mtizedi
JF-Expert Member
- Jan 31, 2008
- 360
- 1
Ni bora kuwa na wanasiasa mafisadi wakivinjari kuliko wanasiasa mufilisi mbele ya vyombo vya habari......
Hawa jamaa wote waliletwa TARIME na ndege aliyokodisha MBOWE. Walipoifika msibani wakaachwa nyuma na kundi la mashabiki wa MBOWE kumuingiza katika eneo la shughuli ya mazishi.
Hawa ndio waliokuwa wakiimba RAISI, RAISI,...MPAKA KIELEWEKE....wakiwa na mabango lukuki yakihoji kifo cha WANGWE lakini hakuna hata moja lilikuwa likihoji uhusika wa CHADEMA au MBOWE. Hawa waliendelea kupiga kelele hata RC MAchibya am baye ni dui number moja wa wakazi wa TARIME alipopanda jukwaani na kuwataka wanyamaze. Hata kufikia kusema watulie ili waweze kumsikia RAIS wao...meaning MBOWE. RC Machibya aliendelea kuongeza lakini hakuna aliyemsikiliza huku vijana wawili wakiendelea kupiga kelele bila ya kutulia. Ni pale tu Zitto alipokuwa akiongea ndipo walitulia kidogo. Cha ajabu ni kuwa RC Machibya aikuwa hafurahishwi na hali hiyo kiasi cha kumnyang'anya Zitto MIC kila vijana hao wakiwa wanatulia na hivyo kuanzisha kelele nyingine. Mkumbuke kuwa MACHIBYA anaendesha operation ya kuzuia kusafirishwa chakula kwenda TARIME kwa madai kuwa wanatorosha chakula kwenda Kenya.
Cha ajabu zaidi ni kuwa Binamu wa Marehemu anayejulikana kama Mzee KEBA ambaye walikuwa na ushindani mkubwa kisiasa na Marehemu CHACHA WANGWE yeye akiwa kada na kiongozi wa CCM, alipanda jukwaani na kuwaonyeshea alama ya dole tupu waliokuwa wakipiga kelele hapo na hata kuchukua BANGO lilikuwa likiuliza kama Ni RISASI ama AJALI na kuliinua juu akilizungusha kwa kila mtu kuliona.
Hata hivyo vijana hao haswa wale wawili hawakuwa tayari kunyamaza hadi Zitto alipochukua MIC tena na kuanza kutumia slogans za CHADEMA ambazo ziliitikiwa kwa nguvu na kuanza kunyamaza ndipo alipomkabidhi MIC Prof Wangwe ambaye alitoa taarifa ya kuahirishwa kwa mazishi na kuwepo kwa uchunguzi mwingine wa mwili wa marehemu.
Baada ya hapo ndipo askari wa polisi na vijana wa ulinzi wa CHADEMA wakawachukua viongozi wote zaidi ya hamsini waliokuwepo plae na kuwaoonda mahala hapo kwa haraka kupitia chumba kilichokuwa na mwili wa marehemu ambacho kina milango miwili mmoja wapo ukiwa ni geti la chuma la kuingilia hala unatokea kwnye uwa wa nyumba kabla ya kupita mlango mwengie unaotokea mbel ya nyumba na kutoka nje kupanda magari.
Wakati wote huo hakuna waliokuwa wametoa silaha za aina yoyote na hata kutupa mawe. Kama ni kushambuliwa magari basi ilikuwa ni magari a serikali ambayo yalikuwa yakigongwa gongwa kwa mkono kama wafanyavyo wapiga debe wa daladala....
Ni kweli hapo nje kulikuwa na mtafaruku ambao ulisababishwa na panick iliyokuwepo miongoni mwa waheshimiwa wengi waliokuwepo hapo na kupelekea kukimbili katika magari yao na hata wegine kuingia katika magari yasiyo yao.
Ni wazi kuwa RC, RPC na watendaji wengine wa serikali walikuwa wamepanick na hata wakati mwengine kuonekana kuwa wanapenda kuonesha hali ya vurugu ipo.
Ni kweli pia katika hali kama ile ilikuwa ni busara kuwaondoa WAHEMSHIMIWA wale kwa haraka kwani eneo lile halikuwa na nafasi yoyote ya kuwalinda. Kilichofanya wao kupita katika kichumba ambacho ndipo mwili wa marehemu ulikuwepo ni kujaa kwa watu katika sehemu ya kuingilia katika eneo hilo ma tu baada ya MBOWE kungia na kundi la mashabiki ambao walijaa eneo lote la kuingilia kuelekea jukwaani na wengine wakijaribu kutoa mikono kwa waheshimiwa walikuwepo hapo haswa MBOWE na SLAA.
Zitto ndio alikuwa kiongozi wa mwisho kutoka eneo hilo na kuelekea nje ambak askari walimlazimisha kuingia katika gari la MHESHIMIWA MKONO akiwa na MESHIMIWA SARUNGI na mlinzi wake mmoja aliyepewa na IGP. Huyu alipewa baada ya yeye kukataa ulinzi wa FFU watatu ambao DC na KAIMU RPC wa MUSOMA walitaka aongozane nao MARA alipofika MUSOMA mjini........
Ukweli maizngira ya uwezekano wa vurugu kubwa na hatari yalikuwepo lakini si kweli kuwa siku ile kuna waliokuwa wakitishia maisha ya MBOWE. Na kama kuondolewa pale na askari hilo lilifanyika kwa wote walikuwa wamekaa kweny viti vya waheshimiwa wakiwemo wabunge zaidi ya 20, viongozi wa vyma zaidi ya 5, Viongozi wa CCM kadha ambao walikuja na mavazi yao ya chama kitu kilichopelekea hata MWenyekiti wa Moa aliyekuwa amekaa katika eneo la viongzi kutolewa na vijana wa CHADEMA na kuhamishiwa sehemu nyingine aliyopaswa kuwepo.
Wakina MREMA wao walichokuwa wakikifanya tangia wakati huo ni kuchochea sumu tu wakisaidiana na baadhi ya wanafamilia na kina MAMA KABAKA, Mzee GACHUMA na wengineo huko. Sumu yao pamoja na reporting ya kina GEORGE MARATO na mwenzake wa CHANEL TEN amao dio chanzo cha habari za kupotosha katika vyomb vingi vya habari ndio vilipelekea hali mbaya zaidi siku iliyofuata kwani hata baadhi ya watoto wake walianza kuamini kuwa marehemu aliuawa na risasi.
Mbaya zaidi ni kuwa hata wakati uchunguzi wa mwili ukiendelea TARIME MJINI kuna mtu alituma msg kijijini kuwa imethibitika kuwa kulikuwa na risasi mbili katika mwili wa marehemu....kitu ambacho kilifanya hata viongozi wengine wa CHADEMA kuamua kurudi TARIME mjini na wengine kuondoka hapo mara baada ya uchunguzi wa pili kwisha.
Kwa kweli sikuona ajabu kwa MREMAna MBATIA kufanya walichokifanya lakini ya Prof LIPUMBA yamenifanya kujiuliza zaidi kama nijiunge na siasa za vyama hivi ama laa. Iweje msomi kama yeye kutumia propaganda hovyo kama za kumhusisha MALLYA na UGAIDI eti kwa kuwa alikutwa na kikaratasi kikiwa na maandishi ya kiarabu ama aliwahi kwenda LIBYA. Hii haina tofauti na taswira iliyojengwa duniani kuhusu waislamu. Yaani hapa anahalalisha sumu hiyo dhidi ya uislamu na waislamu. Na yeye bado anajitambulisha yeye kama muislamu.
Na anaposema kuwa kichwa kilikuwa kimepondeka inabidi ajihadhari na hilo maana ukweli ni kuwa postmortem zote zinapaswa kufanywa na kurekodiwa na video. Nina uhakika wa hilo kwa uchunguzi wa TARIME maana alikuwepo mtaalamu wa ID wa polisi akirekodi zoezi zima.
Hawa kina MREMA na MBATIA waace waendelee kkupalia moto hii chuki inayopandikizwa hapa wakidhani itakwisha kwa WACHAGA Mbowe na Mallya tu.....Hii inakwenda zaidi ya hapo. Hata hivyo sidhangai sana kwao kuvaa siasa hovyohovyo kama hizi kwani upeo wao unajulikana...Lakini la LIPUMBA linatisha....
Kwa mimi niliyekuwepo TARIME kuanzia mwili ulipoingia hadi siku ya kuzikwa nashukuru wengi wenu hapa jinsi mnavyochemsha kwani mnaniwezesha kujielimisha mambo mengi ikiwemo hili suala la kujenga imani kwa misingi ya hisia zilizokosa chembe ya ujuvi......
Tanzanianjema
unatumia nguvu nyingi sana kuuzima moto huu ..tatizo umebeba mafuta ya petrol kwenye ndoo hiyo unayodhani imejaa maji ya kuuzima moto huo..