Anatoa maelezo chini ya kanuni ya 50 ya bunge, anasema kuwa kanuni zinaelekeza masuala ya kufanyika pindi inapotokea kuwa mbunge amefariki, na anasema kuwa yeye aliteuliwa na Mheshimiwa spika kuwa mwenyekiti wa ujumbe aakiwa na Wanyancha, mkono, john chetyo,sarungu,hamad ,mnyaa,slaa,juma kilimba ,zitto,kabaka,masunga joyce,jaeth masaburi.suzan lyimo ,james nsekela ,vedastus manyinyi .
waliondoka saa mbili na nusu asubuhi na kuwasili saa tano kamili asubuhi,na kupokelewa na mkuu wa mkoa akiwa pamoja na viongozi wengine wa kisiasa.
waliondoka na masafara wa magari ya serikali, na ujumbe ulipofika ulibaini kuwa mambo sio shwari kwani vijana wengi walikuwa wanarandaranda na mabaongo na kuonyesha kuwa palikuwa na mtafaruku, na walipodadisi kwa viongozi wa serikali waliambiwa kuwa mazishi hayatafanyika siku hiyo kutokana na ndugu kuwa na wasiwasi juu ya msiba husika , na baada ya hapo walijadiliana na ndugu hao wakiwa na mkuu wa mkioa wa mara na kwa kuwa ujumbe wa spika ulikuwa ni kwa ajili ya kusoma risala na kukabidhi mchango wa rambirambi .
wakataka wasome risala na ujumbe uweze kuondoka ,ila ilipofika saa nane na dakika 30 mtafaruku ulianza na wananchi walisema kuwa wako tayari kiumchagua mwingienwakamuue tena , na katika hali waliyoiona hawakuwa na njia nyingine ila ni kwa ujumbe kuondoka na kuelekea musoma na kurejea dodoma .
kabla ya kuwasilisha maelezo hayo ,walipata taarifa za uhakika kutoka kwa viongozi wa mkoa wa mara kuwa uchunguzi ulifanyika na ndugu kukubaliana na uchunguzi huo,na tayari alishazikwa.
Kwa kuwa mazishi yalishafanyika, wanaandaa utaratibu wa kuwasilisha mchango wa rambirambi ya bunge kwa familia ,anashukuru bunge kwa kuwapa heshima ya kuliwakilisha ,na jukumu lilikuwa zito na nyeti na lenye utata mkubwa.
mwisho anaushukuru kwa dhati uongozi wa mkoa wa mara kwa ushirikiano mkubwa na pia anawashukuru wabunge wenzake kwa uadilifu na pia ushirikiano kwa kipindi chote ,pia anampongeza spiaka kwa kuwezesha TBC kuweza kushiriki shughuli za mazishi na pia kwa wao kuweza kuonyesha mazishi hayo live.
amemaliza.
swali;mbona hakuna cha mapanga, sime,mishale, marungu .n.k?
yeye anasema kuwa waliona mabango na vijana wakiimba kwa uchungu,
hasemi kuwa walisindikizwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ,
sasa jadilini wenyewe,