuwa anaendesha gari, nini kimetokea, Wangwe aliikuwa amekaa kiti gani?

Kama ni hivyo nini maana ya kutumia hela nyingi kusomesha watu wa crime scene na maswala ya evidence collecting? Kitakuwa kitu cha ajabu sana!!
 
Kichuguu na Mkandara.

Nauliza swali, Mbowe alituma press R nyingi kwenye vyombo vya habari kueleza kwanini Wangwe kasimamishwa nafasi yake ya umakamu wa mwenyekiti na hawezi kufanya nae kazi, lakini sijaona tamko lake au rambi rambi kwa ndugu wa marehemu,wana Chadema au marafiki wa Wangwe ameshindwa hata kwenda kuitembea familia ya Wangwe na kuongea nao,yaani hajatoa kauli yeyote juu ya kifo cha WANGWE na amemuachia mtoto mdogo Mnyika kuandika barua kwa IGP,

kwanini hakumuachia Mnyika kuandika juu ya Wangwe kusimamishwa Umakamu?

kitu kingine wazee wa Chadema kama MTEI,Ndesamburo,Ngaiza,Baregu au kundi la wabunge wanawake wa Chadema kama Suzan Lyimo,Grace Kiwelu,Anna Komu na mtoto wa Ndesamburo(Lucy) hawakwenda kwenye msiba hata mmoja kati yao, kama angekuwa kafa Mbowe wasingekwenda? mzee Mtei au Bob Makani kama Mbowe angekuwa amefariki wasingekwenda?

Akifa Pius Msekwa ambaye ni makamu wa Mwenyekiti wa CCM,watu kama mzee Mwinyi,Kawawa na Malecela hawatakwenda kwenye msiba? jee wazee wa Chadema wamejiingiza kwenye ugomvi wa marehemu Wangwe na Mbowe na wao kuwa upande wa Mbowe kiasi cha kususia kwenda kuiaga maiti?

naomba jibu, naona Wangwe hakupewa hadhi yake na watu wa Chadema.
kumtuma Mnyika kwenda kutoa tamko la Chadema ni sawa na Muafaka wa DR.Salmini Amour na Seif Shariff Hamad walipoitwa na jumuiya ya Madola chini ya Chifu anyauko, pande hizo mbili ili kupata suluhu ya muafaka kwa mara ya kwanza, ambapo DR.Salmin hakuhudhuria na badala yake akamtuma sheha(mjumbe wa nyumba kumi) kuwakilisha upande wa CCM. ilikuwa kama dharau kwa Seif Hamad,
jee kitendo cha Mbowe kutotoa kauli hadi sasa na kumtuma Mnyika(sheha wa Chadema) ni dharau kwa Wangwe?
 
Well anaweza kuwa ni trained assassin.....je ni wa serikali yetu au watu binafsi...na kama anajuana na Ghaddafi personally could he be a double agent?

Kuhusu kujisomesha,inawezekana alikuwa tapped na master wake akamsomesha na kumtrain kama most assassins na operatives wanavyokuwa recruited kwa sharti la kutokumtaja, kuhusu computer na kuchora hiyo ni cover up.

So kama ni assassin au spy cover imekuwa blown whats next for him...we all know what happens when your cover is blown!!!
 
Mgagagigikoko,
Nakuuliza nawe pia.
Unajuaje kama Mbowe hakutoa hotuba, barua ya rambirambi na mengineyo huko huko Tarime alipokuwepo!.. Je haya yote ni lazima yafanyike kupitia vyombo vya habari?..
Swala la Mbowe kuandika zile barua ni utaratibu wa kisheria ktk ngazi zote huwezi kumpa mtu mwingine mashtaka yanayokuhusu wewe. Jambo ambalo halihusiani kwa ukaribu hata kidogo na msiba huu.
rambi rambi sio lazima zipitie vyombo vyovyote vile unaweza kumpa mhusika moja kwa moja kama vile unapotoa mchango wa Ubani...Kitu ambacho sijakiona ni rambirambi zako wewe na kina Rostam kwa Chadema na familia..Mbowe ni Chadema ama ndio sababu hamkufanya hivyo!

Kuhudhuria kwa wazee kama kina Mtei, na hao wanawake imehusiana vipi na msiba huu kama sio njia yako ya kurejesha swala la Ukabila!..
Hukutazama chama chako ambacho hakikupeleka mtu isipokuwa wale waliotoka Bungeni lakini umekuja hesabu viongozi wa Chadema kaa vile CCM na Chadema ni maadui wakubwa kiasi kwamba akifa mtu wa CCM basi Chadema hawahusiki ila wana CCM. Hivi ktk akili yako umeiweka kuwa Chacha Wangwe ni msiba wa Chadema sio?.. mkuu hapo utakuwa umekaa upande mwingine kabisa wa jinsi sisi wengine tunavyouchukulia msiba huu..Nilitaka kuuliza wewe kwa nini Kikwete,Tostam, Malecela na kundi kubwa la viongozi wote wa juu wa CCM hakwenda lakini basi sina haja ya kuendelea!..Naona unauchezea sana kimzaha mzaha msiba huu..
Ama kweli Wangwe alikuwa mbunge wa Tarime......imetosha.
 
Kubalini tu ndugu zangu yaishe, tusubiri mwingine, next time CCM, au CUF, au mtu mmoja uraiani mwenye kelele; ajali nzuri kama hii, legit, na next time no survivors n.k nadhani ni mtindo ambao tumeukubali wa kuondoana madarakani. Tusipojifunza kukataa, hatuna budi kuendelea kukubali.
 
Lakini pamoja na moyo wote wa Wangwe kwa wananchi hakuwa na bahati kwani huko Chadema ndio kapata masimango mengi toka kwa Mbowe aliyesema kuwa hawezi kufanya kazi na Wangwe, Kitila Mkumbo alisema kuwa Wangwe ni mzigo mkubwa ndani ya Chadema na hana INTERPERSONAL SKILLS, swali kama hakuwa na INTERPERSONAL SKILLS aliweza vipi kukubalika na wananchi wake?

Misukosuko waliyompa Wangwe hawa jamaaa wa Chadema ni mingi sana, na cha ajabu Mwenyekiti wa Chadema hajatuma wala kuandaa salamu za rambirambi kwa familia au wanachadema, pia wazee wa Chadema hakuna aliyekwenda kuzika kama Mtei,Ndesamburo,ngaiza,baregu,wabunge wanawake wa chadema hawakwenda kuzika.

Mbowe alituma barua nyingi wakati wa Wangwe kusimamishwa lakini kwenye msiba hajatuma salamu za rambi rambi wala pole kwa wana Chadema wala ndugu wa Wangwe ameshindwa kupeleka hata ubani kwa wafiwa.

Nadhani hapa tunachanganya maada, Wangwe alikuwa jasiri kwa ujasiri unaoufahamu wewe.Lakini yeye kuwa shujaa haimaanishi ndio alielewana na kukubaliana na kila mtu.Kila mtu ana mapungufu yake na nguvu zake.Nguvu zake na uzuri wake havikuwa kinga ya yeye kutokutofautiana na wengine katika mambo mengine.uzungumzamvyo ni kana kwamba mlijua kuwa Wangwe atafariki kwa hiyo mlikuwa mnamtetea au kukubaliana na mawazo yake kwa sababu mlijua kuwa atakufa muda si mrefu! Haiwaletei wala hamtakuwa washindi kwa sababu mlikuwa upande wa Wangwe, lakini hii haimpi kushindwa au kuonekana mbumbumbu bwana Mbowe.

Yale aliyoaacha ni mazuri kwa Mbowe kuyafanyia kazi , maana sifa ya kiongozi ni kubadilika na kukubaliana na ukweli.Lakini pia si kwa sababu Wangwe allikuwa vile tunavyomfahamu ndio aonekane alikuwa sahihi kwa kila kitu.Hata baba wa kwanza wa TZ nae alikuwa na mambo mengi ambayo hakuelewana na wenzake.Kutokuelewana au kuelewana katika swala moja havipelekei ukawa dhaifu au na nguvu katika swala lingine.Narudia uzuri wa Wangwe haupelekei au haumkingi kuwa hakuwa na udhaifu katika maswala mengine.Hali kadhalika Mbowe kukosea sehemu moja haimaanishi kuwa ni dhaifu kiasi hicho, na wala haipelekei kuwa wewe nawe huko sahihi sana kiasi cha kuwa mawazo yako ni final!

If i were you, ningempa break Mbowe atafakari kipindi hiki kigumu kwake-ubinadamu uwepo.Kama unaona unaweza ukaandika chochote kwenye internet ili mradi kuandika tu, with your status in JF!.Yaani wewe mwenzetu vifo vyote unatoa rambirambi! yaani unataka mpaka mume aliyefiwa mkewe atoe rambirambi usikie wakati msiba nae unamhusu, kipimo cha upendo kwako wewe ni kutoa rambirambi wala sio hata kutoa hela ya Sanda,fedha za kula na kuitunza familia ya marehemu.Unataka aende redioni aseme ndio ufurahi-Hapa nimekudevalue

Give me a break


“The breath of accusation kills an innocent name, and leaves for lame acquittal the poor life, which is a mask without it” Percy Bysshe Shelley



Waberoya
 
tunaomba profile ya Malya....."kijana anayeweza kudandia ndege, na kudandia misafara ya wabunge"
 
kazi kubwa ipo mbele yetu! hivi kwanini ccm wengi wanakuwa na roho za kikatili? au ni moja ya sera za chama?
 
Kama huyu kijana ndiye alikuwa anaendesha gari, hana leseni, na kwa mwendo kasi; kwanini ameshtakiwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni na kuendesha gari kasi bila kushtakiwa kwa kosa la kusababisha kifo? Akili mukichwa. Tukubali tu ilikuwa ni ajali ya kawaida (kwamba mtu asiye ne leseni, anaenda kasi, anamuendesha Mbunge wa Bunge la Muungano - ni kawaida tu)?

Mkuu MWKJJ,mpaka hapo tulipo sasa hata akishitakiwa kwa kosa la kusababisha kifo siyo hoja kubwa sana kulingana na aina ya tukio.Akishtakiwa tu hivyo na akihukumiwa itakuwa shangwe kwa upande wa wataka mabaya kwani atakata rufaa na atashinda kesi.Niamini mimi.Hadi hapo bado ni traffic case. "KUNA DREVA MMOJA WA DALADALA ALIKUWA ANAFANYA SAFARI ZAKE KILA SIKU KUTOKA POINTI A KWENDA B HUKU GARI LAKE LIKIWA HALINA BREKI.ALITUMIA UZOEFU WA KUSIMAMA KWA KUWEKA GIA KUBWA,SIKU MOJA GARI LIKAMSHINDA AKALIPINDUA NA KUUA ABIRI WOTE.POLISI WAKAMKAMATA NA KUMSHITAKI KUSABABISHA VIFO.AKAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA.BAADAE AKAKATA RUFAA,KATIKA RUFAA AKAACHILIWA HURU KWANI JAJI ALISEMA MSHITAKIWA ALIKUWA ANAFANYA KAZI ZAKE KILA SIKU NA HAKUWAHI KUUA,NA HAIKUWA MARA YA KWANZA KUENDESHA GARI LIKIWA HALINA BREKI.HIVYO IKABIDI AHUKUMIWE AS TRAFFIC CASE KWA KUENDESHA GARI LIKIWA HALINA BREKI NA KUTWOZWA FAINI 20,000/=

Labda tuwekane sawa (kisheria) kuwa ili kesi iwe ya mauaji kuna elements zake za ili tendo hilo lijitokeze la mauaji. Yaani namaanisha kuwa kuna kitu kinaitwa "intetion".Kuendesha gari kwa kasi bado kisheria hai-intend kuua.Mallya kwenye utetezi atasema hivyo.Niamini mimi.Lakini kwa undani wa nje ya sheria utaona dhairi kuwa intetion ya Mallya ilikuwa ni kuua.Sasa hapo ndo kuna utata.Kimsingi hadi hapo mallya alipo atatoka tuu.Ila kama kweli polisi wetu ambao mimi mara zote nawaita wazee wa ku-bold na italic wako serious na issue hii basi waende hatua nyingi tu mbele ya suala hili ili tupate intetion za Mallya kisheria za kuua hili shitaka libadilike na asomewe mauaji.

NINGEKUWA MIMI POLISI,zooote hizi nisingesumbuka nazo sana ila ningeanza tu na upatikanaji wa siraha -pistol.
Jamani tufungue macho,kama kweli mallya alikutwa na pistol,wote tunajua process za kumiliki siraha TZ zikoje.Nimemsoma mallya kwenye picha na nimeona umri wake,hulka na silka yake bado natatizwa na umiliki wake halali wa siraha hasa pistol kama kweli alikuwa nayo.Yaani hapo ndo ningeunganisha dots na kupata pa kumshikia.

Kumpa Mallya ujasusi mimi bado inanipa wasiwasi.Tunamkuza mno.Hakuna jasusi hasiyekuwa makini kiasi hicho.Yaani jasusi anakana hadi kujua kuendesha gari??????Nope.Angekuwa jasusi palepale angekubali kuwa yeye ndo alikuwa dreva.Kwisha habari.Tusingefika kote huku.ILA UKIONA HIYO TREND UTAGUNDUA KUWA MALLYA ALIKUWA ANAPEWA MAELEKEZO NA MTU/WATU WENGINE.Yaani kuna watu walikuwa wanamshauri afanye nini hasa kukubali kuwa yeye ndo alikuwa dreva na mambo mengine kama hayo.so kuna vitu bado vimejificha vingi tuu.
-huyu mallya mimi namuona kama alikuwa ni nyoka tu ila kazi yake ya unyoka anaijua barabara,si wa kucheza nae akikupatia sehemu zake,hata hivyo kajawa na usanii hicho ndo kimemharibu zaidi na haridhiki.
 
Si tunao MAJASUSI kibao humu JF? hakuna anayemfahamu Mallya atujuze kidogo? Au maadili hayaruhusu?
 
Waandishi wengi mikoani ni MAKANJANJA wa kutupa, elimu ndogo ya shule na uandishi wenyewe. Kuwayumbisha waandike au waripoti unachakitaka wewe ni rahisi tu. Kwa mfano huyo GEORGE MARATO alikuwa mhudumu wa baa moja pale maeneo ya SINZA. Hakuwa na elimu ya sekondari.
 
WildCard sheria inakataza to out an agent; Lakini Majita umeesema jambo moja. Naamini tatizo langu binafsi ni kujisahau kuwa marekani mfumo wake wa sheria uko tofauti sana na wa kwetu ambao una msingi wa sheria za kiingereza.

Wamarekani kwenye mambo ya mauaji wana:

Murder - in the first, second and third degree
Manslaughter ambayo na yenyewe ina vipengele vyake halafu kwenye magari kuna specific charge inayoitwa vehicular homicide kama kumgonga mtu kwa makusudi n.k halafu kuna vitu kama accidental death and dismemberment. n.k

Na kuna moja inaitwa criminal negligence; yaani (nitumie mfano wako) sheria inasema gari lazima liwe na breki inayofanya kazi. Sasa wewe ukaamua kuneglect kutengeneza breki zako halafu gari lako ukiwa unaenda likapata ajali na uchunguzi ukaonesha kuwa ni breki ambazo ulikuwa unajua zimekufa, basi zaidi ya kuchargiwa na vitu vingine wanaongeza hivyo ya "criminal negligence" kimsingi ni kosa la uzembe.

Sijui kama Tanzania tuna charge kama hiyo.

Hivyo nakubali sijui sana sheria za Tanzania hususani kuhusu kifo cha ajali.
 
kazi kubwa ipo mbele yetu! hivi kwanini ccm wengi wanakuwa na roho za kikatili? au ni moja ya sera za chama?

Sera za Chama ziko safi tu pengine kuliko chama kingine; haya mambo yanatokea kwa sababu wananchi wengi hawajui haki zao hasa vijijini. Polisi pamoja mahakimu wa mahakama za mikoani nao wanataka kujionyesha kuwa wanaisaidia CCM, kubaki madarakani.!! Ingawaje wahenga walisema samaki mmoja akioza wote wanaoza ila mimi naamini kuna viongozi ndani ya CCM wakisikia uonevu wa aina hii wanakosa amani kabisa. Safari ni ndefu ila tutafika tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom